Riwaya-duka la roho

RIWAYA; DUKA LA ROHO
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
"Tatizo mnakurupuka nyie. Huyo muhudumu wenu katupa taarifa zote na tumemlipa pesa nyingi kuliko zenu." Masai akamchongea yule dada wa mapokezi. Gunner akamgeukia yule mwanamke aliyejikubua hadi kuwa mwekundu, akamuangalia kwa jicho baya.
"Nitakupata tu Masai. Huwezi kushinda vita vyetu hata siku moja. Wewe ni koko kama yalivyo mambwa koko mengine." Gunner alijibu mapigo kwa chuki nyingi.
"Haijalishi. Baadaye mje kuchukua maiti zenu." Masai akamjibu kwa nyodo.
"Okay. Na wewe baadae tutakupa taarifa njema ambayo itakulazimu tukutane tu." Gunner akajibu naye mapigo.
"Ni muda tu! Nasubiri." Simu ikakatwa baada ya maneno hayo ya Masai. Gunner akamsogelea yule muhudumu na kumkaba kwa mkono wake mmoja.
"Nani kakwambia uwaambie wale wajinga kuwa tunakuja hapa?" Hasira zilizojikita moyoni mwa Gunner ilijionesha wazi.
"Sijathemaaa." Dada yule aliongea kwa shida kwa sababu ya kabali aliyopigwa.
"Unasemaje?" Akaulizwa tena baada ya kuachiwa shingo yake. Akakohoa huku kainama kitu kilichomfanya Gunner ampige kofi la mgongoni. Dada yule akasimama huku anajikuna.
"Sijawaambia." Sauti iliyoambatana na kilio ilimtoka yule mwanamke.
"Lobo." Gunner akampa rungu John Lobo, mtu ambaye hana maongezi mengi bali vitendo. Mlango ukafunguliwa, na Gunner akiwa na wenzake wakatoka na kumuacha Lobo na yule dada.
"Huwa sipendi wambea, hilo moja. Pili wanawake wanaotumia muda mwingi kwenye kioo hata kazini, sitaki hata kuwaona. Na tatu, wanawake wanaojitoa rangi walizoumbwa nazo, nawafananisha na shetani mtoa roho. Hakuna anayempenda shetani huyu. Nikibahatika kukutana na huyu shetani, nitamuua. Leo nimekutana na mfano wake, unajua nini kitatokea?" Maneno ya Lobo yaliambatana na tabasamu la kuchonga na wakati huo anatoa bastola yake na kuanza kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Mwanadada yule akaanza kurudi nyuma huku akionesha hali ya kuomba msamaha na uoga ndani yake.
"Una sekunde ishirini za kutubu dhambi zako. Chagua kutubu, au kutotubu." Lobo aliongea baada ya kumaliza kufunga kile kiwambo cha kuzuia sauti.
"Jamani Kaka Jambazi nisamehee." Maneno yalimtoka yule dada na machozi kedekede, lakini Lobo hakujibu kitu.
"Zimebaki sekunde kumi. Kulia hakusaidii." Lobo akampa taarifa yule mwanamke huku akimuangalia usoni kwa macho ya vitisho.
"Naomba unisamehe MUNGU." Dada yule aliongea maneno hayo na muda huohuo Lobo akampiga risasi moja ya kichwa na dada yule hakufurukuta tena bali kudondoka na kupoteza uhai wake.
"Umbea umekuponza." Lobo akamtemea mate yule mwanamke na kutoka katika chumba kile.
****
Katika utaalamu wa kompyuta aliosomea Masai huko China, aliweza kujifunza mambo mengi sana yakiwemo kuunga namba fulani ya simu na kuwa simu zote zinaingia kwake tu. Na hicho ndicho ambacho alikifanya mwanaume yule. Akaunga namba anayowasiliana nayo Gunner na simu zote ambazo angepiga au kupigiwa Gunner, zingeingia kwake. Hata yule dada marehemu wa mapokezi, alikuwa anadhani anaongea na Gunner, alifanyiwa kitu hichohicho na kikamponza mbele ya mkono wa Lobo.
