Riwaya: Afisa usalama

Riwaya: Afisa usalama

RIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri

SEHEMU: 14
ILIPOISHIA

Colotilda akacheka kwa sauti kitu kilichoacha mshangao katika akili ya Godfrey kisha akainuka akatembea tembea ndani ya chumba kile, akamtazama Godfrey, akamwambia

“Najua akili yako ina maswali mengi kuhusu mimi na unataka kujua uhusiano wangu na mdogo wako”

Akacheka tena kwa sauti kisha akaendelea

“Utajua soon, lakini nachotaka kujua kutoka kwako unahusika vipi na kesi yangu? Na kama uhusiki kwanini ulikubali kubeba mzigo wa lawama?”

Akili ya Godfrey ikayakumbuka maneno ya makali ya Colotilda, mwili ukaanza kumtetemeka

“Uso wangu unaonekana nina furaha sana, No! usidanganyike na sura, hakuna mtu mwenye hasira, chuki na visasi katika dunia hii kama mimi”

Mwili uliendelea kumtetemeka, akashindwa kuelewa kwanini Colotilda analazimisha jambo hilo. Hali ya hatari ikampanda akilini mwake baada ya kukumbuka alivyotekwa na wasichana warembo ila hatari sana katika mapigano, akili yake ikashindwa kuelewa Colotilda anamiliki vipi kundi hilo la majambazi tena wenye utajiri mkubwa kiasi kile. Akashtushwa na kauli toka kwa Colotilda

“Nasubiri jibu lako”

Godfrey akamjibu kwa sauti ya chini

“Sina jibu la kukupa, nasubiri hukumu yangu”

Uso wa Colotilda ukabadilika, tabasamu lote likapotea baada ya kuona Godfrey anakua mbishi kujibu maswali yake, akasimama wima kisha akamwambia

ENDELEA

“Nahisi hujui chochote kuhusu mimi ndio maana unakuwa mbishi kiasi hicho...laiti kama ungelijuwa ungelisema mapema hata bila kuulizwa au kubembelezwa na mtu yeyote”

Akasogea alipo Godfrey akakaa kama alivyokuwa amekaa awali kisha akaendelea

“Najua unanifahamu kwa jina la Colotlida Kamanzi, hilo ndio jina langu baada ya wazazi wangu kufariki lakini sio jina langu kipindi cha uhai wao"

Akapumzika kidogo kuruhusu mshangao wa Godfrey upite, alipotaka kuendelea akakatishwa na swali la Godfrey.

“Baada ya wazazi wako kufariki? Mbona mzee Kamanzi namfahamu na bado yupo hai!”

Colotilda akatabatamu, hakika alitegemea swali hilo. Akaendelea

“Naitwa Colotlida Calist na sio Colotlida Kamanzi kama ninavyofahamika…Ni stori ndefu kidogo na ngumu kuielewa”

Akamshika bega Godfrey kwa mkono wake wa kulia kisha akaendelea

“Sijakuteka ili nikuhukumu, No!, upo huru kabisa mahala hapa wala usiwe na hofu yoyote…Wewe pamoja na jamii yote mnanijuwa upande mmoja wa shilingi ambao sio kitu wala lolote kwangu, upande wa pili wa shilingi bado ni kitendawili kwenu na ndio maana hunielewi. Huo upande wa pili ndio maisha yangu halisi, ni upande ambao sikutarajia kuuishi lakini nitauishi mpaka siku ya mwisho ya uhai wangu”

Godfrey akapigwa na bumbuwazi, mdomo wazi asiamini alichokisikia. Akaongeza umakini ili asipoteze neno hata moja toka kwa mrembo huyo

“Sababu ya kukutoa kwenye nondo za gereza sio kukudhuru au kukuua la hasha bali ni kuokoa maisha yako na maisha yangu pia...maisha yangu yapo hatarini tangu utotoni, nahisi kupitia wewe kuna njia ya mafanikio”

Godfrey akamkazia macho Colotilda, ujasiri wa ajabu ukamwingia kisha akauliza

“Mbona sielewi maelezo yako? Naona unanichanganya tu…alafu hakuna msaada wowote ulionipatia mpaka sasa zaidi ya kuniongezea kesi serikalini"

Colotlida akacheka kwa sauti kama awali kisha akamwambia Godfrey

“Msaada wangu utauona siku ukiwa huru kabisa lakini kwa muda huu upo sahihi kusema hivyo...vile vile msaada wangu unategemea sana msaada wako pia"

Colotilda akajinyoosha kidogo kuweka sawa viungo vyake kisha akaendelea

“Ngoja nikuelezee kwanini nimekuteka wewe na kwanini nina majina tofauti”

Godfrey akaifungua akili yake tayati kwa maelezo ya mrembo huyo, Colotilda akaendelea

“Maandishi katika hii tisheti yangu yana maana kubwa sana”

Godfrey akayasoma maandishi yale

“Dad and Mummy”

Colotilda akamtazama Godfrey kwa sura ya upole, sura iliyoonesha wazi kuwa Godfrey ameingia kwenye vita kali kisha akaanza kumsimulia kisha cha maisha yake, kisa kilichosababisha aishi maisha ambayo hakuyapanga hata siku moja kuyaishi. Akaanza kusimulia

“Mimi ni mtoto wa kwanza na wa pekee wa mzee Calist na Bi Loveness Molel. Kipindi cha uhai wa wazazi wangu tulikuwa tukiishi Mjimwema hapa hapa Kigoma. Mzee alikuwa tajiri na maarufu sana hapa mkoani Kigoma miaka ya nyuma, na hakuna mtu aliyekuwa hamfahamu. Alikuwa na mahusiano na watu wa serikali pamoja na wafanyabiashara wenzake. Mama alikuwa akijihusisha na biashara ya vipodozi na saluni katika maeneo ya soko la Kigoma mjini. Hakika niliishi maisha bora sana, nadhani kushinda mtoto yeyote hapa mkoani, huo ulikuwa mtazamo wangu japokuwa sikuufanyia utafiti wowote.

Kuna siku sitaisahau kamwe kwenye maisha yangu, siku iliyobadilisha kila kitu kilichokuwa kikinipa furaha na amani ya kuishi, siku niliyoshuhudia mambo yasiyo vumilika kamwe. Kipindi hicho nilikuwa nipo darasa la tatu. Nakumbuka yalikuwa ni majira ya saa saba usiku niliposhtuka usingizini baada ya kusikia kelele kali sebuleni, niliposikiliza vizuri sauti ile inayopiga kelele niligundua ni sauti ya baba, nilihamaki maana hazikuwa kelele za kawaida hata kidogo kwa usiku ule. Nilishuka kitandani nikachungulia sebuleni sehemu zilipotokea kelele hizo kupitia sehemu ya kupitishia funguo, nilimuona baba akivuja damu mdomoni na puani, mama kawekewa bastola ndogo kichwani ili asiweze kuongea chochote. Mwili ulinitetemeka sana na kwakuwa nilikuwa bado mdogo nilishindwa cha kufanya zaidi ya kuruhusu machozi yashambulie mashavu yangu. Vijana watatu wakakamavu waliovaa soksi usoni walikuwa wakimlazimisha baba asaini karatasi fulani lakini baba alikuwa mbishi, nakumbuka kauli ya mwisho baba aliwaambia

“Mali hizi ni za mwanangu na sio vinginevyo”

Kauli ile iliwakasirisha sana wakamshambulia kwa mabuti kila sehemu ya mwili wake, baba alipiga kelele sana kama mtoto lakini haikusaidia kabisa waliendelea kumshambulia kama nyuki, mama alijaribu kuzuia ili baba asishambuliwe kiasi kile.

KOSA

Nilishuhudia kisu kikizamishwa kwenye tumbo la mama yangu kipenzi, macho yalikataa kuamini lakini haikua ndoto, mama akabaki akilalamika kwa maumivu makali yaliyokuwa yakishambulia mwili wake, mara ajitupe kulia mara kushoto. Hakika aliumia sana. Jamaa mmoja akamwambia baba

“Haya ndio malipo ya ukaidi wako”

Wakamlazimisha anaisi ile karatasi kwa mara nyingine lakini baba alikuwa kama mtu alliyerukwa na akili, alimtazama mama alivyokua akihangaika kwa kujigeuza geuza mara kushoto mara kulia lakini alishindwa afanye nini kuokoa maisha yake. Jamaa wa pili akamuuliza baba

“Hicho kitoto kinachosababisha usisaini hizi karatasi chumba chake kipo wapi?”

Moyo wangu ulinipiga Paaah!

Nikaona kifo kipo mbele yangu. Baba hakuwajibu chochote, mawazo yake yalikuwa kwa mama. Jamaa yule akamuuliza baba kwa mara ya pili lakini baba hakufungua mdomo wake. Walipoona amekuwa mbishi kwa kila alichoulizwa wakaamua maamuzi makali na ya kinyama sana. Nilishuhudia kwa macho yangu baba akipigwa risasi ya kichwa kwa kutumia bastola iliyofungwa kizuia sauti, nilihisi kuchanganyikiwa kabisa mkojo ukanitoka kama mtoto wa miaka miwili. Baada ya kuhakikisha uhai wa baba haupo kabisa wakachukua kitambaa cheupe kisha wakachomoa kisu katika mwili wa mama aliyekuwa bado akihangaika kwa maumivu. Kitambaa kikalazwa vizuri juu ya mwili wa baba wakawa wanachovya damu ya mama na kuandika maandishi katika kitambaa kile, sikuweza kuelewa waliandika nini kwa sababu ya umbali uliokuwepo kati ya chumba changu na sebule.

Walivyomaliza kuandika maandishi hayo wakapeana ishara ya dole gumba kisha wakaondoka. Sikua na uhakika kama wameondoka kweli au bado wapo ndani ya nyumba yetu. Nilikaa kama nusu saa chumbani kwangu huku jicho langu likichungulia sebuleni kwa lengo la kuangalia kama wale jamaa watarudi au laah! Mwili wa baba ulikuwa umetulia kimya kitu kilichonipa jawabu kuwa roho imeshatoweka, mama alikuwa bado anajigeuza geuza japo kwa shida sana tofauti na awali kitu kilichonipa majibu kuwa hali yake imezidi kuwa mbaya na anaishiwa nguvu. Nilisubiri kama nusu saa nyingine kudhibitisha usalama wangu, hali ya utulivu na ukimya iliendelea kutawala ndani ya jengo letu la kifahari. Taratibu nilishika kitasa cha mlango wangu nikafungua kisha nikachungulia sebuleni, sikuona hali yoyote ya hatari, nikatoka ndani ya chumba changu moja kwa moja mpaka ilipo miili ya wazazi wangu.

Hakika siku ile ilikuwa mbaya sana kwangu. Nilikuta baba ameshafariki, macho ya mama yalikuwa yananitazama lakini hakuweza kuongea chochote, alijitahidi kuongea lakini alishindwa kabisa, nililia sana kwa uchungu lakini haikusaidia kurudisha usalama wa wazazi wangu. Hazikupita hata dakika mbili, mama alipoteza maisha yake mbele yangu. Roho yake ilitoka akiwa mikononi mwangu. Kilikuwa ni kilio na kusaga meno, kilio kisichokuwa na msaada wowote. Macho yakatua juu ya kitambaa kilichoachwa na wale wauaji, kitambaa kilichobeba ujumbe mzito, ujumbe uliosomeka

“Very sorry marehemu”

Sikuelewa walikuwa na maana gani, yaani wafanye mauaji wenyewe alafu wamuombe msamaha waliyemuua?.

Nilikitoa kile kitambaa juu ya mwili wa baba nikakiweka chini huku machozi yakiendelea kutengeneza mifereji katika mashavu yangu.

“Walinzi wetu wapo wapi mpaka tukio hili linatokea? Dada wa kazi je!, hivi hawajasikia kelele zilizokua zikipigwa na wazazi wangu?”

Taratibu nikaanza kuelekea uelekeo wa chumba alichokuwa akilala dada wa kazi, kila nilivyozidi kupiga hatua ndivyo nilivyozidi kuona michirizi ya damu. Sikuamini macho yangu, nilimkuta dada wa kazi amelala nje ya mlango wa chumba chake huku kisu kikiwa kimezama kifuani kwake, nilichanganyikiwa nikajikuta nikipiga kelele kama mwendawazimu, nikakimbia mbio kuelekea nje. Huko nako hali haikuwa shwari hata kidogo, nilikuta walinzi wote wawili wameshakua maiti muda mrefu, kipindi bado nikiendelea kushangaa huku moyo ukinienda mbio kwa maumivu makali ghafla nikasikia vishindo vikitoka ndani ya nyumba yetu, nilikimbia nikajificha katika bustari iliyokuwa ikihudumiwa na mama yangu mzazi.

Baada ya sekunde kama kumi na saba nikawaona wale wauaji wakitoka ndani ya nyumba yetu huku wakiangaza mbele nyuma kushoto kulia, nikajua walinisikia nilivyopiga kelele hivyo basi walikua wakinitafuta kwa udi na uvumba ili waniue kama walivyofanya kwa wengine. Safari hii walikuwa watano hata sijui wengine walitokea wapi, watatu walikuwa wameshika silaha za moto, mmoja alikua ameshika visu viwili vilivyoonekana kuwa vikali sana na wa mwisho alikuwa ameshika panga kubwa kama la machinjioni. Nilitulia kimya huku nikiwa nimeziba mdomo kwa mkono wa kushoto. Waliniangaza sana katika maeneo yale, walivyoshindwa kunipata mmoja alichukua simu akatafuta namba akapiga

“Hello The Devil”

Akasubiri upande wa pili wa simu uitikie kisha akasema

“Kama ulivyosema akileta ubishi tusambaratishe kizazi chake, ndivyo tulivyofanya”

Akasubiria maelekezo toka kwa aliyempiga kisha akasema

“Sawa mkuu baada ya nusu saa tutakuwa tumefika”.

Akakata simu kisha akawaamuru wenzake waondoke, wakaondoka vifua mbele kama wamepigwa ngumi za migongo. Niliwasindikiza kwa macho mpaka walipotoweka kabisa kwenye upeo wa macho yangu. Niliapa ndani ya moyo wangu kuwa lazima nilipize kisasi lakini nilipofikiria zaidi nilihisi ni utoto ulionisumbua kwa sababu waliofanya matukio walikuwa wamevaa soksi usoni sasa nitawajuaje?. Huzuni iliendelea kujaa maradufu moyoni, nikainuka bila hofu yoyote, sijui ujasiri huo ulitoka wapi, moja kwa moja nikaelekea chumbani kwa wazazi wangu. Nilikuta mlango upo wazi, nikaingia. Sikuamini nilichokiona, chumba kilikuwa hakieleweki kabisa, makaratasi yalikuwa wametapakaa ovyo kila kona ya chumba. Nilipofikiria vizuri nikajua wauaji walikuwa wakitafuta baadhi ya nyaraka na taarifa muhimu za baba ndio maana wakatapanya ovyo zile karatasi. Kwa mara ya kwanza tangu nione maiti za wazazi wangu tabasamu hafifu likateka sura yangu. Niliitazama picha ya baba iliyokuwa ukutani ikitabasamu bila kuchoka nikakumbuka maneno aliyoniambia siku za usoni kabda ya umauti wake.

“Kama unavyoona maisha ya wazazi wako yalivyo mazuri, haya maisha ndio maisha yako ya baadae lakini kumbuka mtu mwenye maisha mazuri kama mimi ana marafiki na maadui wengi pia. Siku likitokea jambo lolote ukawa unahitaji msaada wangu au msaada wa mama yako alafu kwa bahati mbaya ukashindwa kuupata kirahisi kutokana na umbali tuliopo au sababu nyingine yoyote ile, usihangaike kamwe kwa watu wengine. Ile picha yangu ukutani ni msaada tosha kwako, utaitoa ukutani na kuitazama. Lazima ikusaidie mwanangu”

Kipindi alipokuwa akiniambia nilipuuza maneno yale, kwanza: sikuona umuhimu wowote kwa sababu kila siku nilikuwa nina furaha katika maisha yangu, pili: nilishangaa alivyosema eti picha yake ndio ije kuwa msaada kwangu, nilijiuliza moyoni kivipi? Lakini sikupata jibu na nilipomuuliza baba nae hakunipa jibu kamili bali aliendelea kunipa maneno yenye mafumbo ndani yake. Sikumuelewa kabisa. Niliitazama kwa mara ya pili picha ya baba pale ukutani kisha taratibu nikasogea nikachukua viti viwili nikavibebanisha alafu nikapanda juu yake, nikaichomoa kwenye msumari maalum ilipokua imetundikwa.

Niliitazama vizuri lakini sikuona chochote wala msaada wowote katika picha ile, hasira zikanijaa moyoni nikauona uongo wa baba yangu mzazi mbele yangu. Niliitazama sana sura ya baba machozi yakawa yakinitoka kama maji, nikaamua niifunike picha ile ili nisiendelee kujiumiza moyo pasipo nafuu yoyote lakini nilipoifunika nikaona kitu cha tofauti nyuma ya picha ya baba, kitu nilichohisi labda ndio lilikuwa kusudio la baba kuniambia maneno ya mafumbo kuhusu picha ile. Yalikuwa ni maandishi mazito yaliyoandikwa kwa wino mweusi

“Afisa Usalama”

Chini ya maandishi hayo ziliambatanishwa namba za simu mbili tofauti. Moyo ulinienda mbio sana, nikarudia kusoma tena yale maandishi

“Afisa Usalama”

Sikujuwa maneno yale yalimaanisha nini, hakika nilikuwa mtoto kipindi kile. Nilitazama kushoto kisha kulia nikaiona simu ya mama juu ya kitanda chao, haraka haraka nikaichukua kisha nikaingiza namba moja wapo kati ya namba zilizoandikwa nyuma ya picha ya baba kisha nikapiga, nilisubiri kama sekunde nne simu ikaanza kuita, iliita bila mafanikio yoyote mpaka ikakata. Nikaingiza namba ya pili kwa lengo la kupiga lakini kabla sijapiga namba hiyo simu ya mama ikaanza kuita, nilipoitazama vizuri ilikuwa ni ile namba niliyoipigia awali. Mapigo ya moyo yalinienda kasi nikajiuliza

“Nitaongea nini na mtu huyu nisiye mjua?”

Kauli ya baba iliyonisisitiza kuhusu mtu wa kunipa msaada ikanijia kichwani, nikaona huo ndio msaada wangu. Nikapokea simu na kuiweka sikioni

“Hallo”

Sauti nzito upande wa pili ikaitikia

“Hallo! Nani mwenzangu na mbona usiku sana?”

Nilifikiria nini cha kumjibu lakini hali ya sitofahamu ikaendelea kunisumbua, nilichogundua mtu mwenye sauti nzito hakuwa na namba ya mama ndio maana ameuliza, nikaona nijitambulishe kupitia baba

“Mimi ni mtoto wa mzee Calist mkazi wa Mjimwema – Kigoma”

Alishangazwa sana kupigiwa simu na mimi muda ule, ilivyoonesha alikuwa akinifahamu vizuri japokuwa mimi nilikuwa sifahamu. Aliniuliza maswali mawili yaliyosababisha nianze kulia, maswali yaliyonikumbusha kuhusu tukio la kinyama lililotokea

“Mbona usiku mwanangu? Baba na mama wazima?”

Alivyosikia nikilia pasipo kumpa majibu aligundua kuna kitu tofauti, sikujua kwanini alikuwa na akili ya haraka kiasi kile. Aliniambia nimsubiri hapo hapo nyumbani wala nisimpigie simu mtu yeyote, na akanihakikishia kuwa yeye ndiye usalama wangu pekee. Nilikubali kisha nikakata simu, utafikiri mimi ndiye niliyepiga. Niliitazama saa ya ukutani iliyokuwa chumbani humo ikanionesha kuwa ni saa tisa kasoro robo usiku, nilisubiri kama dakika ishirini ndipo niliposikia vishindo taratibu vikija chumbani kwa baba, nilihofu sana kwa sababu sikuwa na uhakika nani aliyekuwa akiyenyemelea kuingia chumbani humo. Kwa haraka bila hata kutegemea niliingia ndani ya kabati kubwa na nguo za mama nikajifungia kimya. Baada ya kama dakika moja na sekunde kadhaa nikavisikia vishindo vile vikitembea tembea ndani ya chumba cha wazazi wangu, nilikuwa kimya nikitetea uhai wangu. Nilisubiri kuona nini kitachoendelea lakini kabla sijapata jawabu kamili nikasikia simu ya mama ikiita kwa fujo juu ya kitanda nilipoiacha.

Akili ikawaza labda ni wale wajambazi wamerudi au ni yule niliyempigia simu?.

Kipindi nikiendelea kuwaza ghafla kabati nilililokuwa nimejificha ndani yake likafunguliwa kwa nguvu nikakutana uso kwa uso na sura ngumu ikinitazama. Jamaa huyo alikuwa amevaa kofia ya pama na koti ndefu leusi lililofunika mpaka magoti yake huku mkononi akiwa ameshika bastola aina ya Enfield revolver, alinitazama kisha akaweka bastola yake mfukoni akanipa mkono wake, kwa hofu nikaupokea akanitoa ndani ya kabati kisha akaniambia

“Kwa ufupi naitwa Mr Hamisi Ernest, wengi hupendelea kuniita Mr Kidua, ndiye uliyempigia simu muda mfupi uliopita”

ITAENDELEA

Kazi nzuri, mzigo uko pouwa sana
 
RIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri

SEHEMU: 15
ILIPOISHIA

Niliitazama saa ya ukutani iliyokua chumbani humo ikanionesha kuwa ni saa tisa kasoro robo usiku, nilisubiri kama dakika ishirini ndipo niliposikia vishindo taratibu vikija chumbani kwa baba, nilihofu sana kwa sababu sikua na uhakika nani aliyekua akinyemelea kuingia chumbani humo. Kwa haraka bila hata kutegemea niliingia ndani ya kabati kubwa la nguo za mama, nikajifungia kimya. Baada ya kama dakika moja na sekunde kadhaa nikavisikia vishindo vile vikitembea tembea ndani ya chumba cha wazazi wangu, nilikua kimya nikitetea uhai wangu. Nilisubiri kuona nini kitachoendelea lakini kabla sijapata jawabu kamili nikasikia simu ya mama ikiita kwa fujo juu ya kitanda nilipoiacha. Akili ikawaza labda ni wale wajambazi wamerudi au ni yule niliyempigia simu. Kipindi nikiendelea kuwaza ghafla kabati nilililokuwa nimejificha ndani yake likafunguliwa kwa nguvu nikakutana uso kwa uso na sura ngumu ikinitazama. Jamaa huyo alikua amevaa kofia ya pama na Kofi refuses jeusi lililoficha mpaka magoti yake huku mkononi akiwa ameshikilia bastola aina ya Enfield revolver, alinitazama kisha akaweka bastola yake mfukoni akanipa mkono wake, kwa hofu nikaupokea akanitoa ndani ya kabati kisha akaniambia

“Kwa ufupi naitwa Mr Hamisi Ernest, wengi hupendelea kuniita Kidua, ndiye uliyempigia simu muda mfupi uliopita”

ENDELEA

Akatazama saa yake ya mkononi kisha akaendelea

“Hatuna muda wa kupoteza, una chochote cha kuchukua haraka?”

