mapengo junior
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 1,135
- 276
- Thread starter
- #341
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA MIA NA KUMI NA TATU
Daniel Mwaseba alijinyanyua taratibu pale chini, akiwa bado yuko makini na kile kiti cha moto, kiti cha kifo! Daniel Mwaseba alikuwa anakiangalia kiti cha kifo huku akitabasamu. Kwa mwendo wa taratibu alianza kukisogelea kile kiti cha kifo!
Daniel Mwaseba alikitambua kile kiti cha kifo.
Naam...alikitambua!
Daniel Mwaseba alikuwa anazijua vizuri sana habari za kile kiti cha kifo. Ni yeye ndiye aliyetumwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukileta kile kiti nchini, toka katika Jamhuri ya watu wa China. Alikumbuka vizuri kuwa alimuuliza Waziri mkuu kuhusu matumizi ya kiti kile hatari, na alikumbuka kuwa jibu la Waziri mkuu lilikuwa fupi tu..
'Ni kwa sababu za kiusalama'
Daniel Mwaseba alienda China kwa shingo upande. Kwa kuwa hakuridhika kabisa na jibu alilopewa na Waziri mkuu wakati huo. Alikuwa anajua vizuri uwezo na maajabu wa kiti kile. Ni kiti hatari kuliko hatari yenyewe. Pamoja na kuwa na muonekano wa kiti kwa sasa lakini kilikuwa na uwezo wa kubadirishwa na kuwa silaha mbalimbali hatari. Kiti kilikuwa na uwezo wa kuwa Bomu kubwa hatari la Maangamizi na kuleta athari kubwa sana sehemu litakaporushwa ama kutegwa. Kiti pia kilikuwa kinaweza kubadirika na kuwa bunduki kubwa za kivita. Uwezo hatari wa kiti kile nd'o sababu iliyomfanya Daniel Mwaseba aende China kukifata kiti kile kwa shingo upande. Sababu kuu ya mashaka ya Daniel ilikuwa.....Wakati huo nchi haikuwa na uhaba wa silaha katika maghala yake...na wala hakukuwa na tishio la usalama kwa nchi. Sasa kwanini nchi inunue gharama ghali na hatari namna ile? Pamoja na mashaka yake lakini Daniel Mwaseba alienda China, hakutaka kupinga kabisa agizo la Waziri mkuu. Alienda China salama na alirudi Tanzania salama. Na ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkabidhi kiti kile Waziri mkuu tena nyumbani kwake. Utaratibu uliotumika kuleta kiti kile na kukabidhi uliendelea kuongeza mashaka kichwani mwa mpelelezi Daniel Mwaseba. Ashaenda kufata ama kuongoza msafara wa kwenda kuchukua silaha mara nyingi, na mara zote hukabidhi kwa Mkuu wa majeshi na wanajeshi wengine wenye vyeo vya juu huku wakishuhudiwa na Amiri jeshi mkuu. Kwa ujumla utaratibu uliotumika kuleta kiti kile ulimshangaza sana Daniel.
Lakini mshangao na wasiwasi wa Daniel Mwaseba leo hii ulileta jibu, kiti kile hatari sana alikikuta ndani ya kambi hatari ya Six killers.
Kimefikaje?
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA