AsanteeeeeMKE WA RAIS
SEHEMU YA 50
Akahisi kitu cha baridi kikimgusa kwenye paji lake la uso.. Ulikuwa mdomo wa bastola. Akasikia sauti nzito ikinguruma kutoka nyuma kwake.. TULIA MPUUZI WEWE..
Mohamedi akatulia, alitulia katika namna ya kumpa nafasi aliyemshikia bastola aamini kuwa Hakukuwa na madhara. Ndicho kilichotokea... Watu wale waliamini hakuwa mtu hatari kwao kwa kule kujilegeza na kutii kwake.. Wakalegeza mikono yao.. Wakajisahau kuwa waliambiwa wasimuamini mtu katika Eneo hilo. Wakasahau kuwa waliambiwa wamshuti kila mtu ambaye atapita eneo lile. Wakamuacha kumpa nafasi, walijua ni mzee asiye na madhara.. Hakuwajua kuwa walikuwa wakicheza na kifo.. Hawakujua kuwa walikuwa wakicheza na mdomo wa Mauti.. Hawakujua kuwa Alikuwa Mohamedi, Mohamedi anayesakwa na kutafutwa na kamati ya mapinduzi.. Wakamuweka sawa kutaka kuhoji kwa nini yuko pale.. Hawakuipata nafasi hiyo, hawakupata muda wa kuwa tayari.. Wote walishangaa walipomuona mzee akipaa hewani mithili Ya chui, mshangao wao hawakuumaliza.. Wakajikuta wote wakipiga mweleka baada ya mapigo kadhaa kutoka kwa Mohamedi Kuwaingia sawia.. Hawakuweza kuamka kwa wakati kila mmoja alikuwa chini akiugulia maumivu.. Maumivu ya pigo moja takatifu kutoka kwa Mohamedi.. Hakuwapata nafasi hiyo.. Bastola yake ikakohoa mara nne.. Kikohozi ambacho kiliondoa roho za watu.. Alipomaliza kazi Hakusubiri washtuke, alichokifanya nikuondoke Eneo la tukio kwa kupitia njia ambazo Zisingekuwa Rahisi kugundulika. Akatokomea Mtaani huku akiwa na furaha ya kugundua nani alikuwa nani Nyuma ya Mauaji ya mke Wa Rais na Mpango wa kufanya mapinduzi..
Kwa mara ya kwanza alikuwa amepiga hatua kubwa sana.. Akatabasamu na kucheka kisha kutoweka kabisa tayari kwa maandalizi ya kazi Ya kufa na kupona.
******
wakati Mohamedi akipambana huku, Jenifer na kijana kutoka makao makuu DIDAS RUGIMBANA walikuwa katika mitaa ya jiji la Arusha wakiitafuta Nyumba yenye namba ambazo walipewa na Kepteni George kabla ya Kuuawa. Walikuwa wakitembea huku na huko kama wafanyavyo wapenzi.. Walikuwa wakishikana viuno na wakati mwingine hata kushikana mikono na kubusiana. Kila aliyewaona ama kukutana nao alihisi ni wapenzi.. Wapenzi ambao wanapendana sana. Licha ya kile ambacho walikuwa wakikifanya, lakini bado macho Yao hayakuchoka kutizama kila Jengo lililopo mbele yao.. Wakiwa umbali mfupi kutoka Ulipo ukumbi wa Triple A macho Yao yakakiona kitu ambacho walikuwa wakikitafuta. Ilikuwa Nyumba yenye namba husika. Lilikuwa jumba kubwa sana, jumba ambalo lilizungushiwa ukuta mkubwa ulionakshiwa na Marumaru zenye mfano wa Madini Ya Tanzanite. Ukiondoa hilo, jumba lote lilikuwa limepandwa miti mirefu ambayo ilisababisha uwepo wa Giza Nje ya Jumba lile na ndani Yake.
Nje hapakuonekana na mlinzi au walinzi wa aina yoyote.. Sehemu yote ilikuwa kimya kupindukia. Sehemu yote hapakuonyesha dalili ya kuwepo kwa watu na hata kuishi kwa watu sehemu ile. Jenifer na Rugimbana wakaendelea kuliangalia jumba lile kwa namna ya kutokuwa na Hofu huku wakati Mwingine wakiendelea kukifanya kile walichokuwa wanakifanya ili kuwapoteza Maboya watu ambao wangewahisi ama kuwashtukia. Wakiwa wamelipita jumba lile wakiendelea na safari Yao, mara waKayaona magari Mawili yakitoka katika Jumba lile na kuwapita kwa Mwendo wa kasi Huku ndani Yake wakionekana Watu kibao ambao kwa kuwaangalia tu mavazi Yao, ungejua tu wale ni Special Force.. Lakini Kwa nini wametoka katika jumba lile? Wanahusika vipi na Jumba Hili? Ni mawazo Yaliyopita katika vichwa vyao na kusababisha kupatwa na Hamu kubwa ya kukijua kile ambacho George alikiona mpaka kufikia kuwatuma Wao... Jenifer Akamuangalia Rugimbana kwa Mara Moja, Rugimbana naye Akafanya Hivyo.. Punde kila Mmoja akaingia Upande wake.. Wote walikuwa wakirudi katika jumba lile... Jumba ambalo lilionyesha kuwa na Siri kubwa. Kila mmoja alikuwa ameishikilia bastola yake Mkononi.. Wakati Jenifer akinyata kuelekea kwenye Uzio Wa Jumba lile, kwa mbali Macho yake yakawaona watu wawili wakiwa wamelala Chini.
