Riwaya-duka la roho

Riwaya-duka la roho

mkuu kuwa mpole niliahidi utapata mpaka mwisho na pia kumbuka kila mtu ana majukumu kaka so ukiona sijaweka on time jua nimetingwa na ninajitahd sana kutoa update
Nakumbuka niliandika kuhusu hili kuwa litatokea sasa nafurahi kauli yangu haijaanguka chini ila nakupongeza kujibu kistaarabu.
 
wadau sikuwa online ndo nimeingia sahv ngoja niwape kitu roho inapenda
 
RIWAYA; DUKA LA ROHO
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
"Ni Mwanza hii Lobo. Tuanzie kazi hapa au twende tukaanzie Dar es Salaam." Gunner alimuuliza John Lobo ambaye muda mwingi alikuwa akiutumia kutazama maajabu ya jiji lile tajiri kwa mawe.
"Hapahapa ndipo pa kuwapa taarifa wale wajinga. Lazima wajue kuwa Duka La Roho limerudi kuuza na kununua tu!" Lobo alijibu huku uso wake ukionesha chuki isiyo na kifani.
"Watakaa tu." Gunner akampa tano Lobo na wote wakashuka toka katika gari lao na kuwaamuru na wale wanawake washuke kwa sababu walikuwa wamefika katika hoteli moja kubwa na ya kisasa iliyopo Jijini Mwanza.
"Tuna vitendea kazi vyetu." Mrembo mmoja kati ya wale watano aliongea kwa shida lugha ya Kiingereza.
"Njoeni navyo vyote huku ndani." Gunner akawajibu na yeye akiwa na Lobo wakaenda mapokezi ya hoteli ile.
"Vyumba vitatu vinavyokaribiana na viwe vya juu." Gunner aliongea na mhudumu wa mapokezi baada ya kuulizwa aina ya vyumba anavyovihitaji.
"Hizi hapa funguo kaka." Mhudumu akampa kadi maalumu ambazo zinafungua milango waliyokuwa wamepangiwa. Baada ya kukabidhiwa funguo, Gunner na Lobo wakalipia vyumba vyote kwa siku tatu.
Baada ya malipo, wanawake wale watano waliingia wakiwa na mabegi makubwa mawili kila mmoja. Muhudumu alishikwa na butwaa lakini hakuuliza kwa sababu wateja wake tayari walishafanya malipo muhimu.
Gunner na Lobo wakasaidia mabegi baadhi na kuelekea ilipo lift ya kuwapeleka juu ya hoteli ambako kulikuwa na vyumba vyao.
"Wawili ufunguo huu, na watatu ufunguo huu. Mkisha jipanga, njoeni chumba hichi. Kuna kazi ya kufanya kesho asubuhi." Gunner alitoa maelezo huku akiwakabidhi wanawake wale funguo maalumu za kufungulia milango yao. Wakaingia vyumbani na kujifungia huko kwa muda mrefu wakipanga kwa hili na lile.
*****
KITUO KIKUU CHA POLISI MWANZA.
Wanawake watano waliyovalia suruali za jinzi pamoja na fulana nyekundu na nyeusi zilizoandikwa DUKA LA ROHO halafu kwa chini kuna mchoro wa mzani. Upande mmoja wa mzani kuna bunduki kubwa, na upande mwingine kuna mkono umekamata moyo na kuutumbukiza kwenye sahani ya maalumu ya mzani ule. Yaani bunduki, inapimana uzito na moyo wa binadamu, sijui kipi kitashinda mwenzake uzito.
Wanawake wale hawakuziba nyuso zao na watatu kati yao, mikononi mwao walikamata bunduki hatari za kivita. Huku wawili wakiwa wameshikilia kamera za kuchukulia stili picha (video) na wakionesha wapo makini na kazi yao.
"Tanzania." Mwanadada mmoja aliita kwa sauti ya kithilani baada ya kamera kuelekezewa kwake. "You have two days to give us Frank Masai and his crew. Only two days you got. If nothing happen, Duka La Roho is comes to take what's mine.(Mna siku mbili za kutupa Frank Masai na kundi lake. Siku mbili tu! Kama hamna kitakachotokea, Duka La Roho litachukua kilicho chake)" Maneno hayo yakaongozwa na risasi tatu zilizowapata askari polisi wawili na kuwamaliza palepale.
