Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA MOJA

Mhudumu wa baa ya Masoko by night alimkimbilia Dokta Kilumba alitoka kule nje. Dokta Kilumba alikuwa anapepesukia nje bila kulipa bia alizokunywa pale baa. Mhudumu alipomfikia na kumueleza, Dokta Kilumba hakuwa mbishi. Alitia mkono mfukoni na kumlipa Mhudumu hela yake. Baada ya kumlipa Mhudumu yule, Dokta Kilumba akapiga hatua zake za kilevi, huku akiyumba, hatua za kilevi zilizomfikisha Dokta Kilumba hadi katika gari yake ndogo, Toyota corolla.
Kwa bahati mbaya kabisa, Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi hawakuwa wamejiandaa kwa jambo hilo. Walitegemea Dokta Kilumba ataondoka kwa miguu. Wao hawakuwa na usafiri wa aina yoyote ili kumfatilia Dokta Kilumba. Wakiwa pale nyuma ya kibanda cha vocha walimshuhudia Dokta Kilumba akipanda gari lake taratibu na kuiongoza gari yake upande wa bandarini (custom). Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walibaki wakiikodolea macho ile gari aliyopanda Dokta Kilumba ikishika kasi katika barabara ya lami. Kichwani mwa Dokta Yusha alikuwa anawaza wafanye nini ile Dokta yule mwanaharamu asiwapotee katika upeo wa macho yao. Alitafakari harakaharaka bila kupata jibu. Aliamua kushauriana na Mwanasheria, Dokta Yusha alipoangalia pembeni pale alipokuwa Mwanasheria, hakuwepo! Alikuwa amebaki peke yake amejibanza pale katika kibanda cha vocha. Alipoangalia ile barabara alikoelekea Dokta Kilumba, kwa mbali, usawa wa baa ya Makondeko alimuona Mwanasheria akiwa kwa juu ya pikipiki aina ya boxer akielekea upande uleule alikoelekea Dokta Kilumba. Taa zilizokuwa zinawaka pale baa, zilisaidia Dokta Yusha amtambue vizuri Mwanasheria mlevi. Alipigwa na butwaa! Mwanasheria mlevi juu ya pikipiki?
Balaa!

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA

Mwanasheria mlevi ni professor MKUU anaumiza akili zaidi ya tunavyomjua
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI: HALFANI SUDY.
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA KUMI NA TANO

Mawazo pamoja na maswali yasiyokuwa na majibu ya Daniel Mwaseba yalikatishwa na makelele ya kitasa cha mlango, makelele ambayo ilikuwa ni ishara tosha kuwa kuna mtu alikuwa anafungua ule mlango kwa nje na kutaka kuingia ndani. Kwa kasi ya ajabu Daniel Mwaseba alijirusha na kurejea mahali palepale alipolazwa awali. Akalala kwa mtindo uleule kama waliomlaza awali.
Daniel Mwaseba akazimia tena!

Kelele zile za mlango zilienda sambamba na mlango kufunguka. Mle ndani ya chumba hatari cha mateso aliingia Komando Mbili wa Six Killers. Mbili akiwa kanuna kwa hasira. Bila kujulikana hata sababu ya Mbili kununa namna ile. Mbili alikuwa kapania kwenda kumuonesha Daniel Mwaseba kuwa yeye ni nani?. Na kwanini alipewa namba Mbili katika kundi lile hatari. Lakini kwa bahati mbaya kabisa alimkuta Daniel Mwaseba hajazinduka bado toka usingizini, usingizi wa kuzimia. Mbili wa Six Killers alimsogelea Daniel Mwaseba pale chini huku akitabasamu. Sasa Mbili aliacha kununa. Alipofika pale mahali ambapo alipolala Daniel Mwaseba, Mbili alijisachi mfukoni na kutoa sindano ndogo ya kushonea nguo. Nia yake kuu ni kutaka kuiingiza ile sindano katika mwili wa Daniel Mwaseba ili aone na kuthibitisha kama Daniel Mwaseba alikuwa amezimia kweli ama ulikuwa ni mchezo tu ..

Daniel hajazimia..na Mbili anataka kumjaribu kama kazinduka kwa kumchoma sindano... Daniel ataweza kuvumilia au atashindwa...nini kitatokea?

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA.
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA KUMI NA SITA

Mbili wa Six killers alijisachi mfukoni, alitoa kisu kirefu na kikali mfukoni na kuchana suruali ya Daniel Mwaseba ile sehemu ya paja. Paja la Daniel Mwaseba sasa lilikuwa wazi, likiangaliwa na mtu hatari sana! Laiti lingejua paja lile kinachokuja kukutana nacho, bora lingebaki ndani hukohuko.
Mbili alitoa sindano iliyokuwa imeviringishwa katika kipande cha gazeti. Ilikuwa sindano ndogo nyembamba ya kushonea nguo, lakini Mbili aliishika ile sindano kibabe na kuanza kuizamisha taratibu katika paja la Daniel Mwaseba.
Balaa!

Sindano ilianza kuingia taratibu katika nyama laini za paja za Daniel Mwaseba. Mwendo ule wa taratibu wa kuingia sindano ile ulienda sambamba na maumivu. Daniel Mwaseba alianza kupata maumivu taratibu....sindano ilipofika robo na maumivu sasa yakashamiri. Kumbuka Daniel Mwaseba alikuwa hajazimia kweli lakini ilimpasa kuvumilia maumivu yale makali, Daniel Mwaseba ilimpasa kutulia tuli kama maji ya mtungini. Mtikisiko wowote toka kwa Daniel Mwaseba ulikaribisha jambo baya sana..naam mtikisiko wowote ulikaribisha kifo!

Ilikuwa ngumu sana kuvumilia maumivu yale makali ya sindano. kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe maumivu yale yalikuwa hayavumiliki, tusingethubutu hata chembe!
Lakini Daniel Mwaseba hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe. Mafunzo mbalimbali aliyoyapata Daniel Mwaseba yalimtoa katika ubinadamu kidogo na kuanza kumpeleka taratibu katika unyama!
Amini usiamini Daniel Mwaseba aliyavumilia maumivu yale. Hakutikisika wala kuonesha ishara yoyote ile kwamba alikuwa hajazimia. Sindano ilipofika nusu, Mbili wa Six killer akaanza kuichezesha ile sindano ikiwa ndani ya paja. Balaa!
Maumivu yakazidi maradufu! Kama kuna binadamu sugu duniani basi Daniel Mwaseba alikuwa ndio mwalimu wake. Pamoja na mtikisiko ule wa sindano, mtikisiko uliokuja na maumivu makali zaidi lakini Daniel Mwaseba alitulia, ilikuwa kama amefariki vile.
Utulivu ule wa Daniel ukamfanya Mbili aaamini kwamba Daniel Mwaseba alikuwa bado kazimia, akaichomoa ile sindano kwa haraka sasa na kuamua kuondoka katika chumba kile cha mateso....chumba cha kifo!.

Hilo ndio lilikuwa kosa la kiufundi ambalo Mbili wa Six killers atalijutia milele. Kosa la kiufundi na kwa bahati mbaya zaidi alilifanya mbele ya fundi....


ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI! HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA KUMI NA SABA

Kwa mkupuo mmoja Daniel Mwaseba alifungua macho yake yote mawili. Alivuta pumzi kwa haraka na kunyanyuka taratibu. Daniel alitembea kwa mwendo wa kimyakimya lakini wa haraka akimuwahi mbili pale mlangoni. Alimshika Mbili shingoni na kumrudisha Mbili ndani kwa nguvu. Sasa mkao ulibadirika....Daniel Mwaseba akakaa ule upande ulikokuwa mlango huku Mbili akiwa kwa ndani. Wote wakiwa wamejipanga tayari kwa mapambano. Mbili alikuwa na silaha ya kisu tu ambayo ilikuwa imetulia kiunoni, kisu alichotumia kukata suruali ya Daniel Mwaseba. Daniel alikiona kile kisu pale kiunoni. Lakini hakujari.
Sasa Daniel alikuwa anautambua vizuri sana uwezo wa watu wale kimapambano. Sasa aliamua kupiga mapigo ya nguvu! Mapigo hatari wanayofunzwa watu maalum ili kuwapiga watu maalum. Mbili nae alisimama imara....tayari kwa lolote. Daniel nd'o alianza kushambulia, alirusha kareti ya nguvu iliyokuwa inaelekea moja kwa moja katika shingo ya Mbili, lakini mbili aliiona. Kwa kasi ya haraka aliinama kidogo huku akiachia ngumi ya kwa mkono wa kushoto, ngumi iliyokwenda katika tumbo la Daniel. Lakini Daniel nae alijiandaa kwa hilo, aliikwepa ile ngumi kiufundi mkubwa.
Sasa mafahari hawa wawili wakawa wanatazama. Kila mmoja kasimama, tayari kwa lolote, tayari kwa chochote, muda wowote. Daniel ndiye alikuwa wa kwanza tena kuamua, alirusha ngumi nane za harakaharaka, nne kwa mkono wa kulia, nne kwa mkono wa kushoto lakini Mbili alizipangua zote, kirahisi sana. Zilikuwa ni ngumi mzito sana, ngumi moja ikitosha kabisa kumpeleka kuzimu mtu dhaifu kama wewe, lakini Mbili hakuwa mtu dhaifu, alikuwa mtu imara kabisa. Cha ajabu Mbili alikisahau kile kisu kiunoni....alikiacha kimetulia tu, labda alidhani atamuweza Daniel kwa mikono mitupu.
Mbili nae alirusha ngumi usawa wa mwamba wa pua wa Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliiona ngumi ile, aliikwepa huku akiachia ngumi ya nguvu sana kuelekea katika mbavu za Mbili. Mbili aliguna kwa maumivu, alishika mbavu zake kwa mkono wa kulia, lilikuwa kosa! Daniel Mwaseba alipeleka ngumi ya nguvu katikati ya sura ya Mbili. Mbili alipepesuka huku akiwa amechanganyikiwa, ashike mbavu ama sura. Kubabaika kwake kulitoa mwanya mwengine kwa Daniel, aliruka juu huku akipiga teke la kinyumenyume, teke lilomkumba kwa nguvu Mbili na kwenda kumgongesha ukutani vibaya sana!
Mbili alikuwa amepatikana.
Daniel hakutaka kumpa nafasi, alienda na kifuti pale ukutani na kulipata tumbo la Mbili barabara. Mbili alitapika damu! Daniel alimkaba kabali Mbili, akainyonga ile shingo kwa nguvu kuelekea upande wa kushoto! Roho mbaya ya Mbili ilisalimu amri, roho iliuacha ule mwili dhaifu na kuelekea kusikojulikana.....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAAMWANDISHI! HALFANI SUDYSIMU; 0757 633010SEHEMU YA MIA NA KUMI NA SABAKwa mkupuo mmoja Daniel Mwaseba alifungua macho yake yote mawili. Alivuta pumzi kwa haraka na kunyanyuka taratibu. Daniel alitembea kwa mwendo wa kimyakimya lakini wa haraka akimuwahi mbili pale mlangoni. Alimshika Mbili shingoni na kumrudisha Mbili ndani kwa nguvu. Sasa mkao ulibadirika....Daniel Mwaseba akakaa ule upande ulikokuwa mlango huku Mbili akiwa kwa ndani. Wote wakiwa wamejipanga tayari kwa mapambano. Mbili alikuwa na silaha ya kisu tu ambayo ilikuwa imetulia kiunoni, kisu alichotumia kukata suruali ya Daniel Mwaseba. Daniel alikiona kile kisu pale kiunoni. Lakini hakujari. Sasa Daniel alikuwa anautambua vizuri sana uwezo wa watu wale kimapambano. Sasa aliamua kupiga mapigo ya nguvu! Mapigo hatari wanayofunzwa watu maalum ili kuwapiga watu maalum. Mbili nae alisimama imara....tayari kwa lolote. Daniel nd'o alianza kushambulia, alirusha kareti ya nguvu iliyokuwa inaelekea moja kwa moja katika shingo ya Mbili, lakini mbili aliiona. Kwa kasi ya haraka aliinama kidogo huku akiachia ngumi ya kwa mkono wa kushoto, ngumi iliyokwenda katika tumbo la Daniel. Lakini Daniel nae alijiandaa kwa hilo, aliikwepa ile ngumi kiufundi mkubwa. Sasa mafahari hawa wawili wakawa wanatazama. Kila mmoja kasimama, tayari kwa lolote, tayari kwa chochote, muda wowote. Daniel ndiye alikuwa wa kwanza tena kuamua, alirusha ngumi nane za harakaharaka, nne kwa mkono wa kulia, nne kwa mkono wa kushoto lakini Mbili alizipangua zote, kirahisi sana. Zilikuwa ni ngumi mzito sana, ngumi moja ikitosha kabisa kumpeleka kuzimu mtu dhaifu kama wewe, lakini Mbili hakuwa mtu dhaifu, alikuwa mtu imara kabisa. Cha ajabu Mbili alikisahau kile kisu kiunoni....alikiacha kimetulia tu, labda alidhani atamuweza Daniel kwa mikono mitupu.Mbili nae alirusha ngumi usawa wa mwamba wa pua wa Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliiona ngumi ile, aliikwepa huku akiachia ngumi ya nguvu sana kuelekea katika mbavu za Mbili. Mbili aliguna kwa maumivu, alishika mbavu zake kwa mkono wa kulia, lilikuwa kosa! Daniel Mwaseba alipeleka ngumi ya nguvu katikati ya sura ya Mbili. Mbili alipepesuka huku akiwa amechanganyikiwa, ashike mbavu ama sura. Kubabaika kwake kulitoa mwanya mwengine kwa Daniel, aliruka juu huku akipiga teke la kinyumenyume, teke lilomkumba kwa nguvu Mbili na kwenda kumgongesha ukutani vibaya sana! Mbili alikuwa amepatikana.Daniel hakutaka kumpa nafasi, alienda na kifuti pale ukutani na kulipata tumbo la Mbili barabara. Mbili alitapika damu! Daniel alimkaba kabali Mbili, akainyonga ile shingo kwa nguvu kuelekea upande wa kushoto! Roho mbaya ya Mbili ilisalimu amri, roho iliuacha ule mwili dhaifu na kuelekea kusikojulikana.....ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
sehemu nzuri we ndo unakatisha stiry....ngoja tusubiri kesho
 
Hii riwaya tamu sana,sema anachokosea ni:
-Fupi fupi sana.
-Anapumzika muda mwingi sana.
 
Unajua ni vile hakuna jinsi hadithi kali kama hii inatakiwa upate kitabu, hukiweki chini hadi iishe

Kwani mtu akileta story hapa si anakuwa amemaliza kutunga na ipo documented tayari au anatunga na kupost apoapo

Yote yanawezekana,kupost ikiwa ishamalizika kutungwa au ikiwa bado.

Ila pia somtym majukumu yanakuwa tight zaidi
 
Tatzo kasi ya usomaji ni kubwa na ni rahisi kuliko utungaji

Siyo kweli,riwaya nyingine unaposoma unajua tu hii ni fupi na hii ndefu,chukulia TUTARUDI NA ROHO ZETU? na BARUA KUTOKA JELA,je,unaposoma riwaya hizi unaziona fupi?.
 
Back
Top Bottom