Riwaya-duka la roho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Riwaya-duka la roho

Discussion in 'Entertainment' started by mtzmweusi, Dec 8, 2016.

 1. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO

  SEHEMU YA 1.
  SAA 2:50 ASUBUHI.
  JIJINI DAR ES SALAAM, MAENEO YA SINZA AFRICA SANA.

  Wanaonekana watu wawili wakiwa wanafukuzana huku mfukuzaji akiwa kakamata bastola aina ya Baleta ikiwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti.
  Baadhi ya wananchi walikuwa wamesimama wima wakitizama uwezo wa wale watu wawili kukimbia na kuruka baadhi ya magari ambayo yalikuwa yanakuja mbele yao kwa kasi.

  Licha ya wananchi hao kuwa makini na kufuatilia mtanange ule kwa ukaribu zaidi, hawakujua ni nini sababu ya wanaume wale wa shoka kukimbizana tena kimya kimya. Wakashindwa kumsaidia mfukuzaji kwa sababu ugomvi hawakuujua. Kilichobaki kwa hawa wananchi ni kuendelea kujitazamia ufanisi mzima wa wale watu.

  "Kimenuka huko. Boya lazima atakuwa kafumwa anakula mzigo wa watu pale Rombo Green View." Alisikika kijana mmoja ambaye alionekana kama muhuni muhuni kwa jinsi alivyo na hata lugha anayoitumia.

  "Mmmh! Matepa. Rombo hadi huku Sana bado hawajachoka tu kufukuzana? Halafu yule kaka wa nyuma ana bastola, we unadhani ni kufumaniwa au yule wa mbele kakwapua cha watu kwenye gari. Maana huu wizi kwenye magari umekuwa mkubwa sana." Dada mmoja ambaye naye alikuwa kasimama kando ya barabara sawia na yule muhuni, alichangia maongezi kwa kumpinga yule muhuni.

  "Aah! Sister Angel, mwizi gani kapiga suti matata kama ile. Suti ya laki saba ile. Angalia viatu na hata muonekano wa lile jembe. Yule kafumwa tu anakula manzi wa mkuu, acha afundishwe adabu leo." Yule muhuni aliyejulikana kwa jina moja la Matepa, alitetea pointi yake kwa vigezo vichache ambavyo kila mmoja alikubaliana navyo kasoro Angel.

  " Mmmh! Matepa, siku hizi, mwenye suti ndio mwizi na mwenye muoneokano kama wako, ndio msamaria mwema. Hawa wezi wa siku hizi wajinga sana lakini wana akili kama nchwa." Yule dada ambaye naye alijulikana kwa jina moja la Angel, aliongea huku akianza kuondoka eneo lile maana watu aliokuwa anawafatilia walishatitia kutoka eneo lile.

  " Umeona Sister Angel eeeh, hawa wavaa suti ndio washenzi sana. Lakini wakishavaa hivyo, wanaficha hata macho ya jeshi letu na kufanya sisi wavaa majinzi au kaptula kwa tisheti, kuonekana ndio waharifu. Hapo dada yangu umebonga." Matapa aliunga mkono kauli ya Angel ambaye badala ya kuchangia chochote, alipunga mkono wake hewani na safari ya kupotea eneo lile ikazidi kushika hatamu.

  Wale majogoo wawili ambao walikuwa wanafukuzana, hakuna ambaye alisimama na kusaliti amri kwa mwenzake. Kasi ilikuwa inaongezeka kila dakika ambayo walikuwa wanakimbia kuifata barabara ya kwenda Makumbusho.

  Yule mwanaume wa mbele ambaye alikuwa kavaa suti ya gharama, rangi ya kijivu. Chini viatu vya damu ya mzee, navyo vikionekana ni vya gharama. Ndiye alikuwa kivutio cha macho ya watu wengi waliokuwa wamesimama kando ya barabara. Aliweza kuruka baadhi ya magari kwa sarakasi mwanana zilizochanganyika na mbwembwe nyingi kama nyimbo za kibantu.

  Kuna muda aliruka sarakasi na kutua juu ya gari lililokuwa kasi, kisha anajiachia kama mwenye kujitupa ndani ya maji kumbe anajitupa kwenye rami. Anapofika chini ya rami hiyo, hujiviringa kiustadi na kisha huinuka haraka na kuzidi 'kuchanja mbuga'. Manjonjo yote hayo, yalikuwa yanamkosesha raha yule wa nyuma kwani shabaha zake kumrenga mtuhumiwa wake, zilikuwa haziendi ipasavyo.

  "Mkuu, mpo wapi? Huyu mtu si mtu asee, muda si mrefu tunampoteza." Yule jamaa wa nyuma alishika sikio lake ambapo kama utamwangalia kwa makini zaidi, utagundua kuwa kavaa 'earphones' ambazo huvaa wapelelezi au walinzi wakubwa duniani hasa katika kusaidia mawasiliano baina yake na kundi husika.
  Na hapo yule jamaa alikuwa anawasiliana na kundi lake kuona kama atapata msaada juu ya mtu yule anayemfukuza.

  "Okay. Basi mtegeni hapohapo maana naona wazi anakuja eneo hilo." Sauti ya yule mkimbizaji ilisikika tena ikijibu maelezo ya upande wa pili.
  Baada ya hapo, aliachia kisikizio kile na kuzidisha mbio ili kumkaribia yule jamaa wa mbele yake.

  Wakiwa katika kasi ya hatari, ghafla mbele ya yule jamaa wa mbele, inatokea gari aina ya Noah na kupiga msele mkali ambao uliifanya ile gari iseleleke tairi za nyuma lakini ni kama ilikuwa imepangwa itokee hivyo. Kwani baada ya mseleleko huo, ule ubavu wa nyuma wa ile gari, ulimpiga kikumbo kikali yule jamaa aliyekuwa anafukuzwa. Kikumbo hicho kikamfanya arushwe hatua kama nane kwenda nyuma, na wakati huohuo, yule jamaa wa nyuma naye hakuwa mbali na tukio lile.

  Jamaa aliyepigwa kikumbo, akajikuta anarushwa bila kutegemea. Na katika kujiokoa ili asitulie viungo vya mwili ambavyo ni rahisi kuvunjika, akajikuta kasimama mbele ya jamaa mwenye mwili wa wastani na unaonekana kukumbana na mazoezi ya kutosha kila kukicha. Tabasamu likajitokeza kwenye uso wa kijana yule aliyerushiwa mtuhumiwa.

  "Gotcha (Nimekupata)." Sauti ya ushindi ilisikika kwa jamaa yule na kutaka kumkamata mtu aliyekuwa anamfukuza kwa karibu saa moja na robo.
  Lakini kabla hajamkamata, alishtukia akipigwa ngumi kali mbili za maeneo ya mabegani na kufanya bastola na pingu zake kudondoka.

  Kabla hajakaa sawa, mtuhumiwa wake tayari alikuwa kamsogelea na kumgonga kochwa kizito cha pua kilichomfanya yule mfukuzaji kuyumba kidogo na kusimama tena lakini hapohapo mtuhumiwa wake alikuwa kisharuka angani kidogo na kumsindikiza na teke la kifua ambapo safari hii alishindwa kijizua bali kukubali kwenda chini na kusalimia rami iliyopo maeneo yale.

  Ni kama jamaa yule hakukumbwa na gari kwa jinsi alivyokuwa anajimudu kwenye kurusha mateke na kuruka sarakasi ambazo zilikuwa chachu tosha katika kumuadabisha mpinzani wake ambaye alishindwa kujibu mapigo na hivyo kugaa-gaa pale kwenye rami kama swala aliyechomwa upinde wenye sumu.

  Yule kidume ambaye alikuwa amekwishamiliki mchezo mzima, sasa akawa anajiandaa kummaliza mpinzani wake kwa pigo ambalo yule jamaa aliyekuwa anamfukuza alipoliona, alikumbuka ni jinsi gani lilivyobeba uhai wa watu wengi akiwemo Mkuu wa Upepelezi kanda ya kati, Mzee Ismail Ambazeki. Askari muadilifu kupata kutokea katika nchi ya Tanzania.

  Wakati Mzee Suma Ambazeki anapigwa pigo hilo, huyu kijana ambaye anajiandaa kupokea pigo hilo, alikuwa askari mdogo sana kicheo. Cheo chake kikamfanya awe dereva wa Mzee Suma au Ismail. Na siku wakati mtuhumiwa wake anampa pigo bosi wake, yeye alikuwa ndani ya gari akitetemeka hasa baada ya kuona mapigo 'konde' ya jamaa yule.

  Akafumba macho yake ili asione jinsi lile pigo litakavyokita mwilini wake. Yule jamaa ambaye alikuwa anafukuzwa, tayari alishajitutumua na kujifua ipasavyo kwa ajili ya kumdondoshea pigo au tufani, yule kijana wa watu.
  Akaruka juu huku sauti ya juu ya kikomando ikisikika tayari kwa kumwingizia pigo takatifu yule mfukuzaji.

  Ni kama wote wawili walikuwa ndotoni. Hapa nawazungumzia yule aliyekuwa anapigwa na anayepiga. Mpigwaji, aliona kama Malaika mwokovu kamtokea na kumsaidia, lakini mtuhumiwa wake alijiona kama Malaika mtoa roho kamtembelea kwa wakati ule.

  Akiwa juu huku akitoa sauti yake ya kikomandoo, alijikuta akipigwa teke zito la ubavu lililokata hadi sauti yake hiyo mbaya. Kabla hajaelewa wala kujiweka sawa kuangalia ni nini kilichompata, akapokea teke lingine la kijizungusha (round kick) ambalo lilimkuta kidevuni na kuzidi kumrudisha chini badala ya kumsimamisha.

  Dhoruba ikazidi kumuandama yule mbabe wa mwanzo kwani safari hii alijikuta akikaliwa kifuani na kuanza kupigwa ngumi mfululizo kana kwamba mwili wake uligeuka kuwa begi la kupigia ngumi hizo.

  Ndani ya dakika zisizozidi mbili, tayari yule mbabe alikuwa hoi huku uso wake ukiwa umelowa damu zilizochagizwa na kupasuka usoni.
  "Hey. Mubarak, fanya kazi yako." Ni sauti iliyomuamuru yule aliyepewa kichapo na mtuhumiwa wake. Sauti ilienda sambamba na kurushiwa pingu ambazo aliziokota baada ya mbabe mmoja kuzifanya zitoke kwenye mikono ya mwanausalama Mubarak.

  "Yes Madame (sawa mama)." Mubarak au Mubah kama alivozoeleka kuitwa na wenzake, alinyanyuka na kuziweka pingu alizorushiwa vema na kumwendea mtuhumiwa wake.

  Japo yule mtuhumiwa alishasaliti amri, lakini Mubah ni kama alikuwa hajui hilo. Akaanza kumshushia mateke mazito tumboni yule mtuhumiwa.
  "Hey Mubah, mfunge pingu, acha ujinga." Sauti ileile ya kike ilimfokea na Mubarak hapohapo amri akaifuata kwa kumfunga pingu yule mtuhumiwa wao na kumnyanyua, tayari kwa kumpeleka kwenye ile Noah iliyompa kikumbo.

  Baada ya dakika moja, Mubah alikuwa tayari amekwishamaliza kumfunga pingu mtuhumiwa wake na kumuingiza kwenye ile Noah. Ndani ya Noah kulikuwa na wanaume wengine watatu, mmoja akiwa dereva na wengine wawili wakiwa wanacheza na mitambo zikiwemo kompyuta ndani ya gari ile.

  Yule mwanamke, alikaa upande wa kushoto wa siti ya nyuma ya dereva, na Mubah akakaa upande wa kulia wakati huo mtuhumiwa wao akikaa katikati yao.

  " Lisa Lindsay. Mwanamke niliyekupenda kwa moyo wangu wote. Upo mke wangu?" Sauti ya kukeresha ilimuuliza yule mwanamke huku muulizaji mwenyewe akiwa kajiinamisha kichwa chake bila kumuangalia usoni amuulizaye.

  "Kwa nini umeamua kufanya kazi kama hii? Umekosa kabisa hata kazi ya kuuza vitumbua na sasa unajiweka katika kazi za utumwa kama hii? Kazi za kuhatarisha maisha yako na ya uwapendao." Jamaa alizidi kuongea lakini hakuna aliyemjibu.

  "Ooh! Naona maongezi yangu hayawaingii vichwani mwenu. Ngoja nijaribu maongezi haya." Safari mtuhumiwa alinyanyua uso wake na kumuangalia Lisa. "Frank yupo wapi?" Swali likamtoka mtuhumiwa na kumfanya Lisa amwangalie usoni kwa mshtuko. "Nimegusa penyewe hapo. Anapenda kujiita Man'Sai. Mwanaume aliyetikisa dunia kwa kuiba "UKURASA WA HAMSINI" (Hii ni hadithi nyingine ambayo inaanza pale riwaya ya JINA itakapoishia).

  Mwanaume ambaye tulikuwa hatulali baada ya kugundua Lisa Lindsay anatoka naye kimapenzi. Yupo wapi sasa hivi. Yale maneno matamu ya nakupenda na porojo nyingi, vimeishia wapi? Hayupo tena nawe, kwisha habari yako." Yule jamaa aliongea na kumalizia kwa cheko ndefu iliyokera kila mtu mle kwenye gari. Lakini hakuna aliyethubutu kuongeza neno wala kufanya kitendo chochote cha ajabu.

  "Martina Gunner Bokwa. Jina la mtoto wako." Yule mtuhumiwa akaongea maneno mengine yaliyovuta hisia za Lisa na kubaki mdomo wazi. "Kwa nini ulimuita mtoto majina ambayo si yake?" Jamaa akazidi kumshangaza Lisa kwa maneno ambayo yaligusa undani wa Lisa.

  Akiwa kafungwa pingu na mikono yake ikiwa mbele, jamaa yule aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti ulio maeneo ya kifuani kwake na kutoa picha ambayo ilimuonesha mtoto wa kike mwenye umri kati ya miaka miwili hadi mitatu.

  Kwa mshangao na kwa kushtukiza, Lisa akampora ile picha yule jamaa huku uso wake ukijawa na hamaniko la haja.
  "Umetoa wapi hii picha we mpumbavu?" Lisa alimuuliza yule jamaa huku akiwa tayari kamvamia na kumkaba shingoni.

  Ni Mubarak ndiye akiyemuondoa kwenye mwili wa mtuhumiwa na kumpunguza hasira ambazo tayari zilikuwa zimemkamata kooni Lisa.
  Wakati huo gari lao, lilikuwa linazidi kuacha maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam, na kuna sehemu Noah ile ilisimama kwa muda mrefu sababu ya foleni kubwa inayoendelea kutesa katikati ya jiji lile.

  "Koho kohoo." Yule mtuhumiwa alijikohoza baada ya roba ya Lisa huku akijitengeneza na kukaa sawa kwenye kiti cha gari ile.
  "Mubah. Hii ni picha ya Martina, nilimpiga mwenyewe na nilikuwa nimeiweka kwenye mkoba wangu. Sasa huyu kaipataje na mkoba huo nauficha kwani una vitu vingi vya siri." Lisa aliongea kwa sauti iliyojaa machungu huku ikichagizwa na hali ya kutaka kulia.

  "Navijua vitu vyote vya siri. Ukaamua kuolewa na Gunner ili kuficha aibu. Hujui chochote kilicho nyuma ya .....
  .." Jamaa yule hakumaliza sentensi yake, tayari Mubah alikuwa kamtandika ngumi nzito ya shavu hadi damu kiasi zikamrukia Lisa.

  "Ooooh! Ni Prince Mubarak." Jamaa yule aliongea baada ya kujifuta damu zilizokuwa zinamchuruzika. "Na swali.moja tu kwako, na usipolijibu, nitakupa onyo tu." Jamaa alimtazama Mubah kabla hajauliza swali lake.
  "Kwa nini umeamua kuweka dukani roho za uwapendao?" Jamaa alimuuliza Mubah lakini badala ya Mubah kujibu, yeye akachukua gundi aina ya 'sole tape' na kuizungusha mdomoni mwa mtuhumiwa yule mwenye mdomo wa kero na kukereketa.

  "Thats will help, I think. (Hiyo itasaidia nadhani)" Lisa aliongea akikubaliana na kitendo kilichofanywa na Mubah.
  ****

  Safari yao ilikomea eneo moja la ufukwe wa bahari ya hindi. Na baada ya hapo, Lisa alitoa simu yake ya mkononi na kuipiga.
  Maongezi yalichukua dakika chache na simu ikakatwa.

  Baada ya dakika zisizozidi kumi za kukata simu ile, kwa mbali, kwa kutumia darubini yake, Lisa aliona Nyambizi ikiibuka toka chini ya bahari na baadae ikafunguka kwa juu na boti ndogo saba zikatoka ndani yake. Boti hizo ni zile ziwezazo kubeba watu wawili kila boti moja.

  Waendeshaji walikuwa wamevalia mavazi ya kuogolea na bunduki aina M16 zikiwa migongoni mwao.
  Lisa akashushia darubini yake kifuani na kuwapa ishara wenzake ya kujiandaa hasa kutoka mle garini.

  Boti saba zikasimama mbele ya wakubwa wa kazi, na kitendo bila kuchelewa, kundi linaloongozwa na Lisa likiwa na mtuhumiwa wao, wakakwea nyuma ya boti hizo ndogo na safari fupi ya kwenda kwenye Nyambizi moja ndogo kiasi, ikaanza.

  Boti tano zikiwa mbele na nyingine mbili nyuma zikilinda usalama ili yule mtuhumiwa asitoroke, zikazidi kukata maji kuelekea kwenye nyambizi.
  Wakiwa katika umbali fulani, Lisa alimuamuru dereva wa boti yake asimame. Naye baada ya kusimama, Lisa aligeuka nyuma na kuangalia kule alipotoka.
  Kulikuwa hakuna watu wanaozunguka eneo lile, hiyo ikawa nafasi pekee ya Lisa kufanya alichokusudia.

  Akatoa rimoti ndogo ambayo alibofya kitufe kimoja kilichokuwepo katikati. Na hapohapo, mlipuko mkubwa uliikumba ardhi ambayo gari aina ya Noah ilikuwa imeweka makao kwa muda.

  Ni ile gari ambayo walikuwa wanaitumia Lisa na kundi lake. Baada ya kumalizia kazi ambayo waliipanga, sasa waliiteketeza na kuacha Jiji dogo la Dar Es Salaam kutetemeka kwa huo mlipuko. Wafanyakazi wa maeneo yale walikimbia huku na huko wakihisi jiji limevamiwa na magaidi hatari. Hakuna aliyekumbuka kugeuka nyuma, wote walikuwa wakinusuru roho zao. Hakika ilikuwa ni mshike mshike maeneo yale.

  Baada ya kulidhika na kazi yake, Lisa akamgonga bega kumruhusu dereva wake aondoke, naye akatii amri na kwenda sehemu ambayo walipanga waende.
  ****

  Ndani ya nyambizi ile, kulikuwa kuna pilika za hapa na pale hasa wale mafundi mitambo wanaongoza chombo kile maalumu kwa ajili ya kazi za kijeshi au kiusalama.

  Naam, baada ya Lisa na kundi lake wakiwa sambamba na mtuhumiwa wao kuingia kwenye chombo kile, waliongozwa kwenye chumba maalumu na kuoneshwa nafasi zao za kukaa.

  Baada ya kukaa, alitokea daktari mmoja akiongozana na kijana aliyebeba sinia dogo lililokuwa na sindano uwezazo kuzikamata kama bastola. Sindano hizo zenye dawa kiasi, kila mmoja alichomwa begani na baada ya dakika chache, macho ya hawa watu yakaanza kuwa mazito.

  "Kazi za utumwa hizi. Hamtakiwi kujua hata ni wapi mnafanyia kazi na ndio maana mnapigwa sindano za usingizi ili msione mnapoenda. Stupid peoples." Sauti nzito iliyochanganyanyika na ulevi, ilimtoka yule mtuhumiwa aliyekuwa huru kuongea baada ya kutolewa ile gundi aliyozungushiwa na Mubah.


  ITAENDELEA
   
 2. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA PILI

  Ndani ya nyambizi ile, kulikuwa kuna pilika za hapa na pale hasa wale mafundi mitambo wanaongoza chombo kile maalumu kwa ajili ya kazi za kijeshi au kiusalama.

  Naam, baada ya Lisa na kundi lake wakiwa sambamba na mtuhumiwa wao kuingia kwenye chombo kile, waliongozwa kwenye chumba maalumu na kuoneshwa nafasi zao za kukaa.

  Baada ya kukaa, alitokea daktari mmoja akiongozana na kijana aliyebeba sinia dogo lililokuwa na sindano uwezazo kuzikamata kama bastola. Sindano hizo zenye dawa kiasi, kila mmoja alichomwa begani na baada ya dakika chache, macho ya hawa watu yakaanza kuwa mazito.

  "Kazi za utumwa hizi. Hamtakiwi kujua hata ni wapi mnafanyia kazi na ndio maana mnapigwa sindano za usingizi ili msione mnapoenda. Stupid peoples." Sauti nzito iliyochanganyanyika na ulevi, ilimtoka yule mtuhumiwa aliyekuwa huru kuongea baada ya kutolewa ile gundi aliyozungushiwa na Mubah.
  Hakuna aliyemjibu na badala yake, kila mmoja alibebwa na usingizi mzito.
  ****

  FISSA (Federal Intelligence Secret Service Agencies)
  Mlango mmoja mkubwa uliandikwa maandishi hayo ambapo ndipo hasa Lisa na Mubah wanafanya kazi zao. Ule usingizi mrefu ulikuwa umewapaa na sasa walikuwa wanatembea wenyewe huku wakimkwida vema mtuhumiwa wao ili asiwaponyoke.

  "Kazi nzuri Agent Lisa. Mmefanya vizuri na kikosi chako." Sauti ya mtu mmoja mrefu kiasi na mweusi, ilisikika ikiwa kwenye jukwaa dogo ambalo mbele yake kulikuwa na watu wanachakalika na kompyuta zao huku skrini moja kubwa ikionesha kazi nzima wafanyazo wale wafanyakazi.

  "Asante mkuu." Lisa alishukuru huku akiinama kidogo kuonesha heshima kwa mkuu wake wa kazi.
  Mkuu yule akashuka toka kwenye lile jukwaa na moja kwa moja akamfuata yule mtuhumiwa na kumuangalia kwa macho makali kabla hajaanza kuongea.
  "John Lobo. Nilishangaa sana nilipoambiwa kuwa u mzima.

  Nilikuua kwa mikono yangu, lakini leo ni kama nakutana na mzimu." Sauti ya yule bwana ilipenyeza kwenye masikio ya kila mmoja aliyesikia vema maongezi yale. "Sina kesi na wewe. Nilishakuua kipindi kile, hapa naanza na kesi nyingine." Alimaliza Mkuu wa FISSA na kugeuka nyuma kurudi kwenye lile jukwaa dogo.

  "Malocha Malingumu." Sauti ya John Lobo, mtuhumiwa aliyekamatwa na kundi la Lisa, ilimuita yule mkuu wa kitengo cha siri cha huduma za kipelelezi nchini Tanzania. Bwana Malocha akasimama kumsikiliza kimtokacho John Lobo.
  "Siyo kosa langu kuua familia yako.

  Nilinunua roho zao kwa kuamrishwa na shetani langu. Usilalamike sana. Hahahahahaaa." Lobo alimaliza kwa cheko lake la kukera kushinda hata la katuni au fisi.

  "Mpelekeni Hell in Hell." Malocha akaamuru na kila mmoja alishituka baada ya kusikia amri hiyo.
  "Hamjanisikia?" Malocha aliuliza baada ya kuona hakuna kinachotendeka baada ya amri.

  "Lakini Mkuu huyu tutampoteza kule. Kumbuka CIA na FBi wanamtaka mzima." Lisa akiongea kumuelewesha mkuu wake.
  "Kwa hiyo unashauri apelekwe wapi?" Malocha akauliza tena swali.
  "Nadhani twende naye 123K." Alitoa wazo Lisa.

  "Kwa hiyo akakae tu! Kaja kukaa hapa au kusema ukweli?" Malocha alimtupia swali Lisa.
  "Lakini si kumpeleka Hell in Hell. Atasema nini kule?" Lisa alijitetea.
  "Hivi mmenileta huku nije kusema kitu au nije kupiga story na 'school mate' wenzangu?" Lobo alifungua kinywa chake na kuwauliza wale wanaoshauriana wapi wampeleke.

  "Kama mnataka mnijue au niseme chochote, hilo mmekosea. Hapa hampati kitu wajinga nyie." Lobo akamaliza na hapohapo ngumi nzito ya tumbo ilitua. Alikuwa ni Mubah aliyemuadabisha.

  "Utalipa hii dogo." Lobo alimwambia Mubah na Mubah badala ya kutilia maanani yale maneno, alimuongeza konde lingine zito la tumboni.
  "Big Mistake(Kosa kubwa) Lakini bado unanafasi ya kulisawazisha." Lobo alimwambia tena Mubah baada ya kuinuka alipokuwa kainama kwa sababu ya kupigwa ngumi ile.

  "Mpelekeni 123F6."Malocha aliamuru tena. Na kitendo bila kuchelewa, Lisa na Mubarak walimkamata kushoto na kulia na kuanza kumkokota kwenda chumba walichokiita 123F6.

  HELL IN HELL
  Hichi ni chumba kipana kilichopo ndani ya FISSA. Ndani ya chumba hiki kuna kiti cha umeme ambacho hutumika kuwasulubu watuhumiwa nguri na saa nyingine kuwaua.

  Pia kuna tank kubwa ambalo limejengwa kwa vioo, na tank hilo ndani yake kuna maji. Pia hutumika kusulubisha watuhumiwa kwa kuwazamisha humo au wakiona haongei, hufungulia umeme uliyoungwa ndani ya tank hilo na kuanza kumpiga shoti mtuhumiwa. Hizo ni silaha chache zilizopo katika chumba kiitwacho Hell In Hell. Mbali na hayo, kuna vifaa vya kunyongea na kuchania ngozi.

  Ni chumba ambacho kinaogopwa hata na wafanyakazi wenyewe. Kinatisha kwa matendo yanayofanyika huko.
  123K

  Hiki pia ni chumba kilichopo hukohuko FISSA. Chumba hiki pia ni kipana na kina meza moja kubwa pamoja na kioo ambacho ukiwa ndani huwezi kumuona wa nje lakini wa nje anamuona wa ndani.

  Chumba hichi ni kwa ajili ya kumuhoji mtuhumiwa kwa mdomo bila kumsulubisha. Na hata kama watataka.kufanya hivyo, basi hutumia viungo vyao kama ngumi na mateke.

  123F6
  Hiki ni chumba kipana pia kwa ajili ya mahojiano na watuhumiwa. Ndani ya chumba hiki, mahojiano huwa ni ya kulazimisha uongee ukweli kwa kubanwa na silaha mbalimbali pamoja kuchomwa na vitu vyenye ncha kali lakini lengo likiwa utoke mzima.

  Na mara nyingi kama mtuhumiwa ni mgumu, basi hupigwa sindano yenye dawa kali ambayo hufanya ubongo na akili ya mtuhumiwa iwaze kusema ukweli tu.
  Humo ndimo ambamo John Lobo kapelekwa. Nyuso mbili ambazo hazina utani zilikuwa zimesimama pembeni ya chumba hicho huku wakijaribu jaribu vifaa vyao.

  Mzee mmoja ambaye alikuwa anapuliza gesi yenye moto juu, aligeuka haraka baada ya kusikia mlango wa chumba kile ukifunguliwa.
  "Ooh! Lisa. Umefanikiwa kumkamata Lobo. Kazi nzuri sana binti." Mzee yule aliongea kumpongeza Lisa.

  "Asante Babu Pujini, hakuleta shida wakati wa kumkamata." Lisa alimjibu Mzee Pujini ambaye alikuwa ana asili fulani ya Kihindi lakini ni Muafrika halisi kutoka Tanzania.
  "Good Lisa. Ndio umemleta kwenye shughuli eeh." Mzee Pujini aliongea huku akianza kuchezea tena ile gesi kwenye kibubu maalumu kinachotengeneza moto huo wa gesi.

  "Ndio babu. Fanya yako." Lisa alijibu na wakati huo Mubah alikuwa anafungua pingu alizokuwa kamfunga John Lobo.
  Licha ya Lisa na Mzee Pujini kuongea mengi yanayomhusu John Lobo, lakini Lobo mwenyewe hakuwepo kwenye dunia yao bali macho yake yalikuwa yakipepesa huku na huko, chini na juu ya chumba kile.

  "Huyu hapa Mzee." Sauti ya Mubarak ilisikika huku ikifuatiwa na kumsukuma Lobo kwa mzee yule bingwa wa kutoa adhabu kwa watuhumiwa mbalimbali.
  "Beda. Muondoe misuti yake huyu bwana." Mzee Pujini alimsukumia Lobo kwa Beda, jamaa fulani wa makamo na kwenye mwili mkubwa kutokana na kunyanyua vitu vizito.

  Naye Beda bila kuchelewa, akaanza kumwondoa nguo John Lobo na wakati huo Lisa na Mubah walishatoka katika chumba kile na Mzee Pujini alishakifunga.
  ****

  "Lobo. Nia yako na washirika wako ni nini?" Sauti ya kiume ilisikika katika chumba kiitwacho 123F6.
  Ilikuwa ni sauti ya Malocha ikitoka kwenye spika zilizopo kwenye chumba kile.
  Lobo alikuwa akivuja damu nyingi kifuani na maeneo ya usoni. Alikuwa kalegea kwa mateso makali ambayo yalitoka mikononi mwa Beda na Mzee Pujini.
  "Kazi yangu ni kuuza au kununua roho tu!

  Sina kazi nyingine. Sina nia na wala sijui washirika wangu ni wakina nani." Lobo alijibu swali la Malocha na baada ya jibu hilo, Malocha alitoa ruhusa ya mateso kuendelea.

  Mzee Pujini akachukua kile kibubu chenye gesi na kuwasha gesi ile. Baada ya kuweka moto fulani kwenye kibubu kile cha gesi, akamfata Lobo na kuanza kumpitishia machoni bila kumdhuru bali kumsikilizisha joto litokalo mle kwenye kibubu.

  "Joto hili linaenda kwenye maungo yako ya uzazi." Mzee Pujini akiwa kavalia kama Daktari, akaongea huku taratibu akianza kushusha moto ule kwenye maeneo ambayo kayataja.

  Licha ya hayo yote kutukia, uso wa John Lobo ulikuwa si wenye mashaka wala uoga. Ni kama alishazoea yale mateso, lakini yote ni sababu alikuwa mkomavu katika nyanja kama zile.

  Mzee Pujini akafika maeneo ya uzazi ya John Lobo, na bila kusita akapulizia gesi ya moto maeneo yale na kumfanya John Lobo atoe sauti kali iliyochanganyika na maumivu. Hakika mkomavu na kamanda wa mateso, alikuwa anaumia.

  "You fu**n, motherfu***r you're hurting me. (We mpumbavu, (tusi). Unaniumiza)." Sauti ya maumivu makali ilisikika kutoka kwenye kinywa cha Lobo ikifuatana na matusi mazito ya wazazi kumuelekea Mzee Pujini.
  "Sema ukweli tuache hili zoezi." Mzee Pujini aliacha kuchoka maeneo nyeti ya Lobo na kumuomba aseme ukweli.

  "Pale nitakapofanikiwa kusimama kwenye hiki kiti, wewe ndio utakuwa wa kwanza kufa." John Lobo alimwambia Mzee Pujini maneno ambayo yule mzee alitabasamu kwa dharau kisha akaangalia kile kioo ambacho wa ndani hamuoni wa nje ikiwa ni ishara ya kuwaambia waulize swali lingine.

  "Lobo. Hatupo hapa kukuumiza. Ni rahisi tu! Unashirikiana na nani na nini nia yako kwa ufanyayo." Swali lilelile lilitoka kwenye kinywa cha Malocha.
  "Hahahaaa. Malocha, mbona unajiumiza sana. Nimekwisha kwambia, sina nia zaidi ya kuuza na kununua roho za watu.

  Au unataka nikwambie duka la roho lilipo?" Lobo aliuliza huku uso wake ukielekea kwenye kile kioo kana kwamba anawaona wale wanaomtupia maswali kwa kunong'onezana.

  "Lobo. Hatupo katika utani. Umemuua Kamanda wa Kikosi cha Upepelezi kanda ya kati. Umewatishia amani mawaziri mbalimbali na kauli yako ya kununua roho zao. Ukawaua baadhi ya viongozi hao. Ukaona haitoshi, ukaanza kuwaondoa mabalozi mbalimbali wa nchi hii kwa kuwaua. Sasa umegusa pabaya zaidi. Marekani.

  Umegusa nchi ambayo hatuiwezi kwa kitu chochote....." Sauti ya Malocha ilikuwa ikielezea baadhi ya maovu ya John Lobo lakini kabla hajamaliza maongezi yake, sauti yenye hasira kupindukia, ilimkata kauli.
  "Eti hatuiwezi kwa chochote.

  Ni ujinga gani ambao umekujaa kichwani we' mpumbavu? Marekani anachotuweza ni nini? Au ndio kasumba zenu za uoga bado zimewatawala kichwani mwenu?

  Huyu Frank anapambana na kutafutwa kwa udi na uvumba na watu gani? Si ni hawahawa Wamarekani? Mbona hawampati? Mbona hata wakimpata wanamshindwa? Kaua makomando wangapi Wakimarekani. Usiwe mjinga Malocha. Umiza kichwa fala wewe." Kauli chafu zilitiririka toka kinywani mwa Lobo na hakuna aliyethubutu kumkatiza hadi alipomaliza mwenyewe.

  "Sound like it's true. But none of it is real. (Sauti kama ya ukweli. Lakini hakuna kati hivyo chenye uhalisia)." Malocha aliongea kwa kutumia lugha ya ughaibuni.

  "Frank, never killed any commander from America. He just killed the terrorists, and bad guys. (Frank hakuua kamanda yeyote wa Kimarekani. Aliua wavamizi na watu wabaya pekee)." Sauti ya Lisa iliunga maelezo ambayo Malocha aliyaacha kati.

  "Inaonekana hamjui lolote la kwa nini Frank anatafutwa na kwa nini kajificha. Na mbaya zaidi, hao anaowaua ndio mimi na baadhi yenu nyie wapelelezi mnawasujudia. Mtakufa kama panya kwenye sumu kwa mkono wangu." Lobo aliongea kwa hasira huku akijaribu kuchomoa mikono yake toka kwenye kiti alichokuwa kafungwa barabara na wazee wa kazi wa chumba 123F6.

  Hali ya kujikakamua ili atoke pale kwenye kiti, ilifanya mwili wake ututumke na kusambaa misuli kama ananyanyua vitu vizito.
  "Mzee Pujini. Fanya yako." Malocha aliongea kumruhusu tena Mzee Pujini aendeleze adhabu zake.

  Mzee Pujini naye bila kusita, akajaribu moto wake angani kabla hajaanza kazi ya kuchoma ngozi nyeusi ya John Lobo.
  ****

  "Hahahahahaa. Kuna muda hamna haja ya kulia bali kucheka kwa sababu maumivu uyapatayo, ni sawa na kukutekenya tu." Sauti ya John Lobo iliongea baada ya Mzee Pujini kumaliza kumchoma kwa gesi maeneo ya ndani ya mapaja na kifuani.

  "Look like you are so tough. Lets see. (Unaonekana kama mgumu. Ngoja tuone)." Sauti ya Beda, mshirika au msaidizi wa Mzee Pujini ilisikika ikiongea hayo huku ye' mwenyewe akivaa grovu tayari kutimiza majukumu yake.

  Beda akachukua visu fulani vidogo vilivyo kwenye mkoba maalumu kwa ajili ya kuvihifahidhia. Na baada ya kukamata visu hivyo viwili, akawa anavinoa kwa kuvisugulisha vyenyewe kwa vyenyewe huku akitembea mbele ya Lobo huku na huko.

  Visu vilivyokuwa vinang'aa kama almasi lakini ni vya siliva, vilipita kifuani mwa Lobo haraka na kuacha alama kama ya X kifuani hapo, na kabla hata Lobo hajalia kwa sababu ya maumivu, akamwagiwa mafuta fulani spesheli ambayo yanauma si kawaida pale yawekwapo kwenye vidonda, lakini ni tiba tosha kwa ambaye anavuja damu.

  "Fuc*** you FISSA. And fuc** you all and your mama."Lobo alitukana matusi mazito ya Kimarekani kwa sababu ya maumivu makali yaliyokuwa yanampata kwa wakati ule. Hakika alikuwa katika mateso, lakini bado hakuwa tayari kusema ukweli wowote.

  "Lobo. Nia yako ni nini na washirika wako ni wakina nani?" Malocha aliuliza kwa sauti kali tena.
  "Nia yangu ni kusafisha pasafi kwa kuweka uchafu. Washirika wangu ni uchafu, umenielewa?." Lobo alijibu kwa hasira kali zilizokuwa zimemjaa moyoni sababu ya kuchanjwa na kuteswa na FISSA.

  "Mkuu, niachie mimi nikamuhoji mlemle." Mubarak alitoa ombi ambalo halikukataliwa kwa sababu majibu ya John Lobo yalikuwa hayana mashiko hata kidogo vichwani mwao.

  "Ooh! Mubah. Umekuja kuchukua ujumbe wako." Lobo alitoa tabasamu pana baada ya kumuona Mubarak kaingia ndani ya chumba kile.
  Mubah hakuongea chochote zaidi ya kuchukua chuma chenye ncha kali kwenye ule mkoba wa kuhifadhia vifaa hivyo vya mateso.

  "Nauliza swali. Nataka jibu sahihi." Mubah alimwambia Lobo huku akikaa kwenye kiti ambacho alikivutia mbele ya Lobo.
  Lobo badala ya kujibu, alitabasamu tena. Tabasamu la kukereketa hata ubongo wa kichaa.


  ITAENDELEA
   
 3. G

  Guasa Amboni JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 6,983
  Likes Received: 7,500
  Trophy Points: 280
  Mwanzo mzuri shusha vitu kwa fujo
   
 4. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  usikonde hii utaipata mpaka mwisho
   
 5. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA TATU

  "Mkuu, niachie mimi nikamuhoji mlemle." Mubarak alitoa ombi ambalo halikukataliwa kwa sababu majibu ya John Lobo yalikuwa hayana mashiko hata kidogo vichwani mwao.

  "Ooh! Mubah. Umekuja kuchukua ujumbe wako." Lobo alitoa tabasamu pana baada ya kumuona Mubarak kaingia ndani ya chumba kile.
  Mubah hakuongea chochote zaidi ya kuchukua chuma chenye ncha kali kwenye ule mkoba wa kuhifadhia vifaa hivyo vya mateso.

  "Nauliza swali. Nataka jibu sahihi." Mubah alimwambia Lobo huku akikaa kwenye kiti ambacho alikivutia mbele ya Lobo.
  Lobo badala ya kujibu, alitabasamu tena. Tabasamu la kukereketa hata ubongo wa kichaa.

  "Mubah. There's two choices. Buy or Sell. (Mubah. Kuna machaguo mawili. Nunua au Uza)" Lobo alimwambia Mubah kwa sauti tulivu. Mubah hakuwa mwenye wasiwasi bali kumtaza John Lobo machoni."The rules of these choices are very simple. (Sheria za haya machaguo ni marahisi sana)" Sauti ya Lobo ilizidi kuchukua nafasi.

  "Acha kazi yako au endelea na kazi yako. Ukiacha kazi, utakuwa umenunua roho za familia yako. Watanusurika na mikono yangu. Ukiendelea na kazi, utakuwa umeniuzia roho za uwapendao. Rahisi sana." Lobo alimaliza kauli yake na hapohapo kwa hasira, Mubah alikandamiza kile chuma chenye ncha kali kwenye paja la Lobo.

  Kabla hata Lobo hajakaa sawa kusikilizia yale maumivu, akapokea konde zito la shavu la kushoto hadi damu zikaruka upande mwingine.
  Tayari Mubah alikuwa kapandwa na hasira kali ambazo zilimpelekea kusimama na kuanza kumpa mateke mazito John Lobo.

  Hata pale Malocha alipomuamuru aache anachokifanya, hakusikia lolote bali ngumi na mateke ndivyo aliona ni suluhu tosha kumpunguzia hasira.
  Ni Beda na Mzee Pujini ndio walimkamata na kumsogeza pembeni asiendelee kufanya 'unyambirisi' aliokuwa anaufanya.

  Kiti alichokuwa kakalishwa Lobo, kilikuwa kimechimbiwa chini hivyo wakati anapigwa alikuwa hadondoki wala kuyumba, hivyo kufanya maumivu kumwingia vilivyo.
  "Fpuu." Lobo alitema damu pembeni baada ya Mubah kuwa anasukumwa pembeni.

  "Mtoeni nje." Sauti ya kwenye spika ilisikika ikiamuru Mubah atolewe nje.
  "Mubah." Lobo alimuita Mubah kabla hajatoka. Mubah akageuka kumuangalia yule mtu aliyemuita.
  "Sijabadili maamuzi yangu. Anza kuhesabu sasa, unamasaa ishirini na nne kufanya nilichokwambia.

  Angalia saa yako, au angalia ile pale." Lobo alimuonesha kwa macho saa iliyokuwa ukutani. Mubah akaiangalia kisha akarudisha macho yake kwa Lobo.
  "Tick Tock." Lobo aliongea sauti ya mshale wa saa na kumfanya Mubah ajikurupue toka kwenye mikono ya Mzee Pujini na Beda kwa ajili ya.kwenda kumpa kisago tena Lobo. Lakini hakufanikiwa hilo kwa sababu tayari alikuwa kwenye mikono imara.

  "Unafanya nini Mubah." Malocha alimuuliza kwa hasira Mubah baada ya kutolewa katika kile chumba.
  "Ni hasira mkuu. Kaniambia maneno ya ajabu sana yule mjinga."
  "Hasira za kijinga hizo.

  Unadhani wakina Beda wangekuwa wanaendekeza hasira kwa kutukanwa na kutishiwa, watuhimiwa wangekuwa wanapona?" Mubah akainamisha kichwa chini na kujiona amekosa mbele ya Mkuu wake.

  "Embu twendeni ofisini." Malocha aliamrisha na hakuna aliyekataa kati ya Lisa na Mubah ambao walikuwa kwenye kile kioo wakifatilia mateso ayapatayo Lobo kwa makini na ukaribu.

  BAADA YA NUSU SAA.
  Ni king'ora kilichokuwepo ndani ya Shirika lile la siri, ndicho kilichowashtua Lisa, Malocha na Mubah waliokuwa ofisini wakijadili njia mbadala za kumfanya Lobo aongee.

  Kabla hawajajua sababu ya king'ora hicho kulia, mara mlango wa kioo wa ofisi ya Malocha, aliingia mfanyakazi mmoja akiwa kavaa "headphones" masikioni zilizounganika na kipaza sauti moja kwa moja. Ukimuona ni kama mtangazaiji wa radio fulani, lakini sio.

  "Mkuu. Lobo katoroka. Na kawaua Beda na Mzee Pujini." Taarifa hizo zikawakurupua wale vijana wa kazi kwa pamoja na kuanza kuelekea kule walipomuacha John Lobo.

  Wakaingia moja kwa moja kwenye kile chumba ambacho walimuacha Lobo, lakini macho yao yalitua kwenye miili ya wachapa kazi wao ikiwa maiti, tena si maiti pekee, bali maiti za kutisha.

  Mzee Pujini alikuwa kachomwa na kisu kirefu walichokuwa wanatumia kutesea watuhumiwa. Kisu hicho kiliingia kwenye jicho lake la kulia na kubaki kimenata hapohapo.

  Haikuwa hivyo pekee, bali pia shingo yake ilikuwa imechinjwa na alama ya mkato huo wa kisu, ilijitokeza na kuonesha koromeo lake.
  Picha nyingine ni ya Beda, msaidizi wa Mzee Pujini.

  Shingoni, upande wa kushoto kulikuwa na tobo refu kama liliingizwa msumari wa nchi kumi hadi kumi na mbili. Katika paji la uso, pia kulikuwa na kisu kimenatia hapo. Ilikuwa inatisha kuangalia mara mbili.

  Walipoanza kutazama huko na huko ndani ya FISSA, waligundua pia kuwa wafanyakazi wao saba walikuwa wameuawa kwa njia kama ambazo Beda na Mzee Pujini walivyokufa. Ni visu na mikasi ndivyo vilivyohusika kuwamaliza wafanyakazi hao.

  Na kuna maiti ilikutwa haina mavazi. Ni wazi John Lobo alivaa mavazi ya maiti hiyo kabla hajaenda kwenye Jet P112, ndege ya kivita inayokimbia kuliko zote duniani (Nimeilezea kwenye simulizi ya Jina). Na kutoroka nayo.

  "Nadhani alijikamatisha ili aje kuiba hii ndege." Malocha aliongea kwa huzuni baada ya ndege hiyo ghali kuibwa na Malocha.
  Ni ndege ambayo Afrika zipo mbili tu! Tanzania na Afrika Kusini.
  Wakati anaongea hayo, yeye na wafanyakazi wengine, walikuwa wanatazama mkanda wa jinsi Lobo alivyokuwa anatoroka.

  Alionekana akivunja mkono wa kiti kwa kujitutumua, na baadaye akachomoa mkono wa kulia na kile kilichomshika mkono wakati yupo kwenye kiti, kilibaki kwenye mkono huo kikiwa na msumari mrefu uliokuwa umekamata kiti.

  Mzee Pujini alipokuwa anataka kwenda kumshika Lobo, Lobo akawahi kisu kikali alichokirusha kiustadi na kwenda kumchoma kwenye jicho. Kabla ya Mzee yule hajakaa sawa wala kusikilizia yale maumivu, Lobo tayari alishadaka kisu kingine na kuruka sarakasi ya chinichini na kisha akamcharanga mzee yule shingo yake.

  Wakati huo Beda alikuwa akihangaika kufungua mlango lakini alishindwa kwa sababu ya kutetemeka kwa woga.
  Wakati yupo hapo mlangoni, alisikia sauti ya Lobo ikimwambia Mzee Pujini kuwa alimuahidi kuwa atamuua wa kwanza.

  Beda akafanya kosa kubwa kugeuka na kuangalia tukio la mwenzake kufa, kwani kile kisu kilichopita shingoni kwa Mzee Pujini, ndicho kilichorushwa na kutua sawia kwenye paji lake la uso wake. Kabla hajadondoka, Lobo alimuwahi na kuingiza shingoni ule msumari uliokuwa umeshika kile kishikio cha kiti. Na hapohapo akauchomoa kwa fujo huku ukimuacha Beda akidondoka kama mzigo wa gunia la maharage.

  Na baada ya picha ile mbaya ya mauaji ya Beda na Mzee Pujini, Lobo alionekana akienda kwenye mlango wa chumba kile na kubonyeza namba maalumu ambazo hufungulia mlango ule, na baada ya kubofya, mlango ukafunguka.

  "Inaonekana anajua mengi sana ndani ya FISSA. Hadi namba za siri za kufungulia ule mlango." Malocha alionesha wazi mshangao wake wakati video ile ukiendelea kucheza.

  Lobo akatoka nje ya chumba kile lakini baada ya dakika kama moja akarudi tena na kisha akachukua visu kadhaa kwenye ule mkoba maalumu wa kuhifadhia visu hivyo.

  Hakuishia hapo, pia akaenda kwenye mkono wa kushoto wa Mzee Pujini na kumvua saa yake. Akaangalia kama inaenda sawa na ya ukutani, na aliporidhika, akaenda karibu na kamera iliyokuwa inachukua ule mkanda wanaouangalia wakina Malocha muda ule.

  Kisha akatoa ishara kwa kutembeza kidole kama ufanyavyo mshale wa saa, na mdomoni kwake alionekana akitaja maneno yasemakayo TICK TOCK, hiyo ni sauti ya mshale wa saa.

  Baada ya kitendo hicho, uso wa Mubah ukabadilika na kujawa hofu zaidi kwani Lobo ujumbe ule alikuwa anamuelekezea yeye. Mubah akawa hana raha hata kidogo hasa baada ya kuona mauaji ya hatari anayoendelea kuyafanya Lobo.

  Visu alivyovichukua mle 123F6 vilikuwa vinarushwa kiustadi na kuwakuta baadhi ya wafanyakazi ambapo mmojawapo alivuliwa nguo, na nguo hizo, Lobo akazieweka mwilini mwake kabla hajakwea ndege aina ya Jet P112 na kuiondoa kwa kasi toka kwenye shirika lile la siri la kipepelezi.
  ****

  "Kuna kitu kinaendelea nchini kwetu kikubwa sana. Haiwezekani huyu Lobo akawa anajua ramani nzima ya jengo letu. Lazima kuna mtu toka humu au nje, anatoa siri za FISSA. Tunatakiwa kumjua na kumkamata mara moja." Malocha aliongea kwa hasira na kugonga meza moja kubwa ambayo ipo katika chumba maalumu cha mikutano ndani ya FISSA.

  Mkutano huo uliitishwa na Malocha baada ya kumaliza mkanda mzima aliokuwa anaufanya Lobo.
  Wafanyakazi wapatao ishirini, ambao wote ni wakuu katika idara fulani, waliitwa kujadili suala ambalo limetokea saa moja lililopita.

  Hakuna aliyejaribu kuchangia mjadala ule wakati Malocha akishindwa kuzuia hasira zake na kuanza kuiadhibu meza.
  "Mkuu." Sauti moja iliita toka mlangoni. Ni yuleyule aliyekuja kuwapa taarifa kuwa Lobo katoroka. Na sasa alifungua mlango wa chumba kile kutoa taarifa nyingine.

  "Mr. President anakuhitaji kwenye simu." Jamaa alitoa taarifa na kufunga mlango ule na kwenda eneo husika kwa ajili ya kuendelea na kazi yake.Kwa kuwa simu ya mezani ilikuwa mlemle kwenye kile chumba, Malocha aliipokea na kuweka sauti ya juu ili kila mmoja asikie.

  "Heshima yako mkuu." Malocha alisalimia baada ya kuipokea simu ile.
  "Ni nzuri. Nasikia Lobo kaondoka na Jet P112." Sauti ya Rais iliitikia salamu na kuunganisha na swali.

  "Ndio, lakini tutaipata tu Mkuu." Malocha akuongea kwa sauti ya kukata kata.
  "Mnajua ndege hiyo wanaenda kufanyia kazi gani? Mbona mmefanya uzembe wa hali ya juu nyie washenzi" Rais alifoka kwa sauti kali.
  "Mnajua azimio la kuchukua ndege hiyo.

  Vipi wakienda kulipua nchi za watu huko!? Mnadhani Tanzania tutapona? Sasa nasema hivi, ndani ya wiki moja, ndege hiyo iwepo humo. Vinginevyo, watu mtakuwa hamna ajira na maisha yenu yataishia jela. Fanya nachokwambia Malocha." Rais akakata simu ile bila hata kusikiliza upande wa pili.

  "Nadhani mmesikia. Sasa ni kazi tu." Malocha aliongea kwa unyonge huku akitembea kuelekea mlango wa kutokea, lakini kabla hajafanikiwa kutoka, yule mtoa taarifa akaingia tena na taarifa mpya.

  "Prince Mubarak. Simu yako. Kuna mtu anashida na wewe." Baada ya taarifa hiyo, jamaa akaondoka na Mubah bila kuchelewa akaenda kwenye ileile simu na kufanya kama Malocha alivyofanya.

  Malocha akiwa anaelekea kutoka, alijikuta akisimama mlangoni baada ya kusikia sauti itokayo kwenye simu ile.
  "Haloo Mubah. John Lobo hapa." Lobo alijitambulisha na kumfanya Malocha ageuke na kusimama wima akimwangalia Mubah.

  "Nipo kwako hapa. Na mchumba wako ananitibu majeraha mliyonipa huko. Oooh! Ana nywele laini sana, na zinanukia pia." Lobo aliongea kwa sauti ya chini huku pua zake zikisikika zikinusa kitu.
  Baada ya kunusa huko, sauti ya kike ya mtoto ilisikika ikiwa na furaha kwa kulitaja jina la Uncle Mubah.

  "Usijali Mubah. Mama, Mchumba wako, dada na wajomba zako wapo salama. Huyu mjomba mwenye mwaka mmoja, ni mzuri sana Mubah. Fanya chaguzi sahihi, uza au nunua roho zao.

  Acha kazi yako au endelea na kazi yako, chagua ni lako Mubah. Yamebaki masaa ishirini. Tick Tock." Baada ya maneno hayo toka kwa Lobo, simu ikakatwa.
  "Nifanye nini?" Swali la kwanza kuliuliza Mubah baada ya simu ile kukatwa. Alikuwa kama hajielewi pale alipouliza swali lile.

  "Hiyo ndio nafasi pekee ya kumkamata huyu mbwa na kumfikisha mahakama za uharifu duniani." Malocha aliongea hayo huku akirudi katika sehemu yake aliyokuwapo mwanzo.

  "Tutaweka ulinzi wa kutosha katika nyumba yako, hakuna ambaye ataingia ndani wala kusogelea eneo lile. Snipers na walinzi wenye mbwa wawezao kunusa kilometa kadhaa, watazagaa kila eneo la mtaa wako. Hakuna atakayeumia siku hiyo. Usijali kuhusu hilo." Malocha aliongezea kuhusu mkakati wake na kumtoa hofu Mubah ambaye alikuwa akihisi kama anataka kufa.

  "Hapana mkuu. Familia yangu ndio kila kitu kwangu. Kazi si kitu, naomba niache kazi hii mara moja kuikoa familia yangu. Huyu si mtu wa maskhara hata kidogo, ni hatari kama moto. Naomba niachane na hii kazi, naombeni sana." Mubarak alijikuta akiomba kuacha kazi sababu ya ule mkwara mzito.

  "Utakuwa mjinga kama ukiacha kazi ka sababu ya mtu mmoja kama Lobo. Sikiliza Mubah, tunakuhakikisha usalama wa familia yako. Pale walipo, tunawatoa kisiri siri na kuwapeleka nyumba nyingine zenye usalama zaidi ya pale. Na hapo kwako ndipo tutaweka watu wenye sura kama za familia yako lakini wenye uwezo wa kupambana.

  Usiogope kuhusu maisha ya familia yako, watakuwa salama." Mubah akashusha pumzi ndefu kama ahueni ya maneno yale toka kwa Malocha, mkuu wake wa kazi.
  "Asante mkuu." Mubah akashukuru na baada ya hapo,mkakati kabambe ukaanza kupangwa na wanamkutano ule.
  ****

  "Lakini Mkuu, mkumbuke huyu Lobo si mtu wa kuchezea. Na mbaya zaidi tunahisi humu ndani kuna vibaraka wanaosaidiana naye. Huoni kama tutakuwa tunaiuza familia ya Mubah kwa bei rahisi kabisa." Lisa alikuwa ofisini kwa mkuu wake baada ya kutoka kwenye ule mkutano mfupi.
  Alienda katika ofisi ile ili kumpa ushauri kama huo Bwana Malocha.

  ===============
  ================================

  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA NNE

  "Utakuwa mjinga kama ukiacha kazi ka sababu ya mtu mmoja kama Lobo. Sikiliza Mubah, tunakuhakikisha usalama wa familia yako. Pale walipo, tunawatoa kisiri siri na kuwapeleka nyumba nyingine zenye usalama zaidi ya pale.

  Na hapo kwako ndipo tutaweka watu wenye sura kama za familia yako lakini wenye uwezo wa kupambana. Usiogope kuhusu maisha ya familia yako, watakuwa salama." Mubah akashusha pumzi ndefu kama ahueni ya maneno yale toka kwa Malocha, mkuu wake wa kazi.

  "Asante mkuu." Mubah akashukuru na baada ya hapo,mkakati kabambe ukaanza kupangwa na wanamkutano ule.
  ****

  "Lakini Mkuu, mkumbuke huyu Lobo si mtu wa kuchezea. Na mbaya zaidi tunahisi humu ndani kuna vibaraka wanaosaidiana naye. Huoni kama tutakuwa tunaiuza familia ya Mubah kwa bei rahisi kabisa." Lisa alikuwa ofisini kwa mkuu wake baada ya kutoka kwenye ule mkutano mfupi.

  Alienda katika ofisi ile ili kumpa ushauri kama huo Bwana Malocha.
  "Usijali Lisa. Hilo pia nimelifikiria kwa kina na ndio maana pale mkutanoni, nimesema sehemu ambayo tutaificha familia ya Mubah. Lakini kiukweli, sipo huko ambapo tutawapeleka. Wataenda sehemu nyingine kabisa." Malocha alimtoa wasiwasi Lisa huku akimpa vipande baadhi ambavyo walivifanya katika ule mkutano wao.

  "Okay. Hapo sawa. Na kingine tukumbuke kuwa yule pia ni Sniper, nadhani unakumbuka sana alichokifanya nyuma. Tuwe makini zaidi tukiwa maeneo ya mtaa ule. Kila baada ya kilometa mbili, kuwe na mlinzi juu na chini. Hiyo itasaidia sana."

  "Usijali Lisa, nimekuelewa na nitafanyia kazi hilo." Malocha alionesha shukurani zake kwa Lisa ambaye baada ya kutoa ushauri huo, alitoka ofisini mle na kuelekea kwa Mubah ambapo napo alikuwa anamtia moyo na kumueleza mikakati waliyoipanga.
  ****

  Saa tatu asubuhi, yakiwa yamebakia masaa kuna na matano ili ahadi aliyotoa Lobo itumie, gari moja nyeusi ilisimama nje ya nyumba moja kubwa kiasi na baada ya sekunde kadhaa, alishuka kijana Mubah na kuelekea katika nyumba hiyo.

  Katika shirika la siri la kipelelezi, sehemu ambayo Mubah anafanyia kazi, si ruhusa kwa mfanyakazi yeyote kutoka ndani ya shirika hilo mida mibaya hasa usiku. Na ndio maana hata Mubah alipopokea simu ya matatizo ya familia yake, hakuondoka hadi asubuhi hiyo ambayo kwake ilikuwa kama mwaka kuifikia.
  "Oooh! Mubah.

  Ulikuwa wapi mwanangu." Mama yake Mubah ambaye alionekana wazi uzee umemchukua, alimkimbilia kwa shida mwana wake kabla ya familia nzima nayo haijafanya hivyo.
  "Usijali mama. Nipo salama kabisa na nimekuja kwa ajili yenu." Mubah aliwapa moyo ndugu na familia yake.

  "Jana alikuja mtu anaumwa, akamuomba wifi amsaidie kutibu majeraha. Sisi tulikuwa tunamwogopa, ila akasema anafahamiana na wewe. Na hata baadae alipopiga simu, tukasikia sauti yako. Sema akaenda kuongelea nje na baada ya kurudi alimuomba wifi afanye alichokiomba mwanzo. Yaani amtibu yale majeraha."

  Dada wa Mubah alitoa taarifa ambazo kwa Mubah alibaki akiwa kakodoa macho tu. Ye' alidhani Lobo alikuja na kuitishia amani familia yake, na kumbe alikuja kwa njia za kiutu.
  Akakuna kichwa chake kijana huyu huku akishindwa afanye nini kwa wakati ule.

  "Pia alipoanza kuondoka aliacha ujumbe ule pale." Dada wa Mubah alisonta kidole chake ukutani na kuonesha ujumbe aliouacha John Lobo.
  Alisogea karibu maana ni kama alikuwa hauoni japo ulikuwa na maandishi makubwa meusi kwenye karatasi nyeupe iliyochomwa kwa kisu kwenye ukuta huo wa nyumba iishiyo familia ya Mubah.

  Ujumbe ulisomeka "TICK TOCK" na kwa juu yake saa ya ukutani ya Mubah ilikuwa ikienda taratibu kwa mlio huo wa tick tock. Mubah akahisi kuchanganyikiwa.

  "Anko. Anko yule mwingine kanipa hii hapa na ......" Kabla ya yule mtoto wa dada yake, mtoto mwenye umri wa miaka saba hadi nane hajamaliza kauli yake, Mubah tayari alimpora kile kitu ambacho alikuwa kakishika yule mjomba wake.
  Kilikuwa ni kibanio kizuri cha nywele kilichonakishiwa na madini ghali ya dhahabu.