"Tick Tock." Dada mwingine alimaliza maongezi yale na mjadala ukafungwa hapo. Wakatoka nje ambapo walichukua gari fulani walilolikodi pale hotelini, na kwa fujo wakaondoka kuelekea walipopanga kukutana na wakina Gunner.
****
"Sasa hao askari wamefanya nini?" Lilikuwa ni swali la Masai baada ya kuangalia tukio zima lililotokea Mwanza asubuhi ile.
"Nadhani ni ujumbe tu kwenda kwa wanausalama." Malocha akamjibu wakati huo watu wote kasoro Martina aliyekuwa kalala, walikuwa sebuleni wakitazama taarifa hiyo iliyozagaa mtandaoni na katika vyombo vya habari.
"Siku mbili wametoa. Ngoja tuone baada ya siku hizo nini kitatokea." Masai aliongea huku akinyanyuka toka.kwenye kochi alilokuwa amekalia na kuelekea chumbani alipokuwa kalala Martina. Mubah akakamata rimoti na kubadili stesheni ya runinga ile kwa kuweka stesheni ya miziki.
BAADA YA SIKU MBILI
Dar es Salaam ilikuwa imepamba moto kwa mauaji ya polisi na wanausalama wa taifa ambao walikuwa wanajulikana mtaani na sehemu wanazoishi. Polisi wa barabarani walikutwa wamejifia na katika mavazi yao kuliandikwa Duka La Roho. Gari za jeshi zilizokuwa zinawarudisha watu hawa majumbani mwao, zilitekwa na wanajeshi walipata shida na mateso hadi kufa. Ilikuwa ni mshikemshike ndani ya Tanzania.
Ndani ya siku nne, kulikuwa hakuna askari anayeonekana hovyo jijini. Wananchi wenye hila na mioyo isiyopenda amani, ndio ukawa muda wao wa kujidai. Sheria wakazivunja na kijichukulia majukumu hata ambayo hayawahusu. Hapo ndipo wananchi walielewa nini maana ya kuanzishwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Machozi yaliwatoka wale wasiyo na nguvu kwani walishindwa kwenda kudai haki zao sehemu husika. Ubakaji, wizi, uzinzi, unyanyasaji, ukakua na kutanuka kwa kasi ya ajabu ndani ya siku chache tu. Ilikuwa inatisha Dar es Salaam.
Tambua kazi za vyombo vya usalama hasa majeshi yetu ya polisi. Usidharau wakifanyacho kwani wao ndio amani muhimu ya hii nchi.
Hakuna askari, basi amani nayo huwa sifuri na huwa hivyo daima. Kila chozi la mnyonge hutegemea vyombo hivi muhimu. Hata wanasheria, hawawezi kufanya chochote bila jeshi la polisi. Tuheshimu vyombo hivi kama tunavyoheshimu kazi zetu za mikono au tunavyoheshimu chakula. Tuwape heshima yao wanausalama wote. Dharau, kejeli, chuki na hila baina ya vyombo hivi, havijengi nchi bali kuibomoa.
****
"Naona majamaa wamechachamaa jijini." Malocha aliongea huku anamtazama Masai.
"Wamekuwa moto sana na wakifanyacho, nadhani kitakuwa kina madhara makubwa katika mambo yetu." Masai aliongea kwa utaratibu.
"Tunaweza kufanya nini ili kukomboa amani ya nchi hii."
"Hakuna kingine zaidi ya kumpigia simu Rais." Masai akajibu. Malocha akashusha pumzi ndefu kisha akawaita wenzake wote ili wajadiliane suala lile.
"Martina naomba nimpeleke kwa rafiki yangu. Huko nadhani atakuwa salama." Lisa alitoa pendekezo baada ya kukubaliana na mawazo yao ya kumpigia simu rais. Masai alikubaliana na Lisa kuhusu Martina kwa sababu ni ngumu sana kumuhusisha mtoto kwenye matatizo makubwa kama yale.
"Hallow." Malocha aliita baada ya kusikia upande wa pili wa simu aliyoipiga ikiita. "Malocha hapa." Akajitambulisha.
"Afadhali nimekupata kijana, nakuomba urudi FISSA. Ni kweli nina makosa na nilikuwa siyajui ndio maana nikakutoa bila kufikiria. Mambo yamekuwa magumu toka uondoke. Nimenusurika kuuawa mara mbili." Rais alikuwa mpole wakati anaongea hayo na hakutoa nafasi ya Malocha kuongea hadi alipomaliza.
"Yawezekana hujui kama pia ulitakiwa kuuawa siku Rais wa Urusi alipokuja." Malocha akaongeza habari iliyomfanya Rais ashikwe na kigugumizi.
"Mbona huongei mkuu." Malocha akamuuliza Rais wake baada ya kutosikia sauti yake.
"Mambo makubwa haya. Au ndio ule mlipuko uliyotokea siku ile?" Rais akauliza.
"Hata PITRI walikuja kuuteketeza uma. Na hiyo tunakulaumu wewe kwa sababu yasemekana uliwalea."
"Tuyaache hayo Malocha. Nakuhitaji wewe na kundi lako, FISSA inateketea kwa sababu ya upofu wangu. Wale wema wote, wameuawa na Lobo. Kifupi FISSA imekuwa ya magaidi inayoongozwa na Gunner." Rais alionesha wazi kuwa sasa maji yapo shingoni.
"Nipo na Masai hapa." Malocha aliongea huku akimkabidhi simu Masai.
"Ndio mkuu." Masai akaita.
"Kwako sina la kusema kwa sababu unatafutwa sana. Cha msingi, leo tukutane kisiri siri ili tupange mpango utakao tutoa katika hili sakata zito." Rais akashauri.
"Hayo ndio tunataka kuyasikia. Ni sisi na wewe tu. Hatuhitaji mtu mwingine."
"Limepita." Rais akapitisha ombi ambalo wote walinufaika. Wakapanga pa kukutana na kila kitu cha muhimu.
*****
Hali bado ilikuwa mbaya katika jiji la Dar es Salaam. Hakuna watu kuzurula usiku kwa sababu ya kundi lililojiita Duka La Roho kutishia amani ya kila mwananchi. Polisi hawakuenda makazini kwa sababu ya kitete cha kuuawa. Kifupi maisha ya kila mmoja yalikuwa rehani.
Wakati hayo yanaendelea, kundi lililorudi kwa kasi kwa ajili ya kulipa kisasi cha mauaji ya Pinto na Trina, kulipuliwa kwa ndege yao muhimu ambayo ingesababisha Rais wa Urusi kufa na kuharibiwa mtambo wa SGT, lilikuwa linazidi kupanga mipango kabambe ya kufanya ili kuwachimbua Masai na kundi lake kule walipo.
"Dar es Salaam sasa ipo kimya. Wamefumba midomo yao. Mkoa unaofuata ni Arusha. Kama kawaida yetu, ni tifu hadi wamfukue huyo boya wao wanaomuita Masai." Gunner aliongea kwa lugha ambayo kila aliyemsikia pale walipokuwepo, alimuelewa.
"Hapa kazi kwa vitendo. Siku mbili za kuwapa. Hawamfukui mbwa wao, basi kitakachofuata ni mauaji tu." Lobo akachangia mawazo ambayo kila mmoja alitikisa kichwa kukubaliana naye.
"Tomorrow. (Kesho)" Gunner akatabasamu baada ya maneno hayo kumtoka kinywani. Ni kama walikuwa wanafanya jambo la sahihi sana, kumbe walikuwa wanazidi kuhangamia nafsi zao.
*****
"Tuachie kazi sisi mkuu. Hawa tutawazima tu." Malocha alikuwa anampa moyo Rais baada ya kukutana naye katika daraja moja kubwa lililopo nje ya Jiji la Dar es Salaam.
"Niwafanyie nini jamani." Rais aliwauliza Masai na Malocha ambao ndio walikuwa wameenda kukutana naye.
"Tunahitaji silaha nzito. Wale watu tunaopigana nao wamekula kiapo cha damu. Wamezaliwa kufanya yale, hivyo tunaomba silaha ambazo zinaweza kudumu katika mapambano haya." Masai akajibu.
"Okay. Kesho mida kama hii, nitakuwa na mzigo mzima muutakao. Kumbukeni nafanya haya kwa mapenzi ya nchi hii. Ni kweli nimekosea, lakini sasa nataka kurekebisha hali hii. Baada ya kuwamaliza wale wajinga, mtarudi kwenye viti vyenu, ila Masai kuna kazi ngumu unayo ili kuepuka mikono ya wapelelezi wanaokutafuta."
"Usijali kuhusu mimi. Nitakuwa salama baada ya kumaliza haya."
"Huwezi kuwa salama kamwe. Utajificha hadi lini na taifa linahitaji msaada wako? Unatakiwa kuwa huru kijana." Masai akafikiria maneno ya Rais mara kadhaa hasa kuhusu mtoto wake Martina. Akaona wazi anahitaji ukaribu na Martina.
"Fanya uonalo sahihi." Masai akajibu na kuingia kwenye gari walilokuja nalo yeye na Malocha. Rais akakubali kwa kichwa naye akaingia kwenye gari lake na kuondoka. **** Katika jiji kubwa la Arusha, anaonekana mwanaume mmoja akiwa barabarani kavaa sare za jeshi.
Basi kubwa lililosheheni wanajeshi, linafika aliposimama yule bwana na kusimama. Jamaa anaingia ndani ya basi na kusimama katikati ya gari lile kwa sababu sehemu za kukaa zilikuwa zimekwisha.
Alikuwa ni Gunner ndani ya basi la jeshi. Akachomoa kibanio kimoja toka kwenye mifuko yake ya kombati alilovaa, kisha akajidai anajifunga kamba za viatu. Akakiweka kibanio chake chini bila mtu kumuona. Alipomaliza kufunga kamba za viatu, akasimama huku banio lile akiliacha palepale chini. Akasukuma kwa mguu wake banio lile chini ya kiti kimoja mle ndani ya basi.
Akatoka pale aliposimama na kwenda mbele karibu na dereva. Dakika tatu mbele, vikohozi kwa baadhi ya wanajeshi vilianza kusikika. Gunner akatoa kitambaa cha kujifutia jasho na kuziba pua zake huku akijitahidi kutovuta hewa mara nyingi. Mbele kidogo alimuona dereva anaanza kulegea, akawahi 'sterling' ya basi lile na kuanza kuliongoza kwa mkono mmoja na mkono mwingine ukiwa puani umekamata kitambaa.
Dereva yule akadondoka kabisa na kumpa fursa Gunner kukaa na kulisimamisha gari lile lilklokuwa na wanajeshi karibu sitini.
Baada ya kusimama, zikatokea gari mbili za kifahari mbele yake. Ni zilezile walizotoka nazo Burundi. Zikasimama na wanawake wanne wakashuka pamoja na vifaa vya kuchukulia video na mara moja wakaanza kazi yao.
****
Usiku wa saa mbili, Rais alikuwa amekuja na silaha nzito za maangamizi kwa ajili ya kuwawapa watu wake. Licha ya silaha hizo, pia Rais alikuwa katika majonzi hasa baada ya kupokea mkanda uliokuwa unaonesha wanajeshi wakipukutika miili yao na kubaki mafuvu yaliyokuwa yamevalia gwanda maalumu za jeshi.
"Jamani naombeni watu hawa mpambane nao. Mimi nashindwa cha kufanya." Rais aliongea kwa majonzi.
"Usijali mkuu. Maadam umetualika kwenye kalamu yako, basi kila kitu kitatulia." Malocha alimpa moyo Rais huku akitazama bunduki zilizoletwa na Rais kisha kumpasia Masai naye azitazame.
"Leo hii usiku, safari ya Arusha inaanza." Masai akaongea maneno baada ya kulidhika na silaha zilizoletwa. Na hakika zilikuwa silaha nzito.
"Safi sana. Nitawashukuru mkiwanyamazisha hawa washenzi."
"Shaka ondoa." Malocha akamaliza huku anafungia silaha zile kwenye begi kubwa lililokuja nazo.
Wakabeba silaha zile na kuzipakiza kwenye gari lao. Wakaondoka eneo lile kurudi nyumbani kwao kwa matumaini mapya.
Walipofika, wakawapa ujumbe wakundi wao, na kila mmoja alikuwa tayari kwa mapigano dhidi ya kundi la Gunner. Lisa akamchukua Martina aliyekuwa kalala na kumpandisha kwenye gari walilopanga kwenda nalo Arusha.
ITAENDELEA
 
  • Thanks
Reactions: ADK

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

Kabla ya safari hiyo haijaanza, Martina akapitishwa kwa rafiki kipenzi wa Lisa aitwaye Salome Makala. Martina akaamshwa na kupewa maelekezo kadhaa ambayo hakuwa mbishi katika kuyakubali. Baada ya hapo, gari ikaingia barabarani kwenda Arusha.
****
Likiwa limebaki saa moja ili kauli ya Gunner kwenye ile video itimie kwenda kwa vyombo vya usalama. Askari na wanausalama wa aina zote walijipanga barabarani na mabango wakiandamana ili Masai atoke. Waliimba nyimbo za ukombozi huku wakiwa na silaha za moto mikononi mwao. Lengo la kufanya hivyo ni katika kufikisha ujumbe kwa wale wanaomficha Masai. Hakuna aliyekuwa tayari kuona jeshi lao linaendelea kuhangamia pasi na sababu ya msingi. Waliandamana huku wakishinikiza kuwa Masai asipoonekana, basi vita dhidi ya serikali itaanza mara moja.
Wakati hayo yanaendelea, nyuso za Gunner na Lobo ziliambatana na tabasamu zito kwani ni wazi vita yao ilianza kuzaa matunda. Wakiwa ndani ya gari lao mwanana, walitabasamu na kugonga tano kwa mchanganyo wanaoufanya Tanzania.
Upande mwingine wa shilingi, Malocha, Masai, Lisa, Mubah, na wataalam wa mitambo yao, walikuwa wapo ndani ya gari linalokimbia kwa kasi kwenda Arusha kuwahi muda wa Duka La Roho. Masai akiwa nyuma ya usukani, kavalia kaptula ya kombati na juu kaushi nyekundu, alikuwa kama mwehu aliyeanza kuwehuka zaidi kwa jinsi alivyokuwa analiendesha gari lililobeba roho za wenzake. Licha ya hayo yote, hakuna aliyebisha kwani roho ya vita iliwaingia katika viini vyao vya nafsi na kuwaza vita tu.
Saa mbili asubuhi, kundi la Masai lilikuwa limefunga breki mbele ya hotel moja kubwa iliyopo katika jiji la Arusha. Wanaume wakashuka na mabegi yao yenye silaha, kisha akafuata Lisa ambaye yeye alikuwa kabeba begi la kawaida la nguo.
Moja kwa moja wakaenda mapokezi na kutoa kibali ambacho Rais kawapa kwa ajili ya utambulisho wakifika sehemu ile. Hoteli hiyo inamilikiwa na Rais. Mwanamke aliyekuwa pale mapokezi, baada ya kuona kile kibali, haraka akapiga simu kwa tajiri wake na dakika mbili mbele, meneja wa hoteli ile alikuwa anaongea na Malocha jambo fulani.
"Twendeni wazee wa kazi." Malocha aliwaambia wenzake baada ya kumaliza kuongea na Meneja.
Moja kwa moja wakaongozwa hadi chumba kimoja ambacho mlangoni kiliandikwa 'Conference Room' yaani chumba cha mikutano. Meneja akaondoka ndani ya chumba kile baada ya kuwakabidhi wale watu, na kitendo bila kuchelewa, mabegi ya wale watu yakafunguliwa na kila mmoja akatoa kompyuta yake tayari kwa kuanza kazi ya kumsaka Gunner na washirika wake kwa kutumia kifaa alichokuja nacho Masai toka Italia.
Baada ya dakika kumi, kila mmoja akaanza kutoa mafanikio yake kwa kile alichokuwa anakitafuta.
"Nimepata namba zake alizowasiliana nusu saa iliyopita." Mtaalam wao aliitoa taarifa na kuzitaja namba hizo na Lisa akazinakiri mahala.
"Nimepata maongezi yao waliyoyaongea kwa nusu saa iliyopita." Mtaalamu mwingine alitoa taarifa na kucheza yale maongezi ambayo Gunner alikuwa anawasiliana na wenzake na kuwaelekeza cha kufanya. Masai akatikisa kichwa kukubali kazi ya vijana wake.
"Kuna namba nyingine zimeonekana kabla ya nusu saa ya maongezi ya Gunner. Ni namba ya nchi za mbali na sauti yake hii hapa." Lisa naye akatoa alolichokinasa kwenye kazi aliyopewa.
"Ni The Shadow huyo. Naona anafurahi sana wajinga wanachokifanya. Mshenzi mkubwa." Masai aliongea kwa hasira kuliko siku zote ambazo kawahi kuishi katika dunia hii.
"Na hapa mimi nimepata ramani ambayo walikuwepo nusu saa iliyopita. Yaonekana baada ya mawasiliano haya, wameelekea upande wa Kaskazini lakini sisi tukipita barabara nyingine, tutakutana nao mbele japo wametuwahi." Malocha alitoa taarifa.
"Upande wa Kaskazini kuna nini?" Masai akauliza.
"Hapa Kaka. Kuna kambi ya jeshi ambayo ndio ngome kuu ya Tanzania kwenye upande wa Silaha. Wakifanikiwa kuteka eneo hili, basi Tanzania tutakwisha. Silaha zote watakuwa nazo wao." Malocha alitoa maelezo ambayo yakamfanya Masai apumue pumzi ndefu iliyo na mashaka.
"Naona wamepania sana. Ngoja nijaribu kuwatafuta maana majibu yenu ndio mwongozo wangu." Masai baada ya kuongea hayo, akaanza kubonyeza kompyuta yake harakaharaka na kufanya mle ndani kulie kiparaza kile cha kompyuta.
"Masai. Kuna mawasiliano yanafanyika sasa hivi hapa. Namba ya Gunner na hii namba." Mubah aliongea hayo huku anamgeuzia kompyuta yake Masai.
"Angalia hiyo namba nyingine ni ya nani." Malocha alitoa wazo haraka na Masai akaingiza namba hizo kwenye mtandao wake wa kutafuta mahali inapotokea.
"Shit. Ni ya hotel hii. Wajinga wanataka kutuchoma." Masai aliongea huku macho yake kayakodoa kwa hamaki.
"Ni yule mbwa wa mapokezi ndio katoa taarifa." Mtaalamu mmoja aliongea na kucheza sauti ambayo ilisikika ikiongea na Gunner.
"Wamefanya vizuri sana ili kusimamisha zoezi la kwenda kambini. Tuna dakika kumi za kufanya mambo yetu. Wao baada ya nusu saa watakuwa hapa." Masai aliongea huku akiendelea kutafuta mahali ambapo ataweza kuwaona Gunner na kundi lake kwa kutumia Satellite Trace.
"Okay." Baada ya dakika tano, Masai akatoa sauti yake na wote wakatega sikio. "Kuna makundi matatu ya hawa wajinga. Kuna la wanawake ambalo hili linaendelea kusonga Kaskazini lakini kwa taratibu kwa lengo kuwangoja wakina Gunner, kuna lingine la watu watatu ambao nadhani ni wale wataalamu wao, hili naona lipo katikati ya jiji na karibu sana na AICC. Nadhani wanataka kufanya kitu pale. Na kundi la tatu, ni Lobo na Gunner, hawa wapo njiani wanakuja kwetu." Masai alitoa maelezo hayo lakini kabla hajaendelea, Lisa akaingilia maongezi hayo.