Gunner baada ya kutoka mle ndani, akaenda hadi kwenye kibanda cha simu na kupiga simu kwa wale wanawake. Ubaya wanawake wale walikuwa wana simu moja na simu hiyo pia Masai aliiunga kwake. Hata Gunner alipojaribu kupiga namba zile, alikutana na sauti ya Masai ikimcheka.
"Utahangaika sana mbwa wewe. Halafu hata wakitushinda, pale ni karibu na jeshini, tutasaidiwa na wanajeshi tu." Hayo ndio majibu ya dharau aliyoyapata Gunner baada ya.Masai kupokea simu.
Akaikata simu ile na mara hiyohiyo akaipiga Dar es Salaam.
"Andaa kile kitu na kukipeleka lile gholofa kubwa la Posta. Tunakuja usiku huu kumaliza kazi ya hawa wajinga. Tutawapata na kuwaua." Gunner akakata ile simu baada ya maneno hayo kisha akarudi katika gari lao na kumkuta Lobo akiwa katulia anasikiliza nyimbo za Eminem.
"Naweza kuondoka?" Gunner akamuuliza Lobo na Lobo akamuonesha kwa ishara mshirika wake aliyeliwasha gari na kuondoka eneo lile kuelekea barabara itakayowapeleka Dar es Salaam.
****
Masai akiwa makini katika usukani wa gari lao, alipita njia za mkato ili wawawahi wale Wairan na kuwasimamisha kwa kile walichopanga kukifanya. Gari lilikuwa lipo katika mwendo wa kasi kuliko kawaida.
"Tunakaribia kuwafikia wajinga hawa." Masai alitamka hayo huku akizidi kushindilia mafuta na kuyachoma.
Baada ya dakika kumi, wakaingia barabara ya rami na mbele yao kwa mbali walishuhudia gari aina ya Ford ikichanganya mbariga zake kwa kasi ya ajabu. Masai akazidisha kasi na punde wale waliomo kwenye ile Ford ya kisasa, waliliona gari la wakina Masai likiwafukuzia lakini hawakuwa na uhakika kama wanafukuzwa wao.
Masai akiwa makini na barabara, simu yake ikaita na sauti ya kike ikasikika kwa lugha ya kiingereza.
"Gunner. Mpo wapi?" Ilisikika sauti ikiuliza.
"Tupo nyuma yenu kuja kuwaangamiza." Masai akajibu na kukata simu kwa sababu alikuwa anapoteza umakini wa kuendesha gari lake.
Katika hali isiyo ya kawaida, wale wanawake wakaanza kurusha risasi kwenye gari ka Masai. Ilikuwa ni mshikemshike lakini Kamanda Masai alikuwa makini kukwepa hali ile kwa kupunguza mwendo na muda mwingine kwenda huku na huko.
"Malocha. Fanya yako." Kusikia hivyo, Malocha akakoki gobole lake na kutoa kichwa chake kupitia kioo cha pembeni. Akafyatua ule mzinga, risasi zikakita nyuma ya taa za gari lile. Akarudisha kichwa chake ndani na kukoki tena dude lake. Alipomaliza akatoa kichwa tena lakini wanawake wakaanza kutupa mvua ya risasi na kumfanya Malocha arudi ndani haraka.
"Mubah. Sehemu yako hiyo." Mubah aliyekuwa nyuma ya gari lile, akaruka nyuma zaidi na kufungua mlango wa nyuma ya V8 ile na kwa ustadi mkubwa, akachungulia kulia lilipo gari la maadui kuona kama anaweza kupata muonekano mzuri wa gari bila kudhulika na risasi zao. Alipoona hamna tatizo kubwa, akatoa mabomu mawili yaliyo kama viazi mviringo, akatupa moja baada ya jingine kwa nguvu. Mabomu yake yakalipukia pembeni na katikati hali iliyosababisha gari la wale wanawake kuyumba huku na huko.