Ulalaji wao haukuonyesha uhai kabisa.. Akawasogelea watu wale kwa tahadhali Kubwa.. Alipowafikia alishangaa akiwaona wakivuja damu huku wakiwa na matundu Ya Risasi vichwani mwao.. Jenifer akainama na kuugusa mwili wa Marehemu mmoja.. Akaukuta mwili ukiwa Wa Moto Kuonyesha kuwa Muuaji hakuwa mbali na Sehemu Ile. Akaongeza Umakini na kuzidi kutambaa kuelekea kule.. Hatua kumi mbele alikutana na Maiti Wengine wawili.. Hawa walionekana kuvunjwa Shingo. Hisia kuwa Mohamed ndio aliyeifanya kazi ile Zikaanza kumjia Jenifer.. Aliutambua Uuaji wa Mohamed.. Lakini hakuwa na uhakika wa hilo. Akaongeza Umakini huku akiendelea kutembea Nyuma ya Uzia Wa lile Jumba. Mbele kidogo akamuona mtu.. Mtu ambaye alimfahamu sana... Mtu ambaye alikuwa akiuruka ukuta wa jumba Lile.. Ukuta ambao ulionekana kuwa na Nyaya Nyingi na Hatari Sana Za Umeme.. Hakuwa Mwingine Bali alikuwa Mohamedi.. Tabasamu likachanua Usoni kwa Jenifer hasa pale aliposhuhudia maiti Nyingi Zikiwa Zimelaliana..
MuendelezoMKE WA RAIS
SEHEMU YA 51
Miili ya watu ilikuwa imetambarajika kuonyesha kuwa Mohamed alikuwa akikifanya kile ambacho hakukitegemea. Akatabasamu.. Kila hatua moja aliyopiga alikuwa akikutana na Maiti.. Punde akamuana Rugimbana akichupa kuingia ndani ya jengo lile. Ulikuwa ni uchupaji uliyompa Burudani katika macho Yake. Alipenda kuitazama michezo kama ile.. Alipenda kuona watu wakicheza michezo Ya Hatari kama mfano ule.. Hakuchelewa katika kujiunga ndani ya Jengo.. Hakutaka kutafuniwa na wenzake.. Akaudandia mti ulio pembeni mwa jumba lile mfano wa Nyani ama ngedere.. Muda mfupi alikuwa akitua ndani bila kutoa kishindo.. Akajivingirisha na kutulia kwanza. Macho yake yaliendelea kutizama Burudani, Burudani kutoka kwa Mudi na Rugimbana.. Walikuwa wakifanya kile ambacho kilitoa burudani kutizama.. Mudy alikuwa katika aina ya mapigo ambayo hakuwahi kuyaona kabla.. Wote walikuwa wakitembea na mapigo ya Martial Kombart.. Walikuwa wakinesa na kuinuka.. Walikuwa wakiruka sarakasi na kuua... Hakutaka kuangalia kile alichokuwa akikishuhudia..
Akainuka kwa Mwendo usio na mlio wala mchakato wa majani. Akazunguka mpaka upande wa kusini mwa Jumba lile.. Akiwa hapo akashuhudia watu wawili wakitoka ndani huku wakionekana lolote linalotokea katika Jumba lile. Akautumia mwanya huo kutambaa na vivuli vya miti mpaka alipowafikia karibu.. Bado hakuwa ameonekana kwa watu wale na bado hawakuwa wameshtuka kwa lolote. Jenifer akajinyonga mfano wa Nyoka.. Sekunde mbili alikuwa amechupa na kusimama katikati Yao.. Walinzi wote wakashtuka na kuhamaki.. Jenifer hakuwapa nafasi ya kujiandaa.. Mateke matatu ya hewani yalitosha kuwanyamazisha walinzi wale. Akaokota Bunduki zao, mbili akaziweka begani na Moja aliikamatia mikononi. Akaanza kusonga kuingia ndani Ya Jumba lile.. Jumba ambalo lilikuwa kubwa na lenye giza la kutosha.. Akaufikia mlango na kuusukuma.. Akaruka kuingia ndani.. Kuingia kwake kulifuatiea na milio ya Risasi kuelekea kule alipo.. Akachupa kwa haraka na kuangukia pembani kabisa.. Bada watu wale waliendelea kufyatua risasi pasipo na mpangilio.
