MKE WA RAIS
SEHEMU YA 054
AKASIKIA YOWE LIKITOKEA NYUMA YAKE. Mudy akageuka bastola ikiwa mkononi.. Macho yake yakatua kwenye mwili wa mtu uliyolala chini ukivuja damu. Mudy hakujiuliza mara mbili wala tatu, akaondoka katika purukushani zile. Aliondoka huku akijua vijana wake walikuwa Nyuma yake. Kitendo cha kuuona mwili wa mtu ukiwa na matundu ya Risasi lilikuwa ni jibu kuwa Yupo mtu, mtu ambaye alikuwa akisafisha masalia. Hakutaka kubaki katika giza.. Alihitaji kumuona Huyo kijana.. Alitaka kufahamu alitoka wapi? Lakini hakumuona, hakumuona kwa kuwa feri haikuwa salama tena. Watu walikuwa wakikimbia hovyo.. Mudy akajiunga kwenye mbio zile, mbio ambazo hakuujua mwisho wake utakuwa upi. Hakujali hilo, bali alihitaji kuliacha eneo lile. Huku mkono wake ukiwa umekamata bastola iliyofichwa na vazi lake, akatoweka katika macho ya watu.. Sasa alikuwa akielekea kule walipo Jenifer na Didas. Alihitaji kushiriki katika kumlinda Rais. Mawazo yake yalikuwa mbali sana huku akili Yake ikichemka katika kufikiria jinsi Ya kumuokoa Rais.
Wa kwanza kufika msibani alikuwa Jenifer.. Miwani myeusi machoni, mavazi meusi Ya heshima na kuonyesha msiba, alikuwa amewahi na kubana upande wa kushoto wa kuingilia.. Upande ambao ulikuwa na uwezo wa kuona kila kiumbe ambacho kinaingia Eneo lile. Macho yake hayakutulia Sehemu Moja.. Alikuwa akitizama kila upabde kwa hila.. Wakati akitizama akawaona watu wawili wakiingia.. Wa mbele aliweza kumtambua lakini wa nyuma hakuwahi kumuona popote. Mbele alitangulia REVINA MICHAEL na nyuma alikuwa akifuatia mwanadada mwingine.. Mwanadada ambaye hakuonyesha Uhatari wa Aina Yoyote.. Bado alikuwa akiwatizama.. Hata Macho Yake yalipokutana na Yale ya Revina akaliona tabasamu. Tabasamu Ambalo halikuwa Rasmi. Lilikuwa tabasam tofauti sana, tabasamu lililobeba maswali lukuki kichwani kwa Jenifer. Hakujua kwa nini alihisi kitu katika kutokana na tabasamu la revina.. Lakini aliona kuna Ujumbe ambao ulifikishwa kwake pasipokuambiwa. Akatulia.. Alitulia kwa muda wa Dakika kama Tano, punde akawaona wanaume wengine wawili wakiingia. Hawa walionekana kuwa ni wageni. Wageni katika jiji la Dar es salaam, na wageni katika nchi Ya Tanzania. Kila mmoja alikuwa katika suti matata, suti ambazo ziliwatoa na kuwafanya wapendeze sana.. Kengele Za hatari zikagonga kichwani mwake. Mwendo wa wanaume wale ulikuwa mwndo ambao aliufahamu.. Aliufahamu kwa kuuona Sehemu. Lakini hakujua aliuona wapi na katika Shughuli gani, alichokumbuka ni kwamba kuna mahali aliwahi kuuona huu mwendo wa watu hawa. Licha ya kutokukumbuka huu mwendo wa watu hawa bado alikuwa akiwatilia mashaka huku akiwatizama wanapoelekea.
Sehemu yote iliwekwa chini ya vijana kutoka Idara Ya Usalama wa Taifa. Kila mgeni aliyeingia alipewa utaratibu wa kukaa na kusubiri ratiba kamili ya Mazishi ya Captain George.
Wakati yote hayo yakiendelea, katika Jumba fulani karibu na sehemu yenye msiba alionekana mwanadada Akiingia. Aliingia kama mgeni wa kawaida.. Aliingia kama mteja, na hata alipoulizia Chumba hakusita kuambiwa kuwa vipo na vilikuwa vikimsubiri. Haukupita Muda mrefu kukamilisha ulipaji na kukabidhiwa Funguo ambazo zingemuwezesha kuingia chumbani kwake. Alipoondoka tu kuzikwea Ngazi Nyuma Yake akafika mtu mwingine.. Huyu alikuwa mwanaume wa makamo.. Alikuwa mwenye uwalaza na mwenye kuonekana na mvi kichwani. Macho yake yalionekana kuwaka yakitizama kila kona ya Jengo lile. Naye akakiulizia Chumba, alipotajiwa akataka kujua kama ni Jirani na mwanamke aliyeingia Muda mfupi Uliyopita.. Akajibiwa kama alivyotarajia kuwa ni karibu na chumba cha mwanadada aliyeingia hivi punde. Akatabasamu, akabeba mzigo wake na kuelekea juu. Alipanda ngazi huku akiwa makini kwa kila kitu, alitegemea chochote kutokea pale..Kuondoka kwa mwanaume Yule kukaleta ukimya... Ukimya ambao ulivunjwa na kuingia kwa mwanaume Mwingine.. Huyu alikuwa ni mwanaume ambaye alioneka kama mcheza Sinema. Suti yake aliovaa ilimpendeza Sana na kutengeneza maswali kwa Watoto wa kike.. Alipoingia tu hakwenda mapokezi kama waliomtangulia, yeye aliongoza moja kwa Moja kuelekea Juu.
Bastola ilikuwa ikichungulia kuwaonyesha watu kuwa huyu alikuwa mtu Hatari. Mtu ambayr hakuwa na Muda wa kucheka.. Akazipanda ngazi kwa Haraka bila kuhisiwa.. Alipomaliza ngazi akapokewa na Ukimya wa Ajabu.. Ukimya ambao ulimfanya mwanaume Yule kuongeza Umakini, Umakini Uliosababisha Achomoe Badstola Yake.. Akaongeza Hatua mbili mbele, akapokewa na Mwili wa Mwanaume Ukielea Katikati Ya dimbwi la DAMU HUKU KISU KIKUBWA KIKIONEKANA KIMEZAMISHWA TUMBONI. utumbo ulikuwa umetoka nje.. Mwanaume Yule hakujishuhulisha na Ule mwili.. Bado alihitaji kumpata Aliyemkusudia, Kumpata akiwa Hai au Mfu.. Hakuwa Mwanaume Mwingine, hakuwa mpiganaji Mwingine.. Huyu Alikuwa Mohamedi... Naam Huyu alikuwa Mudy akiutafuta ushahidi Kwa udi na Uvumba.. Bado Ukimya Ulitawala na Bado Damu ilinukia.. LANINI MOHAMED HAKUOGOPA..