mapengo junior
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 1,135
- 276
- Thread starter
- #421
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA MIA NA ISHIRINI NA MBILI
Kwa upande wa jeshi la Polisi nalo halikulala kabisa, tangu siku ya kwanza kutokea kwa mkasa huu wa ajabu wa kupotea watu kimaajabu bila sababu kujulikana, jeshi la Polisi waliingia kazini. Jeshi la Polisi walianza kufanya msako wao kimyakimya. Lakini kimyakimya yao haikusaidia chochote. Walikuwa wanazunguka palepale bila kujua chanzo cha upotevu wa watu wale, wala kujua ni nani akiyewaficha watu wale. Unaweza sema bora Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walipiga hatua kubwa sana kuwakaribia wahalifu kuliko jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi hawakuwa wanajua lolote kuhusu uwepo wa kundi hatari la Six Killers ndani ya Kilwa.
Mbinu ya kimyakimya ilivyoleta matokeo hasi hatimaye jeshi la Polisi waliamua kufanya msako wa hadharani. Makundi ya askari yalimwaga mitaani kujaribu kutafuta fununu yoyote juu ya kupotea kwa watu au mahali walikopelekwa na kwa lengo gani. Vijana wa Fresh Nigger walipata sana misukosuko ya kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano. Lakini hata hivyo hawakupata fununu yoyote ile, pamoja na kutumia hadi njia ya vitisho na mateso kwa wale waliokuwa wanawatilia shaka, kwa bahati mbaya kabisa hawakuwa wamepiga hatua yoyote ile.
*****
Inspekta Jasmine Wahabu, alikuwa askari wa kike. Askari shupavu na jasiri aliyekuwa anategemewa sana na jeshi la polisi nchini Tanzania. Inspekta Jasmine alishafanikiwa mara kadhaa kuwatia wahalifu nguli mbaroni. Kufanikiwa huko kwa Inspekta Jasmine kulifanya azidi kutegemewa na nchi, kutegemewa na jeshi la Polisi. Inspekta Jasmine alitegemewa pia na raia wema.
Baada ya wiki kadhaa za kuwatafuta wahalifu pamoja na watu na wanafunzi waliopotea katika mazingira ya kutatanisha kugonga mwamba. Inspekta Jasmine ndiye aliyepewa jukumu na Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania ili kwenda Kilwa kupeleleza juu ya upotevu wa watu hao.
Inspekta Jasmine sasa alikuwa na siku ya pili ndani ya Kilwa lakini upelelezi wake ulikuwa haujamfikisha kabisa karibu na adui....
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA