Riwaya: Mke wa Rais

Riwaya: Mke wa Rais

MKE WA RAIS

SEHEMU YA 064

Revina alikuwa Chini akivuja damu kifuani. Alionekana akiwa ametulia. Akiwa ameigeuza shingo Yake. Macho yake yalionekana kama yanayoangalia, lakini hayakuwa na Uhai tena. Kifua chake kilikuwa kimejaa Matundu Ya Risasi. Revina alikuwa amekufa. Amekufa huku akiipigania Nchi ambayo sio yake. Akimpigania Rais ambaye sio wa nchi yake. Wote wakachoka. Mudy ndio aliyechoka Zaidi. Kwa Muda wa sekunde kumi aliendelea kuuangalia mwili wa Revina pale Chini. Mikono ikamlegea.. Akaliona chozi likishuka taratibu. Wote wakaingiwa na Simanzi na Majonzi. Wote wakasimama kwa heshima mbele ya mwili wa Revina. Ummu Sammy akatoa Heshima Ya Kijeshi. Mudy akauinamia mwili wa Revina. Alimuangalia kwa Muda mrefu bila kuongea kitu, bila kuongea chochote. Matundu sita ya Risasi yalikuwa yamekichakaza kifua chake. ''Tangulia Revina, Msalimie George.. Nakuahidi aliyehusika na kifo chako atafuata Nyuma yako muda mfupi ujao.'' alitamka hayo huku akiyafumba macho Ya Revina. Moyo Ulimuuma sana Mohamedi. Akasimama na kuuruka mwili wa Revina. Bastola mbili zilikuwa mikononi mwake. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kikomandoo. Alikuwa akinesa mithiri ya Wapiganaji wa Banyamulenge. Pembeni Yake alikuwepo Ummu Sammy na Kushoto kwake alikuwepo Jenifer. Kila mmoja alikuwa na Silaha Zake. Ummu Akiwa na Ak 47 Jenifer Alikuwa Ameshikilia Sub Machine Gun. Kila mmoja alikuwa akitembea hatua kwa hatua. Mudy alipogeuka wao walishageuka kitambo. Alipopiga hatua wao walikuwa mbele. Kila mmoja macho Yalimuiva kwa hasira Na Uchungu.

Walipotokea Upande mwingine wa Jengo lile. Wote wakajigawa kila mmoja akienda upande wake. Mudy akikitafuta chumba alichofungiwa Rais, Ummu na Jenifer walikuwa upande ambao walihisi ndipo walipo watoto wa Rais. Wakaingia ndani kila mmoja akiwa makini na kila kitu. Kila mchakato au kishindo walikichukulia kwa Umakini. Hawakutaka kupuuza kila kile wanachokisikia. Kila Mmoja alikuwa jicho la mwenzake. Walilindana katika kutembea na hata pale walipokuwa wakigeuza shingo zao. Kila waliposikia chakachaka haraka sana Midomo Ya bunduki zao ilielekezwa Huko. Miili yao ilikuwa huru, miguu yao ilikuwa tayari kwa kurusha mateke. Wakauona mlango kwa mbele yao, mlango ambao ulitengenezwa kwa Vioo. Wakatembea huku kengele za Hatari Zikigonga katika Vichwa vyao. Walipoukaribia mlango likatokea tukio la Kuburudisha. Wanaume watatu waliovaa mavazi Ya kininja wakatokea pale pale kwenye mlango.. Walitokea bila mlango kufunguliwa.. Ilikuwa tukio la Ghafla ambalo Ummu na Jenifer Hawakulitegemea. Tukio ambalo liliwapa ugumu wa kutumia Bunduki walizonazo. Staili ya maninja iliwafanya washindwe kufanya lolote. Maninja walikuwa wakiruka kama Nyani na Hata ngedere.. Walikuwa wakitembea kwenye kingo za Jumba kile. Hakikuwa kitu kipya kwa wasichana hawa lakini waliujua mziki wa kimapigano kutoka kwa Ninja. Muda mfupi Ummu na Jenifer Walikuwa wapo chini. Wapo chini wakiwa peke yao. Wale ninja Walikuwa wamepotea katika Mazingira Tatanisha. Ummu akachupa na Kusimama. Jenifer Alibaki Chini, hakubaki chini kwa kuwa amechoka, bali alibaki chini kuwasoma Ninja wale. Punde wakatokea tena wakiwa katika Aina tofauti. Hapo ndipo Ummu Alipokumbuka mafunzo Yake kule Nchini China. Alikumbuka Mafunzo Yake Ya Kishaolin Ninja.. Akaikumbuka Sauti ya Mwalimu Wake Yule. Aliikumbuka sauti Ya Master Wake aliyejulikana kwa Jina La Wan Kwan Hang.. Akalikumbuka jumba la MASHAOLIN wote.. Hapo akasimama kwa Mguu Mmoja Akiitanguliza Mikono. Punde alishuhudia kumuona Jenifer Akiwa Hewani, Hakuwa hewani hivi hivi. Alikuwa Akiachia mapigo ya Kininja. Yalikuwa mapigano yaliovutia, yalikuwa mapambano Ya ufundi. Watu Watano wenye mafunzo Ya kininja walikuwa wakipambana. Wakipambana katika kutia Raha. Haikuwachukua muda maninja wale walikuwa chali wakiwa maiti. Ummu na Jenifer Wakaendelea Kusonga mbele.

Wakati Jenifer na Ummu wakifanya kweli Upande Wa Nyuma ya Jengo. Mudy alikuwa ameshaingia katika Chumba ambacho kilionyesha kuwepo kwa Watu Muda Mfupi Uliyopita. Kilikuwa Chumba kipana na kikubwa. Chumba ambacho kilijaa baadhi ya Vitu vya mawasiliano Kuonyesha kuwa ndicho chumba kilichoandalia kwa matumizi Ya Rais kulitangazia Taifa. Mohamedi alitembea Huku macho yake yakitembea mle ndani kwa umakini wa Hali ya Juu. Yalikuwa yakiangalia kila sehemu na kila kitu mle ndani Ya Chumba. Akiwa hana hili wa lile mlango ukafunguliwa kwa kasi kisha Mvua Ya Risasi Ikaanza kumiminwa kuelekea kwake. Mohamedi akachupa na kuangukia Nyuma Ya kochi kubwa huku Bastola Mkononi mwake. Bado Risasi Zikaendelea Kurushwa, bado Risasi Zilikuwa Zikimiminwa kama Matone Ya Mvua. Mudy akaendelea kutulia, kutulia huku akipanga kitu gani cha Kufanya. Muda ukazidi kwenda Huku Mvua ya Risasi Zikimuandama. Haikupita muda Kitu kingine kikatokea, kitu ambacho kilikuwa kitisho katika Uso Wa Mohamed.

Machoni mwake alitokea mwanamke katika mtindo uliomsisimua. Mtindo ambao ulitumiwa sana na ninja. Kutokea kwake Kulifuatiwa na tukio la kukatwa vichwa kwa Watu Wote pale chumbani. HALI TETE
 
MKE WA RAIS

SEHEMU YA 65

HALI ILIKUWA TETE!
akairuhusu mikono yake kushuka chini alipohifadhi bastola yake. Akauruhusu mkono wake kuichomoa bastola ile kwa wepesi wa ajabu. Ikaikamata mkononi, akiangalia kilichokuwa kikitokea. Alikuwa akishangaa mwanadada yule alivyokuwa akichinja na kukata vichwa. Aliushangaa wepesi wa mtu huyu, akaushangaa urukaji wake. Alikuwa akiruka huku upanga umetangulizwa mbele. Kila alipokuwa akiruka upanga ulikuwa akiifacha kazi nzuri. Hatimaye mwanamke yule akatua mbele ya Mohamedi. Kutua kwake kulifuatiwa na mtazamano wa sekunde Zisizozidi tano. Alikuwa akimuangalia Mohamedi Kwa Jicho lenye maswali. Bado Mudy aliduwaa bastola mkononi, bado aliduwaa kutokana na kutokea kile ambacho hakukiamini. Mwanamke aliyekuwa akiuwa kumbe Alikuwa Ummu Sammy. Hilo ndilo lililomfanya Mohamedi kuduwaa. Alimfahamu sana Ummu lakini hakumfahamu katika aina ile ya kininja. Aina ya Ninja mpambanaji. Tabasamu likachanua kwenye nyuso Zao. Wakajiondoa na kuelekea upande mwingine. Kila chumba walichokuwa wakiingia Kumuangalia Rais, Bado hawakuwa wakimuona. Wote wakajigawa kwa mara nyingine. Jengo zima likatawaliwa na milio ya risasi.

Hawakumuacha kila aliyejitokeza mbele yao. Kila mmoja alikuwa akipambana kuhakikisha nchi inarudi kwenye mikono ya Rais aliyemadarakani. Wakauvuka uzio unaotenganisha majengo yale, bado hawakumuacha mtu, bado hawakumuacha yoyote yule. Kuuvuka uzio unaotenganisha jengo lile, kukawafanya watokee sehemu yenye milango mingi. Mohamed akamrudisha Ummu Nyuma, Kisha Yeye kutangulia mbele. Hakuwa akiogopa na hakuwa akihofia. Akauendea mlango mmoja na kujaribu kuufungua lakini ulikuwa mgumu. Hakutaka kutumia risasi wala funguo malaya Alizonazo. Alichokifanya ni Kurudi nyuma na Kuruka kwa Miguu yake miwili na kutua kwenye mlango. Mlango haukuwa na jinsi. Akasalimu amri. Mohamed akaangukia kwa ndani akifuatiwa na Ummu. Baada ya kuingia kwenye Chumba kile walitambaa mpaka nyuma ya mbao zilikuwa chumbani mle. Wakatulia huku wakiangalia kule na Huku. Lakini hawakuambulia kukiona chochote. Wakatulia huku kila mmoja akiwa makini na tayari kwa lolote. Muda ulizidi kuyoyoma huku ukimya ukitawala. Wakaendelea kuuvuta muda lakini hawakuona chochote isipokuwa ukimya tu. Zikapita kama dakika kumi na Tano bila kutokea chochote. Wakiwa wanakaribia kujiondoa pale, wakasikia mlio kama wa nyayo za binadamu zikisogea karibu yao.
Wakatizamana kisha kupeana Ishara. Punde wakashangaa kuiona sehemu yenye ukuta ikifunguka kisha wasichana watatu waliovalia mavazi Ya kijeshi wakatokea. Walikuwa wasichana warembo lakini wakakamavu. Hawakufanana na wanajeshi wa Tanzania. Hawa walionekana ni wanajeshi kutoka nchini Rwanda. Mohamed na Ummu hawakutaka kusubiri. Wakatokea Mbele yao mfano wa Vivuli. Kinyume na walivyotarajia kuwa, Wale madada watashtuka baada ya kuwaona. Haikuwa Hivyo. Sura zao zilibaki kwenye uzuri wao ule ule. Hawakuonyesha kubabaika wala kufanyakitu chochote. Wote wakawatolea macho Mohamedi na Ummu. Waliwatazama kanakwamba wanatizama kinyeshi. Hawakuionyesha Hofu kabisa Machoni mwao. Hili likamshtua Mohamedi. Likamshtua kwa aina tatu tofauti. Kwanza ni Kule kujiamini kwao.
Pili, nikule kuwaangalia kwa kuwadhihaki na chatatu ni kule kuendelea kuongea kwa Lugha Yao bila kujali wapo sehemu gani na Wapo na watu gani.

Tabasamu la kebehi lilizipamba nyuso Zao. Wakata kuwapita wakina Mudy ili waendelee na Safari yao. Hapo ndipo kulichotokea kile ambacho hakikutarajiwa. Walipotaka kupita Mohamed alisogea pembeni kutoa Nafasi kwao. Lakini ni wakati wakiukaribia usawa wa aliposimama Mohamed na Ummu Sammy, mikono mypesi ya wasichana wale ikazama katika mifuko ya Magwanda Yao. Lakini ikaishia kuzama tu, haikuweza kutoka tena, haikuweza kupewa nafasi kutoka na chochote kile. Haikuruhusiwa hata kucheza. Muda ule ule Mohamedi alikuwa hewani Sambamba na Ummu. Kila Mmoja akaachia mapigo matatu mazito. Mapigo ambayo yalishindwa kuzuiwa na Wasichana wale. Wote wakayumba nusura ya kuanguka. Hawakupewa muda wa kusimama Sawa. Mudy na Ummu wakawaendea kwa mitindo tofauti. Wasichana wale wakakaa imara na kuanza kujibu mashambulizi. Yalikuwa mapambano makali sana, mapambano yalioumaliza ufundi wote. Wasichana wale walionyesha kuhimili kila aina ya mapigo. Kila pigo walikuwa wakijibu. Kila pigo walikuwa wakijaribu kuzuia na kushambulia. Lakini mwisho hawakuweza tena kuhimili, kuhimili mapigo, mapigo ambayo yalipigwa kwa Ufundi, utaalam na hata uzoefu. Walishindwa kuzuia staili za Ninja kutoka kwa Ummu. Wote wakaregea na kutambarajika. Damu zilikuwa zikiwavuja, sura zao na Urembo wao ulikuwa Umepotea kwa Sababu ya kipigo. Kila Mmoja alionekana kama amekanyagwa na kusagwa na Mashine. Hawakutaka kuwaua, bali walitaka kuwatumia kujua Wapi alipofungiwa rais. Lakini hawakuambulia kitu, kwani walipotaka kuanza kuwahoji Wakashangaa Kuwaona mateka Wao Wakiwa wamepoa Huku macho yao yakiwa Yametoka. Ndipo walipowagusa kuangalia kilichotokea: WAKASHANGAA KUKUTA WOTE NI MAITI KILA MMOJA AKITOKA MAPOVU MDOMONI
 
Back
Top Bottom