Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

Shem wangu wa ukweli hongera sana jpili kazi ni moja nishaweka kwenye desktop
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 47

Mudy akatabasamu, kisha akainuka na kuongoza kuelekea alipoambiwa. Alikuwa akitembea bila wasiwasi
wowote.. Licha ya kujua kuwa anafuatiliwa lakini bado aliupa ubongo wake Utulivu.. Utulivu ambao aliuhitaji sana katika kazi yake ya Hatari. Akauvuka mlango wa kuelekea ndani Ya
hoteli ile.. Alipouvuka akaongoza moja kwa moja mpaka sehemu husika.. Alianza kuhesabu chumba kimoja baada ya kingine. Alipokifikia Chumba namba 14 B akakipita kama
hakuwa na umuhimu nacho. Akaendelea na Safari kuelekea upande Mwingine.. Wakati akiumaliza upande wa chumba kile, akahisi kusikia vishindo vya mtu.. Hakujipa kazi Ya kugeuka
bali aliongoza kama hakuhisi kitu. Kila alipokuwa Akisonga ndivyo vile vishindo vilivyozidi kusiki

Mkuu huo ni msisimko hatari sana hongera kaka duuuh
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 61

ulikuwa mchezo wa hatari sana kuucheza, ulikuwa mchezo wa kukitaka kifo kucheza na watu wale. Watu waliozoea kucheza na manyani, simba na Hata chui. Watu ambao waliishi msituni kama wanyama. Lakini Kwa Ummu Sammy Hilo halikuwa tatizo, haikuwa shida kwa kuwa hata yeye alipitia huko. Alikuwa Tayari kufa lakini sikuona Mohamed, Revina na Hata Jenifer wakipotea. Akaendelea kufuatilia gari zile. Gari ambazo ziliongoza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Hakutaka kujiweka mbele kuogopa kuonekana ama kushtukiwa. Aliendelea kuendesha pikipiki akipita hapa na kupita kule. Muda wote hakutaka kuupoteza ule msafara wa Magari. Alihakikisha anakifanya kile ambacho alihitaji kukifanya.

Wakati Ummu akiwa nyuma ya msafara ule. Huku ndani ya gari waliyopakiwa Mohamed na Wasichana Wale, Mudy alikuwa ameanza kuupata ufahamu. Lakini hakutaka kuonekana mapema. Hivyo akaendelea kuzuga kupoteza fahamu huku akifumbua macho yake kwa hila kutazama watu waliomzunguka. Bado macho yake yalikuwa mazito na bado hayakutaka kufunguka, lakini alipambana na kufanikiwa kuuondoa ule usingizi. Jicho lake la kwanza lilitua kwa wasichana wawili, wasichana ambao mmoja alikuwa akivuja Damu begani Kuonyesha kuwa alipigwa Risasi wakati wa mapambano. Alikuwa Revina na Jenifer huku Revina akionyesha kuvuja damu. Akaendelea kuyatembeza macho yake mle kwenye gari.. Kando Yake walikaa makomandoo watatu wakiwa na Bunduki nzito Mikononi mwao. Wote walikuwa wakiangalia mbele huku mara Moja moja wakimtizama Mohamedi.

Kila walipokuwa wakigeuza macho kumuangalia Mohamedi alikuwa akijikausha na kuzuga kuwa bado amepoteza fahamu. Baada ya kuuangalia ulinzi na kuridhika kuwa anaweza kulianzisha, akaanza kuupima mwili wake kama unaweza kumudu mapambano na kuondoka akiwa salama. Alijikuta bado, alijikuta bado akiwa hana nguvu za kutosha. Akaendelea kutulia huku akivuta kumbukumbu. Kumbukumbu juu ya watu wawili waliofunikwa vitambaa vichwani wakati anachukuliwa na Makomandoo wale. Hakujua walikuwa ni Watu gani, Hakujua kuwa Rais Alikuwa Hatarini na hakujua kuwa nchi ilikuwA ikielekea kwenye mapinduzi Muda mfupi Ujao. Bado alihitaji utulivu na Bado alihitaji Kuupa mwili wake nguvu.

Wakati akiendelea kulisubiria Hilo, punde akamuona Jenifer akijitingisha. Kujitingisha kwa Jenifer kukaleta Mshangao kwa walinzi waliokaa pembeni Ya Mohamed. Mmoja akainuka kuelekea pale kwenye siti walipolazwa Jenifer na Revina. Alipiga hatua Ya kwanza na kupiga Nyingine Ya Tatu. Hilo likawakosa kubwa kwa mlinzi Yule. Hakuna aliyetegemea kati yao, Hakuna Aliyetegemea kwamba Jenifer angefanya Shambulizi.. Shambulizi lililomuamsha Revina na kumpa Nguvu Mohamedi. Ni hatua ya tatu aliyopiga mlinzi Yule akajikuta akipokea Teke kali la katikati Ya Miguu.. Teke lilimuacha ameinama huku akiisahau bunduki. Hakupewa nafasi Nyingine.. Mikono migumu ya mwanadada Jenifer alitosha kuinyonga shingo ya mtu yule. Wote wakageuka Nyuma kumuangalia Mlinzi Mwingine. Hawakuamini walichokiona pale Macho yao yalipotua kwenye Mwili wa Askari Ukiwa chini Ukionyesha kutokuwa na Uhai, Huku Mudy Akiwa amesimama na Mkononi akiwa amekamatia Bunduki. Kilichofuata Ilikuwa kazi Ya kumfuata Dereva. Haikuwa kazi ngumu sana kumteka na kumuamrisha kuelekea kule ambako walikuwa wakipelekwa. Mohamed alikuwa pembeni Ya dereva akiwa amevaa mavazi Ya askari wale, huku mdomo wa bunduki Ukigusa kwenye mbavu za Dereva wa Gari lile.

*****
Ummu bado Alikuwa Nyuma akiifuatilia ile gari, alikuwa makini kwa kila kitu. Bastola mbili bado zilikuwa zimetulia kiunoni zikusubiri kuanzisha Rabsha. Wakati Gari ikiendelea kutembea akashangaa kuwaona watu wawili wakichumba na kila mmoja kuangukia pembeni. Uchupaji ule ulimpa burudani na kumshtua kuwa sasa palikuwa pamekucha. Aliwajua watu wale lakini bado alikuwa akitamani kumuona Mohamedi naye akifuatana na Jenifer na Revina.

Lakini halikutokea hilo, bali sekunde chache akausikia mlipuko ukitokea mbele ya macho yake. Katikati ya moto ule macho yake yakamuona Mohamedi akiwa hewani akiruka samasoti kuingia katika geti kubwa huku akiliacha gari likiteketea kwa Moto. Ummu akatamani kutabasamu. Akatamani kwenda kumkumbatia Mohamedi. Lakini hakuweza hilo. Alikuwa akivutiwa na burudani machoni Mwake. Akaiachia mikono na kusimama Juu ya pikipiki. Sekunde iliyofuata alikuwa hewani Huku bastola ikitema Risasi kuelelekea walipomaadui. Alipotua chini akajitupa na kujigeuza mateke Mfululizo, alikuwa akijipinda na kujipundua. Alikuwa sambamba na Mohamed, alikuwa akipiga pale Mudy alipopiga. Jenifer na Revina walikuwa ndani Ya Jengo. Risasi Zikisikika kila pembe. Kila mmoja akionyesha kile ambacho anakijua. Yalikuwa mashambulizi yalioitingisha Nchi. Mapambano Ambayo yalikuwa ni Ya Kufa na Kupona. Walinzi Walikuwa wakiendelea kuisha, Walikuwa wakiendelea kumalizwa. Mpaka wanaufikia Mlango Wa Kuingilia Ndani, Nyuma Yao kulikuwa na Maiti Wengi Wa Kutosha. Ni Hapo Walipotaka Kuingia Ndipo likatokea Tukio la Kushangaza na kuogopesha. MKE WA RAISI ALIYESADIKIKA AMEKUFA AKITOKEA AKIWA HAI!!
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 62

