Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

Mapengoooo....! mambo? aaah...akah...! mm cna neno,nmekubal kwa mwendo wa haruc 2tafka,naona page ya 23 na 24 znapta zkiwa empty set(i.e {},{} )
 
Mapengoooo....! mambo? aaah...akah...! mm cna neno,nmekubal kwa mwendo wa haruc 2tafka,naona page ya 23 na 24 znapta zkiwa empty set(i.e {},{} )

Hahahaha! Unanikumbusha nyimbo moja hvi, cjui ni Dada gan yule anasema even the heaven cry, and every body cry, it's OK to die you say sometimes, usiumie Kwa ndan kaka mpe Maneno yako mapengo Jr hko alipo, but I know na yy hapend hii ki2 bt ipo nje ya uwezo wake
 
Itakua huyo anayetupia kwa group lao la watsup ndo anazingua so inabidi kuwa wapole tu
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA ISHIRINI NA SABA

Daniel Mwaseba alikuwa aneshatambua tayari nia ya Tatu wa Six Killers, labda pengine kabla ya yeye kufikiria kufanya hivyo. Kumbuka siku zote Daniel Mwaseba alikuwa anaendeshwa na hisia, na mara zote hisia zake zilikuwa sahihi, hisia za Daniel Mwaseba hazikuwa kuwa hisia za uwongo.
Ujio wa Tatu kwa kutumia kichwa Daniel Mwaseba aliutambua. Hakutaka kukwepa kile kichwa, Daniel alikomaza tumbo lake, kichwa cha Tatu wa Six Killers kilienda kukutana na tumbo imara la Daniel Mwaseba. Tumbo lililokuwa tayari kwa mkutano huo. Kama kichwa cha Tatu wa Six killers kilidhani kuwa kimekomaa basi kilikuwa kinajiongopea chenyewe, tumbo la Daniel Mwaseba lilikuwa zaidi yake. Tumbo lilikuwa limekomaa hasa! Au tunaweza sema limekomazwa na mmiliki wa tumbo lile, ambaye ni Daniel Mwaseba.
Baada ya zuio la kichwa kile Daniel Mwaseba hakushangaa, alirusha teke la nguvu kwa kutumia mguu wake wa kushoto, teke ambalo lililokwepa na Tano wa killers kwa ufundi mkubwa sana.

Upande wa pili wa mapambano, ule wa Dokta Yusha na Moja ilikuwa balaa. Dokta Yusha alipanga ngumi tayari kwa lolote huku Moja wa Six killers akimwangalia, najua unajua kwanini alipewa namba Moja huyu mtu. Moja wa Six Killers alikuwa mtu hatari zaidi ya watu wote katika kundi hili. Moja alikuwa makini na mtulivu sana katika mapambano, alikuwa anazijua mbinu zote za mapambano, hakuwa mtu wa papara kabisa. Kwa ujumla alikuwa anatumia akili na hesabu wakati wa mapambano.

Dokta Yusha alirusha teke! Teke lililodakwa na mkono imara wa Moja wa Six Killers. Mguu wa Dokta Yusha ukiwa umeshikwa kwa juu, Moja alirusha ngumi Kali, ngumi iliyotua sawia katika korodani za Dokta Yusha. Dokta Yusha alitoa ukelele mkali huku akidondoka chini mithili ya gunia. Moja akimfata hadi pale chini. Alipiga kareti moja ya nguvu iliyompata Dokta Yusha kifuani. Dokta Yusha alikohoa bila kupenda, alikohoa damu! Moja hakutaka kumpa nafasi wala nafuu Dokta Yusha. Akiwa palepale chini, alimpiga kichwa cha nguvu Dokta Yusha katikati ya mwamba wa pua. Akiwa amelala ardhini sasa Dokta Yusha alianza kuchanganyikiwa. Aliiona dunia inazunguka, tena inazunguka kwa kasi kubwa sana, huku malaika mweusi mtoa roho akimsogelea palepale alipolala huku katanua mikono yake...

Dokta Yusha na Malaika mtoa roho...nini kitatokea?

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Umesema wanapatikana wapi?

niwafuate na panga maana naona mwaseba atazidiwa.nikamalize ubishi sasa hivi.
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU: 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA ISHIRINI NA NANE

Ilikuwa lazima Malaika mtoa roho aende maeneo yale. Moja hakuwa na huruma kabisa. Alikuwa anampiga Dokta Yusha mapigo mazito sana. Mapigo ambayo Dokta Yusha hakuweza kabisa kuyavumilia hata kidogo.

Mara mlango wa ile nyumba ndogo ulifunguliwa. Walitoka watu wawili toka katika mlango ule...Don Genge mwenyewe akiwa na Nne wa Six killers walisimama katikati ya mlango. Wakishuhudia mapambano yale yasiyo rasmi.

Kule nje Polisi wakiwa wana ongozwa na inspekta Jasmine walikuwa wamejipanga vizuri. Walikuwa wanasubiri amri tu ya bosi wao ili wavamie ile kambi. Hawakutaka kufanya makosa, kosa lolote lingeleta madhara makubwa sana, maana wale watu walikuwa wamewateka raia wema mle ndani.

Ndani ya nyumba mapambano yaliendelea. Wakati Dokta Yusha kadhibitiwa barabara na Moja wa Six Killers, Daniel Mwaseba alikuwa bado anapambana na Tatu wa Six Killers. Daniel sasa alikuwa amemkaba roba kwa nyuma Tatu, huku Tatu jasho lilikuwa linamtoka.

Ghafla katika uwanja wa mapambano akaongezeka mtu mwengine. Moja alimwacha Dokta Yusha pale chini na kumfata huyo mtu, huyo mtu alikuwa anaitwa Songelael Ntenga. Songelael Ntenga aliingia mle ndani wakati muafaka. Angechelewa dakika moja tungesema mengine juu ya maisha ya Dokta Yusha....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI! BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA ISHIRINI NA TISA

Dokta Yusha akiwa pale chini alimshuhudia yule jamaa akiyepambana nae sasa akimfata Mwanasheria mlevi. Pamoja na kuchoka sana lakini Dokta Yusha alimuhurumia sana Mwanasheria mlevi, alijua hana uwezo wa kupambana na yule jamaa hatari, ambaye sasa aligeuka mbogo. Yeye mwenyewe alikuwa taabani lakini alijinyanyua juu kwa nguvu. Akitaka kumzuia Moja asiende kumdhuru Mwanasheria mlevi, kwake Mwanasheria mlevi alikuwa zaidi ya rafiki kwake, huku akiamini Mwanasheria mlevi hawezi kupambana kabisa.
Alijidanganya.....

Dokta Yusha hakutambua kabisa kama mtu tunayemtambua sisi kama Songelael Ntenga yeye alikuwa anamtambua kama Mwanasheria mlevi. Naam, Mwanasheria mlevi hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa ni afisa usalama wa Taifa wa ngazi za juu. Mtu makini anayeheshimiwa na Taifa hili, mzuri katika kupigana aina zote za mitindo ya kimapigano. Mwanasheria mlevi alikuwa ameenda Kilwa kwa kazi maalum. Kazi ambayo ipo ndio hii iliyopo mbele yake sasahivi.

Mguu wa Moja ulivyokuwa unapiga hatua ya tatu haukufika chini mguu ule, Mwanasheria mlevi alimfata kwa kasi huku akiachia mapigo mawili hewani!
E bwana eeee!

Wote walioshuhudia alichokifanya Mwasheria mlevi walibaki midomo wazi!
Moja alianguka chini kwa nguvu, mithili karushwa na shoti ya nguvu ya umeme. Akipigania roho yake.

Don Genge aliyashuhua vizuri sana yale mapigo hatari ya Mwanasheria mlevi. Mapigo ambayo nashindwa hata kuyaelezea hapa. Sasa Don Genge akaona mambo mazito, maji yamezidi unga!
Kwa kasi ya haraka akachomoa bastola yake na kumlenga Mwanasheria mlevi.
Wakati huohuo Daniel Mwaseba alikuwa kamkaba Tatu wa Six Killers, nae alishuhudia kitendo kilichotaka kufanywa na don Genge. Kumbuka Daniel Mwaseba pia alishuhudia mapigo ya Mwanasheria mlevi, lakini hakushangazwa na mapigo yale. Alikuwa anamfaham Mwanasheria mlevi vizuri sana. Sasa Daniel Mwaseba alikuwa anapiga mahesabu nini cha kufanya.

Dokta Yusha alibaki kahemewa tu, alihemewa na yale mapigo hatari toka kwa Mwanasheeia mlevi, alihemewa na ile bastola iliyo mikononi mwa Don Genge, ikiwa inamlenga rafiki yake mwenye maajabu, Mwanasheria mlevi. Dokta Yusha alikuwa haelewi kipi cha kufanya kipi cha kuacha.

Don Genge huwa hatanii !!!

Don Genge alivuta triga ya bastola tayari kwa kufyatua..

Paaaaaaa!

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Mwanasheria mlevi, lets meet on suturday, iyo kesho uwe unaitoa hapo chini, story iko poa sana
 
SIMULIZI; BALAA.
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MWISHO

Paaaaaaaaaaa!

Ulisikika mlio mkali wa bastola hewani. Kila mtu alipigwa na butwaa bila kujua nani kapigwa risasi ile, wote walijua kwamba Don Genge ndiye kafyatua risasi ile.
Haikuwa hivyo!
Ilikuwa ni bastola ya askari makini wa kike, inspekta Jasmine iliyopigwa hewani. Ndio iliyofanya kazi ile ya kuokoa uhai wa Mwanasheria mlevi. Kabla hata akili za watu pale hazijatulia, ghafla eneo lote lilizungukwa na askari Polisi. Ama hakika, kundi la Six killers walikuwa wamewezwa kisawasawa. Don Genge akiwa na bastola yake mkononi alitulia tuli, kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa bado kimeigusa triga ya bastola yake, ilikuwa afyatue ili afyatuliwe! Don Genge aliwaangalia askari wale lukuki kwa zamu. Akajua mwisho wake umefika, mwisho wa mchezo wao mchafu umefika. Sasa alitafuta namna ya kujiokoa. Hakuwa tayari kuingia katika mikono ya Polisi.

Tokea palepale mlangoni aliposimama aliruka sarakasi za kinyumenyume kurudi ndani ya nyumba ya bluu!
Askari wote walibaki mdomo wazi, hawakutegemea kabisa kutokea kitendo kile. Bila kujiuliza mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kasi kukimbilia mle ndani, huku akifuatwa kwa nyuma na Songelael Ntenga au Mwanasheria mlevi.

Pale nje Moja, Tatu na Nne waliwekwa chini ya ulinzi imara wa askari Polisi, wakafungwa pingu. Wakawekwa chini ya ulinzi wa askari kumi kuwalinda, huku askari wengine wakiizunguka ile nyumba ya bluu aliyoingia Don Genge. Wakihakikisha Don Genge hana pakutokea. Askari walichanga karata zao vizuri sana.

Kule ndani Daniel Mwaseba na Songelael Ntenga walifanya msako wa nguvu. Walitafuta kila chumba, walitafuta kila mahali, Daniel Mwaseba alipanda hadi darini lakini Don Genge hawakumuona! Ilikuwa kama hakuingia mle ndani. Daniel Mwaseba hakukubaliana na ukweli kuwa Don Genge alikuwa ameyeyuka! Atayeyuka vipi?
Askari thelathini waliingia ndani ya nyumba ile, walipekua sana, lakini majibu yalikuwa yaleyale. Hakukuwa na Don Genge mle ndani. Walianza kuwatesa mateka wao ili wawaambie mahali atakapokuwa amejificha Don Genge. Hakuna aliyethubutu kusema. Wote walijibu kijeuri, wote walikuwa sugu!

Hawakuwa na namna nyingine, wale kina Moja walipelekwa kituo cha polisi. Walionesha mahali walipowaficha watu waliowateka lakini hawakuonesha mahali alipo Bosi wao, Don Genge. Walikubali kuwataja wale madaktari wote waliohusika katika mpango huu wa BALAA lakini sio Don Genge, hawakumtaja kabisa. Manesi na madaktari wote walikamatwa kama vifaranga vya kuku. Ilikuwa rahisi sana. Hawakuwa na mbinu zozote za kuwazidi kina Daniel Mwaseba.

Baada ya mwezi mmoja wale wahalifu wa Six killers na madaktari wote walihukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama kuu kanda ya Kusini iliyopo huko Mtwara. Haikuwa kesi ngumu sana, wahalifu wote walikubali makosa yao. Ilimshangaza kila mtu.

Suala la kupotea kwa Don Genge likabaki kitendawili kisicho na majibu. Wapo walioamini kuwa yule mtu katili kabisa alikuwa mchawi. Aliingia mle ndani na kuyeyuka! Lakini mawazo hayo hayakupata nafasi katika kichwa cha Daniel Mwaseba, hayakupata nafasi katika kichwa cha Songelael Ntenga, hayakupata nafasi katika kichwa cha Dokta Yusha, wote walikula yamini lazima wahakikishe wanamtia mikononi Don Genge, bila ya kujua watampata kwa namna ipi?

HUU NI MWISHO WA HADITHI YA BALAA SEHEMU YA KWANZA.
 
BALAA sehemu ya kwanza imeishia hapo...tutaendelea sehemu ya pili panapo majaaliwa...kama una maoni, ushauri, swali niulize hapa Leo..kabla hatujaendelea na RIWAYA itakayofuata..ikianza RIWAYA mpya mchango wa sh 2000 utakusanywa...
 
Nawashukuru wote mlio kuwa mnafatilia hapa ahsantene kwa comments zenu mwandishi ameahidi ata zifanyia kazi...kama nitabahatika kusoma sehemu ya pili nitawarushia au kama ntasoma hiyo inayotarajia kuanza nikipata ruhusa ya mwandishi ntawarushia...km nilimkwaza mtu anisamehe bureee na mlonikwaza nimewasamehe bureee mungu awabariki...kwa anaetaka kujiunga na group la whatsap kusoma ikiwa hot ikianza mpya anipm nitamuunganisha
 
Hyo mwandishi kiukwel ana nia ya kuendelea kula hela, anaweza leta hadi sehemu ya 3 mpka 5
 
Back
Top Bottom