  Mjomba yule wa Mubah alikuwa anafuraha kila alipokiangalia, lakini kitendo cha Mubah kumpora na kuanza kukikanyaga kanyaga, kikafanya yule mtoto asiseme kitu kingine ambacho kapewa. Alikuwa kavaa pambo zuri katika nkono wake, pambo hilo pia alipewa na John Lobo.

  Mjomba wa Mubah akakimbilia chumbani kwa mama yake na huko safari ya kilio ikachukua nafasi yake. Aliona kama Mjomba wake kamkatili sana nafsi yake kwa kile kitendo. Watoto bwana.

  "Naomba mjiandae. Leo saa mbili usiku tutaondoka katika nyumba hii. Tupo katika hatari kubwa sana. Na ninaomba, jirani au mtu yeyote asijue ni wapi au muda gani tunatatoka hapa. Tupo katika hatari." Mubah akiongea huku uso wake ukiwa na mashaka makubwa sana hali iliyofanya familia yake kuzingatia maneno yake.

  Familia nzima ilimjua Mubah kama askari wa Tanzania. Hivyo aliposema maneno hayo, kila mmoja akaamini kuna kitu cha hatari hasa pale walipovuta sura ya yule mtu aliyekuja usiku wa jana yake.

  "Usiwe na wasiwasi dear. Mambo yote tutayafata." Ilikuwa ni sauti ya Zakia Bin Ashib ikimfariji mpenzi wake walipokuwa chumbani wakipanga baadhi ya vitu vyao kwa ajili ya kuondoka usiku huo.

  Maneno hayo ya faraja, yalikuja pale Mubah alipomueleza mkasa mzima uliomsibu siku ya jana yake tangu alipoanza kukimbizana na Lobo hadi unyama alioufanya kule FISSA.

  Ndani ya maongezi hayo, Mubah hakuthubutu kuongea kuhusu ndege iliyoibiwa au mahali ambapo anafanyia kazi.
  Zakia Bin Ashib, kila kukicha alikuwa anamuomba mpenzi wake amueleze ni wapi anafanyia kazi zake, lakini Mubah alikuwa anakataa kusema ukweli kwa sababu ya masharti ya shirika lake.
  ****

  Saa mbili usiku, kwa kutumia handaki dogo lililo katika sebule la Mubah, familia yote iliingia huko na kutokezea katika zizi la ng'ombe, kilometa kadhaa kutoka kwenye nyumba ya Mubah. Hakuna aliyewahi kufikiria kuwa nyumba ya Mubah inahandaki hilo. Awe mama yake au mchumba wake.

  Hivyo kitendo cha wao kuingizwa huko na kutokea kwenye zizi la ng'ombe, likawa ni hadithi nyingine ya kusisimua ambayo Mubah alipaswa kuilezea.
  Baada ya kuibukia zizini huko, gari moja ya kimarekani, ilifunguka milango yake na watu idadi ya familia ya Mubah, walijitojeza.

  Macho ya familia ya Mubah ikazidi kushangazwa hasa wale watu wanavofanana nao. Watu wale, wakaipita familia ya Mubah na kuingia katika handaki lile lile ambalo walitokea familia ile.

  Familia ya Mubah, ikapanda na gari ile na safari ya kwenda pasipojulikana ikachukua nafasi yake wakati huo Mubah alirudi nyumbani kwake na kuanza kutoa maelezo yote yanayofaa.

  Huko nje ulinzi ulikuwa ni wa hali juu kuliko hata ule ambao huwekwa rais wa nchi fulani akifika nchini.
  Wapelelezi walikuwa wakipita katika mtaa huo kama wapita njia na hakuna ambaye alihisi kuwa wale ni wapelelezi. Wadunguaji (Snipers) walikuwa kila upande katika eneo lile wakiwa na bunduki zao maalumu kwa ajili ya kudungulia mtuhumiwa wao.

  Huko FISSA, Lisa na Malocha walikuwa wanawapa taarifa watu wao wa kazi hasa kwa picha ambazo zilikuwa zinatumwa kwa satellite. Kila mtu tofauti waliyemtilia mashaka akipita, FISSA walitoa taarifa kwa kikosi kazi chao kilichoongozwa na Mubah.

  Hatimaye zikabaki dakika kumi na tano za ahadi ya Lobo kutimia. Kila mtu moyo ukawa unamdunda kwa sababu mtu wanayemtega si mtu mdogo. Ni eidha wamkamate hai au akiwa maiti. Lakini je!?

  Uhakika wa kumkamata upo? Swali hilo ndio likafanya mioyo ya wachapakazi wale kutokuwa na amani.
  Mbwa wasiojua kubweka bali kufanya kazi yao, nao wakawa wananusa kila sehemu walipopitishwa. Ulinzi ulikuwa mkubwa haswa. Mtaa mzima anaoishi Mubah ulitapakaa ulinzi wa hali ya juu.

  Zikiwa zimebaki dakika saba za jambo alilopanga Lobo kutimia, simu ya Mubah ilianza kuita mbele ya familia yake ile mpya. Namba ya mpigaji haikuonekana bali kuandika neno 'private call'.

  Mubah akawapa ishara wale watu waanze kutimiza maadhimio waliyoyapanga.
  Bila kuchelewa, meza kubwa ya mle ndani ikafunuliwa na watu wote wakasogea pale mezani na kutazama mahanjumati na mapochopocho kadhalika yaliyoandaliwa kiufundi na wafanyakazi wa FISSA.

  Wakaanza kusali kwa sauti na ndipo Mubah akasogea pembeni kidogo na kupokea simu ile.
  "Hallow." Mubah akaita baada ya kupokea simu.
  "Heloo Mubah. Niambie kamanda wangu." Sauti ya Lobo iliitikia upande wa pili na wakati huo wale waliondaliwa kupambana na Lobo, walizidi kupamba moto kuombea chakula.

  "Stupid Lobo." Mubah akatoa tusi dogo.
  "Mmmh! Siku hizi mmeokoka Mubah. Mnasalia chakula kwa kukemea kwa jina la Yesu. Muislamu halisi kama wewe!?" Lobo aliongea na kucheka sana na hapohapo wale washirika wa Mubah walikatisha sala zao na kugundua kuwa walikuwa wanasali Kikristo wakati familia ya Mubah ni Waislam.

  Japo Mubah alikuwa mbali nao, lakini wao pia waliyasikia yale maongezi kwa kutumia vinasa sauti vilivyokuwa masikioni mwao kama vishikizo.
  "Okay. Ondoa shaka Kamanda, siwezi kuingilia maisha uliyoyaanza na familia yako ya kujibambika.

  Nipo hapa kukukumbusha kuwa zimebaki dakika tano na sekunde kadhaa ili ahadi yetu itimie. Huku ulipoileta familia yako, nadhani panafaa sana kufanya kazi yetu. Na kingine, kabla sijafanya chochote kwa huo ugeni ulioniletea kwako, naomba utoke nje na ushuhudie mara ya mwisho mtaa wako. Toka, waweza kuniona navyoua vimbwa vyenu." Lobo akamaliza kuongea lakini hakukuta simu.

  Mubah akawa kama kachanganyikiwa, akatoka nje kasi na kuanza kuangaza huko na huko, akasogea hadi barabarani na kuzidi kushangaa. Aliweza kuwaona wapelelezi wenzake na wakamuoneshea ishara ya kumuuliza vipi? Lakini Mubah ni kama alikuwa kapandwa na kichaa na wakati huo simu ikiwa sikioni kwake.

  "Ha ha hahahaaa. Mubah, Mubah, Mubah. Bado dakika mbili. Embu ongea kwanza na mjomba wako." Lobo alisikika tena kwenye simu ile aliyoipiga.
  "Ankoo tusaidie tumefungwa kamba na jambaziii." Mjomba wa Mubah alipiga kelele kwa nguvu na kumfanya Mubah ahisi kama anamabawa lakini hawezi kupaa kwenda kutoa msaada. Akabaki katikati ya barabara na simu ikiwa sikioni kwake.

  "Ooh! Nasikia pia ulikanyaga-kanyaga kibanio changu. Zawadi nzuri kabisa kutoka Malyasia. Nimemletea anko wako lakini umekiharibu. Ila hamna tatizo, bali tatizo litakuwepo kama pale chini ulipokikanyagia kitabaki palepale. Najua kipo palepale, embu nenda kakiangalie." Mubah akatoka mbio tena na kuingia tena nyumbani kwake. Hapo alichokishuhudia, hakika hakuwahi kukifikiria katika kichwa chake.

  Miili minne, akiwepo na yule mtoto ambaye walimfanya kama mjomba wa Mubah ilikuwa imelala kifudifudi kwenye viti walivyokalia huku moshi mdogo ukiwatoka midomoni mwao. Nyuso zao zilijikunyata na kuwa kama za wazee wa miaka mia moja. Damu ilikaushwa katika miili yao kwa kutumia sumu kali inayosambaa kwa hewa.

  Mubah alipoangalia sehemu alipokanyagia kile kibanio, alikuta kuna majivu machache ambayo yalitokana na kile kibanio kuungua.
  "Nadhani umeona. Sikutaka kukuua wewe. Na hata hicho kimdoli mlichokifanya ni kitoto kidogo, nacho kingekuwa na uhai, ningeua tu! Na nitakiua hichi nilochonacho huku baada ya dakika tatu kupita." Lobo aliongea kwa sauti iliyojaa chuki.

  "Hiyo sumu inatoka kwenye madini ya yellowstone. Madini yafananayo na almasi sema yenyewe ni ya njano na yanayeyuka. Husambaa kwa sekunde thelathini baada ya kuchomwa moto na hupotea kwa sekunde kumi na tano baada ya kusambaa. Kibanio hicho nilieweka jiwe dogo sana la madini hayo.

  Na nilitega kifyatulio ambacho kikifyatuka, hutengeneza moto. Nimefanikiwa hilo Mubah, asante kwa kuniletea wateja hao. Bado dakika mbili." Lobo akamaliza kuongea na kuacha simu hewani ili asikie upande wa pili.
  "Nooooooo. Don't do that Lobo. Please." Mubah alijikuta akipiga kelele ya nguvu huku akijaribu kuomba msamaha.

  Kelele hizo zikawafikia walinzi wa nje nao wakakimbilia ndani wote, hata wale wadunguaji nao ikabidi kushuka kule juu haraka na kwenda ndani kutazama kile kinachoendelea. Walichokikuta ndani, hakika kiliwatoa machozi na kuwaacha katika mshangao.

  Sasa hivi miili ile ilikuwa ikipukutika kama majivu ya karatasi na mwisho wake yakabaki mafuvu yamekaa kwenye viti.
  "Sasa naweza kukusikiliza Mubah, unadakika moja. Toka nje na mtu yeyote asikuone kama umetoka. Nataka nikuoneshe kitu." Sauti ya Lobo ilisikika ikimuongelesha Mubah kwenye simu.

  Mubah akafanya kama alivyoambiwa.
  "Sogea mbali na nyumba yako. Na itazame kwa macho ya umakini, utaona kitu cha kukupendesha. Zimebaki sekunde kumi na tano muda wetu uishe." Lobo alitoa ombi ambalo Mubah alilifanya haraka na kukazia macho yake kwenye nyumba yake ambayo ndani yake kulikuwa na wafanyakazi wenye uhai wapatao kumi na moja.

  "Tano, Nne, Tatu." Lobo akaanza kuhesabu sekunde zilizobaki hadi akafikia moja, kisha sifuri.
  Macho ya Mubah yakajawa na taharuki ya ajabu. Hakuwahi kufikiria katika maisha yake kuwa kuna siku atashuhudia kile anachokishuhudia kwenye nyumba yake. Alishazoea ni kwenye filamu za kivita tu! Ndio awezapo kuona yale mambo.

  Lakini sasa anajionea kwa macho yake yale ambayo alikuwa anayaona kwenye filamu.
  Nyumba yake ililipuka yote na kuteketea kama vile uonavyo kwenye filamu ndege au meli inapopigwa bomu. Nyumba ikazidi kuteketea na kuteketea hadi vile vilivyomo ndani.

  Mubah akapiga magoti na kulia kwa sauti huku akipiga chini ngumi kadhaa lakini bado hakukuta simu bali kusikiliza kilichokuwa kinataka kujiri.
  "Woooou. I like that sound of boom, yoo. (Waau. Nimeipenda hiyo sauti ya buum, yoo)" Lobo alisikika akiongea hayo kwenye simu baada ya ule mlipuko mkubwa kutokea kwenye nyumba ya Mubah.

  "Please Lobo, naomba uiache familia yangu. Nakuomba Lobo, nitaacha kazi kama utakavyo." Mubah akikuwa anaomba msamaha huku kapiga magoti katikati ya barabara ya lami iliyokuwa inapitwa watu huku na huko kukimbia ule mshikemshike wa bomu.

  "Too late Mubah. Umechelewa mwenyewe kufanya chaguo lililo sahihi na mimi huwa sikwepeshi kauli yangu." Lobo aliongea hayo na hapohapo sauti ya 'kitoto kichanga' ikaanza kulia.


  ITAENDELEA
   
 6. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  itaendelea saa 18:00
   
 7. G

  Guasa Amboni JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 6,983
  Likes Received: 7,500
  Trophy Points: 280
  Ipo vizuri inasisimua hongera sana kuleta uzi huu.
   
 8. KENZY

  KENZY JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2016
  Joined: Dec 27, 2015
  Messages: 6,253
  Likes Received: 5,241
  Trophy Points: 280
  HE! nimeipenda nangoja muendelezo:D
   
 9. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA TANO

  Mubah akapiga magoti na kulia kwa sauti huku akipiga chini ngumi kadhaa lakini bado hakukuta simu bali kusikiliza kilichokuwa kinataka kujiri.
  "Woooou. I like that sound of boom, yoo. (Waau. Nimeipenda hiyo sauti ya buum, yoo)" Lobo alisikika akiongea hayo kwenye simu baada ya ule mlipuko mkubwa kutokea kwenye nyumba ya Mubah.

  "Please Lobo, naomba uiache familia yangu. Nakuomba Lobo, nitaacha kazi kama utakavyo." Mubah akikuwa anaomba msamaha huku kapiga magoti katikati ya barabara ya lami iliyokuwa inapitwa watu huku na huko kukimbia ule mshikemshike wa bomu.

  "Too late Mubah. Umechelewa mwenyewe kufanya chaguo lililo sahihi na mimi huwa sikwepeshi kauli yangu." Lobo aliongea hayo na hapohapo sauti ya 'kitoto kichanga' ikaanza kulia.

  "Muache mwanangu we kafiri. Na kwambia muache." Sauti ya dada wa Mubah ilisikika na kupenya kwenye ngoma za Mubah. Wakati huo sauti ya.kichanga iliendelea kulia na mara ikakata ghafla baada ya mlio mkali wa bastola kutoka.
  "Nooo." Sauti ya dada wa Mubah ilisikika mara moja na baada ya hapo haikusikika tena.

  Lobo akiwa anachalaza mluzi usioeleweka ni wa wimbo gani, akaongea kwenye simu ambayo Mubah alikuwa bado hajaikata.
  "Dada yako kazimia baada kuona mwanaye mdogo nikitoboa kichwa chake kwa risasi yangu. Hahahahaaa. Nasikitika hutoona maiti zao kwa macho yako bali utaona picha za maiti yao.

  Naua na kupiga picha." Lobo alimpa taarifa Mubah ambayo ilimzidishia maumivu moyoni.
  "Lobo tafadhali, nisamehe. Kuwa na utu we' mtu. Naomba uniachie familia yangu." Mubah aliongea kwa sauti ya kitetemeshi iliyojaa kilio.
  "Ankoo tuokee." Sauti ya mjomba kipenzi wa Mubah ilisikika.

  Mubah akahisi mwenye kutaka kufa lakini hakufa bali alizidi kushikilia simu yake sikioni.
  "Anko kwa heri. Labda tutakuja kuonana tena. Nakupenda sana ank....." Yule mjomba wa Mubah hakumaliza kuongea kitu akamezwa na mlio wa bastola ya John Lobo na hapohapo hakusikika tena.

  Mubah alilia kwa sauti ya juu ambayo ilimfanya adondoke kwenye lami alipokuwa kapiga magoti na wakati anadondoka, akaliona gari moja jeusi likipita karibu yake na mtu aliyekuwamo mle ndani, alimuangalia kisha akatabasamu kwa tabasamu pana kabla hajafunga kioo cha upande wake kilichokuwa cheusi.

  Sura ile ya kiume haikuwa ngeni kwake, lakini alisahau kaiona wapi. Na wakati huo alikuwa hana nguvu zozote za kuinuka pale alipo ili akimbize lile gari. Badala yake, alilala pale chini taratibu huku akianza kuona giza likitanda usoni pake.

  "Huyu nimeingiza bastola mdomoni na kufumua ubongo wa nyuma kwa bastola yangu. Ha ha haaa raha sana kuua." Hiyo ndiyo sauti ya mwisho ya kutoka kwa Lobo ambayo Mubah aliisikia.
  Fahamu zikapotea kwa sababu ya machungu tele yaliyojengeka moyoni mwake.
  ****

  Ilichukua karibu saa moja kwa Mubah kuamka na kushtuka tena baada ya kukumbuka yale ya nyuma. Tayari alikuwa yupo ndani ya FISSA baada ya wafanyakazi wenzake kuja kumuokota pale chini alipokuwa kazimia.
  "Husna, Husna, Husna, Husnaaa. Kweli umeenda uncle wangu niliyekupenda kuliko wote nyumbani?

  Nitacheka na nani tena, nani atanifurahisha pale niwapo na machungu. Ooh! Mungu wangu nisaidie." Mubah alikuwa akilia kwa uchungu mbele ya wafanyakazi wengine ndani ya FISSA.

  "Nyamaza Mubah. Pole sana. Hakuna ambaye hana hayo machungu. Tuliizoea familia yako na tuliwazoea wafanyakazi wetu, lakini wote hatunao tena. Inatuuma sana." Dada mmoja mrefu na mweusi lakini mwenye mvuto wa aina yake, alijaribu kumbembeleza Mubah aliyekuwa akilia kama mtoto mdogo.

  "Atalipa tu huyu mbwa. Nitamuua kwa risasi zangu. Nitamuua Lobo na washirika wake wote. Nishamuona mmoja, nitamsaka na kumuadhibu pumbavu yule." Mubah aliongea kwa hasira huku akinyanyuka katika kitanda cha dispensari iliyopo mlemle ndani ya FISSA.

  Akashika kitasa cha mlango wa kituo kile cha afya na kutoka humo kituoni na kuanza kuelekea ofisi za kipepelezi hasa kule zinapokaa kamera maalumu za kufatilia mienendo yote ya kazi za FISSA.

  "Niwekee mkanda wenye tukio zima la pale nyumbani." Mubah aliongea mbele ya mwanakaka mmoja aliyekuwa anacheza na kompyuta za mle.
  Yule jamaa hakuwa na kipingamizi hasa kwa kuwa ule mkanda unamgusa sana aliyemuamuru auweke.

  Akauweka na kisha ukaanza kucheza matukio yote yaliyokuwa yanaendelea siku hiyo kabla Mubah hajazimia.
  Mkanda huo ukaenda hadi mahali ambapo nyumba ya Mubah ilipolipuliwa.
  "Rudisha hapo kidogo." Mubah akamwambia maneno yale yule opareta. Jamaa bila ubishi akarudisha sehemu ambayo inaonesha nyumba ya Mubah ndio inataka kulipuka.

  "Umeona hapo?" Mubah akaonesha kwa kidole sehemu husika anayotaka yule opareta aione.
  Opareta akatazama kwa makini, alipoona kama hapaoni, akapavuta kwa ukaribu kisha akatoa mawimbi ambayo yanasababisha picha isionekane vema.
  "Okay. Hili ni bomu toka kwenye RPG hili." Opareta akaongea baada ya kugundua hilo jambo.

