Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

Kwanini ifutwe? Mbona kwenya magazet watu wanasubiri week nzima??

Iletwe upya ikikamilika. We uliona wapi mtu anaachia hadithi huku bado inaendelea kutungwa? Ataihariri saa ngapi?
Lazima itakua chini ya kiwango.
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA KUMI NA NANE

Baada ya kufanikiwa kumuuwa Mbili wa Six Killers Daniel Mwaseba akauacha mwili wa Mbili pale chini na kuusogelea ule mlango wa kile chumba cha chumba cha mateso.....chumba cha kifo!
Alifungua mlango taratibu na kuchungulia kwa nje, kulikuwa shwari. Hakukuwa na lolote la kutilia shaka. Daniel Mwaseba akaiangalia ile nyumba ya bluu kwa hasira. Akijua kuwa watu wale makatili walikuwa mle ndani. Daniel Mwaseba akapiga hatua za haraka kuelekea kule kwenye nyumba ile ndogo ya bluu.

Kule nje ya nyumba ile, walikokuwa Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi waliomaliza usiku ule wakiwa katika hali ya kusubiri. Hadi asubuhi inafika Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa bado wanasubiri, walikuwa hawajapata namna ya kuingia mle ndani ya kambi ya Six killers. Walibaki wamejibanza vilevile, sehemu ile nyuma ya mti mkubwa wakisubiri kudra tu za Mwenyezi Mungu ili waweze kuingia mle ndani. Na kwa bahati mbaya sana hadi sasa hizo kudra za Mwenyezi Mungu zilikuwa hazijawafikia bado..nao waliendekea kuzisubiri....


Nakubali fupi...ila nd'o niliofanikiwa kuedit kwa Leo...

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI_; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA KUMI NA TISA

Kule nje ya kambi Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi bado walikuwa wanasubiri, walikuwa wanasubiri nafasi yoyote ile ya kuwawezesha kuingia katika kambi hatari ya Six Killers. Hadi muda huo hawakuiona nafasi yoyote ya kuweza kuingia mle ndani. Na kwa kujificha tu pale nyuma ya mti sidhani kama wangeiona...... Hata wangekaa mwezi....

Baada ya kusubiri sana, Dokta Yusha alipata wazo na kumshirikisha Mwanasheria mlevi.
Walikubaliana.
Dokta Yusha alitoka pale nyuma ya mti walipokuwa wamejificha na Mwanasheria mlevi, kwa mwendo wa taratibu na umakini mkubwa alianza kuizunguka ukuta wa kambi ile hatari. Mwanasheria mlevi alibaki pale kwenye mti kwa dhumuni maalum. Yeye alikuwa anamlinda Dokta Yusha kwa macho na kutoa ishara endapo itatokea hatari yoyote. Hivyo ndivyo walivyokubaliana mashujaa wale.

Dokta Yusha bila kujijua alikuwa anafanya mchezo wa hatari sana. Kuizunguka nyumba ile ilikuwa ni zaidi ya hatari, tena asubuhi namna ile.
Mzunguko ule wa Dokta Yusha hatimaye ulimfikisha sehemu ulipokuwepo ule mti ulio karibu na ukuta wa kambi ile, mti uleule aliotumia Daniel Mwaseba kuingia mle kambini. Dokta Yusha nae alipata akili sawa na alizopata Daniel Mwaseba. Naam Dokta Yusha alipanda juu ya ule mti. Tofauti ilikuwa wakati Daniel Mwaseba alipanda mti ule na kuingia ndani ya kambi usiku wa manane... Yeye alipanda katika mti ule asubuhi na kutaka kuingia ndani ya kambi ya Six Killers asubuhi. Dokta Yusha alikuwa amefanya jambo hatari sana, kujianika mbele ya wauaji hatari wa Six Killers namna ile!

Kumbuka Daniel Mwaseba katoka ndani ya chumba cha mateso..anaelekea katika jumba lao...Dokta Yusha nae amejianika juu ya ukuta asubuhiiii..bila kujari..bila kuogopa..nini kitatokea?

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA ISHIRINI

Dokta Yusha alifika hadi pale kileleni, juu ya ukuta. Kutokea kule kwa juu alishuhudia vizuri mandhari ya kule ndani ya kambi, ambayo yeye alikuwa anayafahamu vizuri kabla......

Kumbuka Dokta Yusha alipanda ule ukuta wa kambi ile hatarii asubuhi jua likiwa limechomoza, na pia Dokta Yusha alikuwa kashawahi kuingia katika kambi ile, na kwa bahati nzuri zaidi alibahatika kutoka salama. Akiwa pale kwa juu alipeleka macho yake katika kibanda kilichokuwa pembeni kidogo mwa ile nyumba ya bluu. Dokta Yusha alikumbuka mengi sana wakati anakiangalia kibanda kile. Alimkumbuka yule askari aliyepoteza uhai wake katika kiti cha kifo ndani ya kibanda kile. Askari aliyekufa kwa kubadirika rangi na kuwa nyekundu sambamba na kiti kile na kupotea katika ulimwengu kwa kuyeyuka palepale katika kiti cha kifo.
Dokta Yusha alimkumbuka yule jamaa aliyepambana nae katika kibanda kile, na kufanikiwa kumsukuma katika kiti cha kifo! Kilichopo ndani ya kibanda alichokuwa anakitazama. Nae aliyeyuka huku akibadirika rangi sambamba na kiti. Akiwa kule juu Dokta Yusha alijipa moyo, huku akijivika ujasiri kuwa lazima akapambane!
Sasa dokta Yusha alifuta kabisa hali ya hofu katika moyo wake na kuona ni heri kufa kishujaa, kuliko kuishi ukiwa unashuhudia maovu yakiendelea kufanyika ulimwenguni. Kilikuwa ni kiapo alichoapa Dokta Yusha akiwa juu ya ukuta hatari....na alipania kukitekeleza kiapo chake.

"Nitakufa nikipambana..." Dokta Yusha alihitimisha mawazo yake kwa kujisemea mwenyewe kimoyomoyo.

Kwa taarifa tu, ule mti uliokaribu na ukuta wa kambi ya Six Killers uliachwa kwa makusudi na kundi la Six killers sehemu ile. Hawakutaka kuukata ingawa walikuwa na uwezo huo. Ni Moja wa six Killers ndiye aliyeshauri mti ule uachwe, kwa makusudi ili utumike kama mtego. Ndio...... Waliuacha mti ule wakijua adui yoyote akitaka kuingia katika ile nyumba lazima atautumia ule mti. Maana ndo sehemu pekee iliyokuwepo kwa mtu mjanja kuingia mle ndani ya kambi yao. Nao kule ndani hawakuzubaa hata chembe, wakiwa kule kwa ndani walikuwa wanaulinda kwa kuuangalia ule mti kila baada ya dakika tatu....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Utajibeba mxiuuu achana na mimi, mimi sio dada ako wala sina undugun wewe tafadhal

Si bure umerogwa!
Nimekuita dada nakujua mie? Naanzaje kumuita dadaangu bidada?
unalo lilokuganda.
 
Si bure umerogwa!
Nimekuita dada nakujua mie? Naanzaje kumuita dadaangu bidada?
unalo lilokuganda.

Peleka kichaa chako uko mxiuuuu ,usinizoee sina undug na wewe na ukome kuni quote mbuzi wewe mxiuu
 
SIMULIZI: BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA ISHIRINI NA MOJA

..........Komando Moja wa Six killers akiwa kule kwa ndani alimshuhudia vizuri sana mtu akipanda katika mti wao. Mti wa mtego ulioachwa kwa sababu maalum. Na sasa sababu za kuachwa ule mti zilileta matokeo. Tena matokeo yenyewe yalitokea na kuonwa na Moja mtu ambaye ndiye alishauri mti ule uachwe kama mtego. Yeye ndio alikuwa zamu kuulinda mti ule. Na ilikuwa kazi rahisi sana kwake kumshudia mtu yule akiwa katika kilele cha ule mti wa mtego. Na alimshuhudia yule mtu hadi jinsi akivyoruka toka kule mtini mpaka pale katika ukuta wa kambi yao. Alivyofika juu ya ukuta alimshuhudia mtu yule akiangalia kibanda chao cha kufanyia mateso..kibanda chenye kiti cha siri, kiti cha kifo!
Moja alimtambua mtu yule...

"Dokta Yusuph Shaweji, daktari mfukunyuku umekifata kifo chako! Tena umekifata ukiwa unakikimbilia kwa kasi! Hahaha...umekutana na malaika mtoa roho hahaha" Moja aliongea peke yake huku akitoka nje taratibu kwa kicheko chake cha karaha.

Wakati uleule ambao Moja wa Six Killers alikuwa anatoka nje ya nyumba ile ya bluu ili kwenda kumvia na kumuua kabisa Dokta Yusha kama alivyojiahidi mwenyewe akiwa ndani ndio wakati uleule ambao Daniel Mwaseba alikuwa anatoka kule kwenye kibanda cha mateso. Alikofanikiwa kumuua Mbili.

E bwana wee!

Komando namba moja wa kundi hatari la Six killers na Mpelelezi mahiri nchini Tanzania Daniel Mwaseba walikutana uso kwa uso.....Kumbuka Dokta Yusha bado yuko juu ya ukuta...

Nini kitatokea......

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Back
Top Bottom