MKE WA RAIS
SEHEMU YA 58
Akayaacha macho yake yamshuhudie Mohamedi akiondoka. Akiondoka katika namna ya kuvutia machoni mwa watu.. Alikuwa akitembea kana kwamba hakukuwa na lolote lililotokea. Akashuhudia Mohamedi akipotea machoni mwake mfano wa kivuli ama karatasi iliyopeperushwa na Baridi. Ummu akatabasamu huku akitamani kama angekuwa na Mohamedi.. Bado alijiona yupo gizani katika kile ambacho kilikuwa kikiendelea kutokea, alikuwa mgeni katika kutambua na kulijua jukumu lililobebwa na Mohamedi. Akasahau kwamba yupo kazini, alisahau kuwa anatakiwa kuripoti makao makuu kuhusu tukio la kuuawa kwa bosi wao. Lakini alionekana kutabasamu kila alipokuwa akimkumbuka Mohamedi, alikuwa akiyakumbuka mapigo yake. Alikuwa ni kama kichaa aliyepekee mbele ya Jumba la Waziri..
Baada ya kutoka katika jumba la waziri wa mambo ya Ndani, Mohamefi alikuwa njiani akielekea nyumbani kwa Waziri Wa katiba na Sheria bibie CeCilia Bruno Peter. Bado alikuwa akiwaza na kujiuliza juu ya mtu aliyefanya mauaji nyumbani kwa Waziri. Kitendo cha Waziri kuuawa akiwa na familia yake tena walinzi wakiwepo. Kulimpa picha kuwa kazi Ile Ilifanywa na mtu mmoja, mtu ambaye nu mtaalamu wa kazi Ya mauaji.
Kukuta vitu vikiwa vimesambaa huku na huko kulionyesha kuwepo kwa mapambano makali kabla ya mauaji yenyewe. Pia kulionyesha ni jinsi gani watu hao walivyokuwa wakikitafuta kitu, kitu ambacho kilionekana kutopatikana. Purukushani aliyoiona kwenye jumba la Waziri ilikuwa purukushani iliyomvutia kupita kiasi. Alitamani kuwapata watu hao, alitamani kuimaliza kazi mapema sana. Akaendelea kutembea kwa kupitia njia za mkato, alipoufikia Uzio Uliotenganisha jumba la Waziri wa katiba na Jumba la mtu mwingine. Mohamedi alishuhudia gari Ndogo Aina Ya Vitz ikiondoka kwa mwendo wa kazi huku nyuma akitokea mwanamke ambaye alionekana kuvuja damu kuonyesha kuwa alikuwa amepigwa Risasi. Mwanamke Yule alikuwa akiifuatilia ile gari kuonyesha kuwa kulikuwa na uvamivi kutoka ndani Ya Jumba la Mheshimiwa Waziri. Wakati Mudy akiendelea kuliangalia lile tukio, akashuhudia watu wengine wakitokea Nyuma ya Yule mwanamke. Hawa walikuwa wauaji haswa, hawa walionekana ni watu wasio na Huruma. Wote walikuwa na Bastola mkononi.. Wote walikuwa wakifanana na Wote walikuwa wakitembea mwendo mmoja.. Sekunde Ya kwanza Mohamedi alikuwa akiwaona wakitoka Ndani, na Sekunde Ya pili akauona Ubongo wa Yule mama Ukiruka Angani baada Ya kufumuliwa na risasi ya bastola Aina Ya Revolver colt 43.. Mama akarushwa juu na kwenda kuangukia umbali kidogo kutoka pale alipo. Kila kitu kilikuwa kikifanyika Huku Mohamedi akiangalia.. Alikuwa akiona kile ambacho kilikuwa kikifanyika mchana kweupe.. Hakuiona Sababu Ya kuendelea kujibanza.. Alihitaji kuwajua watu hawa, watu ambao walikuwa wakimuua waziri mchana kweupe.. Hakutaka kufikieia sana, Hakutaka kusubiri watoweke Machoni mwake na pia hakutaka kuitumia bastola kufanya chochote kile, alitaka kuwaonyesha kwamba hata Yeye ni Mpiganaji, Mpiganaji aliyeaminiwa na Rais. Akauparamia Ukuta mithiri ya Ninja.. Akatua kama Unyoya wa Kuku bila kutoa kishindo. Akatembea kama Upepo bila kuonekana.. Akawazunguka kwa Utembeaji wa kishaolin, Mfupo baadae alikuwa amesimama Mbele Yao, mbele ya Watu wale wawili. Watu ambao hawakuuficha mshtuko wao baada ya kumuona Mudy akiwa amesimama Mbele yao. Ulikuwa kama muujiza kwa kuwa muda mfupi walikuwa wakijitanua wenyewe lakini sekunde ya pili wakashangaa kumuona mtu.. Mtu ambaye alikuwa amekamatia bastola mkononi, Bastola ambayo ingekuwa na Uwezo Wa Kuwamaliza hata kabla ya kufika pale. Kwa nini hakuwaua? Kwa nini aliamua kujitokeza kuonyesha kuwa hana wasiwasi? Huyu ni nani na kwa nini Yupo hapa? Hawakumaliza kile walichokuwa wakijiuliza pale mapigo mawili ya Mohamedi Yalipowatupa chini.. Wakati wanachupa na kusimama ili kukabiliana na Mohamedi, wakashangaa kuliona geti likusukumwa.. Wakaingia wasichana wawili warembo, wasichana walioingia mithiri Ya makomandoo.. Alikuwa Jenifer na Revina. Watu wale wakageuka kutizama Kule getini, wakasahau kuwa Mohamed alikuwa mbele Yao.. Akawashtua kwa mapigo matatu Ya Kung fu, mapigo ambayo Yaliwaingia na kuwawika Sawa.. Hawakuwa wataalam wa mapigano kama Mudy alivyodhania.. Walikuwa waoga kupindukia, walikuwa hawana lolote katika nyanja za kimapigano.. Ndani ya Sekunde kumi wote walikuwa Chini Wakitweta. Walikuwa wakitweta kama Majogoo.. Wakatiwa Pingu na kuinuliwa kutolewa katika jumba lile.. Wakati Watu wale Wakitolewa Nje, Mohamedi pamoja na Jenifer wakaingia ndani ya jumba lile. Kuufungua mlango tu Wa Kuingilia Ndani Macho Yao Yakapokewa na mwili wa mtu Ukiwa umelala Chali katikati ya Dimbwi la Damu. Mwili ambao ulikuwa Umezungukwa na Makaratasi mengi sana.. Wote wakaaangaliana kisha kupiga hatua kuufuata Mwili wa mtu Yule. Walipoufikia Wote Wakapigwa na Butwaa Wasiamini kile wanachokiona.. Mwili uliokuwa Umelala Chini Ulikuwa Mwili Wa WAZIRI MKUU WA NCHI ukiwa na matundu mengi Ya RISASI.. WOTE WAKACHOKA