Niliamini ni mwema kwangu japokuwa nilikuwa simfahamu wala sijawahi kulisikia jina lake likitajwa na baba. Hakika alikuwa ni malaika wa Mungu kipindi kile. Nilimwambia

“Kuna nyaraka muhimu za baba zipo chumbani kwangu”

Baba alikuwa akihifadhi nyaraka zake zenye kuonesha uhalali na umiliki wa mali zake katika kabati langu la nguo. Nakumbuka niliwahi kumuuliza kwanini anaweka chumbani kwangu na sio chumbani kwake, jibu lake lilikuwa dogo sana

“Bado hujakua, ipo siku utajua”

Siku hiyo ndio nilijua kwanini nyaraka zile alizihifadhi chumbani kwangu. Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Mr Hamisi Ernest au Mr Kidua alinishika mkono akaniongoza mpaka chumbani kwangu akafungua mlango wa kabati akazitoa zile nyaraka zote akaziweka ndani ya begi langu dogo lililokuwa juu ya kitanda changu kisha akaniamuru tuondoke. Nilishangaa sana nikajiuliza

“Amejuaje chumba changu na nani aliyemuonesha mahala zilipohifadhiwa nyaraka muhimu za baba?"

Lakini sikupata jawabu kamili, nikajisemea moyoni

“Hakika huyu alikuwa rafiki kipenzi wa baba”

Tulitoka ndani ya chumba changu tukatambuka miili ya wazazi wangu, jamaa hakuonesha hali yoyote ya huzuni wala kusikitika alipoona miili imetapakaa ndani na nje ya nyumba yetu, bali aliniambia

“Hutakiwi kuwaza yaliyopita, sasa fikiria maisha yako ya mbele”

Hakika nilihisi akiichezea akili yangu,

eti nisifikirie yaliyopita?.

Yaani nisifikirie majanga yaliyowakuta wazazi wangu?

Hakika nilihisi anaota ndoto za mchana. Tulipofika nje ya geti la nyumba yetu niliona gari la Kimarekani la kifahari linalofahamika kwa jina la Tesla toleo la 3 (Tesla model 3) linalokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani 46,000 sawa na Milioni 106 za kitanzania likiwa limeegesha pembeni kidogo ya geti la kuingilia ndani. Gari hilo la kimarekeni linaaminiwa ndio gari bora kwenye masuala ya ulinzi kwa sababu lina kamera za dashboard, yaani dashcam kila upande wa gari, hivyo basi huweza kuchukua matukio yote yanayolizunguka gari kwa kiwango cha nyuzi 360. Gari hilo halina injini kabisa, linatembea kimya kimya pasipo kutoa mlio wowote na halina funguo bali hutumia rimoti yenye umbo sawa na gari hilo. Vile vile, gari hilo lina Autopilot kamera kama za kwenye ndege zinazoweza kuona sehemu ya mbele zaidi ya barabara, hivyo basi kama barabara sio rafiki linatoa mlio wa alamu (alarm) kumtambulisha mtumiaji ili mchukue taadhari. Jamaa yule mwenye sura ngumu akaniambia

“Itazame nyumba yenu kwa mara ya mwisho, sizani kama utaweza kuishi ndani yake tena...itabakia kuwa mali yako lakini yenye utata katika umiliki wake”

Sikuwa na neno la kuchangia, kichwa changu kilikuwa mbali sana kwa mawazo. Tulipanda ndani ya gari yake ya gharama kisha safari ikaanza, kwakuwa nilikuwa bado mdogo sikuweza kuelewa tulikuwa tukielekea wapi usiku ule, nilikuwa naona gari likienda mara likikata kona kushoto mara kulia, nikaamua kumuuliza.

“Tunaelekea wapi?”

Alinitazama kisha akanijibu

“Nyumbani kwangu, hapo ndipo nyumbani kwako pia”

Nafikiri hakunielewa nilikuwa nina maana gani, nikaamua kufafanua zaidi

“Namaanisha, tunaenda mtaa gani?”

Mr Hamisi Ernest alinitazama kisha akatabasamu, nikaona meno yake ya dhahabu yaliyopendezesha kinywa chake, akaniambia

“Utaelewa tu Colotlida hacha kuwa na haraka kiasi hicho"

Nilihamaki kwa mshangao aliponiita jina langu

“Unalifahamu jina langu?”

Akacheka tena kwa mara ya pili kisha akajibu huku akitazama tunapoelekea

“Nafikiri nakufahamu zaidi ya unavyojifahamu mwenyewe, hujajiuliza nimefahamu vipi chumba unacholala? Nyaraka muhimu za baba yako zilipo na vinginevyo?”

Nilimjibu kuwa ninashangaa sana kwa anavyonifahamu, alitabasamu kisha akaniambia

“Ndio maana baba yako alikuambia ukiwa na shida yoyote unitafute mimi, ulikuwa unaishi chini ya kivuli changu muda mrefu sana pasipo wewe kujua. Sasa kivuli kimemfuata mtu wake”

Sikumuelewa ana maanisha nini kipindi kile sababu ya utoto niliokuwa nao lakini sasa naelewa. Nilipozidi kumuuliza maswali aliniambia nitulie maana huo ni muda wa kulala sio muda wa kuongea. Nikajiuliza swali kimoyomoyo

“Eti muda wa kulala! Wakati tupo ndani ya gari?”

Ukimya ukatawala, baada ya kama dakika ishirini gari likapiga breki mbele ya jumba kubwa la kifahari linalokadiriwa kuwa na gharama zisizo pungua Milioni 270 za kitanzania, jumba hilo lilikuwa likiwaka mataa ghari sana kila upande utafikiri kasino zinazopatikana nchi za Magharibi. Alifungua mlango wa gari kisha akashuka akaenda kufungua geti mwenyewe, nikabaki najiuliza

“Nyumba nzuri kama hii bado geti anafungua mwenyewe?, ameshindwa kumuajiri mlinzi atakayekuwa anamfanyia kazi hiyo?”

Sikuwa na jibu kamili la swali langu, baada ya kufungua geti akarudi ndani ya gari kisha tukaingia moja kwa moja mpaka sehemu ya kuegesha magari, nilikuta magari ya kifahari zaidi ya saba yakiwa yamepangwa vizuri utafikiri maua, hapo ndipo nilipoamini hakika tajiri rafiki yake ni tajiri. Tukaingia ndani moja kwa moja akanipeleka katika chumba alichopanga nianzie maisha yangu mapya, sikuamini macho yangu baada ya kuona vilivyomo ndani ya chumba hicho, katika ukuta wa kulia nilikuta picha yangu kubwa iliyokuwa imebandikwa huku imeambatanishwa maneno yaliyosomeka kwa herufi kubwa

“SILENT NOTORIOUS"

Macho yalinitoka nikashinda kuelewa, nikageuka nyuma kumuangalia Mr Hamisi Ernest kwa lengo la kumuuliza maswali yaliyojengeka kichwani kwangu lakini nilikuwa nimeshachelewa, alikuwa ameshaondoka zake. Nikasogea ndani zaidi nikapanda kitandani huku macho yangu yakiendelea kufanya utafiti kama vile mtu anayetafuta kitu alichokipoteza muda mfupi uliopita, utafiti wangu haukwenda bure, niliona picha ndogo juu ya droo ya kitanda nikaichukua na kuitazama, ilikuwa picha ya miaka mingi iliyopita, nilifahamu hilo kwa sababu ilikuwa imefifia sana. Nilipoitazama vizuri niliwagundua waliokuwa kwenye picha hiyo, alikuwa ni marehemu baba yangu pamoja na Mr Hamisi Ernest enzi hizo wakiwa vijana wadogo wa miaka isiyozidi ishirini na tano mpaka saba. Hapo ndipo nilipogundua urafiki wa baba na Mr Kidua ulianza tangu walipokuwa vijana wadogo.