Bado Jenifer aliendelea kutulia,, kutulia huku akiwasoma watu wale wanapotokea.. Punde akasikia mayowe na sekunde Nyingine ukimya wa Ajabu Ukatawala Eneo lote. Jenifer bado aliendelea kutulia kuangalia kinachoendelea.. Mara akashangaa kuona taa Za jumba lile Zikiwaka.. Akapeleka macho Yake kwa Haraka kule kulipokuwa kunatokea Milio ya Risasi. Macho Yake yakamuona Rugimbana lakini kilichomburudisha Zaidi ni kuwaona watu watano wakiwa wamelaliana Jini wakivuja Damu.. Jenifer Akainuka na Kujitokeza. Walipotizamana na kugunduana kila mmoja alionyesha kidole gumba kuonyesha mambo yako sawa.. Muda mfupi baadae Mudy naye akafika na kuungana na wenzake. Hakujua kama Jenifer alikuwa pale, walipoonana wakakumbatiana na walipoachiana wote kwa pamoja wakagawana kuangalia kila kitu katika Jumba lile. Ulikuwa ni Uchunguzi uliochukua Muda mfupi sana kutokana na kugundua uwepo wa ghala la silaha katika mahandaki ambayo yalichimbwa ndani Ya Jumba lile.. Kulikuwa na Silaha Nyingi na mabomu makubwa makubwa.. Kulikuwa na ndege za Kirusi aina Ya Rocket Rangers, kulikuwa na ndege za mashambulizi za B52.. Pia kulikuwa na Bunduki Za kila aina, kuanzia Rifle, Rpg, Ak 47, SmG na Bunduki Nyingine nyingi nyingi..
Kila Mmoja wao hakuwa anakiamini kile ambacho alikuwa akikishuhudia.. Kilikuwa kitu ambacho huwezi kukidhania kuandaliwa na watanzania Wenyewe.. Uroho Wa Madaraka wa Baadhi Ya Viongozi ulitaka kulipeleka Taifa katika Taharuki. Taharuki ambayo ingeharibu sifa ya Nchi hii. Kwa nini walitaka kufanya mapinduzi, kwa nini Walithubutu kumuua Mke Wa Rasi? Ni nani yupo Nyuma Ya Hili ukimuondoa Waziri Mkuu? Je mke Wa Rais Alikuwa mmoja Wao? Na kama ni ndio kwanini aliuawa mwanzo kabisa? Au walitaka kumtumia kupata baadhi Ya vitu kisha watekeleze Mauaji Juu Yake? Hapana ni lazima tulijue hili, ni lazima tulifichue kwa Uwezo wetu.. Hata kama ni kufa nipo Tayari Kufa. Alikuwa akiwaza Mohamed Huku akiangalia Silaha Zale... Wote walikuwa wakisubiri Neno kwa Mudy Ili wajue kipi cha kufanya.
Mohamed hakuongea kitu kama Walivyotarajia.. Wakashuhudia Akichomoa bomu moja kutoka kwenye Hadhina ya Mabomo.. Akalifungua kwa kutoa Ufunguo wake kisha kuliseti katika Dakika Walizojua Wanaweza kutumia mpaka kufika nje, Kisha Wao wakatoka kwa haraka kutoka Eneo hilo kuelekea mahali walipoliacha gari lao Kwa Safari Ya Kurudi Dar Es Salaam ndani Ya Usiku Huo. Walitaka kuacha vilio vya kusaga meno kutoka kwa Viongozi wale.. Wote wakafanikiwa kutoka katika Jumba lile.. Wakaingia katika Chochoro moja baada Ya Nyingine walipokuja kusimama Walikuwa wamefika karibu na Walipoiacha Gari Yao. Lakini hawakuifikia na hawakuipanda.. Wakashuhudia Mlipuko mkubwa ukiisambaratisha Gari Yao.. Wote Wakachupa na Kuangukia upande mwingine.. Sekunde tano Baadae mlipuko mwingine Mkubwa Zaidi Ukasikika.. Jiji la Arusha lilikuwa katika Hali ambayo Haikutazamika.. Moto Mkubwa Ulikuwa Umetanda Angani.. Hawakuchelewa, Ilikuwa ni lazima waondoke pale.
NzuriMKE WA RAIS

Hahahaha sure inaboaKama kuna watu wanaoniudhi humu ni wanaocopy kisa kizima halafu ndo wacoment. Naudhikaaaaaaaaaaaaa
Sawa Mkuu sasa ngoja nianze kuisomaHii itaisha mkuu kwa kuwa naimiliki mwenyewe
Inaitwaje?