Siri ya Chumba cha Maiti

Siri ya Chumba cha Maiti

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,982
Reaction score
4,363
Wakuu naombani majibu

Siri ya Chumba cha Maiti,
Hivi nyie "Team Osha na Kamua" yale maji na uchafu mnaoukamua mnapeleka wapi?

Acheni na roho mbaya, leo nataka tuvunje mwiko wa usiri na tuingie moja kwa moja kwenye lile eneo linaloleta hofu na maswali mengi zaidi kwenye jamii yetu.

Tunajua kuna hawa wataalamu wanaojidai kuosha miili ya marehemu, lakini leo hatuongelei tu juu juu tunaongelea yale maji yanayotumika kuoshea na ule uchafu mnaoukamua matumboni mwa watu wetu,

Inakuwaje kile chumba kinawekwa usiri mkubwa kiasi hicho hata ndugu wa karibu hawaruhusiwi kusogea wala kuchungulia? Huu usiri uliopitiliza ndio unaothibitisha kuwa kuna madudu ya hovyo na unyama unafanyika huko ndani. Na leo lazima niongee mashaka yote mazito na skendo zinazovuma mtaani kuhusu kile kinachoendelea na yale maji.

Kwanza, kile kisingizio chenye ujinga wa hali ya juu cha kuminya na kukua matumbo. Mnamkanyaga marehemu na kumkamua kwa nguvu zote ili kutoa vinyesi na mabaki ya chakula kuelekea puruni. Sasa swali la msingi: Yale maji yaliyochanganyika na sabuni, damu, na ule uchafu wa matumboni.

Mbona kuna skendo nzito mtaani kuwa maji hayo hayatupwi kikawaida?
na mambo ya giza na ushirikina unaotisha. Kuna uvumi mkubwa sana uswahilini na majukwaani kuwa baadhi ya waoshaji wasio na ubinadamu na wenye roho mbaya, huchukua yale maji ya maiti na yale makamasi au uchafu wa tumboni na kuwauzia watu wenye nia ovu.

Inasemekana maji hayo yanauzwa kwa bei mbaya kwenda kutumika kwenye ramli chonganishi, kafara, na kuwadhuru binadamu wengine. Huu ni upumbavu na ukatili wa kiwango cha kikubwa

Tatu, skendo ya kuchanganywa kwenye vyakula vya shughul I,Misosi. Hili ndilo linaogopesha zaidi, kuna maneno yapo wazi kuwa maji hayo ya hovyo hutumiwa na baadhi ya watu wenye biashara au wanaotaka nyota za biashara ziwake, ambapo wanayachukua kwa siri na kwenda kuyachanganya kwenye vyakula vya shughuli au mikahawa ili kuvuta wateja au kuzuia watu wasihoji huduma zao.

Huu ufal na unyama uliopitiliza unatokana na usiri wenu wa hovyo chumbani. Kama mambo yenu ni masafi, mbona hamtaki kuwe na uwazi wa wapi hayo maji yanamwagwa?

Hapa ndipo pointi kuu inapokuja, Kama utaratibu wenu huu wa siri unahusisha fujo za kukamua watu matumbo, ambapo kama mtu alikuwa kwenye koma nzito ndio mnamalizia kabisa uhai wake, halafu bado kuna hizi hofu za yale maji kuchezewa na kwenda kudhuru jamii, kwa nini huu utaratibu usipigwe marufuku?

Acheni ushamb, ukatili na roho mbaya ya kufanya mambo ya giza chini ya kivuli cha mifumo yetu, Kama mtu amefariki, mwili wake uoshwe kisasa hospitalini au kwa uwazi mbele ya ndugu, na maji yamwagike kwenye mifumo rasmi ya majitaka inayofahamika. Huu uhuni na ukatili wa chumba cha siri ukomeshwe mara moja.
 
Kobaz ni wachafu wakidhani ni wasafi.

mdogoee Al-mukheef Makebo Kubwa la Maadui

adriz de mbusii
 
Watu wa mochwari ni waajabu sana,kama mara mbili tatu nimeenda mochwari ila uwa wanataka mkae nje wamwandae marehemu wenyewe baadae walete mwili wa marehemu ukiwa kwenye jeneza tayari, sijui uwa wanaficha nini
 
Huwa napinga sana hizi propaganda za kijinga na hii inadhihirisha kuwa sisi Watanzania wengi wetu elimu bado sana.

Moja, hakuna hopsital inayokataza usishuhudie mwili wa mpendwa wako ukioshwa ama kuuvesha nguo. Ila kuna vizuizi kutokana na watu kushikwa na hisia kali pindi wakimuona marehemu wao.

Pili, sehemu za kuoshea maiti huwa kuna bomba la kutolea uchafu moja kwa moja.

Tatu, hakuna ndugu anakatazwa kusimamia zoezi lolote kuhusu mwili wa mpendwa wao. Nina mdogo wangu mmoja alifariki miaka ya nyuma. Tuliitwa kwa ajili ya zoezi la usafishaji mwili, tukatoa mwili kwenye jokofu hadi pale unapopaswa kulazwa kwa ajili ya usafi. Hata ule uchafu tulioukuta kwenye lile beseni la kwenye jokofu tuliimwaga wenyewe palepale hospital. Zoezi la kusafisha mwili tulilikataa sababu alikuwa wa kike na kingine wenzangu walishikwa na hisia kali palepale so wote tukaiachia Hospitali.

Ninachoweza kusema ni hiki, ile harufu ya pale Mortuary ilikaa ndani mwangu kwa miezi isiyopungua 6. Ikifika wakati nikipita sehemu yenye harufu mbaya ikawa ni kama na mimi inanirudia harufu ya pale Mortuary. Zoezi la mule ndani tuwaachie wahusika.

Mwisho, kama madai yako yangekuwa sahihi kuwa uchafu huo ni pesa nzuri, basi hao watu wa Mortuary tungewaona na maisha mazuri sana, zamani watu walikuwa wanafanya tu hii kazi ila kwa sasa kazi ya Mortuary inafundishwa kabisa mavyuoni na hao ndio wanaoajiriwa. So tusifanye hitimisho ZITO katika mambo ambayo tunaweza tukatumia akili pia kuyaelewa.
 
Nikienda kwenye zikili (sherehe) huwa nanawia chini. Sitakagi maji ninayonawa yakusanywe
Ukila nyama mifupa hua unatafuna na kumeza au unatema?? Kwenye hizo shughuli?? Kama jibu ni hapana basi bado hujakwepa kitu.

Kama unafanya kazi sehemu na unaweza kurudi nyumbani kula ni bora uwe unarudi au mkeo anakuletea. Hili swala wengi wanalipuuza
 
Uzuri sirikali haijawahi kuingilia maswala yetu kuhusu bia!!
Hizo story za maiti hazina maana, watu wanywe bia
 
Back
Top Bottom