  "Sasa kumbe John Lobo hayupo peke yake. Wakati nyumba hii inalipuka, mimi nilikuwa naongea naye na alikuwa na familia yangu mbali na pale nyumbani. Lazima tuwasake hawa washenzi." Mubah aliongea kwa hasira na kukita ngumi nzito kwenye meza iloyomo mle ndani.

  Kwa hasira akageuka nyuma na kutaka kuanza kutoka lakini baada ya kugeuka, akakutana na sura ya Malocha.
  "Mubah. Unatakiwa kupumzika kwa miezi miwili. Hii kesi tuachie sisi, tutaimaliza tu!" Malocha alimwambia Mubah ambaye alimtazama kwa jicho kali na la ghasia.

  "Huu ushauri ungenipa kabla familia yangu haijaondoka duniani. Ungeniambia niache kazi kabisa ili familia yangu ipone, lakini siyo sasa hivi. Nitapigana kufa na kupona ili huyu mbwa nimkamate. Nimeshajua hayupo peke yake, nitamsaka tu!" Mubah alimueleza Malocha na kumpita pale aliposimama kwa kutaka kutoka ndani ya ofisi ile. Lakini Malocha akamkamata mkono na kumrudisha mbele ya upeo wa macho yake.

  "Nilipoteza familia yangu kwa mkono wa huyuhuyu Lobo. Kwa risasi tano alizopewa, hakumkosa yeyote katika familia yangu. Nilijawa na jazba kama wewe hivyo, nikapania kumuua na nilifanikiwa kukamatiwa huyu mtu, nikawa naye uso kwa uso akicheka kwa dharau. Nilikata shingo yake, kisha nikamvunja miguu kwa risasi mbili na tatu nikamchapa nazo kifuani (MKASA HUU UPO KWENYE RIWAYA YA JINA).

  Nikadhani amekufa, lakini leo hii tunapambana naye tena. Naona ni kama mzimu au shetani ambaye hafi, au jini. Lobo huwezi kupambana naye peke yako na ukashinda vita yake. Utapotea Mubah." Malocha aliongea kwa makini na kwa upole huku machozi yakiwa yanataka kumtoka kwa mbali.

  "Baada ya kupoteza familia yako, ukamsaka na kumpata kisha ukamuua. Niachie na mimi, nimepoteza familia yangu, nimsake nimpate kisha nitakuletea kiwiliwili chake." Sauti ya kujiamini toka kwa Mubah ilipenya masikioni mwa wale wanaofatilia yale maongezi, akiwemo Malocha.

  "Nimekwisha kwambia, acha hiyo kesi. Ni amri siyo ombi. Nakupa miezi miwili ya kupumzika, utake usitake, utaenda mapumziko." Malocha ikabidi atumie nguvu za uongozi wake kuwasilisha hisia zake. Mubah akatulia kwa muda kabla hajarudi kwa yule opareta na kuchukua ule mkanda wenye tukio zima la siku hiyo.

  "Familia yangu ipo?" Mubah alimuuliza Malocha kabla hajachukua hatua nyingine kutoka mle ofisini.
  "Nyumba na walinzi wakiwa na familia yako, vyote vilipigwa kiberiti. Hakuna ambacho kimesalia, labda majivu." Malocha alimjibu Mubah huku uso wake akiutazamisha mbele na chozi la kiume likamtiririka jasiri huyu upande wake wa kulia.

  "We will be fine boss. Don't cry sir (Tutakuwa sawa mkuu. Usilie)" Mubah akamwambia mkuu wake huku akimgonga gonga bega lake kumfariji.
  Baada ya hapo, akatoka nje ya ofisi ile na kuelekea kwa Lisa ambaye baada ya kumuona Mubah, alimkimbilia na kumkumbatia.

  "Upo sawa Mubah." Lisa alimuuliza baada ya kumuachia.
  "Nipo sawa Lisa. Lakini bado sijajua ni vipi Lobo alijua kuwa familia yangu ipo kule." Mubah alimuuliza Lisa.
  "Nadhani kuna kitu alikiacha katika mwili wa mwanafamilia wako, hicho ndio kilikuwa na GPS ambayo inaonesha popote waendapo."

  Lisa akamjibu Mubah na hapo Mubah akakumbuka kile kibanio kilichokuwa kina sumu hatari kutoka kwenye Yellowstone. Lakini pia akakumbuka maneno ya mjomba wake kuwa alipewa kibanio na kitu kingine ambacho yule mjomba hakumalizia kukisema baada ya Mubah kumpora kile kibanio.

  "Nadhani itakuwa hivyo maana kuna sumu waliivuta wale wenzangu wengine, ilitoka kwenye banio ambalo mimi nilimpora Husna, mjomba wangu. Lakini pia Husna alipewa kitu kingine na Lobo, nadhani kiliambatana na hiyo GPS. Ila hamna tatizo, naenda likizo ya miezi miwili, lakini sitalala.

  Nitakutumia sana kukupa taarifa za kila upelelezi wangu." Mubah alimwambia Lisa na kisha wakaongea maneno machache ya kufarijiana kabla Mubah hajachukua jukumu la kwenda chumba cha mapumziko kilichomo FISSA.
  ****

  "Bado sijaipata mkuu. Na familia yote ya Prince Mubarak imeteketea." Ni sauti ya Malocha ikiwa inaongea kwenye simu ambayo ilipigwa usiku ule wa saa tano. Alikuwa rais wa nchi akiulizia ndege kama imepatikana.
  "Nasemaje. Mi' sijali hayo mambo yenu ya kijinga kwenda kukamata mtu mmoja kwa kutumia watu mia badala ya kufata maelezo ya mtu anachokitaka.

  Nachotaka mimi hapo ni hiyo ndege tu! Jumamosi ijayo Rais wa Cuba anakuja, unadhani kuna nini kitatokea kama hiyo ndege haijapatikana? Naitaka hiyo ndege kabla ya Jumamosi." Rais akakata simu na kumuacha Malocha akiwa katika wakati mgumu kuliko nyakati zote ambazo kawahi kuzipitia kimaongezi.

  Akiwa na hasira za kuweza kufanya jambo lolote bila kujizuia, akatoka nje ya ofisi yake na kisha akaita wafanyakazi wote wa lile shirika.
  "Ondokeni wote usiku huu. Sitaki mtu humu." Malocha aliongea kwa hasira baada ya mjumuiko wa wafanyakazi wake kuja eneo husika.

  "Lakini mkuu, si ruhusa kuondoka usiku." Mfanyakazi mmoja alikumbusha sheria ya shirika lao.
  "Ninekwishasema. Lawama zote nitabeba mimi, na si yeyote humu. Poteeni haraka kabla sijafanya kitu cha ajabu humu." Walimjua Malocha vilivyo, hivyo baada ya kauli ile, wakazima vitendea kazi vyao na kwenda kwenye usafiri maalumu kwa ajili ya kuwatoa nje ya shirika lile.

  Sasa shirika lote la kipelelezi likawa limebaki patupu. Hakuna mtu zaidi ya Malocha aliyekuwa analanda huku na huko akijaribu kutafakari hili na lile kuhusu John Lobo.
  "Kanishinda huyu mbwa. Sina jinsi, inabidi nimtafute tu! Nadhani nitafanikiwa." Yalikuwa maneno ya Malocha akiongea peke yake.

  Baada ya maneno hayo, akaenda moja kwa moja ofisini kwake na kutwaa simu ya mezani, kisha akaifungua na kuweka kitu fulani ambacho kilisaidia watu wasinase maongezi ambayo watakuwa wanayaongea kupitia simu hiyo.
  "Halo kaka." Malocha aliitika baada ya simu kupokelewa.

  "Vipi Malocha." Jamaa wa upande wa pili alisalimia.
  "John Lobo karudi." Malocha alimwambia yule jamaa wa pili.
  "Mkamateni sasa." Jamaa akajibu kifupi na kukata simu.
  Malocha akapagawa kwa kitendo kile cha jamaa. Hakujua atafanya nini ili kumshawishi yule jamaa amsikilize.

  Akatulia kwenye kiti chake akitafakari njia za kumvuta mtu wake amsikilize. Baada ya dakika kadhaa, akapata wazo la cha kufanya. Akatwaa simu yake tena na kupiga namba zilezile.
  "Usinipigie tena Malocha." Jamaa alisikika akilalamika kwenye simu.
  "Lisa yupo katika hatari ya kuuawa na Lobo." Malocha akaongea kwa kifupi na kisha akakata simu.
  *****

  NYUMBANI KWA LISA.
  Alifika mida ya usiku sana na kukuta aishio nao wamekwishalala. Akafungua mlango wa nyumba yake kwa funguo ambazo anazo na kisha akaingia chumbani kwake ambapo alivua mavazi yake ya kazi na kuyaweka pembeni. Akavaa mavazi ya kwenda kuogea na baada ya hapo akaelekea bafuni kujisafi.

  Dakika saba za kujisafi zikatimia, ndipo akatoka akijipukuta na kuelekea katika kitanda ambacho analala na mume wake Bwana Gunner, jamaa mwenye asili ya Kameruni na Kirusi.
  Lisa akavuta kipande cha shuka alichojifunika mumewe na yeye akajifunika tayari kwa kuutafuta usingizi.

  "Kazi zako vipi. Na leo mbona usiku?" Gunner alimuuliza mkewe Lisa.
  "Kuna matatizo makubwa ofisini." Lisa alijibu kimkato na kutulia kabla ya kushtuliwa na mkono wa Gunner uliopita kiunoni kwake na kumgeuzia upande wake. Wakawa wanabadilishana pumzi kwa sababu sasa walitazamana.
  "Kumetokea nini?"

  Gunner akamuuliza Lisa swali ambalo Lisa alilijibu pia kwa kifupi lakini lilieleza kila kitu ambacho kilitokea.
  Baada ya maelezo hayo, Gunner alimbusu Lisa mdomoni na Lisa naye hakuwa nyuma bali kumpa ulimi kabisa bwana yule mweusi na aliyejengeka mwili sababu ya mazoezi ayafanyayo.


  ITAENDELEA
   
 10. G

  Guasa Amboni JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 6,983
  Likes Received: 7,500
  Trophy Points: 280
  Shukran umetimiza ahadi yako ya 12 sasa sijui tutarajie muda gani tena au ndio kesho? najua ilivyo kazi kuandika ila ukipata wasaa tupia tena.
   
 11. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA SITA

  Dakika saba za kujisafi zikatimia, ndipo akatoka akijipukuta na kuelekea katika kitanda ambacho analala na mume wake Bwana Gunner, jamaa mwenye asili ya Kameruni na Kirusi.
  Lisa akavuta kipande cha shuka alichojifunika mumewe na yeye akajifunika tayari kwa kuutafuta usingizi.

  "Kazi zako vipi. Na leo mbona usiku?" Gunner alimuuliza mkewe Lisa.
  "Kuna matatizo makubwa ofisini." Lisa alijibu kimkato na kutulia kabla ya kushtuliwa na mkono wa Gunner uliopita kiunoni kwake na kumgeuzia upande wake. Wakawa wanabadilishana pumzi kwa sababu sasa walitazamana.

  "Kumetokea nini?" Gunner akamuuliza Lisa swali ambalo Lisa alilijibu pia kwa kifupi lakini lilieleza kila kitu ambacho kilitokea.
  Baada ya maelezo hayo, Gunner alimbusu Lisa mdomoni na Lisa naye hakuwa nyuma bali kumpa ulimi kabisa bwana yule mweusi na aliyejengeka mwili sababu ya mazoezi ayafanyayo.

  Baada ya dakika tano, ni sauti za raha ambazo zilitawala mle ndani. Mabusu motomoto aliyokuwa anayatoa Gunner kwenda kwa Lisa, hakika yalifaa kuitwa pole yenye raha kwa Lisa. Mtoto wa kike akawa hoi kabla hata ya mshikemshike wa mapenzi kuanza.

  Gunner akazidi kuonesha utundu wake kwenye mwili wa Lisa. Akabusu la kupitisha ulimi wake huku na huko hadi pale alipohakikisha mwili wa Lisa upo tepetepe na hoi kwa mambo mazito ambayo si rahisi kwa msichana wa kileo kuyapokea kwa mwanaume wake.

  Gunner akampa mtoto wa kike ile thamani ya ndoa yake, akampa kile ambacho kiukweli huzidisha hamu ya wapenzi kuwa pamoja. Na zaidi, huongeza chachu ya penzi. Lisa akajikuta mwenye faraja mpya baada ya shughuli nzima aliyoifanya mumewe.

  Na shughuli kama hiyo ndio hasa iliyomfanya Lisa asimfiche mumewe ambaye alikuja katika wakati mgumu alioupitia Lisa. Wakati ambao Lisa alikuwa hana msaada kifikra zaidi ya maumivu tele baada ya kupotea kwa kipenzi chake Frank Masai na wakati huo anasumbuliwa na baba yake akiyegundua ujauzito wake.

  MIAKA KADHAA NYUMA.
  "Lisa. Tumbo lako limebarikiwa kuliko wanawake wote katika dunia hii. We' ndiye thamani ya moyo wangu. Hakuna Frank bila Lisa na Lisa bila Frank." Ni sauti ya Frank ikiwa kitandani pamoja na Lisa ambaye Frank alikuwa akilipapasa tumbo lake.

  "Naupenda sana ulimi wako Man'Sai. Kila mara hunipa faraja ya masikio yangu na kinywa changu." Lisa akamjibu Frank kwa sauti ya mahaba na kumuongezea busu zito lililoenda sambamba na kumbate la kushiba.

  "Lisa. Nahitaji tumbo hili libebe kiumbe changu. Upo tayari?" Frank alimuuliza Lisa baada ya muda mchache wa kumaliza mahaba yao.
  "Nakukaribisha Man'Sai. Sitajutia maamuzi yangu. We' ndiye kila kitu." Maneno hayo yalimtoka Lisa akiwa kitandani kwa Frank kipindi wapo chuo kikuu mwaka wa kwanza.

  Mapenzi yao yalianza tangu sekondari na muda huo yalikuwa yameshamiri kama maua yaonayo asubuhi au ndege wa anga wasonapo jua limechomoza.
  "Asante Lisa. Nategemea mwaka wa tatu tutatimiza ndoto hii." Frank akaweka nyongeza katika maongezi yao.

  "Anytime Man'Sai."
  "Thank you dear." Baada ya maneno hayo, purukushani za mahaba zikapamba moto tena na kufanya kitanda cha Frank kulalamika kwa kile kinachoendelea.
  ****

  MIAKA MIWILI MBELE.
  Ikiwa ndio wanamaliza chuo, kama kawaida ya Frank na Lisa, wakakutana kimapenzi zaidi lakini wakati huu walikuwa wanalengo la kusaka mtoto tu! Wiki hiyo wakawa wanakutana kimwili kila pale walipohitajiana. Lisa akiwa anajua wazi ndani ya wiki hizo ndipo awezapo kupata ujauzito, akawa haishi miguu yake kwa Frank. Na Frank alionesha urijali wake kwenye maeneo ya kitandani. Akawa mtu wa kutoa raha kwenda kwa Lisa na Lisa akitoa raha hizo kwenda kwa Frank.

  Baada ya wiki mbili wakahitimu chuo kikuu. Huo ndio ukawa mwisho wa Frank na Lisa kuonana. Baba yake Lisa ambaye ni Gavana wa jimbo fulani huko Marekani, akamchukua Lisa kwa ombi la Rais wa nchi, na kumpeleka chuo cha mafunzo ya Ujasusi. Huko ndipo ambapo Lisa alipata wasaha wa kujifunza mbinu mbalimbali za kipelelezi na ujasusi.

  Lakini kabla ya kuingia katika chuo hicho, ilibidi apimwe kwanza afya yake. Hapo ndipo alipogundulika anaujauzito wa mwezi mmoja. Baba wa Lisa, Mzee Lindsay, aliumia sana kwa kitendo kile. Ili kuficha aibu ile, akaamua kumtafutia mwanaume mtoto wake amuoe akiwa na mimba ile.

  GUNNER SAMUEL BOKWA. Kijana mpole na mtulivu katika mambo yake. Anamiliki biashara kadhaa nchini Marekani, Ufaransa, Urusi na Kameruni alipotokea marehemu baba yake ambaye ndiye aliyemuachia urithi wa mali zote hizo. Siku zote katika maisha yake alikuwa ni mtu wa kumsumbua Mzee Lindsay kuhusu mtoto wake.

  Na baada ya baba wa Lisa kugundua mwanawake anamimba, akamkimbilia Gunner bila yeye kujua na kumuomba amuoe mwanaye kabla hajaenda chuo cha ujasusi.
  Gunner hakuwa na kipingamizi chochote kwa sababu mapenzi ni upofu. Akamfata Lisa ambaye tumbo lake bado lilikuwa halijaanza kuchipuka bali uzuri wake ulizidi maradufu.

  Gunner akawa boya na bwege kabisa hasa pale alipopewa ruhusa ya kusadifu umbo mwanana la Lisa likiwa halina mavazi. Akalichezea wiki nzima kwa mahaba mazito. Mwisho wa yote ukawa ni harusi kubwa kufungwa katika jiji la Dar es Salaam.

  Lisa alijitahidi kuonesha furaha yake, lakini ukweli ni kwamba, hakuwa na furaha hiyo hasa baada ya kusikia mkasa ambao Frank na Malocha umewakumba kipindi hicho. Mkasa wa Jina la Chude Bobo. Walikuwa wanatafutwa kama dhahabu machimboni.

  Na baada ya ndoa hiyo wakaenda nchini Uswiss kula fungate lao la miezi mitatu. Baada ya kutoka huko, Gunner ndipo alipopewa taarifa kuwa mkewe anamimba yake. Jamaa alifurahi kupita maelezo na kumnunulia kila kizuri huyu mwanamke baada ya taarifa hizo za faraja kwake. Hakutaka kuhesabu muda alioutumia na Lisa katika mapenzi, alichojua yeye katundika ampendaye mimba.

  Hatimaye mtoto akazaliwa na wakampa jina la Martina, jina la mama wa Lisa. Mwaka mmoja mbele, ndipo Lisa akamuacha mwanaye katika kituo cha kulelea watoto na yeye akaenda kusomea mambo ya ujasusi kwa miaka miwili.
  Alipotoka, moja kwa moja akaingizwa katika shirika la FISSA wakati huo linaongozwa na Juvenile.

  Shirika likiwa lina uchafu mwingi kuliko shirika lolote la kipelelezi duniani. Shirika ambalo halikuwa na usawa kwa wananchi wake.
  Pale Malocha alipokataa kusema ukweli kuhusu Jina la Chude Bobo, FISSA walimtuma mdunguaji wao hodari kwenda kuiangamiza familia ya Malocha.
  Hayo yalifanyika kipindi Lisa yupo chuoni.

  Baada ya Lisa kutoka chuoni, maisha na mumewe yakaendelea huku akiwa mtu wa kuficha siri katika ndoa yake.
  Miaka minne akatimiza Martina, Gunner akawa na uhitaji wa mtoto mwingine. Bila kumwambia mkewe shida yake, akawa mtu wa kusaka mtoto huyo kwa kila hali lakini hakufanikiwa.

  Ndipo alipoamua kwenda kuchukua vipimo vya uzazi katika hospitali moja iliyopo nchini Afrika Kusini. Huko akaambiwa kuwa hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito na tatizo hilo kazaliwa nalo. Roho ilimuuma sana Gunner baada ya kugundua kuwa analea kiumbe kisicho chake.

  Akarudi Tanzania na kupekua pekua nyaraka mbalimbali za Lisa na ndipo alipokutana na picha ambayo ilimuonesha Martina akiwa na miaka miwili na kwa nyuma iliandikwa "Ndoto zimekuwa kweli Man'Sai, mtoto wetu huyu.
  To Frank Masai."

  Ni wazi picha hiyo ilitakiwa kutumwa kwa Frank Masai wakati Martina ana miaka miwili, lakini haikumfikia mlengwa na Lisa akaihifadhi.
  Mbali na picha hizo, Gunner alikuta siri mbalimbali zikiwemo za FISSA. Akajizuia asifanye chochote kwa wakati ule lakini akijiahidi kuwa ipo siku Lisa atatakiwa kuujua ukweli na atatubu.
  ******

  "Lisa, ni asubuhi mke wangu." Sauti nzito ya Gunner ilimtoa usingizini Lisa ambaye alikutana na chai nzito ya maziwa aliyoandaa mumewe. Kwa kiingereza wanaiita 'Bed and Breakfast' yaani kifungua kinywa kiandaliwachwo wakati mtu bado yupo kitandani.

  "Mmmh! Swetie. Haya mambo umeanza lini tena." Lisa akamuuliza mumewe huku akinyanyua mgongo wake tayari kwa kukitafuna kile alichoandaliwa.
  "Siyo mimi peke yangu. Na Martina kachangia kukuandalia." Gunner akaongea huku kagubikwa na pambo zito la tabasamu usoni pake.

  "Mmmh. Miaka sita tu! Kishajua hadi ku........" Lisa hakumaliza kauli yake akaweka mkono wake mdomoni huku macho akiwa kayaweka kama mtu asiyeamini kitu fulani. Wakati huo na Gunner alikuwa kachanua tabasamu lake kama kawaida.

  "Ni birthday ya Martina leo." Lisa aliongea huku akimuangalia Gunner kwa hali ya sintofahamu.
  "Najua majukumu ya kazi ndio yanakufanya uikumbuke birthday ya mwana wetu sasa hivi." Gunner aliongea huku bado tabasamu halimuondoki katika uso wake.

  "Asante Gunner. Sijui hata nimpe nini aisee."
  "Usijali, nimekwisha kuwakilisha. Na kaipenda zawadi niliyompa kwa ajili yako."
  "Asante Baby." Lisa akashukuru na kumkumbatia Gunner kwa upendo wa hali ya juu.

  "Labda ananipenda kwa sasa na hamkumbuki mtu wake. Ni kwa sababu sina uwezo wa kuzalisha tu! Naamini kama ningekuwa naweza kumpa ujauzito mwanamke huyu, basi sidhani kama Martina angekuwa tatizo. Ngoja niendelee kuvuta subira." Gunner aliwaza hayo kichwani wakati wamekumbatiana na Lisa.

  "Kula sasa baby. Baadae nendeni mkatembee huko na Martina ili naye afurahi." Gunner aliongea hayo huku akimtoa Lisa mwilini mwake na kummiminia chai hiyo ya maziwa kwenye kikombe alichokiandaa. Lisa akatabasamu kwa furaha kwa matendo yale toka kwa mumewe.
  Akaanza kunywa taratibu na vitafunwa kadha vilivyoambatanishwa na chai hiyo.

  "Mamiee." Sauti ya Martina iliita kwa nguvu na kumrukia mama yake ambaye alikwishamaliza kunywa chai ile.
  "Ooooh! Malaika wangu. Hujambo eeh." Lisa akamkumbatia mwanaye huku anazilaza nyuma nywele za singa alizoumbwa nazo. Nywele zinazofanana na baba yake, Frank Masai.

  "Nipo salama mama. Baba kanipa zawadi, na kila siku natoka naye. Leo nataka na wewe tutoke." Martina aliongea kwa deko mbele ya wazazi wake waliokuwa wanatabasamu kwa maneno mengi ya mwana wao.

  "Kwani mimi sijakupa zawadi?"
  "Umenipa na nitaivaa leoleo tukitoka."
  "Haya basi, kajiandae twende tukacheze cheze huko mbali." Baada ya maneno hayo, Martina alitoka nje akikimbia kwa ajili ya kwenda kujiandaa na mtoko ulioandaliwa na mama yake.

  "Alikumiss sana." Gunner akimwambia Lisa.
  "Nilimmiss pia. Vipi wewe, huendi na sisi?"
  "Mi nitabaki. Labda twende bafuni kuoga tu! Si wajua kitambo kidogo." Gunner akichombeza na kubakiza tabasamu ambalo Lisa alilipokea kwa tabasamu pia.
  Hapo Gunner akachukua jukumu la kumbeba hadi bafuni mkewe na kuanza oga naye hadi pale walipodhika.
  ****

  Ni furaha tele zilitwala katika nyuso za mama na mwana, yaani Lisa na Martina. Michezo kama bembea na kuteleza, vilikuwa vinajenga raha hiyo.
  Masaa mawili yote yaliishia kwenye kucheza na kufurahi kwa pamoja, lakini hali hiyo ilikatishwa kwa simu iliyopigwa na Mubah.

  "Hey Lisa. Unaweza kuja huku Kitunda." Mubah alimuuliza Lisa.
  "Mmmh! Nipo Mwenge huku. Leo birthday ya Martina, nafurahi naye hapa."
  "Njoo mara moja. Kuna jambo la muhimu sana nataka unisaidie."
  "Okay. Nakuja. Nipe saa moja na nusu."

  Simu ikakatwa na Lisa akamchukua mwanaye mida hiyo ya saa tisa alasiri tayari kwenda alipoambiwa na Mubah.
  Baada ya saa moja na dakika zipatazo kumi na tano, tayari Lisa alikuwa uso kwa uso na Mubah eneo la Kitunda kabla Mubah hajachukua simu ya Lisa na kuifunga kisha kuitupia kwenye ndoo ya uchafu.

  Baada ya hapo, akampa simu nyingine kama ileile na kupachika kadi ambayo Lisa huitumia kuwasiliana na watu wake.
  "Okay. Sasa twaweza kwenda Lisa. Lakini si kwa gari lako bali lile pale." Mubah alimuonesha Lisa gari lingine ambalo wangelitumia kwenda makao mapya ya Mubah.

  Lisa akaliweka gari lake katika usalama, kisha akamchukua Martina na kwenda naye kwenye gari la Mubah bila kipingamizi.
  "Hey Martina. Happy Birthday." Mubah alimtakia heri ya kuzaliwa Martina huku akimlaza nywele zake kwa nyuma wakati huo dereva wa gari hilo alishakamata njia ya kwenda Kivule.

  Wakati Mubah anakamata nywele za Martina, mkono wake ukwama kwenye banio la nywele alilobania Martina.
  "Hey. Kibanio chako kizuri. Umekipata wapi?" Mubah alimuuliza Martina baada ya kukiangalia kibanio hicho.

  "Zawadi ya mama hii. Kanipa leo." Martina akajibu na kumfanya Mubah amtazame Lisa kwa macho ya kiulizo.
  "Embu simamisha gari mara moja." Mubah akamuamuru dereva wake na yeye akatii.
  "Lisa naomba tushuke mara moja." Sauti ya Mubah ikatoa ombi dogo ambalo Lisa akalitimiza na kwenda naye mbali kidogo kisha wakaanza kuteta kitu.


  ITAENDELEA
   
 12. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA SABA

  Wakati Mubah anakamata nywele za Martina, mkono wake ukwama kwenye banio la nywele alilobania Martina.
  "Hey. Kibanio chako kizuri. Umekipata wapi?" Mubah alimuuliza Martina baada ya kukiangalia kibanio hicho.

  "Zawadi ya mama hii. Kanipa leo." Martina akajibu na kumfanya Mubah amtazame Lisa kwa macho ya kiulizo.
  "Embu simamisha gari mara moja." Mubah akamuamuru dereva wake na yeye akatii.

  "Lisa naomba tushuke mara moja." Sauti ya Mubah ikatoa ombi dogo ambalo Lisa akalitimiza na kwenda naye mbali kidogo kisha wakaanza kuteta kitu.
  "Kile kibanio umempa wewe kweli?" Mubah akamuuliza swali Lisa.
  "Hapana. Kapewa zawadi na baba yake. Lakini aliambiwa mimi ndiye niliyempa kwa sababu sikuwa na zawadi hii leo. Kwani vipi Mubah?"

  "Hamna tatizo. Ila ni kibanio ghali sana kile, hadi nimeshtuka." Mubah alidanganya lakini ukweli ni kwamba kile kibanio alichokuwa nacho Martina, ndicho ambacho mjomba wake alipewa na Lobo. Yaani vinafanana.
  Ndicho kile kilichotoa sumu hatari kutoka kwenye Yellowstone.
  Wakarudi kwenye gari baada ya maongezi machache na kisha gari likakaza mwendo kuelekea Kivule.

  Kichwa cha Mubah hakikutulia hata kidogo kimawazo. Akiwa katika mawazo hayo, ndipo akakumbuka sura ile iliyompita kwenye gari wakati yeye anazimia.
  Akakurupuka tena na kumuangalia Lisa kwa macho ya kushuku kitu. Lisa akabaki mwenye mshangao wa hali ya juu kwa matendo nadra ayafanyayo Mubah.

  "Yule ni Gunner, mume wa Lisa. Mshenzi anashirikiana na Lobo. Mungu wangu." Mubah akajisemea mwenyewe moyoni huku akimkodolea macho makali Lisa.

  "We' Mubah unamatatizo gani!? Hiyo tabia umeitoa wapi." Ikabidi Lisa amuulize Muhah jambo linalomsibu hasa baada ya kuona macho ya Mubah hayakauki usoni pake.
  "Hakuna Madam. Basi tu!" Mubah alijichekesha huku akijaribu kuumba tabasamu la mbao usoni pake.

  "Usinifanye mimi mtoto Mubah. Mi' ni Jasusi na pia ni mpelelezi kuliko wewe. Najua unafahamu kitu, haya haraka eleza nini kipo nyuma ya pazia." Lisa akauliza tena akiwa katika uso usio na masikhara. Wakati huo, gari lao lilikuwa likizidi kusonga mbele na Martina akionekana kufurahia mwenendo mzima wa safari ile.

  "Hamna kitu madam Lisa. Nitakwambia tukifika kwani kwa sasa kidogo, itafanya kazi yetu kugoma." Mubah alijitetea huku akijing'ata ng'ata bila kujua sababu ya kufanya hivyo.
  "Basi sitaki unitazame tena usoni. Acha kabisa." Lisa alifoka na kumuangalia mtoto wake ambaye alikuwa anacheza kwa kumrusha mdoli fulani aliyenunuliwa na mama yake.

  Mubah akaamua kutulia kama si yule wa mwanzo. Na kwa bahati mbaya au nzuri, alikuwa anajali kazi zaidi kuliko matukio yaliyompata. Akili yake yote ilijaa kisasi kuliko jambo lolote lile.
  Gari ikazidi kutitia kwa mwendo wa madaha hasa kwa sababu ya barabara mbovu ya kuelekea Kivule.

  "Mama, baba ananifundishaga kupiga kwa kutumia hiyo." Martina alimwambia mama yake huku akisonta kidole kwenye kiuno cha dereva wa gari lile.
  Alikuwa kapachika bastola yake ambayo ilionekana vema baada ya shati lake kujivuta na hiyo ndio ikampa wasaa Martina kuongea hayo.

  "Anakulengeshaga nini?" Mubah alimuuliza Martina kwa hamasa huku Lisa akiwa kama haamini kile ambacho anakisikia.
  "Anakunywagwa bia, halafu ananiwekea chupa nilenge. Siku nyingine ananipeleka porini na kuniwekea mbao zikizochongwa kama watu, ananiambia niwe nawapiga kichwani au kifuani. Hao ni maadui." Mtoto Martina alizidi kutiririka bila uoga.

  "Na kingine anachokufanyiaga." Mubah akatupa swali lingine.
  "Ananipaga picha na kuniambia huyo ni adui yetu, nikimuona kama nina bunduki nimpige kichwani."
  "Picha hiyo yupo nani?"

  "Mubah muache mwanangu. Nitashuka sasa hivi. Sitaki huo ujinga kuusikia ukimuuliza mwanangu." Ikabidi Lisa amfokee Mubah kwa sababu ya maswali makavu amuulizayo mtoto wake wa pekee.
  Mubah akameza mate ya hasira lakini akakaa kimya kwa sababu angeendelea, angemkosa Lisa katika mipango yao.

  Kimya kikachukua nafasi yake na safari ya kwenda Kivule ndio ilikuwa inaendelea kwa wakati huo.
  ****

  Malocha alikuwa hajui cha kufanya baada ya kuisubiri simu ya jamaa aliyemtegemea labda atapiga baada ya kusikia kuwa hata Lisa atakuwa matatizoni. Akawa amechoka kuisubiri kwa sababu jamaa hakupiga wala kubipu au kutuma meseji.

  Usiku wa manane Malocha akawa analanda landa ndani ya FISSA bila kujua ni nini anatafuta au nini anataka kufanya. Mara anaenda huku mara huko ili mradi awe anatembea tu.

  Mwisho wake ulikuwa ni ofisini kwake na mawazo tele yakimwandama hasa kwa sababu ya mtu wake kutopiga wala kuitikia anachokitaka.
  "Ina maana Masai amekwisha sahau ahadi yetu? Kasahau kabisa kuwa nitakapomuhitaji nitamtaarifu? Lakini hilo si kitu, inamaana pia kamsahau Lisa? Kamsahau kabisa mtu aliyesema anampenda kila mara. Frank atakuwa anamatatizo huyu mtu." Malocha alijisemea peke yake muda wa saa kumi usiku.

  Ama kwa hakika alikuwa kapagawa hasa kwa matendo kama kuwafukuza wafanyakazi wake wote usiku huo.
  Asubuhi ya saa moja, akiwa kidogo kapitiwa na usingizi, simu ya ofisini kwake ililia kwa nguvu na kumfanya akurupuke kama mwenye kuwehuka. Alipoangalia kioo kodogo cha simu ile ya mezani, aliona ni namba ya Ikulu ndio yenye kupiga.

  "It's over now. (Yameisha sasa)" Malocha aliongea hayo wakati akiiangalia simu hiyo ikiita.
  "Hallow mkuu." Malocha aliita kwa sauti ya taratibu.
  "Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama wewe. Jinga la kutupwa kama mbwa lililokosa matunzo.

  Yaani unadiriki kufukuza wafanyakazi wote usiku kama vile shirika ni lako. Unavunja sheria za shirika kama vile umelianzisha wewe." Rais alikuwa anaongea kwa sauti ya juu kana kwamba alikuwa anaongea na mtu wa maili kadhaa mbali.

  "Kwa hiyo unataka nini mkuu. Nimeshafanya." Malocha akamuuliza mkuu wake kwa nyodo.
  "Unasemaje we mbwa? Dharau umezianza lini? Sasa kwa taarifa yako, nimekwisha andaa uongozi mpya. Wewe, na mbwa wenzako hao wawili, Mubarak na Lisa, wote mtakuwa nje ya FISSA.

  Katafuteni pa kufanyia kazi, si hapo. Sihitaji washenzi tena." Maneno hayo yakaenda sanjari na kukata simu.
  Malocha akatabasamu kisha akaanza kukusanya kilicho chake kabla ya huo uongozi mpya haujafika.
  ****

  "Usafiri uwatoao nje wafanyakazi wa FISSA ni usafiri ambao si rahisi kwa mtu wa ndani kuona nje. Na hata Malocha alipoamua kwenda kuupanda, ilikuwa ni vivyo hivyo.

  Usafiri huu hutambua sauti za wafanyakazi wote wa shirika lile la siri. Na pindi wapandapo, basi hutoa sindano ndogo ambazo zinachomwa mikononi na usingizi mzito huwachukua waliopanda usafiri huu. Pia hujiendesha wenyewe kwa kuwa umetengenezwa maalumu kuwafikisha wafanyakazi wake sehemu husika.

  Muda wa saa sita, Malocha tayari alikuwa amekwishakwea kwenye usafiri mwingine ambao huo ulikuwa ni wa wananchi wa kawaida. Wale wazoefu wa jiji na miji wanauita usafiri huu ni tax, na ndio Malocha alikuwa kaupanda.
  "Mkuu tunaelekea wapi."

  Dereva mmoja mchangamfu alimuuliza mteja wake ambaye alikuwa kama katoka kulewa pombe kali usiku wa jana.
  "Nipeleke Kivule Kamanda." Malocha alijibu na dereva yule hakujali gharama ambayo itatokea kwa sababu muonekano wa Malocha, haukuwa wa kukosa fedha ambazo atamtajia.

  "Hallow Mubah." Malocha alisikika kwenye simu.
  "Ndio mkuu."
  "Hatuna chetu FISSA. Fanya hima tukutane Kivule ukiwa na ripoti nzima ya Lobo."
  "Sawa mkuu. Rais ndio katutoa au?"
  "Yaap. Ni mkuu."
  "Na nani mwingine kamtoa."
  "Lisa naye katolewa."

  "Okay. Basi na mimi nakuja huko Kivule sasa hivi." Mubah aliongea kwa shahuku kubwa.
  "Na mimi ndio nipo Posta hapa, nakuja taratibu." Malocha akamalizia kabla ya kuanza maongezi mengine ya kijamii na maisha na Mubah kupitia simu.
  ****

  "Najua umeona hilo bomu lilivoenda na kulipua nyumba yako. Lakini sasa unatakiwa kuangalia mazingira ambayo bomu hilo limetokea. Rudisha huo mkanda nyuma na kuanza kuchunguza kimoja baada ya kingine." Sauti ya Malocha ilikuwa ikimuelekeza mtaalamu wa mmoja wa kompyuta aliyekuwa anacheza mkanda mzima ambao ulionesha tukio zima lililotokea nyumbani kwa Mubah.

  Nyumba hiyo ya Kivule, ilikuwa ni nyumba moja kubwa kiasi na huwezi kujua ndani kunafanyika nini kama hujaingia na kuchunguza.
  Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa kumetapakaa dhana mbalimbali za Kijasusi na kipelelezi.

  Bunduki za kila aina na vifaa vya kipelelezi, vilipendezesha chumba ambacho Mubah na Malocha walisimama wakiwaangalia wale jamaa wanaocheza video nzima ya tukio la Mubah.

  "Hapo hapo Banchi. Umeona hilo gari jeusi?" Mubah alimsimamisha jamaa mmojawapo wa kompyuta na kumuonesha gari ambalo alilishuku vibaya.
  "Hilo ndilo nililiona wakati nazimia. Naomba ulichunguze."
  "Kama ndio hilo, basi tutaanzia kazi zetu hapo. Cha msingi tupate namba za usajili za gari hili (plate number)." Malocha aliongea huku kafumbata mikono yake kifuani.

  "Namba hizi hapa mkuu. Ni T 900 QJG." Opareta wa kompyuta zile, alitoa taarifa hizo na kuwafanya Mubah na Malocha kusogea kwa karibu na kuzitazma.

  "Okay. Safi Banchi. Sasa Mubah, hapa tunamuhitaji sana Lisa kwa sababu yeye ni mwanamke awezaye kuwavuta watu wowote na wakafungua vinywa vyao kusema siri. Cha msingi, mpigie simu sasa hivi mwambie muonane Kitunda. Halafu mkikutana, mpe hii hapa simu halafu ndio mje huku." Malocha alimpa maelekezo ambayo Mubah alikuwa anatikisa kichwa kukubaliana nayo.

  "Sasa kwa nini unampa simu hii?" Mubah akamuuliza Malocha.
  "Lisa yupo hatarini bila yeye kujitambua. Mume wake si mtu kama anavyodhani, muda wowote anamgeuka. Huyo ndio sababu ya Lobo kujua njia nyingi za FISSA kwa sababu anamuwekea GPS kila anapojua zimetolewa. Nakwambia haya lakini usimwambie chochote kile.

  Atakuja kujua ya kumaliza mambo haya." Malocha alimuelekeza Mubah mambo kadhaa, kisha kuanza kumpa siri za Lisa ambaye alikuwa anacheza na mwanaye anayesheherekea siku yake ya kuzaliwa.
  "Kwa hiyo mume wa Lisa anashirikiana na Lobo."

  "Hilo ndilo jibu." Malocha akamjibu kifupi na kumuacha Mubah bila swali na badala yake akatwaa simu yake na kubofya namba kadhaa ambazo alimpigia simu Lisa.
  ****

  Ukimya ulitawala ndani ya gari alilochukua Mubah kwenda Kivule yalipo makao mapya ya FISSA ndogo ikiongozwa na Malocha. Ukimya huo ni kwa sababu Lisa alichimba mkwara ambao Mubah alikubali yaishe kuliko kuzidi kuchongoa mdomo wake.

  Baada ya dakika kadhaa, walikuwa wamekwishafika kwenye nyumba hiyo ambayo wanaitumia kama makazi yao.
  "Heee! Malocha leo upo huku." Lisa akamuita mkuu wake jina ambalo walishazoeana kuitana shuleni.