"Safi jamaa." Malocha alimpongeza Mubah baada ya kurudi ndani.
"Wife." Masai akaita na kumpa ishara Lisa ambaye alitabasamu kabla hajafanya alichopangiwa.
Mtoto wa kike akasimama na kufungua paa la gari lile kisha akatoa bunduki ya kudungulia. Akaweka jicho lake kwenye lenzi na wakati huo gari analoendesha Masai lilitulia na lilikuwa haliendi kasi kama mwanzo.
Gari la maadui wao lilikuwa limetulia na kuendelea na safari kwa kasi ya ajabu.
Lisa akafyatua risasi ya kwanza, ikakosa lengo alilolenga. Akakoki na ganda la risasi likadondokea ndani, akaweka tena jicho lake kwenye lenzi na kufyatua bunduki yake. Risasi akanyooka na kutua katika tairi la wapinzani wao. Gari ya wakinadada wale inapoteza mwelekeo na kujikuta ikiyumba na baadae kugeuka na mbele kukawa nyuma huku nyuma kukiwa mbele.
"Malochaa." Masai akaita kwa sauti na Malocha akatoa uso wake tena akiwa kakamata gobole lake, akafyatua na risasi zikatua kwenye boneti la gari lile na kuifunua kabisa.
Masai akapiga breki ya gari lake na kushuka haraka pamoja na RPG 4. Akaiweka begani na kulenga gari ile ambayo ilikuwa imepoteza dira. Akafyatua mashine ile na bomu la mashine ile likachomoka na kutua kwenye gari lile. Mlipuko mkubwa ikatokea eneo lile ukiambatana na moto mkali. Wale wanawake wakawa hawana chao mbele ya Watanzania watata.
Kundi zima la Malocha likatoka na kwenda kushangilia ushindi wa kuliteketeza kundi lile la kishenzi. Wakashangilia na kucheza kwa furaha katika pori lile kubwa lakini limepitiwa na barabara.
"Mikono juu." Sauti kali ya amri iliwaamrisha wakina Masai waliokuwa wanashangilia kwa furaha.
"Tupa silaha zote." Sauti nyingine ilitoka nyuma yao. Wakatii kwa kufanya wakitakacho.
"Haya geuka." Amri nyingine ikatoka. Walipogeuka walikutana na sura za wanajeshi nane wakiwa na M16 silaha hatari kabisa kwenye mapambano.
"Naitwa Malocha Malingumu." Malocha alijaribu kujitetea kwa kujitambulisha.
"Mnafanya nini katika eneo la jeshi tena na silaha za kivita?" Aliyeonekana kiongozi wa kikosi kile aliuliza kwa sauti ya juu.
"Tumekuja kuwamaliza magaidi waliokuwa wanakuja kuteketeza kambi yenu." Sauti hiyo ya Malocha iliwafanya wale wanajeshi kunyamaza kidogo na kisha kuwaamuru Malocha na wenzake kusogea walipo wao.
Wakasogea huku mikono yao ikiwa juu kama mateka wa Kimarekani mbele ya Wavietnam.
"We ndiye Masai. Shenzi, unasakwa." Maneno yakamtoka yule mkuu na kumlenga Masai jambo lililofanya kila mwanajeshi kufanya hivyo.
"Tumetumwa na Rais kazi hii. Msijidai mnajua sana, mtapotea wote." Malocha ikabidi atumie sauti yake ya kiume.
"Rais hawezi kuwatuma magaidi mahiri kama nyie." Kiongozi wa jeshi lile akazidi kuzogoa.
"Mpigie simu na muulize." Malocha aliongea huku akiingiza mkono wake mfukoni bila uoga na kutoa simu ambayo alimrushia yule mkuu.
Simu ikadakwa na mwanajeshi aliyeonekana mjuzi wa mambo mengi, akapiga namba za Ikulu tukufu ya Tanzania. Na sekunde kadhaa, akawa anaongea na mtu wa mapokezi aliyemuunga moja kwa moja hadi kwa Rais baada ya kujitambulisha kwa jina la Meja Jenerali Kiroboo Mapombe.