Nilirudisha macho ukutani nikaitazama tena picha yangu iliyoambatanishwa na maneno machafu niliyoshindwa kuyaelewa kabisa kipindi kile dhumuni la kuambatanishwa kwenye picha ile, lakini sasa nina majibu yote kwanini maneno yale yaliandika pale, hayakuandika kwa bahati mbaya. Kipindi nikiendelea kushangaa shangaa chumba kile nikapitiwa na usingizi mzito. Kelele za mwanamke na mtoto nisiowafahamu zilinishtua toka usingizini, nikatazama saa yangu ya mkononi ikaonesha kuwa ni saa moja kasoro dakika kumi asubuhi na moja asubuhi. Mwanamke yule alimbembeleza mtoto aache kulia lakini hali haikuwa kama alivyotarajia. Alimnyamanzisha kwa maneno matamu lakini mtoto aliendelea kulia kwa sauti kali, hakika maneno yale matamu yalikuwa kama shubiri kwa wana yule. Hali ile iliendelea mpaka mwanaume mwenye sauti nzito na sura ngumu akaingilia kati

“Huyo mtoto analia nini?”

Mwanamke yule akajibu kwa sauti ya upole

“Hata sielewi, darling”

Sauti ya mwanaume mwenye sura ngumu, Mr Hamisi Ernest, ikawa inaongezeka kila baada ya sekunde moja kupita kitu kilichopelekea kufahamu alikuwa akipiga hatua kuelekea sebuleni alipo mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa akilia.

“Ulifikiri ukimleta sebuleni ndio atanyamanza?”

Mwanamke yule hakumjibu chochote bali aliendelea kumnyamanzisha mwanae kipenzi. Mr Hamisi Ernest akamwambia mke wake

“Kuna taarifa mbaya kidogo zimetokea usiku wa jana...usiku wa kuamkia leo"

Akaruhusu ukimya upite kidogo kuruhusu mshangao wa mke wake kisha akaendelea

“Familia ya Mr Calist imeuliwa yote, kuanzia Calist mwenyewe, mke wake, mfanyakazi wa ndani mpaka walinzi wake wote wa getini”

Kauli hiyo ilipenya ndani ya moyo wangu kama kisu cha moto kama vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kuisikia, akili yangu haikuwa sawa hata kidogo, nilihisi kuchanginyikiwa zaidi kwa mawazo kila muda ulivyozidi kwenda. Kauli ya vifo vya watu wa familia yangu ilimshitua sana mke wa Mr Hamisi Ernest, nilimsikia akihamaki kwa sauti kubwa, akamuuliza mume wake

“Nani amekupatia taarifa hizi?”

Ukimya ulipita kama sekunde tatu ndipo niliposikia sauti ya Mr Hamisi Ernest ikijibu

“Ni story ndefu kidogo, lakini kwa ufupi nilipigiwa simu usiku wa manane na binti yake, Colotlida, nilishindwa kumuelewa katika maongezi yetu maana alikuwa akiongea kwa hofu sana huku kilio kikimtawala”

Akapumzika kidogo kisha akaendelea

“Nilihisi kuna hatari, nilikutazama nikaona umelala fofofo nikaamua kuchukua gari na kueleka nyumbani kwao….Duuuh!!! nilichokikuta ni michirizi ya damu mbichi na maiti tu…Hali inatisha sana, Colotlida pekee ndiye aliyenusurika kwenye mdomo wa kifo”

Mke wa Mr Hamisi Ernest akazidi kupiga kelele za mshangao akasahau habari za kusumbuliwa na mtoto wake, akauliza swali lingine

“Colotilda yupo wapi? Umemuacha kwenye nyumba yenye harufu ya vifo kila kona?”

Nilisogea mpaka kwenye mlango nikachungulia sebuleni kupitia sehemu ya kitasa ya kuingizia funguo, nilimuuona Mr Hamisi Ernest akimfuata mke wake akamkumbatia kisha akamwambia

“Calist alikuwa rafiki yangu sana na nimekufahamu wewe kupitia yeye…Siwezi kumuacha mtoto wake katika mdomo wa mamba”

Akamwachia kutoka katikati ya mikono yake kisha akaendelea kuongea huku akinyoosha kidole katika chumba nilichokuwemo.

“Yupo ndani ya chumba hicho amepumzika”

Nilivyoona vile nilirudi haraka kitandani nikajilaza usingizi wa uongo, kama vile nilijuwa nini kingetokea dakika chache mbele. Mke wa Mr Hamisi Ernest aliingia chumbani huku akilia kwa sauti kubwa iliyozidi kuniongezea uchungu wa kifo cha wazazi wangu. Ndani ya shuka machozi yakawa yakinimwagika kama maji. Alipofika kitandani alinifunua shuka akanikuta nikilia, alishindwa kujizuia alinikumbatia kwa nguvu huku kilio chake kikazidi zaidi ya awali. Alilia sana na kuongea maneno mengi ya uchungu yaliyoonesha alikuwa na ukaribu sana na baba yangu. Mr Hamisi Ernest alikuja kututuliza huku mikononi akiwa amemshika mtoto aliyekua akilia awali. Ilimchukua muda mrefu kututuliza kilio chetu. Mke wa Mr Hamisi Ernest akanichukua akanipeleka bafuni nikaoga, sikua na nguo yoyote ya kubadilisha hivyo basi alinifunga rubega kama mmasai kwa kitenge chake kisha akaniambia

“Baadae tutaenda kununua nguo zako”

Tulipofika sebuleni nilimkuta Mr Hamisi Ernest akiwa bize kupekua nyaraka muhimu za baba, zenye kuonesha uhalali wa umiliki wa mali zake nilizozichukua usiku kabda ya kuondoka nyumbani. Baada ya kuniona hakuonesha hali yoyote ya kushituka bali aliendelea na zoezi lake, nilipata hofu kidogo. Moyo ukaanza kunienda mbio kama mtu niliyetoka kukimbia mbio ndefu. Nikahisi usalama wa mali za baba unaweza potea bila mwenyewe kutegemea. Kipindi bado mawazo yakiendelea kusumbua ubongo wangu Mr Hamisi Ernest akaniambia kwa bashasha

“Hakika wewe ni Silent Notorious”

Sikumuelewa alikuwa akimaanisha nini, nikapiga hatua mpaka mbele yake, akavuta kiti akaniwekea nikae kisha akanitazama usoni akaniambia

“Mali za baba yako zipo salama kabisa, nimekagua vizuri, nyaraka zote muhimu zipo kama zinazovyotakiwa kuwepo”

Akavuta pumzi ndani kisha akaendelea

“Kuna faili moja tu ndilo halipo, faili la kesi aliyokuwa akiifatilia kimya kimya pasipo watu kujua”

Nilimtazama kwa mshangao wa hali ya juu kisha nikamuuliza kwa jazba

“Faili la kesi? Kesi ya nani na ilikua inahusu nini?...kwanini baba afatilie kesi? Amekuwa polisi?"

Mr Hamisi Ernest akatabasamu, tabasamu lililoonesha wazi lilikuwa maalumu kwa ajili ya kuniweka sawa kisha akanijibu

“Kitu cha msingi unachotakiwa kujua ni kuwa mali za baba yako zipo salama kabisa. Kuhusu masuala ya faili utajua wakati wa kujua ukifika”

“Nachofahamu, wewe ndiye unayejua jinsi ya kuziongoza mali za baba yako na sio vinginevyo”

Alinikabidhi zile nyaraka kisha akaongea

“Utakuwa mtoto mzuri sana chini ya mikono yangu”

Hofu niliyokuwa nayo yote ikafutika kama giza lifukuzwalo na mwanga wa alfajiri. Kipindi hicho mke wa Mr Hamisi Ernest alikuwa akiandaa chai mezani, nikatizama saa iliyokuwa ukutani ikanionesha ilikuwa saa mbili na nusu asubuhi. Nilimkumbuka baba, nikakumbuka alivyokuwa akinikaririsha neno siri (passwords) za akaunti zake za benki, hapo ndipo nilipoelewa alichomaanisha Mr Hamisi Ernest aliposema

“…Wewe ndiye unayejua jinsi ya kuziongoza mali za baba yako na sio vinginevyo”

Hakika mimi pekee ndiye ninaejua passwords za akaunti zote baba hivyo hakuna anayeweza kutoa wala kuingiza pesa bila idhini yangu.
Baada ya maandalizi ya chai tulijumuika wote mezani japokuwa kwa upande wangu chai ile haikuwa tamu hata kidogo. Kichwa kilikuwa kimejaa matukio ya vifo. Mr Hamis Ernest na mke wake waligundua hali hiyo wakanilazimisha nile, nilikula kwa shida sana chini ya usimamizi wao mpaka walipolidhika. Baada ya chai Mr Hamisi Ernest aliniambia niwaeleze nini nilichoshuhudia usiku wa matukio ya mauaji. Niliwasimulia kila kitu huku machozi yakinitoka, mke wa Mr Hamisi Ernest alilia kama mtoto mdogo kila alipokuwa akisikia sauti yangu ikisimulia mkasa huo. Nilipomaliza kusimulia Mr Hamisi Ernest akanitazama usoni kisha akaniambia

“Nitazame vizuri”

Akavuta pumzi ndefu ndani kisha akaitoa haraka, akachukua jagi akamimina maji kwenye glasi akanywa kisha akaendelea

“Kuanzia leo hapa ndio nyumbani kwako…sahau shule uliyokuwa ukisoma, sahau kutumia ubini wa baba yako, sahau marafiki zako wote, sahau kila kitu cha nyuma. Unachopaswa kukumbuka ni kutunza mali za baba yako tu…Unaanza ukurasa mpya wa maisha yako, ukurasa utakao kuweka huru siku zote za maisha yako”

Kauli ile ya kushangaza na kushitusha haikunishitua mimi peke yangu bali hata mke wake alihamaki kwa mshangao ulioambatana na maswali

“Mbona sikuelewi mume wangu, atasahau vipi mambo hayo? Mpaka ubini wa baba yake!...kwanini? Kuna nini hasa kilichojificha?"

Sauti laini ya wimbo wa Monica Seka uitwao Missounwa ulikuwa umeiteka sehemu yote ya sebule ya nyumba hiyo, msanii huyo toka nchini Ivory Coast anayeiburudisha dunia kupitia nyimbo zenye mahadhi ya Zouk, Afrobeat na Soukous alikuwa kipenzi cha Mr Hamis Ernest tangu enzi za ujana wake.

ITAENDELEA

* Naendelea kuchukua orodha ya wahitaji wa kitabu cha Afisa Usalama. Usipange kukikosa.

  • Yupo wapi God Mother?
  • Nini hatima ya Godfrey na Colotilda?
good

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mim

Mimi nahitaji soft copy
 
na mimj nakitaka boss usiache kuniambia kikiwa tayar nipe na bei kabisa japo part hii naisoma now saa 00:40 but imenifanya nilengwe na machoz uko vizur mzee
 
Tutaongea ndg, nitumie namba yako
 
na mimj nakitaka boss usiache kuniambia kikiwa tayar nipe na bei kabisa japo part hii naisoma now saa 00:40 but imenifanya nilengwe na machoz uko vizur mzee
Kama utahitaji nitumie namba yako
 
RIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri

SEHEMU: 16

Hofu niliyokuwa nayo yote ikafutika kama giza lifukuzwalo na mwanga wa alfajiri. Kipindi hicho mke wa Mr Hamisi Ernest alikua akiandaa chai mezani, nikatizama saa iliyokua ukutani ikanionesha ilikua saa mbili na robo asubuhi. Nilimkumbuka baba, nikakumbuka alivyokua akinikaririsha neno siri (passwords) za akaunti zake za benki, hapo ndipo nilipoelewa alichomaanisha Mr Hamisi Ernest aliposema

“…Wewe ndiye unayejua jinsi ya kuziongoza mali za baba yako na sio vinginevyo”

Hakika mimi pekee ndiye ninae jua passwords za akaunti zote baba hivyo hakuna anayeweza kutoa wala kuingiza pesa bila idhini yangu.
Baada ya maandalizi ya chai tulijumuika wote mezani japokuwa kwa upande wangu chai ile haikua tamu hata kidogo. Kichwa kilikua kimejaa matukio ya vifo. Mr Hamis Ernest na mke wake waligundua hali hiyo wakanilazimisha nile, nilikula kwa shida sana chini ya usimamizi wako mpaka walipolidhika. Baada ya chai Mr Hamisi Ernest aliniambia niwaeleze nini nilichoshuhudia usiku wa matukio ya mauaji. Niliwasimulia kila kitu huku machozi yakinitoka, mke wa Mr Hamisi Ernest nae alilia kama mtoto mdogo kila alipokua akisikia sauti yangu ikisimulia mkasa huo. Nilipomaliza kusimulia Mr Hamisi Ernest akanitazama usoni kisha akaniambia

“Nitazame vizuri”

Akavuta pumzi ndefu ndani kisha akaitoa haraka, akachukua jagi akamimina maji kwenye glasi akanywa kisha akaendelea

“Kuanzia leo hapa ndio nyumbani kwako…sahau shule uliyokua ukisoma, sahau kutumia ubini wa baba yako, sahau marafiki zako wote, sahau kila kitu cha nyuma. Unachopaswa kukumbuka ni kutunza mali za baba yako tu…Unaanza ukurasa mpya wa maisha yako, ukurasa utakao kuweka huru siku zote za maisha yako”

Kauli ile ya kushangaza na kushitusha haikunishitua peke yangu bali hata mke wake alihamaki kwa mshangao ulioambatana na maswali

“Mbona sikuelewi mume wangu, atasahau vipi mambo hayo? Mpaka ubini wa baba yake!...kwanini?”

ENDELEA

Mr Hamisi Ernest akanitazama kisha akarudisha macho kwa mke wake, akaongea

“Mr Calist nimefanya nae biashara miaka mingi kidogo, kwa mazingira ya kifo chake waliomuua watakuwa maadui katika biashara yake na lengo lao ni kutaka kumnyang`anya mali zake, hivyo basi wakimtambua huyu mtoto kuwa ni mtoto wa marehemu Calist lazima watamdhuru tu…Tunazungukwa na watu wabaya sana katika biashara zetu bila kujua”

Mke wa Mr Hamisi Ernest hakuridhishwa kabisa na jibu lile, akanitazama kisha akamtazama mume wake, akamuuliza swali

“Kwa hiyo una maana hata ndugu zake hutaki wajue alipo? Hutaki ahudhulie mazishi ya familia yake?”

Mr Hamisi Ernest alimwita mke wake kwa jina lake, hapo ndipo nilipofanikiwa kujua mke wake anaitwa Warioba Messo

“Warioba Messo, waliofanya mauaji ya kikatili wanaweza kuwa ndugu zake pia, msibani akafanye nini? Akajioneshe ili wammalizie!”

Kauli hiyo iliniuma sana baada ya kumsikia Mr Hamisi Ernest hataki niudhurie mazishi ya familia yangu eti kwa kuhofia usalama wangu, akili yangu ikapingana na maamuzi yao nikaamua kuwa ni lazima niende kuwazika baba na mama. Nikavunja ukimya

“Lazima niende kuwazika wazazi wangu”

Mr Hamisi Ernest alinitazama kisha akaongea kwa sauti ndogo ila yenye mkazo

“Baba yako alikwambia mimi ndio msaada pekee katika maisha yako, ukinipinga mimi ni sawa unapinga maamuzi ya baba yako”

Nilikaa kimya huku nikitafakari maneno hayo, kipindi nikiendelea kushambuliwa na mawazo kichwani mke wa Mr Hamisi Ernest akaongea kwa hasira

“Siku zote huwa nakwambia mume wangu una agenda nyingi za siri ambazo mimi sizijui, nahisi unajua mengi zaidi ya haya uliyoongea kuhusu kifo cha Calist”

Kauli hiyo ilinipa mashaka nikabaki najiuliza

“Anajua mengi kuhusu kifo cha baba? Kivipi?”

Mr Hamisi Ernest alimtazama mke kwa hasira za wazi wazi zilizoambatana na chuki kisha akamwambia

“Naona tunashindwa kuelewana na unaanza kuongea ujinga wako wa kila siku mbele ya mtoto anayehitaji msaada na faraja, nikufiche wewe ili iweje? Acha utoto wewe mwanamke”

Mke wa Mr Hamisi Ernest akamtazama mume wake kwa jicho la hasira, kweli alikuwa amefura hasira maradufu, hakumjibu chochote bali alimchukua mtoto wake aliyekua amelala kwenye sofa kisha akatokomea chumbani. Mr Hamisi Ernest akanitazama kisha akaniambia

“Aunt yako ana hasira sana…Twende sokoni nikakununulie nguo na vitu vyako vingine vya matumizi”

Nilimtazama kwa jicho la udadisi kisha nikamuuliza

“Hivi hivi nilivyovaa?”

Mr Hamis Ernest akatabatasu kisha akanijibu

“Huna nguo Colotilda, inuka twende haraka kabla aunt yako hajazua mengine”

Alichana karatasi toka kwenye kijidaftari cha kuandikia (notebook) kisha akaandika maneno machache kwa herufi kubwa yanayosomeka

“TUMETOKA KIDOGO, DARLING”

Akaiweka karatasi ile juu ya meza ya chakula kisha tukaondoka ndani ya sebule ile. Tulipofika nje alichukua gari lenye vioo vyeusi vyote vinavyomzuia mtu aliye nje ya gari kumuona aliye ndani ya gari, awali sikujua lengo lake lilikua ni nini lakini baadae kila kitu kilikua wazi. Tulifika mwanga sokoni saa tano kasoro asubuhi, nilichagua nguo nyingi ambazo sikumbuki hata idadi yake. Viatu, cheni, mikoba, mafuta na vingine vingi. Hakika nilikua malikia siku hiyo. Manunuzi niliyofanya siku ile sikumbuki kama niliwahi kuyafanya kama yale kipindi cha uhai wa familia yangu. Baada ya kukamilisha manunuzi yote Mr Hamisi Ernest aliniambia

“Tunaelekea nyumbani kwenu kuangalia nini kinachoendelea, sharti ni moja tu, hutakiwi kushuka ndani ya gari wala kupiga kelele tutakapofika”

Akakohoa kidogo kisha akaendelea

“Kila kitu utashuhudia kupitia kwenye dirisha la gari, mtu aliye nje hawezi kukuona ndani ya gari, uwe na amani”

Akanitazama usoni kisha akanishika bega, akaendelea

“Hivyo ndivyo utakavyohudhuria kilio na mazishi ya wazazi wako”

Nilimtazama vizuri usoni, nikamuuliza swali

“Kwanini aunt anasema unajua mengi kuhusu kifo cha baba, kuna nini hasa?”

Alitabasamu kidogo kisha akapakia mizigo yangu katika buti la gari akarudi nilipo akanifungulia mlango kisha akaniambia

“Waweza kuingia malaika wangu”

Niliingia ndani ya gari kisha na yeye akaingia, safari ya kuelekea Mjimwema nilipokua naishi na wazazi wangu ikaanza, huku mikono yake ikiwa makini kwenye usukani wa gari Mr Hamisi Ernest akarudisha macho kwangu akatabasamu tena, akaniamba

“Wewe bado mtoto mdogo sana lakini umeshashuhudia uchafu wa dunia hii, Aunt yako hajui chochote kuhusu dunia ndio maana anielewi kabisa”

Jibu hilo bado lilikua ni fumbo kwangu sikuweza kumuelewa amemaanisha nini, nilishindwa kuona uhusiano wa mimi kushuhudia vifo vya wazazi wangu na maswala yao ya kila siku, nikamwambia

“Sijakuelewa father”

Akatabasamu tena kisha akaniambia

“Ipo siku utanielewa”

Majibu yake yalimaanisha kuwa kuna taarifa ananificha, nikaamini hicho ndicho kinachomuuzi sana mke wake, swali likatambaa katika ubongo wangu

“kwanini ananificha mambo yanayohusu familia yangu”

Niliamua kukaa kimya safari ikaendelea kimya kimya pasipo mazungumzo yoyote mpaka tulipofika karibu na nyumbani. Mr Hamisi Ernest aliniamuru nikae kiti cha nyuma ili nisiweze kuonekana na mtu yeyote atakapo fungua mlango wa gari. Nyumbani hali haikua shwari hata kidogo, polisi walikua wamezagaa kila kona ya nyumba huku silaha za moto zikiwa mikononi, walikua wamezungusha kamba za njano kuzunguka nyumba yetu, kamba zenye maandishi yaliyosomeka

“POLICE”

kwa lengo la kuzuia raia wasiweze kuingia ili kupisha uchunguzi na upelelezi ufanyike vizuri. Magari zaidi ya kumi na tano yalikua yamejipanga pembeni ya nyumba yetu, kitu kile hakikunishangaza hata kidogo kwa sababu nilijua ni matajiri wenzake na baba walimekuja kushuhudia majanga yaliyoikumba familia ya baba, niliyatazama magari yale kwa hasira baada ya kukumbuka maneno ya Mr Hamisi Ernest kuwa walioua familia yangu wanaweza wakawa ni wafanya biashara wenzake. Gari la Mr Hamisi Ernest lilipiga breki jirani na magari yale kisha Mr Hamisi Ernest akageuka nyuma akanitazama akanishika kichwa kama mtu anayekipapasa kisha akaniambia

“Hutakiwi kushuka wala kufungua mlango, mimi naenda ndani kushuhudia nini kinachoendelea, hapo ndipo nitakapojua nini cha kufanya ili ushuhudie mazishi ya wapendwa wako”

Nilimjibu kwa ishara ya kidole gumba nikimaanisha kuwa nimemuelewa, alinishika mkono wangu wa kulia akasema

“Utajua kila kitu siku za mbeleni, wewe bado mdogo sana”

Nilishindwa kuelewa kwanini anapenda kuniambia kauli hiyo mara kwa mara, alitabasamu kisha akashuka moja kwa moja akaenda kwenye ule umati uliozuiliwa na kamba ili wasiingie ndani. Alimwita polisi mmoja mwenye umri kati ya miaka ishirini na tatu na ishirini na sita akaongea nae, sikuweza kujua waliongea nini kutokana na umbali uliokuwepo kati yangu na umati ule. Haikumchukua muda hata wa dakika moja kamba iliyokua imeweka uzio ikainuliwa kisha Mr Hamisi Ernest akaruhusiwa kuingia ndani ya geti kitu kilichonishangaza

Kwanini yeye ameruhusiwa wakati watu wengine wote wamekataliwa?.

Ule umati ulipiga kelele za hasira nikahisi wamekasirika na kitendo cha polisi kumruhusu Mr Hamisi Ernest aingie ndani ya geti wakati wao wamekataliwa. Vijana watatu waliokua kwenye umati ule waliondoka wakaja moja kwa moja mahari yalipopaki magari jirani kabisa na mimi wakiwa wanabishana, walionekana ni watu wenye pesa za kutosha kimuonekana, walikua wamevaa mavazi, cheni, pete na viatu vya gharama. Kichwani walikua wamevaa kofia aina ya kepu zilizofanana zenye herufi zilizosomeka

“VSM”

Sikuweza kuelewa nini maana ya zile herufi nikahisi ni kofia za kawaida tu zinazovaliwa na vijana wa mjini.

KOSA

Mmoja wao akaropoka kwa hasira yenye chuki dhidi ya watu alioona wanakwamisha zoezi lao.

“Ndio maana wanakufa mapema”

Sauti ile haikua ngeni hata kidogo katika masikio yangu, ni sauti niliyokwisha isikia muda sio mrefu tena kwenye mazingira yasiyo salama hata kidogo, nilipojaribu kuitafakari nikakumbuka ni sauti iliyomwambia baba

“Haya ndiyo malipo ya ukaidi wako”

Kauli aliyoambiwa baba baada ya mama kuchomwa kisu cha tumbo mbele yake, Hakika ni wale wauaji waliosambaratisha familia yangu. Nilijaribu kuwatizama vizuri ili niweze kufahamu sura zao lakini kofia zao zilikua kama ngao iliyonizuia kuwatambua. Moyo uliniuma sana nikatamani nifungue mlango ili nitoke ndani ya gari niwashuhudie ana kwa ana lakini kauli ya Mr Hamisi Ernest iliyonisisitiza nisitoke ndani ya gari wala nisifungue mlango ikajirudia kichwani kwangu. Bila kutarajia machozi yalinitiririka katika mashavu yangu yakaroanisha nguo mpya niliyonunuliwa muda mfupi uliopita. Vijana wale wakaingia ndani ya magari yao ya kifahari wakaondoka kwa mwendo kasi huku nyuma wakiniachia maswali mengi akilini mwangu

“Ndio maana wanakufa mapema”

Kauli hiyo ikajirudia tena kwenye akili yangu nikabaki nikijiuliza kwanini wanaua watu?. Lakini sikupata jibu lolote. Baada ya kama dakika kumi Mr Hamisi Ernest alirudi ndani ya gari akakuta mashavu yangu yameloa machozi, hakushangaa sana maana alijua nimewakumbuka wazazi wangu baada ya kuiona nyumba yetu. Alichukua chupa ya maji akaiweka mdomoni akanywa maji yote kisha kopo akalitupa nje ya gari pasipo kujali kuwa anachafua mazingira kisha akageuka nyuma akanitizama, nilihisi anataka kuongea kitu lakini kabla hajafungua mdomo wake nikamuuliza haraka

“Mbona wewe umeruhusiwa kuingia ndani ya geti?”

Alinishika nywele zangu kisha akazipapasa kwa kupeleka mkono mbele na nyuma huku akitafakari jibu la kunipa, akaniambia

“Polisi waliopo getini nafahamiana nao vizuri, unajua sisi watu wenye pesa tuna mahusiano mazuri na jeshi la polisi kwa lengo la kujihakikishia usalama wetu na mali zetu”

Jibu lake lilikua zuri lakini sikuliamini moja kwa moja, aligundua hilo akaamua kubadilisha mada

“Naona mashavu yako yameloa machozi, punguza kulia Colotilda”

Ilinibidi nimuelezee kila kitu nilichoshuhudia kuhusu wale vijana waliovaa kofia zenye herufi zilizosomeka ‘VSM’ nikamuhakikishia kuwa wale ndio walioua familia yangu pamoja na wafanyakazi wetu. Mr Hamisi Ernest alihamaki sana akanitazama kwa umakini kisha akaniuliza

“Wameelekea njia ipi?”

Nilimuonesha kwa ishara ya kidole walipoelekea vijana wale waliovaa vitu vya gharama, Mr Hamisi Ernest akauliza swali lingine sasa akiwa makini zaidi ya awali

“Wakoje? na wapo kwenye usafiri gani”

Nilimjibu

“Kama nilivyokwambia wamevaa kofia zenye herufi zinazosomeka VSM, Wapo watatu na kila mmoja amepanda kwenye gari lake…Wote wana magari tofauti aina ya BMW”

Nililifahamu jina la gari hizo kwa sababu gari la aina hiyo ndio mama alikua akipenda kulitumia katika mizunguko yake. Mr Hamisi Ernest hakuongea tena chochote bali aliwasha gari haraka kuelekea uelekeo niliomwonyesha kuwa wale vijana wameelekea, macho yake yalikua makini sana kuangaza barabarani mara kushoto mara kulia. Akavunja ukimya akaniambia

“Ukiona gari linalofanana na magari ya wale vijana niambie”

Niliitikia kwa kichwa akaendelea kuangazana barabarani bila mafanikio yoyote, tulifika mpaka mwanga sokoni kwenye njia panda ya kwenda Mwandiga, Ujiji na Airport, alisimamisha gari akashindwa ashike njia ipi, akanitizama kisha akaniuliza

“Umekariri namba za gari hata moja”

Nilimtazama nikashindwa kumjibu chochote, aligundua maana yake nini akaniambia

“Siku nyingine usisahau kukariri namba ya gari ni muhimu sana…alafu usimwambie Aunt yako kuwa umewaona majambazi walioua familia yako”

Akafungua chupa lingine la maji akanywa kisha akaendelea

“Usije ukamwambia kuwa tumefatilia watu tunaohisi ni majambazi, usithubutu”

Aliwasha gari na safari ya kwenda nyumbani kwake ikaanza. Nilifikiria sana inakuaje Mr Hamisi Ernest hataki mke wake ajue mambo hayo, nikajiuliza mwenyewe akilini mwangu

“Kuna nini hapa?”

Nilishindwa kuvumulia nikaamua kumuuliza

“Aunt akijua kuna ubaya gani?”

Alitabasamu huku macho chake yakitazama mbele gari linapoelekea kisha akanijibu

“Aunt yako siku zote hapendi nidhulike, akisikia nafatilia majambazi atahofia sana usalama wangu”

Akanywa tena maji yake, akalegeza tai kisha akaendelea

“Biashara tunazofanya wakati mwingine lazima tuingie kwenye shida na watu wabaya, sasa hapo ndipo Aunt yako asipotaka…yeye anataka kusamehe kila kitu”

Nilimtazama Mr Hamisi Ernest maana sikuridhishwa kabisa na majibu yake kila ninapomuuliza swali, nikaamua kumwambia

“Sasa nimekuelewa lakini inatakiwa tupeleke taarifa polisi”

Alicheka tena kwa sauti kubwa kitu ambacho kilinishangaza, akanitazama kisha akaniambia

“Polisi sio watu wa kuwaamini kiasi hicho, wanaweza kukugeuzia kesi ukaonekana wewe uliyetoa taarifa ndio muhusika”

Alizidi kunichanganya kabisa baada ya kuona hataki hata polisi wajue masuala yangu kuwa nimewaona wauaji, nikaamua kumuuliza

“Sasa nitawapataje wauaji kama taarifa hizi hazitawafikia polisi”

ITAENDELEA

* Simuelewi Mr Hamis Ernest

* NAENDELEA KUCHUKUA MAJINA YA WAHITAJI WA RIWAYA YA AFISA USALAMA. NITUMIE JINA NA NAMBA YAKO. USIPANGE KUKOSA KIGONGO HIKI. View attachment 1851519

Shukrani Boss
 
Back
Top Bottom