  "Leo nimekuja kuwatembelea aisee." Malocha akajibu huku anatabasamu.
  "Mmmh! Haya karibu." Lisa aliongea kwa sauti ya furaha huku akisogea kwenye kochi lililo sebuleni pale walipofikia.

  "Hey. Martina, hujambo mama." Malocha akamsalimia Martina mtoto wa Lisa.
  "Sijambo shikamoo."
  "Marahabaa. Mimi ni Anko Malocha."
  "Shikamoo Anko Malocha."
  "Leo sherehe yako ya kuzaliwa. Nikupe zawadi nisikupeee." Malocha alimuuliza kwa furaha Martina.
  "Nipee Ankoo." Martina naye akajibu huku mikono yake akiipunga kama vile kaungua. Malocha akatabasamu baada ya kumuona mtoto mwenye furaha kiasi kile.

  Akaenda chumba fulani kisha akatoka na baiskeli moja ya rangi ya pinki, rangi ambayo hakuna watoto wa kike wasiyoipenda.
  "Asante Anko." Martina alimshukuru Malocha na kumkumbatia kwa nguvu.
  "Haya Martina. Nenda na yule pale mkaendeshe baiskeli huko." Malocha alimkabidhi Martina kwa jamaa mmoja ambaye alimchukua Martina na kumpeleka uwani mwa nyumba ile walipoanza kufurahia zawadi hiyo.

  "Okay Lisa. Nimekuita hapa kukwambia kuwa FISSA tumefukuzwa kazi lakini tutarudi baada ya mambo fulani kukamilika. FISSA sasa hivi wameingia watu wapya lakini ni watu ambao kwangu mimi siwapi sana nafasi." Malocha akaweka tuo kabla ya kuzidi kutiririka.

  "Sasa kwa kuanzia, tuanze na kazi ya kuutafuta ukweli kuhusu Lobo. Ila kwanza nataka kusikia kama upo tayari kufanya kazi na sisi." Malocha akatupa swali kabla hajaendelea na mengine.
  "Nimezaliwa kufanya hayo.

  Siwezi kukataa na wakati huyo ndiye mimi." Lisa akajibu kwa kujiamini na Malocha akamchukua mwanadada huyu jasiri na kwenda naye kwenye chumba maalumu kwa ajili ya upelelezi. Wakati huo Mubah alikuwa kimya akiwafuata wafanyakazi wenzake kwa nyuma.

  "Kazi yetu inaanzia hapa." Malocha akamuonesha gari ambalo waliling'amua namba zake.
  Maelezo kadhaa yakaanza baada ya kumuonesha gari lile. Hiyo yote ni katika kumuelekeza Lisa ili aelewe nini sababu ya kuoneshwa picha hiyo.
  "Sasa tumekwisha fatilia gari hili ni la nani na ninataka wewe na Mubah muongozane hadi kwa huyu bwana kisha mumuhoji maswali kadhaa.

  Kama hatojibu, basi tumieni mbinu za kumchukua na kumleta huku. Atajibu tu." Malocha akamaliza maongezi yale na kuwatazama watu wale.
  "Hamna tatizo. Ila naomba mkae na Martina vizuri." Lisa akatoa ombi na.kuchukua dhana kadhaa kwa ajili ya kujilinda na kujijulisha (vitambulisho).
  Baada ya hapo akatoka nje na kuwaacha Mubah na Malocha wakiwa na opareta wao wakijadiliana.

  "Mkuu. Wakati nazimia nilikwambia nimemuona mtu kwenye hii gari. Mtu huyo ni Gunner, mume wa Lisa. Kitu kilichonifanya nijue ni kibanio cha Martina ambacho ni sawa na kile ambacho kilimwaga sumu kule nyumbani. Na mbaya zaidi, huyu mtoto anafundishwa ujasusi na baba yake." Mubah akatoa taarifa kadha wa kadha hadi pale aliporidhika ndipo alipoamua kutoka nje akiongozana na Malocha.


  ITAENDELEA
   
 13. Nichumu Nibebike

  Nichumu Nibebike JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 28, 2016
  Messages: 6,255
  Likes Received: 10,029
  Trophy Points: 280
  Hongera mtunzi na muandishi...
   
 14. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  vipi wakuu stori mnaionaje?niipige chini au tuendelee?
   
 15. KENZY

  KENZY JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2016
  Joined: Dec 27, 2015
  Messages: 6,253
  Likes Received: 5,241
  Trophy Points: 280
  wasukuma wanasema kajagi lolo! tuendelee mkuu
   
 16. G

  Guasa Amboni JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 6,983
  Likes Received: 7,500
  Trophy Points: 280
  Shusha vitu story ina bamba sana tu.
   
 17. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  itaendelea punde
   
 18. G

  Guasa Amboni JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2016
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 6,983
  Likes Received: 7,500
  Trophy Points: 280
  Shukran tunaisubiri tuone mubah alibenjuka vipi katika kadhia hii
   
 19. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  DUKA LA ROHO

  SEHEMU YA NANE
  Baada ya hapo akatoka nje na kuwaacha Mubah na Malocha wakiwa na opareta wao wakijadiliana.
  "Mkuu. Wakati nazimia nilikwambia nimemuona mtu kwenye hii gari. Mtu huyo ni Gunner, mume wa Lisa. Kitu kilichonifanya nijue ni kibanio cha Martina ambacho ni sawa na kile ambacho kilimwaga sumu kule nyumbani. Na mbaya zaidi, huyu mtoto anafundishwa ujasusi na baba yake." Mubah akatoa taarifa kadha wa kadha hadi pale aliporidhika ndipo alipoamua kutoka nje akiongozana na Malocha.
  "Hicho kibanio lazima kibaki ili nacho tujue ni wapi kimetoka." Malocha aliongea huku wakiendelea kwenda sehemu nyingine.
  "Sawa mkuu. Ngoja sisi twende." Mubah alikubali wakati alipofika sebuleni na kumuona Lisa akiwa anawasubiri.
  "Umemuaga kijana wetu." Malocha alimuiliza Lisa kama kamuaga Martina.
  "Ndio. Naona hana tatizo. Yupo na furaha." Lisa akajibu huku akinyanyuka ambapo alitoka nje na kukwea gari ambalo wameandaliwa kwa ajili ya kwenda walipopanga.
  ****
  Majira ya saa moja jioni, Mubah, Lisa wakiwa na dereva wao, walifika eneo la Sinza na moja kwa moja wakaenda nyumba ambayo walipata maelezo kuwa mtuhumiwa wao anapatikana. Lakini cha kushangaza walipofika, walikuta watu wamefurika na vilio vikisikika huku na kule.
  Walisogea na kuuliza kuna nini, wakajibiwa kuwa Mzee Mofo, ambaye ndiye walimfuata amefariki dunia kwa kuchinjwa kama kuku.
  Ilikuwa ni hadithi ya kusikitisha kwenye kila kichwa cha aliyeisikia, lakini hakuna ambaye alikuwa tayari kuingilia hayo maswala kwa kuwashuku watu fulani.
  "Lisa tunafanyaje sasa. Doa limeshaingia kwenye nguo nyeupe kama uonavyo." Mubah alimuuliza Lisa baada ya kufuata watu kadhaa na watu hao kutotoa ushirikiano wowote katika kujibu.
  "Mambo magumu hapa Mubah. Ila tujitahidi tuonane na mke wake kabla hawajaenda mazikoni hiyo kesho." Lisa alishauri huku macho yakiwa yametua mbele ya mwanamke mmoja, mnene kiasi na mwenye weupe wa asili.
  Alikuwa katika majonzi mazito na baadhi ya wanawake wenzake walikuwa pembeni yake wakimpooza kwa kila neno zuri.
  Mara kwa mara alijigonga kifua na kuwa mtu wa kulalamika kwa lugha ya Kidigo.
  "Sawa sawa. Yaonekana kuna jambo analalamika kwa sababu ya kifo cha mumewe. Ikibidi tumtoe pale sasa hivi tukamuhoji pembeni." Mubah alishauri kitu ambacho Lisa hakukawia kukifanya.
  Akasonga hadi pale ambapo yule mwanamke anapolia, na kisha kwa chati akamuomba watoke eneo lile mara moja wakazungumze.
  Ilikuwa ngumu kwa mwanadada yule kukubali, lakini baada ya Lisa kujitambulisha vema, hatimaye mwanamke yule alikubali na kwenda naye katika chumba ambacho aliona ni sawa kwa kumpasha yote yaliyojiri.
  "Sijui dada yangu. Roho inaniuma sana kumpoteza mume wangu. Ila yote hiyo ni kwa sababu ya upinzani wa kibiashara tu. Wameniulia mume wangu ofisini kwake, na kisha kwenye ukuta ule wameandika Duka La Roho." Ni maneno ya yule mwanamke akijaribu kuelezea kilichokuwa kinaendelea mbele ya Lisa, wakati huo Mubah alikuwa nje.
  "Ofisi yake ipo wapi."
  "Zipo Ukonga, Madafu."
  "Okay. Ngoja twende huko tukaangalie taarifa yoyote. Naomba funguo za huko na kibali pia." Lisa aliongea na yule dada, kisha akamuacha atafute alichokihitaji.
  Baada ya sekunde kadhaa, mke wa Mofo alikuwa amekamata funguo za ofisi zile za akiba na karatasi moja ambayo itasimama kama kibali.
  Lisa akapokea vitu hivyo na kisha akataka kutoka mle ndani. Lakini ni kama Mke wa Mofo alikuwa kasahau jambo, akamuita huku akiwa na uoga mkubwa machoni pake.
  "Dada. Maisha yangu pia yapo matatani kwa sababu ya mume wangu. Roho yangu pia ipo dukani. Njia ya kuinunua ni kutosema ukweli juu ya hili jambo. Lakini siwezi nikakaa na siri hii kwa sababu tayari mume wangu si naye tena. Naomba nikwambie wewe." Mke wa Mofo alikuwa akiangalia huku na huko wakati akitamka haya.
  "Eheee! Niambie dada yangu." Lisa akasogea karibu na kumshika mkono na kumkalisha kwenye kitanda cha chumba kile.
  "Mume wangu alikuwa anauza madawa ya kulevya na ni mshirika mkubwa wa makundi haya makubwa ya kuuza madawa. Watu kama Mafia, Yakuza nakadhalika, alishirikiana nao sana. Baada ya kuona kapata mafanikio, akaomba kujitoa kundini ili aendeshe maisha yake kiuhalali. Kitendo hicho kilimpa machaguo mawili. Kama anataka kujitoa basi auze roho yake au anunue. Yaani angetaka kununua roho yake, akubali kufirisiwa. Angetaka kuuza, basi afe lakini mali zitabaki chini ya familia yako. Wakampa siku mbili ya kununua au kuuza.
  Mume wangu akadhani ni utani na hakuna ambaye ataweza kumuua. Akajidhatiti na kuweka walinzi nyumbani na popote alipokuwapo. Siku ya pili inatimia tu! Mume wangu akauawa na maiti kukutwa ofisini huku mwili umekaa kwenye kochi na kichwa kimewekwa juu ya meza." Mke wa Mofo alimaliza maelezo kadhaa anayoyajua.
  "Hiyo kampuni ni yake kweli?" Lisa akatupa swali lingine na kumfanya yule dada kuzidi kuwa na mashaka. Ila kwa kuwa aliyavulia maji nguo, basi kuyaoga ni njia inayofuata.
  "Si ya kwake. Na ndio ofisi kubwa ya kusambaza madawa nchini Tanzania." Akajibu dada wa watu.
  "Sasa ipo chini ya nani?" Mke wa Mofo akaangalia tena pande kadha wa kadha ijapokuwa chumba kile walikuwamo wawili tu.
  Akasogea karibu zaidi kwa Lisa na kwa sauti ya chini akaanza kujibu.
  "Ipo chini ya tajiri mmoja Mkam......" Kimya kikamkumba dada yule. Hakumaliza sentensi yake. Lisa alipomuangalia mwanamke mwenzake, alimshuhudia akidondoka kitandani kama mzigo huku damu zikimvuja kichwani palipokuwa pana tobo la risasi. Ukuta nao ulikuwa umechafuka kwa damu hizo.
  Yote hayo yalitokea saa mbili usiku. Kwa bastola ambayo imefungwa kifaa cha kuzuia mlio wa risasi, ikamtoa uhai mke wa Mofo.
  Lisa akatazama huku na huko lakini hakuona chanzo cha risasi ile.
  Akajaribu kwenda dirishani, ndipo alipoona dirisha limefunguliwa kidogo. Yeye akafungua lote na kisha akapita hapo kwa sababu kulikuwa hakuna kizuizi kikubwa cha yeye kutopita.
  Alipotoka alikutana na teke zito la uso. Hajakaa sawa kiakili, akakutana tena na ngumi ya uso iliyomrudisha nyuma zaidi kimawazo. Hadi anakuja kutulia na kukaa sawa, tayari alishapokea kipigo cha maana toka kwa mtu ambaye hakumuona.
  Alisikia vishindo vya kukimbia ndipo naye akajaribu kukimbia wakati huo lile eneo la nyuma kulikuwa hamna watu.
  Katika kukimbia, alimuona mtu yule akimalizia kuruka geti kubwa la nyumba ile. Hapo Lisa ndipo alipoamini kuwa alikuwa hapamabani na 'kinyangala mafuta' bali chatu mwenyewe.
  Naye akajitahidi kuruka na kutua nje. Akakuta mtu wake anahangaika kuwasha pikipiki aliyokuja nayo, huo ndio ukawa upenyo pekee wa Lisa kujitambulisha katika nyanja za mapigano.
  Teke zito la kifuani likamkuta yule mtu na kumrusha nyuma ya pikipiki ile. Kabla hajanyanyuka, Lisa akateleza chinichini na kumkung'uta teke lingine la uso. Adui wa Lisa akadhani yataishia hapo, kumbe mwenzake ndio kwanza anayaanza.
  Sarakasi mbili za kujibetua kwenda nyuma, zikapigwa na Lisa, kisha akamaliza kwa kujitupa kwenye tumbo la adui yule. Hapo akasikia sauti kali ikitoka kwenye kinywa cha mtu yule.
  "Kumbe ni mwanamke." Lisa akajikuta akiropoka baada ya sauti ile. Kwa mavazi ya kininja aliyovaa mtu yule, ni ngumu kujua anajinsia gani. Baada ya kipigo akajitambulisha kwa mlio huo wa kike.
  Lisa akajisahau kidogo na huo ndio uliokuwa wasaa wa yule adui kupitisha miguu yake shingoni kwa Lisa na kisha kumkaba kwa nguvu bila kumuachia. Kila Lisa alipojaribu kufurukuta, hakuchomoka na badala yake, roba ikawa inazidi kumbana hadi akasaliti amri kwa kuzimia palepale.
  Hapo yule Mwanamke ninja, akawahi pikipiki yake na kuipa kiki ya nguvu, nayo ikakubali sheria. Mwendo wa ajabu ukachukua nafasi yake baada ya kuwaka. Akaondoka eneo hilo huku akimuacha Lisa hana fahamu.
  ****
  "Lisa, Lisa, Lisa." Sauti ya mwangwi ilisikika kwenye kichwa cha Lisa. Akajaribu kufumbua macho na kuona nani anamuita.
  Ilikuwa ngumu kwake kurudiwa na fikra zake lakini alijitahidi na kufanikiwa kufungua milango yake ya fahamu.
  Sura za rafiki au wafanyakazi wenzake aliziona zikiwa zinamtazama. Akatulia dakika kama tatu kisha akafyonza baada ya kukumbuka tukio zima lililotokea nyumbani kwa Mzee Rofo.
  "Mbwa yule ni kweli hayupo peke yake. Leo nimepambana na mwanamke mwingine." Lisa aliongea huku akinyanyuka kwenye kitanda ambacho alikuwa kalazwa.
  Ni katika nyumba ileile ya Kivule ndipo aliporudishwa tena.
  "Vipi hali yako lakini?" Malocha alimuuliza Lisa.
  "Nitakuwa vizuri. Martina yupo wapi?" Lisa akamkumbuka mwanaye.
  "Yupo chumba cha mapumziko kalala." Akajibiwa.
  "Kwani sasa hivi saa ngapi?"
  "Ni saa nne hii."
  "Oooh! Mungu wangu. Sijui mume wangu atakuaje."
  "Usijali tumempa taarifa kuwa upo kwetu na utarudi kesho."
  Lisa akapumua pumzi ya ahueni kisha akatulia kitandani na kuanza kusimulia mkasa mzima ambao ulimtokea.
  "Daah! Hawa watu si wa kuchezea kabisa. Wapo vema kila idara. Hapa cha msingi ni kujitahidi kucheza na silaha." Mubah alitoa ushauri kabla hawajamuacha Lisa peke yake mle chumbani.
  "Sasa kama ulivyoona, tumepoteza chanzo kingine. Hapa tumebaki na hicho kibanio tu! Tumejaribu kufuatilia vinapotoka, tumegundua ni Malyasia. Huko itabidi uende peke yako Mubah." Malocha alikuwa akimpa mchakato mwingine wa kufanya Mubah.
  "Mmmh! Mkuu, kwa nini tusimwambie ukweli Lisa ili tushirikiane naye kupambana? Wajua siwezi peke yangu. Tumwambie tu ukweli." Mubah alitoa ushauri ambao Malocha aliinamisha kichwa chake chini kabla hajatoa maamuzi.
  "Wajua ni ngumu sana. Halafu maisha ya Lisa tutayaweka matatani zaidi." Malocha akatoa jibu.
  "Lakini hata hivyo siku akijua tayari maisha yake yatakuwa hatarini." Mubah aliweka neno ambalo nalo halikuwa baya.
  "Okay. Tutamwambia. Lakini siyo leo wala kesho. Hiyo ni kwa usalama wa.mwanaye zaidi." Malocha aliongea.
  "Kwani mtoto naye ana nini. Mtoto wao halafu wamdhuru?" Mubah akapatwa na mshangao.
  Malocha akamsogelea Mubah pale alipo kisha akaanza kwa kumgonga gonga bega.
  "Jambo usilolijua, ni sawa na usiku wa kiza. Tuyaache hayo, nishatoa neno na litimizwe. Utaenda Malyasia." Malocha akamaliza.
  "Sitaenda kama huwezi kumwambia ukweli Lisa. Lisa yapaswa aambiwe ukweli." Mubah alimfata mkuu wake na kumwambia maneno hayo kwa msisitizo.
  "Mnataka kunificha nini?" Lisa akatokea na kuwauliza Malocha na Mubah huku akiwaangalia kwa zamu.
  "Mnataka kunifanya na mimi ni mtoto mdogo? Niambieni mlicho kificha. Yawezekana hata yule mtu aliyemuua mke wa Rofo mlinitegea nyie. Tangu natoka pale Kitunda, huyu alikuwa ananiangalia kwa mashaka. Sasa nataka mniambie ukweli sasa hivi." Lisa akaweka mkazo kwenye akitakacho huku sauti yake ikiwa katika hasira.
  "Lisa tulia. Kila kitu kitakuwa sawa. Na kila....." Hakumaliza kauli Malocha, ikawa imekatwa na Lisa.
  "Sitaki maelezo ya kipumbavu kama hayo. Nataka muwe straight katika majibu nayoyataka. Nini mnanificha?"
  "Mume wako anashirikiana na Lobo." Malocha akamwambia Lisa na kuondoka lile eneo huku akiwa kakunja sura yake.
  Akabaki Mubah ambaye alikuwa akimtazama Lisa aliyekuwa katika mkanganyiko wa hali ya juu baada ya maneno yale.
  "Haiwezekani." Lisa akatamka hayo huku taratibu akishuka na kujikuta akikaa chini.
  "Ni kweli Lisa. Na ndiye niliyemuona mara ya mwisho kabla sijazimia ile juzi wakati nyumba yangu inalipuliwa." Mubah alichomelea ukweli ambao anaujua.
  "Na hata hicho kibanio cha mwanao, kinafanana na kile ambacho kilitema sumu na kuua wenzetu kule nyumbani. Na yewezekana yule mtu uliyepambana naye, kakuacha sababu ya ukaribu wako na Gunner." Mubah akamaliza huku naye akienda na kukaa pale alipokaa Lisa.
  "Yawezekana ile picha ya Martina aliyonionesha Lobo wakati tumemkamata, kampa yeye Gunner. Kama kampa yeye, basi tayari anajua siri nyingi sana zituhusuzo." Lisa akaamua kufunguka.
  "Ni kweli. Kakuwekea GPS katika mifuko yako mingi unayokuja nayo kazini. GPS hizo ni ngumu kujulikana pale unapokaguliwa na vifaa vya FISSA kwani GPS hizo ni za plastiki na hazitumii aina yoyote ya umeme." Mubah akamtobolea ukweli uliokuwa mgumu kuamini kwa yeyote mwenye mapenzi.
  "Okay. Sasa naanza kupata picha kwa nini anamfundisha Martina kutumia silaha. Mjinga sana yule, kesho naenda
  kumuua." Lisa aliongea kwa kiapo na kunyanyua uso wake ambapo alikutana na uso wa Malocha ukiwa unamtazama kwa makini.
  "Lisa. Hata ukipewa miaka ishirini ya kumuua Gunner, hutoweza. Yule umuonavyo, sivyo alivyo. Ni heri ukutane na treni ya umeme relini, kuliko kukutana na uso halisi wa yule mtu. Tutakupoteza dakika sifuri tu." Malocha alimtahadharisha Lisa kwa maneno machache.
  "Sasa nifanyaje?" Lisa alimuuliza Malocha.
  "Cha msingi ni wewe kutulia hapa. Hatofika mtu hapa. Au kama waweza, rudi kwako na kujifanya hujui lolote. Na kingine, mtoto wako anafundishwa kulenga huku akioneshwa picha ya Frank." Malocha akamaliza na kuelekea chumba kilichokuwa na mitambo ya kipelelezi.
  Akamuacha Lisa akiwa kakodoa macho asijue ni nini afanye kwa wakati ule. Mubah naye akanyanyuka na kuondoka eneo lile akiwa na amani kiasi baada ya Lisa kuugundua ukweli.
  ****
  Kesho yake asubuhi, Lisa alikuwa wa kwanza kuamka na kumtazama mwanaye kama kaamka. Alipomuona hajaamka, akatwaa simu yake ambayo alibadilishiwa na wakina Mubah, kisha akampigia mumewe.
  "Nakuja asubuhi hii Gunner. Naomba nikukute." Lisa aliongea na upande wa pili ukamjibu.
  Akamuamsha mtoto wake na kumuuliza maswali ambayo alikuwa anayauliza Mubah kwenye gari.
  "Hiyo picha ambayo anakuonesha, yupoje huyo mtu." Swali mojawapo la Lisa kwenda kwa Martina.
  "Mweusi hivi, mrefu kiasi halafu ananywele za kung'aa na nyeusi." Martina alimjibu Lisa majibu ambayo yalimfanya apumue kwa shida.
  ITAENDELEA
   
 20. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2016
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,224
  Likes Received: 2,689
  Trophy Points: 280
  RIWAYA; DUKA LA ROHO
  SEHEMU YA TISA
  Kesho yake asubuhi, Lisa alikuwa wa kwanza kuamka na kumtazama mwanaye kama kaamka. Alipomuona hajaamka, akatwaa simu yake ambayo alibadilishiwa na wakina Mubah, kisha akampigia mumewe.
  "Nakuja asubuhi hii Gunner. Naomba nikukute." Lisa aliongea na upande wa pili ukamjibu.
  Akamuamsha mtoto wake na kumuuliza maswali ambayo alikuwa anayauliza Mubah kwenye gari.
  "Hiyo picha ambayo anakuonesha, yupoje huyo mtu." Swali mojawapo la Lisa kwenda kwa Martina.
  "Mweusi hivi, mrefu kiasi halafu ananywele za kung'aa na nyeusi." Martina alimjibu Lisa majibu ambayo yalimfanya apumue kwa shida.
  "Okay. Basi twende nyumbani kwa baba eeeh. Leo tutamuaga na kuja kukaa huku. Si ndio eeh." Lisa akamwambia mwanaye huku akijitahidi kuchongesha tabasamu.
  "Haya mama." Martina alijibu kwa furaha hasa kwa sababu atakuwa karibu na mama yake kuliko kipindi chochote cha maisha yake.
  ****
  "Nitakuwa nyumbani tu leo, sitaondoka kabisa." Lisa alikuwa anamwambia Gunner huku akiwa katabasamu kana kwamba hajui kitu.
  Alishaondoka Kivule na sasa alikuwa uso kwa uso akitazamana na Gunner.
  "Okay. Basi mimi naelekea ofisini. Nitarudi usiku leo." Gunner aliongea na kumpa busu dogo mke wake. Akatoka nje na kuondoka.
  BAADA YA SAA MOJA.
  Lisa alikuwa akitupia nguo zake haraka haraka kwenye begi lake kwa lengo la kuondoka katika nyumba ile. Akafanikiwa hilo na hata kuandika ujumbe ambao atauacha mezani baada ya kuondoka.
  Akanyanyua begi lake tayari kwa kutoka nje ya chumba chake. Akatoka na kuanza kuelekea sebuleni huku akiita jina la Martina.
  "Una safari mke wangu." Macho ya Lisa hayakuamini pale alipomkuta Gunner kakaa sebuleni na Martina ambaye alikuwa hana habari wala kuhisi kitu kibaya.
  Lisa akashindwa kujitetea na badala yake akawa anatetemeka huku akimuangalia mwanaye ambaye Gunner alikuwa akizilaza nywele zake kwa taratibu.
  Gunner akanyanyuka pale kochini na kumfuata Lisa kisha akampora karatasi aliyokuwa kaikamata. Ni ujumbe ambao alikuwa kauandika Lisa na alitaka kuuacha mezani kabla hajaondoka.
  "Kwa hiyo umekwisha nifahamu. Safi sana. Ndivyo mpelelezi unavotakiwa kuwa." Gunner aliongea hayo baada ya kuusoma ule ujumbe.
  Hakuishia hapo yule mwanaume, akaongea kwenye kinasa sauti alichokuwa kakivaa na baada ya dakika mbili akaingia msichana ambaye Martina alipomuona alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha akimuita mama mdogo.
  Lisa alikuwa katoa macho asiamini kile anachokiona mbele yake. Ni mzimu au nini?
  "Huyu ndiye ulikuwa ukipambana naye jana Lisa." Gunner aliongea kwa utaratibu kama kawaida yake.
  "Zakia!?" Lisa akaita kwa mshangao asiamini kile akionacho.
  "Ndiye mimi Lisa. Mchumba wa Mubarak. Prince Mubarak au Mubah." Mtu aliyeitwa Zakia alijibu kwa nyodo nyingi huku akimpapasa Martina kwa upendo.
  "Kweli jambo usilolijua, ni sawa na usiku wa kiza. Malocha aliongea haya hapo jana." Lisa akajikuta akiropoka.
  “Kuna muda unatakiwa kutambua kuwa hakuna siri inayodumu katika moyo wa mtu. Ukikuta siri imedumu baina yenu wawili, basi ujue ipo karibuni kuvunjika.
  Umenificha jambo dogo sana Lisa. Na kila siku nilikuwa nasubiri ulitamke, lakini ulishindwa kuniambia. Sijui ni mke wa aina gani wewe." Gunner alikuwa anaongea kwa makini hasa akitaka Martina asiyasikie yale maongezi."Baada ya kujua kuwa sina uwezo wa kuzalisha, nikatafuta ukweli juu ya hiki kijimtu nachokilea. Kishetani kipya, kidogo-dogo." Gunner alinyoosha kidole kwa Martina wakati anaropoka maneno haya.
  "Usimuite mwanangu hayo majina we' mshenzi mkubwa." Lisa naye kwa umakini alijikuta akimkaripia Gunner.
  "Nikafatilia kwa makini sana kuhusu hiki kishetani, ni cha nani? Ndipo nikapekua vitu vyako na kukuta ile picha aliyokuonesha Kamanda Lobo. Hapo ndipo nikajua kishetani baba yake ni yule mbwa muoga. Mbwa anayeogopa kurudi nchini kwao na kulowea nchi za watu. A coward." Lisa alijikuta akijawa na hasira na kurusha mkono wake lakini Gunner aliudaka vema na kumkamata Lisa kiuno wakawa kama wachezao nyimbo za taratibu.
  "Baada ya kugundua kuwa ni mtoto wa yule muoga au mzamiaji, nikaamua kuutafuta ukweli zaidi. Nikamfuata baba yako na kumuuliza kuhusu hali ile." Gunner alikuwa akiongea taratibu huku bado kamkamata Lisa kiuno na kucheza naye blues.
  "Jinsi baba yako alivyokuwa mjinga, akaanza kuniomba msamaha kama vile mimi ni MUNGU. Lakini kwa bahati mbaya, alinikuta si mimi yule niwezaye kucheka kama katuni. Akanikuta ni Gunner mwingine kabisa. Kwa hii mikono yangu." Gunner akamuachia Lisa na kukunja mikono yake hadi misuli kadhaa ikatutumka na kumuonesha ukubwa wa mwili wake."Nikamnyonga baba yako hadi akafa hapo hapo. Hiyo ndiyo ikawa ahueni kwangu Lisa, nikapunguza hasira zangu kihivyo." Gunner alimaliza akiwa na tabasamu pana kana kwamba kile akiongeacho ni kitamu sana kukimeza.
  "Martina. Nenda na mama mdogo kule nyumba nyingine, mimi nitakuja na mama eeh."Gunner alimwambia Martina ambaye hakupinga lolote bali kujawa na furaha hasa kwa kuwa huko kuna raha na starehe za kila aina kwa watoto.
  "Bayi mama." Martina alimuaga mama yake huku akiwa na furaha tele.
  "Muage mtoto wako Lisa." Gunner akamnong'oneza Lisa lakini Lisa hakufanya chochote zaidi ya kupumua kwa kasi kutokana na hasira zilizojishindilia akilini mwake.
  "Kama hutaki, basi. Muache aende." Lisa akashuhudia mwanaye anaondoka bila kuaga.
  "We mshenzi kumbe ndiye uliyemuua baba yangu." Lisa akamsukuma Gunner aliyekuwa akicheka kwa nyodo kutokana na hali ambayo Lisa alikuwa nayo.
  "Tena baada ya kumuua, tukavumisha kiharusi ndicho kilichombeba yule Mmarekani. Pesa tu." Gunner akazidi kumjaza hasira Lisa.
  Lisa akaanza kumpiga ngumi nyingi kila mahali mwanaume yule lakini ngumi zile zilikuwa kama kumpiga mwizi kwa ndala, hazimuumizi.
  Lisa akajikuta akiishiwa nguvu sababu ya hasira na hizo ngumi alizokuwa anazitupa.
  "Umemaliza wife?" Gunner aliuliza huku akiwa anatabasamu pana usoni pake. "Okay. Sasa ni muda wa wewe kwenda kumsalimu baba yako huko kuzimu. Nadhani kakumiss sana." Gunner akaongeza huku akianza kumufata taratibu Lisa ambaye naye alianza kusogea nyuma huku akitetemeka na maneno ya Malocha yakamrudia kichwani kuwa ni heri akutane na treni ya umeme relini kuliko kukutana na sura halisi ya Gunner.
  Mwisho wa safari ya Lisa ilikuwa ni kugota ukutani ambapo alishindwa kwenda zaidi nyuma.
  "Midomo yako, ni midomo ambayo nilienjoy sana pale nilipokuwa nainyonya. Ni milaini na inatoa sauti mororo pale inapokutana na kitu kitamu. Mmmh! You're so sweet my sweet Lisa." Maneno hayo yaliongozana na mkono wa kuume wa Gunner kushika midomo hiyo mwanana ya kiumbe Lisa.
  Hakuishia hapo, akashuka hadi kifuani na kuanza kuminya matiti murua na yenye mvuto aliyobarikiwa kuumbwa nayo Lisa.
  "Hapa ndipo ubovu wangu ulipo, always nilijihisi mwenye bahati kula mbivu kama hizi. Hakika zilinipeleka katika sayari nyingine ya mahaba. Kama usingekuwa na kosa hili ulilolifanya, ningeendelea kula kifua hiki mwanana." Akatoka kifuani Gunner na kuhamia katika kiuno chembamba na kilichojichimbia ndani kiasi na kisha kuibuka tena kwa chini kwa shepu matata.
  "Oooh Lisa. Unanichanganya na hichi kiuno chako hasa pale kinapozunguka katika maumbile yangu. Ulinichanganya kwa kila hila we' mwanamke. Kiuno chako hakifiki kwa yule Waziri malaya wa Wanawake. Alikuwa anajitahidi sana kukilandisha, lakini ni kama kabanwa na plaizi ya kiuno. Kiuno kigumu kama kinu." Gunner akacheka sana kutokana na maneno hayo. Akaendelea,
  "Najua utashangaa, lakini ndivyo ilivyo. Nilikuwa nachepuka naye mara kwa mara kwa sababu ya miradi anayomiliki. Lakini alifanya kosa moja tu! Ndilo lilimpeleka kaburini mpumbavu yule.
  Sijui alitumwa na nani kunichunguza. Akakosea akagusa pasipogusika. Nikampa roho yake Lobo. Na Lobo hafanyi makosa, akampa masaa. Akashindwa kutimiza kuachia madaraka na kuondoka nchini. Roho yake ikawa yetu baada ya kushindwa kuinunua." Gunner alizidi kumtisha Lisa ambaye alikuwa anatetemeka kama mwenye ugonjwa wa tetenasi.
  Gunner akazidi kushuka chini ya mwili wa Lisa. Akafika kwenye kitovu chake na kuanza kukifikicha kwa chati na kumfanya Lisa azidi kutetemeka lakini kwa kujisikilizia.
  Gunner akaenda mbali zaidi na kuingiza mkono wake ndani ya sketi matata aliyovaa Lisa. Akaanza kuukita mkono wake ndani zaidi.
  Kwa mwanamke anayejiheshimu na kujitambua, hiyo ni dharau isiyo na kifani. Na Lisa alitambua hilo. Kwa nguvu zake zote, akazitumia kumsukuma Gunner kutoka kwenye maungo yake.
  Gunner kweli aliyumba na ilikuwa kidogo adondoke.
  Wakati Gunner akitafuta balansi kutokana na ule msukumo, Lisa tayari alishajiachia kwa kuruka juu kidogo akiwa tayari kwa kumpa pigo la teke Gunner. Lakini bahati haikuwa yake, Gunner tayari alishamuona na teke la Lisa lilidakwa kiustadi na kisha akamrusha juu mwanamke yule ambaye naye alikubali hali ile. Mwisho wake ulikuwa ni kutua kwenye meza ya kioo iliyokuwapo sebuleni mle, ikavunjika vipande vipande.
  Gunner tayari alikuwa kajaa gesi ya hasira. Akamfuata Lisa pale chini na kuanza kumpa kipigo cha haja. Ngumi zisizo na idadi zilipigwa katika uso wa Lisa. Gunner hakuishia hapo, akazidi kumsulubu yule mtoto wa kike.
  Akamuinua na kumkwida blazia yake aliyokuwa kaivaa.
  Ngumi nyingi za tumbo zikaanza kupigwa kwenda kwa Lisa. Mtoto wa kike akawa anakohoa pumzi nyingi zisizo na idadi. Akalegea na kuwa tayari kwa kifo au kwa lolote toka kwa Gunner.
  "Nilikuwa naisubiri siku hii kwa hamu. Sasa imetimia. Nakuua kama nilivyomuua baba yako." Gunner aliongea hayo huku kamsukuma Lisa ukutani na kumkabia hapohapo hadi macho ya Lisa yakawa yanageuka na kuwa meupe. Hakika mwisho wa Lisa ulikuwa umewadia.
  Ilikuwa ni kama ndoto ambayo Lisa alikuwa anaiota kila wakati ili itokee. Kama ni sala, basi yawezekana MUNGU aliijibu haraka kuliko sala zake zote ambazo kawahi kuzisali.
  Gunner akiwa katika hatua za mwisho kummaliza Lisa kwa roba nzito aliyokuwa kamkaba, alishituka mlango wake ukifunguliwa na kabla hajakaa sawa alikutana na teke zito la kuzunguka kutoka kwa mvamizi huyo. Akiwa anayumbayumba kama mlevi, wakati huo kamuachia Lisa aliyekuwa anagaa gaa chini akikohoa kutokana na roba ya mumewe, akapokea teke lingine la kifuani na kumrusha hadi kwenye kochi lake. Akili ilikuwa haijakaa sawa kabisa kichwani kwa Gunner. Akijitahidi kuiweka sawa, anakutana na makonde mazito toka kwa mvamizi wake. Gunner ikabidi asaliti amri na kutulia pale kwenye kochi.
  Na hiyo ndiyo ilikuwa pona yake. Yule mvamizi akaenda hadi kwa Lisa na kumuinua kwa kumkalisha katika sakafu ya sebule lao.
  "Hahahaaa. Malocha Malingumu. Naona unajitahidi kuwalinda watu wako. Safi sana tena sana. Lakini kuna jambo moja ambalo hauwezi kutuzuia, Jumamosi hii, Rais wa Urusi tunamuangamiza. Itakuwa raha sana." Gunner aliongea huku meno yake yakiwa yamejaa damu
  "Hayo hayatuhusu tena. Ni kazi ya watu wengine. Go to hell Gunner." Malocha akampiga teke la kisogoni Gunner na hapohapo fahamu za yule bwana zikamtoka.
  Malocha haraka akamnyanyua Lisa na kuanza kutoka naye nje. Akaenda upande mwingine wa gari lake na kumpakiza Lisa aliyekuwa bado hajarudiwa na nguvu zake kama kawaida. Akampakiza nafasi ya mbele karibu na dereva kisha yeye akazunguka upande wa dereva na kutaka kuingia kwa ajili ya kuondoka. Lakini ni kama aliyekuwa kasahau kitu, akatoka haraka garini na kutaka kwenda ndani kwa Gunner ili amchukue.
  Lakini kabla hajafanya hayo, yaani hata hajafunga mlango wa gari lake, ilitokea pikipiki moja kubwa kiasi na mtu ambaye alikuwa kavalia kofia maalumu ya kuendeshea pikipiki, alitoa bunduki aina ya SMG na kuanza 'kumwaga njugu' kwenda kwenye gari la Malocha. Zaidi alikuwa anavamia upande wa Lisa ambaye aliingia chini ya uvungu baada ya kuona hali ile.
  Malocha naye alichutama huku akiwa makini kutokana na risasi ambazo zilikuwa zinamwagwa bila mpangilio.
  Baada ya sekunde kadhaa ya patashika kutoka kwa yule mtu mwenye pikipiki, risasi zikamuishia na alikuwa anaikoki tena kwa ajili ya kuendeleza 'tifu' alilolianza. Lakini kitendo cha kumaliza risasi, kikawa ni nafasi kubwa kwa Malocha ambaye alitoka eneo alilokuwa kajificha na kwa haraka akapanda juu ya boneti ya gari lake, na kwa ustaha wa ajabu, akaruka huku katanguliza mguu. Na mguu huo ukamkuta yule mwenye pikipiki na kumrusha pembeni ya pikipiki yake huku bunduki yake akiitupa pembeni kabisa na yeye.
  Wakati anajiuliza akiwa chini, Malocha alishafika na kumtwanga teke zito la kidevuni kama vile mpira na kuifanya kofia ya pikipiki kumvuka.
  Nywele ndefu zikavurugika na kupepea hewani baada ya kofia lile kuvuuka.
  "Ooh! Ni Zakia. Nadhani mwisho wako unaishia hapa leo. Umekutana na Israel mtoa roho,mbwa jike wee." Malocha hakuwa na maneno mengi mdomoni mwake, akakimbia kwa mwendo wa hatua za karibu~karibu lakini za haraka na Zakia bila kutambua, alikuta mtoto wa kiume yupo naye uso kwa uso.
  Ngumi za haraka toka kwa Malocha zilitiririka kwenda usoni kwa Zakia kabla hajamalizia kwa ngumi nyingine nzito ya kidevu iliyomrusha yule mwanamke hadi karibu na bunduki yake. Zakia kwa haraka akaishika bunduki yake tayari kwa kuinyanyua, lakini haraka yake haikuwa kitu mbele ya kasi ya Malocha.
  ITAENDELEA
   
Loading...