MKE WA RAIS AMBAYE ALISADIKIKA AMEKUFA NA WATU KWENDA KUMZIKA AKATOKEA. Alitokea mbele ya Wapiganaji wanne. Wapiganaji ambao watu kati ya wanne hawakuamini macho yao. Kila mmoja akaduwaa asijue la kufanya, kila mmoja akaduwaa kutokuamini macho yake. Kila mmoja akaonekana kupigwa na bumbuwazi. Mke wa Rais alikuwa akikimbia kuwajia pale walipo. Akikimbia huku akionekana kudhoofu mwili na hata afya yake. Wote wakanyoosha bunduki zao kuelekea kwake. Kunyoosha huku wakionyesha kutokuwa tayari kuruhusu Risasi. Mbele ya macho yao alikuwa Mke halisi wa Rais. Mwanamke ambaye alipigwa Risasi akiwa Ikulu. Mwanamke ambaye alionekana kuzikwa katika makaburi Ya kinondoni. Huyu ni nani? Kwa nini yupo hai? Yalikuwa maswali katika Vichwa vya Mohamed, Ummu pamoja na Jenifer. Lakini Upande Wa Revina alionyesha kutambua kila kitu kwani hata pale mke wa Rais Alipotokea ndani hakushtuka wala hakuinua bastola kumlenga. Mohamedi akagundua hilo.. Akamuangalia Revina kwa Jicho lenye maswali.. Jicho ambalo lilitaka kujua kile ambacho kilikuwa nyuma ya Miujiza ile. Mtu kuzikwa na kufufuka. Mtu kuuawa ikulu na kujakutokea huku. Bado kilikuwa kizungumkuti. Bado kilikuwa kitendo Cha kutilia shaka. Macho ya Revina yakaongea, yakaongea kwa Ishara aliyowafanya wote wazinduke kwenye Pumbazo.. Pumbazo liliochukua Muda Wao..

Bado mama alikuwa akikimbia.. Bado alikuwa akiupigania uhai wake.. Punde nyuma yake akatokea mtu, Mtu ambaye alikuwa na Bunduki Aina ya Rocket Range.. Bunduki Hatari inayotumika katika hatari tupu. Mtu ambaye walikuwa wakimfahamu. Huyu alikuwa Mkurugenzi Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa mr Adnan Kassim Kwangaya. Mtu ambaye aliamua Kuasi kwa sababu za Uroho Wa Madaraka.. Hawakusubiri Rocket Range ifanye kazi Yake, Hawakutoa Nafasi aifikie Triggle. Mudy Akapawa hewani na kumpiga kikumbo mke Wa Rais nakuanguka naye pembeni.. Risasi Mithili ya Mvua kutoka kwa Wanadada Watatu zikaingia katika mwili Wa Adnan na kumtupa mbali. Hata alipoanguka chini bado Risasi Ziliendelea kumfuata. Kipindi hilo likifanyika Mohamedi alikuwa Tayari ameshamtoa Mke Wa Rais na kumuondoa kabisa katika eneo lile. Alikuwa ameshangazwa na lile tukio, licha ya kuambiwa na Revina lakini bado aliona kuna kitu kizito kimejificha. Alijua kuna kitu ambacho si cha kawaida. Wakati anataka kuondoka akashtukia akivutwa shati lakE, alipogeuka alikutana na tabasamu hafifu la Mke Wa Rais. ''NCHI IKO HATARINI MOHAMED. NENDA KAPAMBANE UMUOKOE MUME WANGU. YUPO NDANI YA JENGO LILE AKILAZIMISHWA KULITANGAZIA TAIFA KUWA ANANG'ATUKA MADARAKANI NA KUIACHA NCHI KWA MAKAMU WA RAIS.'' yalikuwa maneno yaliouzindua ubongo wa Mohamedi. Akataka kuuliza, akini hilo halikufanikisha.. Kidole cha mke wa Rais kikauziba Mdomo wake. Kuuziba kumwambia kuwa Haukuwa Muda wa maswali. Ulikuwa muda wa kazi.. Muda ambao ni wa kufa na kupona. Akautia mkono kwenye sidiria Yake na kumpa Mohamedi Ufunguo. Huu ufunguo ni Wachumba walichofungiwa Binti yangu Mwajuma Rashid na Kijana wangu Ibrahim. Nenda kawaokoe, nenda kamuokoe Mzee wako.

Mudy akautwaa Ufunguo na kuondoka katika sehemu ile Ya siri. Safari hii akiwa na hasira kupindukia. Rais ametekwa na analazamishwa kulitangazia Taifa kuwa anaondoka madarakani. Huku Makamu Wa Rais akionekana kuhusika kwa hiki kisa. Tatizo liko wapi? Ni nani aliutengeneza Huu mchezo? Nani alikufa kama Mke Wa Rais Yupo hai.. Makamu Wa Rais atanijibu maswali yangu. Akaichomoa Bastola Yake Colt 33 Iliyotengemezwa Czechslovakia. Akaikamata mkononi na kuanza kurudi katika Jumba lile kwa kupitia Upande Mwingine. Kila alipokuwa akipita bado milio ya Risasi na Milipuko Ya Mabomu ilisikika na kuonekana machoni mwake. Alikuwa anachuki na Makamu Wa Rais na alikuwa akimtafuta kwa Udi na UVumba. Akaifikia fensi Iliyozunguka Jengo lile.. Hakuhitaji kuangalia mazingira, alichupa kama ninja na kutua ndani bila kusikika. Akatambaa na ukuta huku akiyasikia mapambano kwa Karibu Sana.. Watoto Wakike Walikuwa wameuwasha moto kupindukia.. Walikuwa wakiwanyanyasa makomandoo kupindukia, walikuwa wakitumia bunduki pamoja na mikono.. Walitia fora kuwatizama.. Ilitia fora kumtizama Jenifer alivyokuwa akinyumbulika na kusababisha.

Ilitia raha kumuangalia Ummu Sammy Akipiga mateke aina Ya round kick na kuongeza na Martial Combart. Ilitia Furaha kumuangalia Revina alipokuwa akiruka Samasoti hewani. Ilitosha kuamini na kutambukuwa walikuwa wanawake wenye uwezo wa kupambana.. Walikuwa wanawake wenye uwezo wakuifanyakazi na Kuimaliza Wenyewe. Lakini hakutaka kumpoteza Hata Mmoja.. Aliwaacha wapambane, aliwaachaa waifanye kazi ile Ya Hatari. Muda Huo yeye akienda kuwaokoa watoto Wa Rais. Akauvuta Mguu wake Wa Kulia, Akaruhusu upige hatua Ya Kwanza, kisha Hatua Ya pili, lakini alipotaka Kupiga Hatua Ya Tatu.. Mlango wa Mbele Yake Ukasukumwa..
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 063

Wakati anataka kupiga hatua ya tatu, mlango wa mbele yake akasukumwa. Kilikuwa kitendo cha sekunde moja mkono wa Mudy kushuka ilipo bastola na sekunde ya pili Bastola ikakohoa. Ikahoa huku watu wanne wakianguka chini. Walikuwa maiti na hawakuwa wakipumua. Mudy akawaacha na kuendelea kusonga mbele. Alikuwa akitembea katika namna ya kivuli, alikuwa akitoka hapa na kuingia pale. Alikuwa akifanya hiki na kufanya kile. Kila sehemu kulisikika milio ya Bunduki, kila Sehemu kulisika mapambano. Mapambano matakatifu kwa sababu ya ukombozi wa Nchi. Kila kitu kilikuwa kikitakiwa kukamilishwa katika Muda ule. Muda ambao ulikuwa mahsusi kuyazima mapinduzi. Revina alikuwa akiutumia Ujuzi wake Wote alioupata katika Kikosi maalum Kilichokuwa kinailinda Ikulu ya Rwanda. Alikuwa Akipiga na kuua.. Hakupenda kuacha mtu hai, hakupenda kuwaona wakipumua. Kila mapigo yake matatu, basi pigo la tano lilikuwa ni kuchinja shingo. Alikuwa akiuburudisha Moyo wake pale alipokuwa akiichezea damu, alikuwa akitabasamu na kujisikia furaha pale alipokuwa akichinja watu. Alipiga mateke na alipiga ngumi. Alitumia Karate na Hata Kung fu. Pale alipokuja kubadilisha Tai Kwond ilikuwa burudani tosha. Yalikuwa mapambano makali kuwahi kutokea. Jenifer na Ummu walikuwa wakipokelezana hili na lile. Kila mmoja alikuwa akionyesha kile ambacho alikuwa nacho. Mudy hakuwa Nyuma, Bado alikuwa akisonga kukitafuta chumba walichofungiwa watoto wa Rais. Chumba ambacho kingempa mwanga wa kujua pale alipo Mheshimiwa Rais. Bado alikuwa akichungulia Huku na Kule. Alipotokea kwenye kaukumbi kadogo ndani ya Jumba lile akashangazwa na Milango kufunguka na Kufunga. Kila alipokuwa akitembea bado milango ilikuwa akifunguka na Kufunga. Akaendelea kutembea kwa Umakini Zaidi. Akitembea huku miguu na mikono ikiwa tayari. Masikio yakinasa kila mlio na Macho kuangalia kwa Hila. Akaifikia nusu ya Ukumbi akiwa bado hajamuona wala kumgundua mtu. Akataka kuipita ile Nusu. Hapo ndipo alishuhudia watu watano wakiingia katika chumba kile. Walikuwa wanaume watano walioshiba. Walikuwa katika vazi la Jeshi, vazi ambalo lilipambwa na Kitu mfano wa Bawa katika Moja ya Sehemu za Vazi lile. Juu walikuwa na Kofia Nyekundu. Walikuwa Makomandoo. Makomandoo Ambao thamani ya comandoo mmoja ni Sawa na Askari wa Kawaida mia tatu. Alama ya Bawa iliyokwenye Mavazi Yao, ilikuwa alama inayotambulisha kiwango cha juu cha Ufaulu wa comando Husika. Ufaulu Ambao ni lazima Umalize Zoezi la Kutupwa Umbali mrefu kutoka angani. tena Ukiwa Ndani Ya Helkopta Huku ukitakiwa utue ardhinI Bila kusaidiwaa na Msaada wa Parachuti. Hilo ndilo funzo la Mwisho katika kuhitimu mafunzo ya ukomandoo.

Pale walipoingia na kutizamana na Mudy, wote walitambuana. Walitambuana kuwa walikuwa wamoja katika fani moja. Fani ya mapambano. Wakaangaliana tena na Tena. Mohamedi akiwalazimisha wamtazame Usoni ili wakisome kile kilichopo ndani yake. Naam kile alichopenda wakione wakakiona. Hapo ndipo mapigano Yalipoanza kila mmoja akitumia Ujuzi wote katika kuzuia na Kushambulia. Yalikuwa mapigano mazito. Haikuwa kazi ndogo kupambana na comando mwenzako aliyeiva. Ndani ya Sekunde kumi na Mbili Mudy Alijikuta akiwa chini akivuja Damu juu Ya Jicho baada ya kupata kipigo mfululizo. Akainuka huku akuiweka Mwili wake kwenye Uimara, akailamba damu yake iliyokuwa ikimvuja Juu Ya Jicho. Punde Mohamed akaonekana akichupa hewani huku akiachia mapigo.

Yalikuwa mapigo mazito, mapigo ambayo alitumia uwezo wake wa ziada. Lakini hayakufanikiwa kufika katika miili au kuwagusa kabisa makomandoo wale. Akajikuta akiisalimia Ardhi kwa mara Ya pili baada ya kupigwa mapigo kadhaa. Mudy Alikuwa chini akigalagala, alikuwa amekutana na watu ambao hawakuwa wepesi kama alivyotarajia. Hapo ndio akauona Umuhimu wa kuirudisha Akili yake katika Mapambano. Akasimama tena kwa Mara Ya pili. Akisoma kila hatua za makomandoo wale, ikisoma kila kitendo kutoka kwa Makomandoo wale. Akasimama vizuri kukabiliana nao. Akaona aubadili Mfumo wake Wa kupigana. Ni hapa makomandoo wale waliposhangaa, ni hapo makomandoo wale walibaki midomo wazi. Huyu alikuwa Mohamed Yule wa MOSSAD, huyu alikuwa Mohamed Wa KGB na huyu alikuwa Yule Mohamed Wa Scotland Yard. Aliinua kwa kujigeuza mfano wa tairi, akajiachia akiwa hewani huku akiachia mapigo.. Mapigo mazito.. Mapigo ambayo kwa mara ya kwanza yaliigusa miili Ya makomandoo, na sio kuwagusa tu, bali yaliweza kuwaangusha Chini. Sasa ukawa muda wa mapambano. Mapambano mazito, mapambano ambayo yalikuwa ni Kufa na Kupona.. Haukupita Muda mlango ukasukumwa, wakaingia Jenifer na Kisha Ummu. Wakakutana na kile ambacho hawakukiamini.. Ummu Hakusubiri, Hakusubiri kuupoteza Muda Kumuangalia Mudy Akipambana. Akaruka kwa Aina zao, aliruka akiutanguliza Mguu mbele.. Kilichofuata Hakikusemekana wala Kuhadithika. Lakini ndani Ya Muda Wa Dakika kumi wale makomandoo Wote Walikuwa Chini. Hawakuupoteza Muda, Wakatoka Mle ndani na Kuendelea Kusonga mbele. Wakati Wakitaka kutokea Upande wa Pili. Wakamuona REVINA AMELALA..
 
Niamini shem kama nimeweza kumchunia siku NNE bila salamu basi tambua hata chini nitamuacha tu. Nasubiri mambo yangu yawe njema nihamie mbali

hongera shem itabaki historia endelea kumkumbuka christina
 
Back
Top Bottom