"Naona wanawasiliana na kundi lililo jijini. Wanasema wakutane hapa." Lisa akatoa taarifa.
"Safi wife." Masai akampongeza mchumba wake. Lisa akatabasamu tu.
"Wanadakika ngapi kufika hapa." Malocha akauliza na Masai akabonyeza vitufe fulani kwenye kompyuta yake. Kompyuta ikaonesha gari walilopanda wakina Gunner na umbali lilipo toka pale walipo. Kisha akabadili ule umbali ukawa katika muda. Hapo akapata majibu ya kumjibu Malocha.
"Dakika kumi na tano tu."
"Tufunge vitu tuondoke." Malocha akashauri na kila mmoja akaanza kupakia vitu vyake haraka, lakini Masai akawa anaendelea kubonyeza kiparaza cha kompyuta mpakato yake. Hadi wenzake wanaliza kufunga, na yeye ndio alikuwa anamaliza kazi yake.
Bila kuifunga kompyuta yake, akaiweka mezani na kutoka na wenzake ndani ya chumba kile cha mikutano.
"Kwa nini umeacha mashine." Mubah akamuuliza Masai.
"Kuna meseji ya Gunner na Lobo, wanatakiwa waipate." Masai akajibu huku wakizishuka ngazi baadhi zilizopo katika hoteli ile.
"Huyo dada wa mapokezi msiongee naye chochote. Tupite tu." Malocha akatoa ushauri baada ya kuanza kukaribia mapokezi.
"Heee! Mnaondoka? Mbona mlisema hadi jioni mtakuwepo." Yule mwanamke aliyekuwa na weupe wa 'kosmatiksi' alijibalaguza lakini watu wa kazi walikuwa hawana muda naye zaidi ya kupita pale alipo na kutoka zao nje.
Kwa umbea zaidi, yule dada alikimbia hadi mlangoni na kuwatazama wakina Lisa wanavyoingia katika gari lao. Kwa bahati mbaya Masai akageuka na uso kwa uso wakakutanisha macho. Masai akapinda vidole vyake na kuwa mfano wa bastola, akamuelekezea na kufanya kama anashuti. Yule dada akashtuka na kijasho kikamtoka ghafla, akakimbia hadi katika ofisi yake na kukaa huku akitetemeka kama mgonjwa mwenye kifadulu.
Dakika mbili mbele, ndipo akapata wazo na kunyanyua simu ambayo alipiga namba za wakina Gunner.
"Haloo. Wameondoka wale watu." Dada wa mapokezi aliongea kwa kitete.
"Usijali tumeshaona wanapoelekea." Sauti ya upande wa pili ilijibu.
"Haya. Mkija, njoeni na dau langu." Dada yule akawakumbusha watu anaongea nao kuhusu aluchoahidiwa.
"Usijali." Simu ikakatwa na ahueni ya yule dada ikarudi.
****
Baada ya gari walilopanda wakina Masai kuondoka, zikapita dakika kumi ndipo magari mawili, moja la Gunner na Lobo na lingine la wale wataalam wao akiwemo yule mwenye mapengo, lilifunga breki kwenye hoteli ambayo wakina Masai walishaiacha muda mrefu.
Gunner na Lobo wakashuka na kufuatiwa na wenzao. Wakanyoosha hadi mapokezi walipomkuta yule dada akajipaka 'angel face' na kutengeneza muonekano wa maiti.
"Wapo wapi wale wajinga." Gunner alimuuliza na dada yule akashtuka hasa kwa sababu alikuwa hajawaona wale watu kama wamekuja.
"E.... e..... e.... e......" Yule dada alikuwa anakitete na macho kayatoa.
"Wapo wapi? Hatujifunzi kusoma hapa." Gunner akafoka na kumfanya yule dada arudi nyuma kwa uoga.
"Nili.... nili.... niliwa...pigia nyie ....si... si...si.... simu na kuwaambia wameooondo.... ka. Sasa sijui hamkunielewa." Maneno ya mwisho yakamtoka vema yule mwanamke baada ya yale ya mwanzo kutoka kwa kukatakata.
"Ulimpigia simu nani? We' mbwa nini. Embu usituletee uchuro hapa. Chumba walichokuepo kipo wapi?" Gunner alibwata na dada yule akatoa ufunguo uliobaki na kuanza kuwaelekeza chumba kile kilipo.
"Twende wote." Lobo kwa mara ya kwanza aliongea kwa sauti nzito na kumchomoa yule dada kwenye kitalu chake cha kupokelea wageni. Akamkamata mkono kwa nguvu na kwenda naye hadi chumba cha mikutano. Hata mlango haukufungwa, wakaingia na moja kwa moja macho yao yakatua mezani na kuona kompyuta aliyoiacha Masai ikiwa inapumua kutokana na AC yake kuwa nzima.
Gunner akaifata ile kompyuta na kubonyeza kitufe kimoja. Kioo kikaonesha maneno yasemayo 'Press Enter', Gunner akabonyeza kama alivyoelekezwa. Mara kompyuta ile ikaanza kuonesha gari la wale wanawake linapoelekea kwa kasi. Baada ya kulionesha gari hilo, kamera inayoendeshwa na satellite, ikaonesha gari la wakina Malocha ambalo lilikuwa kasi zaidi ya lile la wale Wairan wa kike. Ikaonesha umbali wa gari zile jinsi zilivyoachana. Kisha ule umbali ukabadilika na kuwa muda. Kutoka umbali wa gari analoendesha Masai hadi kwenye gari la wale wanawake, ni masaa mawili hadi kufikiana kwa mwendo waendao.
Gunner akatabasamu hasa alipoona kuwa ule muda ni mkubwa sana kwa wale wanawake kufanya anachotaka. Lakini wakati anatabasamu, mara kompyuta ile ikaonesha neno 'Plan B'.
Picha waliyokuwa wanaiangalia wakina Gunner, ikavutwa kwa mbali zaidi. Gari zikawa zinaonekana ndogo kiasi lakini zote zilionekana vema vilivyo.
Katika gari walilokuwa wakina Masai, kukaonekana mstari mwekundu, mstari huo ukaanza kuchora gari la Masai litakapopita.
Ni wazi plan B ilikuwa inaonesha njia ya mkato ambayo Masai angepitisha gari lake.
Gunner akawa kakodoa macho asiamini akionacho. Mchoro ule ukazidi kutembea hadi kwenye barabara ambayo itakutana na ile inayopita gari la wale Wairan. Baada ya kukutana ikaonesha muda ambao watakuwa wamezidiana, ni dakika tano tu.
Kompyuta ikazidi kudadavua na sasa ikaonesha baada ya dakika tano kitakachotokea. Neno lililoandikwa kwa herufi kubwa likatokea kwenye kompyuta. "WAR (VITA)" Baada ya neno hilo, kikatokea kibozo kikubwa na kuanza kucheka kwa nguvu. Kikacheka na kucheka lakini kilikuja kunyamaza baada ya Lobo kupiga risasi kioo cha kompyuta ile.
Gunner akiwa anatokwa na jasho la mgongoni, akachomoa simu yake haraka na kuanza kubofya namba za wale wanawake, kisha akaweka sikioni.
"Haloo Gunner. Umeona hiyo?" Badala ya sauti ya mwanamke mmojawapo kuitikia simu ile, akaitikia Frank Masai. Gunner akabaki kinywa wazi.
"Tatizo mnakurupuka nyie. Huyo muhudumu wenu katupa taarifa zote na tumemlipa pesa nyingi kuliko zenu." Masai akamchongea yule dada wa mapokezi. Gunner akamgeukia yule mwanamke aliyejikubua hadi kuwa mwekundu, akamuangalia kwa jicho baya.
"Nitakupata tu Masai. Huwezi kushinda vita vyetu hata siku moja. Wewe ni koko kama yalivyo mambwa koko mengine." Gunner alijibu mapigo kwa chuki nyingi.
"Haijalishi. Baadaye mje kuchukua maiti zenu." Masai akamjibu kwa nyodo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom