Riwaya: Afisa usalama

Riwaya: Afisa usalama

Sio mbaya sadaka maana hata kitabu watapeana tu
Ila Afisa Usalama ungeimalizia humu
Mm mwenyewe nilimshauli hivyo, kwanza unatengeneza jina kwa kazi moja nzuri and then watu watavutiwa tu kazi zako automatically
 
Leo hii unatoa simulizi ya 03 kwenye thread ya simulizi moja na zote hazitoshi.

Soko halitafutwi hivyo mkuu
 
Usalama wa TZ kama wachawi vile, hawataki mambo yao yafahamike kwa wasiohusika nayo. Inabidi uwashukuru sana kama wamekuruhusu uendelee na kazi yako, tofauti na hapo ungeiendelezea kule waliko watu wengi (kimyani).
 
Mpendwa Msomaji, Mpendwa Mwandishi

Nakumbuka nilitoa ahadi kuwa riwaya yangu pendwa ya AFISA USALAMA ilitakiwa kutoka kabla ya tarehe 20/08/2021 lakini haikuwa kama nilivyoahidi, kuna mambo yaliyo juu ya uwezo wangu yalisababisha nishindwe kutimiza ahadi niliyotoa.

Ilikuwa siku ya Jumatano ya tarehe 11/08/2021 nilichukuliwa (nilikamatwa) na polisi kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo ya kina juu ya riwaya hiyo iliyokuwa mbioni kutoka. Niliwekwa ndani ya chumba cha mahabusu kwa muda wa siku sita, yaani kuanzia Jumatano ya tarehe 11/08/2021 mpaka Jumatatu ya tarehe 16/08/2021, lakini naendelea kuripoti polisi kila Jumanne na Ijumaa ya wiki mpaka kila kitu kitakapokuwa sawa.

Vitendea kazi vyangu vilichukuliwa na polisi kwa ajili ya kupekuliwa yaani simu na vinginevyo (Ndiyo maana nilikuwa sipatikani hewani). Nilihojiwa mara kadhaa, nikaeleza maudhui ya kitabu, polisi nao walinijuza mtazamo wao. Hakika walikuwa sahihi kulingana na hoja waliyoweka mezani (sikuwa na ruhusa ya idara ya Usalama wa Taifa kutumia jina lao). Riwaya yangu ilitumwa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) ili ichunguzwe maudhui yake na mwisho wa siku watoe maamuzi na mustakabali wangu na kazi yangu.

BAKITA walitoa maamuzi, baadhi ya maamuzi hayo ni kubadilisha jina la riwaya na vitu vichache ambavyo haviathiri chochote katika mpangilio wa riwaya, nawashukuru sana kwa hilo. Leo hii tarehe 03/09/2021 nimerudishiwa simu yangu hivyo basi nitakuwa hewani kama kawaida. Nawashukuru polisi pia kwa ushirikiano wao. Nipo nafanya marekebisho niliyoagizwa ili mzigo uingie sokoni. Marekebisho yakikamilika nitawasilisha ofisi ya BAKITA na polisi ili watoe idhini ya kazi kuanza kuchapwa upya.

Nakumbuka siku moja kabda ya kukamatwa niliwasiliana na mchapaji niliyempa kazi ya kuchapa vitabu, ndugu Malle Hanzi akaniambia yupo hatua za mwisho za kukamilisha kazi niliyompa (kazi ilikuwa imefikia zaidi ya asilimia sabini na tano kukamilika), hivyo basi kauli ya BAKITA ya kunitaka kubadilisha kichwa cha riwaya na baadhi ya mambo machache imeathiri kazi yote iliyokuwa mbioni kukamilika. Hasara. Siwezi walaumu kwa sababu walifanya kazi yao kama baraza.

Nilitamani kuiacha kazi hiyo kwa sababu ya hasara iliyonipa lakini ushawishi wa watu wangu wa karibu umesisitiza nisiitupe kazi niliyoiandaa kwa akili kubwa, akili iliyoleta taharuki. Nimeamua kuzivaa upya gharama za uchapishaji wa riwaya hiyo. Naomba mnisaidie kidogo kwenye suala la bei ya manunuzi, mwanzo nilipanga kuuza kitabu kwa bei ya Tsh 12,000 lakini kutokana na changamoto hiyo kitabu kitauzwa Tsh 15,000 lakini ukihitaji kununua kwa bei zaidi ya hiyo unaruhusiwa pia. Naomba mnishike mkono kwenye jambo hili.

Nitawafahamisha lini kitabu kitakuwa tayari, mambo yakienda vizuri kama hali ilivyo sasa hakitachelewa kutoka kwa sababu marekebisho ni machache sana. Ndani ya wiki ijayo nitawajulisha jina jipya la riwaya yetu iliyokuwa ikiitwa AFISA USALAMA, lakini kava (cover) la kitabu litabaki kuwa lile lile kwa sababu jina jipya lazima liendane na riwaya husika.

Kuhusu riwaya ya UWAHI WA MWANANGU iliyokuwa ikiendelea katika kurasa zangu za kijamii itaendelea kama kawaida kuanzia sasa.

NB: Waweza weka ODA ya kitabu kama bado hujaweka, tuma jina na namba yako kwenye namba 0758 195 890 au nitumie inbox.

Sikuwatenga ndugu zangu bali vyombo vinavyotupa miongozo sahihi vilikuwa kazini. Nimeona niwape taarifa kwa sababu nyie ndiyo wasomaji wangu, wateja wangu na hadhira yangu kwa ujumla.

Mwandishi Chipukizi,
Emmanuel Phiri, Mwandishi Phiri,
emmanphiri141@gmail.com
0758 195 890,
Kigoma, Tanzania.
Pole sana!bora ungeiweka hapa tusome tu!kuliko shida hizo ulizopata!
 
Back
Top Bottom