"Watu wangu hao. We hujui Dar imekuwa vurugu huku? Nimewatuma waje kuwamaliza hao wajinga. Waachieni wafanye kazi yao." Sauti ya Rais iliongea na Meja Kiroboo alisaliti amri kwa heshima kubwa.
"Sawa mkuu." Akakata simu baada ya maneno ya Rais. "Okay. Shusheni silaha zenu wazee." Kiroboo aliwaamuru wenzake na wao wakatii. "Shusheni mikono nanyi." Akatoa ombi kwa wakina Masai ambao walikuwa bado wamenyoosha mikono juu kasoro Malocha.
Baada ya hayo, wanajeshi wale waliwasogelea wazee wa kazi na kuwasalimia kiheshima kama wafanyavyo kwa wakuu wao.
"Kwa hiyo hawa ni wale wanawake magaidi?" Kiroboo aliwauliza wakina Masai baada ya kupata mkasa mzima uliyotokea.
"Ndio hao aisee. Walijidai maninja sana." Mubah aliwajibu baada ya kuona swali lile hakuna aliyelitilia maanani kwa sababu tayari kila kitu kilishawekwa hadharani.
"Okay. Basi twendeni hapo mbele tuwape gari lingine maana hili sidhani kama mtafika nalo mpatakapo."
"Sawa kabisa. Ila kuna vitu vyetu, naomba wazee mvitoe na silaha zetu tuokoteeni." Malocha aliongea huku wenzake wakiwa kimya wakimfatilia kwa makini.
Kiroboo akawatuma vijana wanne na kwenda kulipekua gari lile na kuchukua kila kitu ambacho kilikuwemo ndani yake. Baada ya kumaliza, wakaokota silaha ambazo walizitupa wakina Malocha na kisha wakaelekea ambako wenzao wameelekea.
Lilikuwa ni gari pana la jeshi aina ya Hummer, gari zinazotengenezwa Marekani. Ilikuwa ina matairi mapana na imara kitu kinachoyafanya magari haya iwe ngumu kupinduka au kukwama kwenye tope au kushindwa kupita sehemu zenye kutitia.
"Okay wakuu. Gari lenu ndilo hili. Kuna msaada mwingine mnaoutaka?" Kiroboo akauliza.
"Ndio Meja." Kwa mara ya kwanza Masai akaongea.
"Sema mheshimiwa." Kiroboo akatoa ruhusa.
"Nguo zangu zimechafuka. Naweza kupata kama zenu hizo."
"Hamna tatizo Kamanda." Kiroboo wala hakuwa na pingamizi kuhusu hilo. Akachukua simu ya sauti ya upepo na kuwasiliana na mwanaugavi wa kambi yao na kumuomba aje na mzigo alioutaja kwa namba wazijuazo wao.
Simu ya upepo ikakatwa na wazee wa kazi wakaanza kupanga vitu vyao kwenye gari lao jipya ambalo kwa mbele ya kioo kulikuwa kuna nyavu maalumu ya kuzuia majani na uwezekano wa kioo kuvunjika.
Baada ya dakika kumi na tano, ikaja Jeep ya jeshi na wanajeshi wawili walishuka wakiwa na mabegi mawili makubwa kiasi. Wakamkabidhi Kiroboo na kupiga saluti. Kiroboo akawapa yale mabegi wakina Masai.
Masai akawa wa kwanza kufungua. Akapekua na kukuta kombati zikiwa 'full'. Palepale akavua nguo za juu na kuvaa kombati zile. Baada ya hapo, akavua na kaptula yake kisha akapachika mwilini suruali ya jeshi la Tanzania.
Kwa kumuona tu! Huwezi kukataa kuwa jamaa ni mwanajeshi hai wa jeshi la wananchi wa Tanzania. Urefu, rangi na muonekano wake, wala huulizi kama ni mwanajeshi.
Wote walitabasamu na kila mmoja akapendezwa na muonekano wa Masai. Wakapekua nao kwenye mabegi na kwenda vichakani kuzivaa kombati walizoletewa. Baada ya kuvaa, wakarudi na kukwea gari walilopewa na kuanza kurudi mjini ikiwa tayari muda umeenda.
****
John Lobo, Gunner Samuel Bokwa, Boyka na wataalamu wenzake wawili, walikuwa wanachoma mafuta mida ya saa kumi na mbili jioni kuelekea Dar es Salaam kutoka Arusha walipotoka mida ya saa saba mchana. Gunner akiwa nyuma ya usukani, injini ya gari lao ilikuwa inakoroma kwa sauti kali kutokana na kukanyagwa mafuta kwa wingi.
"Saa mbili usiku tutakuwa Jijini." Gunner Bokwa akatamka hayo huku gari yake akizidi kuichochea kwenye rami mtelezo ya Tanzania.
"Nadhani wakina Hulyaman wamekwishapotea katika uso wa dunia hii." Mlinzi yule aliyepigwa kichwa na Masai hadi meno yakang'ooka, aliongea kuhusu wale wanawake na kumfanya Gunner amtazame kwa jicho la ubaya. Baada ya jicho hilo, akamgeuka Lobo na kumpa ishara fulani. Lobo wala hakufikiria jambo, akachomoa bastola yake na kumpiga risasi ya kichwa yule bwana.
Gunner akakanyaga breki kali na kusimama, kisha akawaambia wale wataalamu wa kompyuta waitoe ile maiti na kuitupia porini. Baada ya kumaliza, wale majamaa, wakarudi garini ambapo waliwakuta Lobo na Gunner wakiwasubiri kwa kuliacha gari likinguruma.
"The most died man in this world, is a coward. (Mtu anayekufa sana dunia hii, ni muoga)" Gunner aliongea msemo ambao ulimuingia kila mmoja kichwani. "A coward never lives long but died so simple, just like this bastard. (Muoga haishi muda mrefu lakini hufa kifo rahisi sana, ni kama huyu mpumhavu)" Gunner akazidi kutiririka. "It's better dies like a man, than a coward. Am I clear? (Ni bora kufa kama mwanaume kuliko kama muoga. Nimeeleweka?"
"Ndio mkuu." Wakajibu wale mabwana kwa heshima.
 
RIWAYA; DUKA LA ROHO
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
Gunner akakanyaga breki kali na kusimama, kisha akawaambia wale wataalamu wa kompyuta waitoe ile maiti na kuitupia porini. Baada ya kumaliza, wale majamaa, wakarudi garini ambapo waliwakuta Lobo na Gunner wakiwasubiri kwa kuliacha gari likinguruma.
"The most died man in this world, is a coward. (Mtu anayekufa sana dunia hii, ni muoga)" Gunner aliongea msemo ambao ulimuingia kila mmoja kichwani. "A coward never lives long but died so simple, just like this bastard. (Muoga haishi muda mrefu lakini hufa kifo rahisi sana, ni kama huyu mpumhavu)" Gunner akazidi kutiririka. "It's better dies like a man, than a coward. Am I clear? (Ni bora kufa kama mwanaume kuliko kama muoga. Nimeeleweka?"
"Ndio mkuu." Wakajibu wale mabwana kwa heshima.
"Pandeni ndani ya gari. Bado wale wanawake wapo hai. Hakuna atakayekufa." Gunner akaongea na wale jamaa wakakwea ndani ya gari lililowashwa na kuondoka kwa kasi ileile waliyokuwa nayo kabla hawajasimama.
Saa tatu usiku, gari linaloendeshwa na Gunner lilikuwa nje ya nyumba moja kubwa kiasi. Ilikuwa ni nyumba nzuri na ya kisasa lakini huwezi kuamini ukiambiwa anayeimiliki ni msichana mdogo tu! Ambaye hajulikani anafanya kazi gani, na mbaya zaidi hajawahi kuonekana na mwanaume yeyote huyu dada.
Gunner na kundi lake wakashuka ndani ya gari lao na kupakua mizigo kadhaa ikiwemo mtambo mdogo ambao walikuja nao wale wanawake kwa ajili ya kuchapa fulana walizokuwa wanazivaa. Wakaingia ndani wakiwa wapo kamili kwa lolote. Hiyo ni baada ya yule msichana kufungua mlango.
"Yule kuku unaye au ulimpeleka kule gholofani nilipokwambia." Gunner akamuuliza yule msichana.
"Sikupata mtu wa kumuachia kule. Hivyo ninaye bado hapa." Yule dada alijibu kwa ujasiri.
"Okay. Good. Yupo macho?" Gunner akatupa swali lingine wakati huo Lobo alikuwa kajiegesha kwenye kochi moja na kukunja nne.
"Ndio bado hajalala. Kutwa nzima anawaulizia watu aliowazoea."
"Embu mlete hapa." Yule dada akatoka eneo lile na kwenda chumba cha pili baada ya sebule lake. Baada ya dakika moja, alitoka na mtoto wa kike.
"Babaaaaa." Sauti ya mtoto mdogo iliita na kwenda kumkumbatia Gunner.
"Hayaa Martina. Hujambo katoto kangu." Gunner alimuuliza mtoto yule ambaye ni Martina, mtoto wa Lisa na Masai. Yule rafiki ambaye Lisa alimuona kama mwokozi wake, sasa kamsaliti na kumuuza mwanaye kwa wakina Gunner.
"Sijambo. Mbona hukunitafuta tena?" Martina aliuliza kwa unyonge.
"Ndio nimekuja hivyo. Umemuona anko?" Gunner akamuonesha Martina alipo Lobo. Kwa furaha Martina alienda na kumsabahi John Lobo.
"Shikamoo anko."
"Marahabaa Tina. Hujambo." Gunner akaonesha upendo wa usoni na kumfanya Martina kucheka hadi mapengo yake ya pembeni yakaonekana. Mtoto akawa na faraja baada ya kukutana na timu ambayo yeye alidhani ni familia yake na kumbe ni chui ndani ya ngozi ya kondoo.
"Mama yupo wapi baba?" Martina alimuuliza Gunner baada ya kupiga story hizi na zile.
"Oooh! Unataka uongee na mama eeh." Martina akaitikia kwa kichwa. Gunner akatoa simu yake na kupiga namba za wale wanawake ambapo kwa uhakika alijua ni lazima itaita kwa Masai.
"Haloo Gunner." Sauti ya Masai ilitikia.
"Mpe mke wangu aongee na mwanaye." Gunner akaongea huku katabasamu. Masai akashtuka na kujihisi kutaka kudondoka na wakati huo walikuwa pembeni ya jiji la Arusha wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kesho kurudi Dar Es Salaam.
"Hey. Mpe mke wangu simu." Gunner akarudia kauli yake tena.
"Haloo." Sauti ya Lisa ikasikika.
"Haloo wife. Ongea na Martina." Gunner akampa simu Martina.
"Hey mamy. I miss you." Martina aliongea kwa furaha baada ya kupewa simu. Lisa akawa kama mtu aliyepigwa ganzi la mwili kwa kitendo kile alichokifanya Gunner.
"Martina. Anti Salome yupo." Lisa aliuliza kwa taratibu.
"Yupo. Nachezaga naye."
"Nipe niongee naye kidogo.",
"Haya." Martina akakubali na kumwambia Gunner kuwa mama yake anataka kuongea na Salome, yule mwanamke aliyemkabidhi mwanaye.
"Haloo Lisa. Mambo vipi shosti." Salome aliongea kwa madaha.
"Mbona nilikuamini sana Salome? Why?" Lisa aliongea kwa uchungu.
"Never trust a woman. A woman is like a coin, have two sides. Don't you remember this quote from our teacher? (Usimuamini mwanamke. Mwanamke ni kama sarafu, ana pande mbili. Hukumbuki hii kauli kutoka kwa mwalimu wetu?)"
"Nimekuelewa Salome. Nakuja kukuangamiza kwa mikono yangu. Msaliti mkubwa wee."
"Trust No One. Ongea na mumeooo." Salome alimpa simu Gunner kwa kujiamini na bila kuogopa ile kauli ya Lisa.
"Okay Lisa. Hayo ni yenu na 'best' wako, siingilii."
"Unataka nini Gunner." Lisa akauliza kwa hasira.
"Hujui nikitakacho?"
"Ndio sifahamu."
"Mpe simu Masai. Atakuambia tukitakacho."
"Ipo 'Loud Speaker' simu yetu, ongea tu." Malocha akadakia kwa nguvu.
"Oooh! Malocha. Mambo vipi jamaa." Gunner akasalimia huku akimpa ishara Salome amwondoe Martina pale sebuleni.
"Ongea shida yako." Malocha alifoka wakati huo Masai alikuwa kimya ndani ya kombati zake akitafakari hili na lile hasa kutekwa kwa mwanaye.
"Sina jipya miye. Ongeeni na Lobo." Gunner akampelekea simu Lobo wakati huo Martina alikuwa amekwishaondole
wa pale.
"Nahitaji kumsikia Masai tu. Nyie wengine kaeni mbali au kimya. Atakayeongea neno moja, ni sawa na kidole kimoja cha Martina. Sheria nitaifata na nitatimiza hilo." Kihere here kikawaisha waropokaji wote hasa kwa sababu walimfahamu Lobo maneno yake.
"Ongea shida yako." Masai akaanzisha maongezi.
"Kitambo sana sijaongea na wewe Masai."
"Na mimi ni kitambo sijakuvunja pua yako." Masai akajibu.
"Siku nyingine nitakuvunja yako." Lobo akajibu mapigo.
"Shida yako nini?"
"Roho ya Martina ipo dukani. Nunua au uza, chaguo ni lako. Ukitaka kununua, njoo haraka Dar es Salaam na tukutane katika gholofa lile la Posta. Ukitaka ninunue mimi roho ya Martina, basi usije. Nakupa masaa arobaini na nane kuanzia sasa. Tick Tock." Lobo akamaliza kwa sauti yake nzito.
"Nakupa masaa arobaini. Usipomuachia Martina, roho yako naiuza kwa Mubah. Niamini nikwambiacho. Kabla ya masaa arobaini na nane, tayari roho yako itakuwa mikoni mwa Mubah." Masai naye akatoa sheria yake.
"And let the game begins. Tick Tock." Lobo aliongea na kumpa simu Gunner. "Hakuna sheria katika huu mchezo. Ruksa kuja kundi lenu lote. Tick Tock." Gunner hakusubiri majibu ya upande wa pili, akakata simu yake.
*****
Pumzi ndefu ya uoga ikamtoka Lisa. Mawazo yakawa tele juu ya mwanaye. Akatoka mle ndani alipokuwa na wenzake na kwenda nje ya hoteli ile. Masai naye akatoka na kumkuta mpenzi wake akiangalia angani kama mwenye kuhesabu nyota za usiku ule.
Masai akamkamata kiuno na kumkumbatia kwa nyuma mwanamke wake.
"Usijali Lisa. Mambo yote yatakuwa sawa." Maneno hayo toka kwa Masai ni kama ndio yakamwambia Lisa alie. Mtoto wa kike akaanza kulia kwa kwikwi na kuanza kumpa wakati mgumu Masai ambaye alokuwa anajitahidi kumbembeleza.
"Frank. Naomba tuondoke sasa hivi kwenda Dar." Lisa alitoa ombi baada ya kulia kwa muda mrefu.
"Hapana Lisa. Tupumzike kwanza. Kesho asubuhi, tutakuwa barabarani." Masai alimuomba Lisa ombi ambalo Lisa hakupinga japo moyoni alitamani waondoke muda ule.
Akamchukua mpenzi wake na kumpeleka chumba ambacho wangelala usiku ule.
"Nakuja Lisa. Naenda kuongea na Malocha." Masai alimuaga Lisa ambaye alikuwa kajikunyata kitandani huku akajifunika blanketi zito sababu ya kuzuia baridi kali iliyokuwa inaendelea katika Jiji la Arusha.
"Mubah. Malocha yupo wapi?" Masai akamuuliza Mubah ambaye alikuwa katika chumba alichotakiwa kulala na Malocha.
"Katoka mara moja." Akajibu Mubah kwa upole.
"Okay. Usiku mwema." Masai akataka kutoka baada ya kuaga lakini Mubah alimuita na kumuomba aongee naye. Masai akarudi chumbani na kwenda kukaa kitandani kwa Mubah.
"Kaka. Nakuita kaka kwa sababu umenizidi mambo mengi sana." Mubah alianza kuongea. "Katika maisha yangu, sijawahi kupitia nyakati ngumu kama hizi. Naishi kama njiwa aliyeachwa na wazazi wake ili akajitegemee. Nimepoteza familia yangu yote akiwemo mjomba wangu kipenzi." Chozi likamtoka Mubah wakati anatabainisha maneno yale.
Masai akamshika bega na kumgonga gonga kama kumpa faraja. Mubah akafuta machozi na kuendelea.
"Mpenzi wangu niliyedhani ni mpenzi, akanisaliti na kuuza familia yangu kama rafiki wa Lisa alivyofanya. Mwanamke niliyempenda kuliko kitu chochote, kumbe ni joka lenye mapembe. Shetani mkubwa kabisa kuliko shetani mwenyewe. Akaisababishia familia yangu iteketee. Inauma sana Kaka Masai. Inauma vibaya sana.
Lakini nimekuwa jasiri kama ambaye sijakutwa na mkasa. Ninejitahidi kulia ndani ya maji ili machozi yangu yasiwe.kikwazo cha kazi yangu, na nimefanikiwa.
Leo hii nasikia mtu yuleyule aliyeondoa roho za familia yangu, anataka kuondoa roho ya mtoto anayelingana na mjomba wangu. Haiwezekani Masai, nipo tayari kufa mimi na si Martina. Nitapigana hadi kufa." Mubah akafuta chozi lililokuwa linatiririka na kuapa kiapo cha nguvu.
"Hakuna atakayekufa Mubah. Niamini mimi. Hakuna kifo tena kati yetu." Masai aliongea kwa kujiamini.
"Nitakufa kwa hili Masai. Lakini kabla sijafa, Lobo atakufa kwa risasi zangu." Mubah akaapa tena.
"Huwezi kufa. Lobo ni mali yako." Masai aliongea huku ananyanyuka na kutoka chumbani kwa Mubah.
Saa kumi na mbili alfajiri, kundi la Malocha lilikuwa limekwishaanza safari ndefu ya kutoka Arusha kuelekea Dar Es Salaam. Wakiwa katika mavazi yao ya jeshi la wananchi pamoja na gari pana ya Jeshi hilo hilo, hakuna hata mmoja ambaye akikuwa anawaza jema nafsini mwake. Akili yao ilikuwa imetapakaa kisasi pamoja na vita kati yao na kundi hatari la Gunner.
Kila Malocha alipojaribu kukanyaga mafuta ya gari lile, aliona kama hayakanyagiki bali kupungua mwendo japo gari lilikuwa katika kasi isiyo ya kawaida.
"Malocha slow down." Ndita, mtaalam wa kompyuta alimuonya Malocha juu ya kasi anayoendeshea gari. Malocha hakuwa hata na wazo la kujibu chochote bali kuendeleza kazi yake ya kulikimbiza gari lile.
"Yupo kazini, muache." Masai akamtaarifu Ndita.
****
Upande wa Gunner na Lobo, hali yao ilikuwa ni imara kimawazo na kimwili. Walikuwa hawana wasiwasi hata kidogo kuhusu maisha yao. Kila muda walitazama saa zao na kuangalia kama muda umefika.
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom