InshaalahSaa tisa ndg
kazi na dawa, umeeleweka mkuuRIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri
SEHEMU: 21
ILIPOISHIA
Ofisi ya Rais ilimpa kazi Mr Paul Siafu kuchunguza na kubaini wahalifu wanaofanya mauaji na kuacha kitambaa chenye maandishi yanayosomeka ‘very sorry marehemu’. Alipewa muda wa miaka mitatu, miaka hiyo imeisha na inasemekana Mr Paul Siafu ameshakamilisha kazi hiyo na ameshaandaa ripoti maalumu ya kuwasilisha ofisi ya Rais”
ENDELEA
Colotilda akauliza kwa shauku
“Unamaanisha Mr Paulo Siafu Siafu aliandaa ripoti yenye majina ya wahalifu, ripoti yenye ufafanuzi wa wahalifu wa kundi la The Devil?”
Mr Hamisi Ernest akamshika kichwa Colotilda kisha akamwambia
“Una akili sana ndio maana nikaamua kukuingiza ndani ya idara hii, akili yako nyepesi sana kufikiria”
Akatoa mkono kwenye kichwa cha Colotilda kisha akaendelea
“Ndio, kuna ripoti yenye majina hayo, kitu kinachonishangaza Mr Paulo Siafu kauliwa kipindi ambacho alitakiwa kuwasilisha ripoti hiyo ofisi ya Rais na ikiwezekana apandishwe cheo kama alivyoahidiwa kuwa mkuu wa idara ya Usamala wa Taifa kanda ya Magharibi”
Akapiga mwayo mrefu kisha akaendelea
“Tuliokuwa tunajua habari hii ya marehemu kufanya kazi ya kutafuta majina ya wahalifu ni viongozi wakubwa wa idara, Maafisa Usalama mwengine hawakushirikishwa jambo hili. Sasa nani atakua amemuua kama sio kiongozi mwenzetu wa idara hii? Na kama jibu ni ndio basi kiongozi huyo wa idara atakua anashirikiana na kundi hilo la majambazi sugu”
Akatazama saa yake ya mkononi, ikamuonesha ni saa saba mchana akapuuzia kisha akaendela
“Ripoti aliyoiandaa ndio itakuwa chanzo cha kifo chake”
Colotilda akainamisha kichwa chini akatafakari kwa muda wa kama sekunde tatu kisha akainua kichwa chake, akasema
“Kati yenu viongozi wa juu kuna msaliti anayeendesha kundi hilo au anayeshirikiana na magaidi hao, ugumu unakuja jinsi ya kumfahamu kiongozi huyo”
Mr Hamisi Ernest akaendelea kumfafanulia Colotilda
“Nimekabidhiwa kazi ya kufatilia kifo cha Mr Paulo Siafu ili kumbaini au kuwabaini wahalifu, sasa najua nafatiliwa kila hatua ninayopiga”
Akatazama saa kwa mara nyingine kisha akaendelea
“Nakukabidhi kazi hii ufatilie juu chini mpaka tubaini nani anaongoza kundi hilo la majambazi, pia tujue taarifa kamili kuhusu ripoti aliyoiandaa Mr Paulo Siafu yenye majina ya wahalifu. Hutakiwa kumshirikisha yeyote ndani na nje ya idara yetu kwa sababu hatufahamu nani mwema na nani adui”
Akameza mate funda moja kisha akaendelea
“Najua umemzoea sana Magoela lakini naomba uelewe kuwa hata yeye hutakiwi kumwambia lolote. Kazi yako ya ushushushu imeanzia hapa, japokuwa kazi hii ni ngumu lakini ndio kipimo halisi cha ukomavu wako”
Colotilda alikua kimya akimsikiliza kwa makini Mr Hamisi Ernest, mzee yule akaendelea
“Utakua unaripoti kwangu kila hatua utakayopiga kwenye kazi hii, kumbuka lazima tushirikiane kila kitu ili kazi iishe haraka iwezekanavyo”
Mapigo ya moyo ya Colotilda yakaongeza kasi kama mtu aliyekimbia riadha, akili yake ikafikiria haraka sana, sasa akaona anaingizwa kwenye mdomo wa kifo. Atakataa vipi kuifanya kazi hiyo wakati ndio taaluma aliyoandaliwa kuifanya? Atakataa vipi wakati anamuheshimu sana Mr Hamisi Ernest na ndio baba yake aliyebakia kwenye ulimwengu huu uliokithiri machafuko na maafa?. Colotilda akamtazama usoni Mr Hamisi Ernest kisha akamwambia
“Wewe ni mzee wangu, nina kuhakikishia kuwa lazima nifahamu kila kitu kuhusu kazi uliyonipatia. Huyo anayejifanya Afisa Usalama mkubwa kumbe ni jambazi lazima afahamike kabda hali haijawa mbaya zaidi”
Maneno hayo yalimfurahisha Mr Hamisi Ernest, akaamini Colotilda ameiva hasa hasa kwenye idara hiyo. Mr Hamisi Ernest aliona uoga wote wa Colotilda aliokua nao utotoni sasa umetoweka, Colotilda amekua mpya. Msichana mrembo mwenye roho ya simba. Mr Hamisi Ernest akamwambia Colotilda
“Wewe ni Silent Notorious kama ulivyoitwa tangu ulipokua mtoto, lazima udhibitishe hilo. Vile vile ukichunguza kwa umakini unaweza ona kuna uhusiano mkubwa kati ya hawa wauaji na vifo vya familia yako”
Kauli hiyo ikamuongezea hasira Colotilda akachukua kitambaa toka kwenye mfuko wa jinzi aliyovaa kisha akajifuta chozi jembamba lililokua likitengeneza mfereji katika shavu lake la kulia. Baada ya dakika kumi Colotilda alimuaga Mr Hamisi Ernest Ernest kisha akaenda kwa mzee Calist alipofikia baada ya kuwasili Tanzania. Kipindi Mr Hamisi Ernest na Colotilda walipokua wakiongea na kupanga jinsi ya kupambana na maadui waliomuua Mr Paulo Siafu, upande wa pili wa shilingi ndani ya chumba namba 17 katika hoteli maarufu ya kifahari mkoani Kigoma inayoitwa ‘Hill Top’ walikuwemo Mr Aloyce Ndosi na Magoela. Mr Aloyce Ndosi alifikia katika hoteli hiyo siku aliyofika mkoani Kigoma kutokea Dar es salaam. Kikao kizito cha siri kilikuwa kikiendelea kati ya Mr Aloyce Ndosi na Fortunatus Magowela . Mr Aloyce Ndosi akamwambia Magowela
“Kuna kazi nataka kukupa, kazi itakayokufanya kuwa na uadui na Mr Hamisi Ernest”
Kauli hiyo ilimshtua kidogo Mago, akamtazama vizuri Mr Aloyce Ndosi kisha akauliza
“Nimesikia vibaya au ndivyo ulivyokusudia?”
Mr Aloyce Ndosi akacheka kinafiki kisha akamwambia Magoela
“Najua mliandaliwa kuja kulitetea Taifa la Tanzania lakini kuna kipindi lazima uangalie maslahi yako binafsi, usiwe mjinga kiasi kwamba ukasahau umasikini uliokua nao”
Mr Ndosi akachukua maji yaliyokua kwenye glasi akamwa fundo nne mfululizo kisha akaendela
“Nilikupigania uwe Afisa Usalama kwa sababu lengo langu lilikua uje kunisaidia kwenye mambo yangu, mambo ambayo yanahitaji umakini wa hali ya juu. Umri wangu umekwenda sana nahitaji kijana kama wewe wa kusimamia kila hatua”
Akili ya Magoela ilikua bado ikifikiria juu ya suala la kuwa adui wa Mr Hamisi Ernest, mzee ambaye alikua kama mzazi wake siku zote za masomo na mafunzo yake ya Uafisa Usalama, sasa itakuaje amlipe kwa ubaya?. Mr Aloyce Ndosi akaendelea
“Kama unavyojua nilikua mkuu wa idara ndani ya mkoa wa Dar es salaam lakini sasa nimeletwa mkoani Kigoma, siku yoyote nitakabidhiwa ukuu wa idara ndani ya mkoa huu. Kwa lugha nyepesi ninahamishwa toka Dar es salaam kuja Kigoma"
Akapumzika sekunde mbili, akaendelea
“Mkuu wa idara mkoani hapa alitakiwa awe mkuu wa idara wa kanda nzima ya magharibi lakini ndio kaishatangulia kwa Mungu, hilo sio tatizo bali tatizo limekuja baada ya kifo chake”
Magoela akauliza kwa shauku kutaka kujua zaidi
“Tatizo gani?”
Mr Aloyce Ndosi akainuka kwenye kiti alichokua amekaa akaanza kutembea tembea ndani ya chumba hicho huku akiongea
“Nasikia marehemu ameacha ripoti yenye majina ya watu wanaosadikika ni waharifu, watu wanaohujumu uchumi na kufanya matukio mengine yenye kutishia usalama wa nchi. Nataka ufatilie kuhusu ripoti hiyo, nataka inifikie kabla haijamfikia kiongozi yeyote wa idara hii. Hapo ndipo uadui wa wewe na Mr Hamisi Ernest unapoanzia, kwa sababu na yeye lazima afatilie pia kuhusu ripoti hiyo ili akamilishe kazi aliyopewa”
Magoela akamtazama kwa makini Mr Aloyce Ndosi kisha akamuuliza swali lingine ili apate ufafanuzi zaidi
“Kwanini unapingana na Mr Hamisi Ernest?”
Mr Ndosi akamjibu Mago huku akimtazama usoni kwa macho yake makavu
“Kwa sababu nataka siku za usoni uje kurithi mikoba yangu, nataka uje kuongoza kundi langu, kundi lenye matawi yake karibu kila kona ya nchi hii. Nataka upambane na Mr Hamisi Ernest kwa sababu anajifanya anajua kufatilia haki anasahau duniani hakuna haki kabisa, haki tutaikuta kwa Mungu tu”
Maneno hayo yakazidi kumchanganya Magoela, maswali mengi yakajazana kwenye kichwa chake. Akaamua kuuliza swali moja kati ya maswali hayo
“Una maanisha wewe ndiye uliyemuua Mr Paulo Siafu?”
Mr Aloyce Ndosi akatabasamu kidogo, meno yake yaliyoathirika na moshi wa sigara yakaonekana vizuri, akamjibu Magoela
“Hapana! Bali vijana wangu ndio waliomuua”
Akachukua tena glasi yake ya maji akanywa mafundo matatu kisha akaendelea
“Kiherehere chake ndicho kilichosababisha atangulie kwa Mungu. Naona Mr Hamisi Ernest anataka kumfuata Mr Paulo Siafu”
Mr Aloyce Ndosi akamueleza Magoela kuwa yeye ndie mmiliki wa kundi la majambazi wanaoua na kutelekeza kitambaa chenye maandishi yanayosomeka ‘Very sorry marehemu’. Hakuishia hapo bali alimueleza pia kuwa alimuua Mr Paulo Siafu baada ya kiongozi kutaka kutoa ripoti yenye kufichua maovu yake hadharani, lakini baada ya kumuua waliitafuta ripoti hiyo bila mafanikio. Uchunguzi ndani ya nyumba ya Mr Paulo Siafu uliendelea taratibu ndipo walipofanikiwa kukuta kijitabu kidogo ndani ya droo ndogo ya kitanda, ndani ya kijitabu hicho ilikutwa picha ndogo ya pasipoti saizi (passport size). Walipoigeuza nyuma picha hiyo walikua imeandikwa maneno machache yaliyosomeka “Ripoti kwa Rais”. Mr Aloyce Ndosi akamalizia maji yaliyokua kwenye glasi kisha akaendelea
“Baada ya kuona picha hiyo yenye ujumbe huo kazi ikabadilika. Sura ya kijana aliyekua kwenye picha ilikua ngeni kwa kila mmoja wetu lakini nashukuru Mungu nina vijana wengi kila sekta. Juzi nimeletewa taarifa na kijana wangu anayefanya kazi katika jeshi la polisi kuwa amebaini kijana huyo yupo gerezani, gereza la bangwe”.
Mr Aloyce Ndosi akapumzika kidogo kisha akaendelea
“Inasemekana ana miaka miwili gerezani, anatumikia kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na kesi ya kupanga kulipua jengo la mahakama mojawapo inayopatikana jirani na uwanja wa mpira wa Lake Tanganyika. Hapo nashindwa kuelewa kidogo, yaani inakuaje mtu mwenye ripoti hiyo yenye majina ya wahalifu awe gerezani wakati muda wa kuwasilishwa ripoti hiyo umeshafika?”
Akili ya Magoela ikazunguka haraka, ikashindwa kuhimili maswali yaliyojengeka kichwani kwake akaamua kuuliza ili kupunguza mrudikano wa maswali hayo.
“Kama huyo muhusika yupo gerezani kwa hiyo una maanisha nimfuate huko? Namfuata vipi wakati mimi sio mfungwa?”
Mr Aloyce Ndosi akatabasamu kwa maswali aliyoulizwa na Magoela, aliona katika maswali aliyowahi kuulizwa na kijana huyo maswali ya sasa ni rahisi kujibika, akamjibu huku akimpiga piga begani.
“Polisi aliyeniletea taarifa ya kijana tunayemtafuta anafanya kazi katika gereza la bangwe, vile vile hufanya kazi katika kituo cha polisi kilichopo jirani na mahakama ya mkoa. Hivyo basi suala la wewe kutengenezewa kesi na kuingizwa moja kwa moja gerezani pasipo kupitia mahakamani ni jambo dogo sana”.
Mago alifikiria suala hilo akaona hana jinsi zaidi ya kufanya kazi iliyo mbele yake, aliifikiria familia yake aliyoiacha jijini Dar es salaam akaona jinsi ilivyoathiriwa na umasikini uliokithiri. Akajiona yeye ndiye msaada pekee anayetegemea, sasa lazima achukue maamuzi magumu ili atengeneze pesa nyingi zaidi zitakazoweza kuwasaidia wazazi pamoja na ndugu zake. Japokua alikua akipewa pesa nyingi zilizoweza kukidhi mahitaji yake ipasavyo lakini alitamani maisha aishiyo yeye waishi jamii yake yote ya Dar es salaam. Kichwani kwake aliapa hataweza kumuua Mr Hamisi Ernest hata kama ukitokea ugumu wa namna gani katika kazi iliyo mbele yake, alimfikiria Colotilda pia akaona kuna ugumu katika kazi yake. Kwa akili yake ya ajabu akahisi Colotilda anaweza kuwa nyuma ya kazi ya Mr Hamisi Ernest, sasa aliona vita kati yake na Colotilda, alifikiria atafanyaje ili kukwepana kukutana ana kwa ana na Colotilda. Colotilda alikua kama dada yake wa tumbo moja, sasa aliona ugumu wa kazi iliyo mbele yake. Mago akamwambia Mr Aloyce Ndosi
“Kazi iliyo mbele yangu ni ngumu sana kwa sababu nahisi Colotilda atakua amevaa viatu vya Mr Hamisi Ernest , sasa akijua nipo gerezani kila kitu kitakua kigumu kwa sababu najua uwezo wake wa uchunguzi na utafiti”
Mr Aloyce Ndosi akakuna kichwa chake, kichwa kiwaka moto, awali hakufikiria kabisa uwepo wa Colotilda. Jambo aliloambiwa na Magoela aliona lina ukweli asilimia zote. Kama ilivyo kawaida yake roho ya ukatili ikamwingia, yakamtoka maneno makali yaliyomchanganya zaidi Magoela
“Kila atakayeibuka kuwa kipingamizi kwenye jambo hili atakua amejiingiza mwenyewe kwenye mlango wa kifo, sitaki siri yangu ifichuke”.
Magoela aliona ukatili halisi wa mzee huyo, akaona kweli amezamilia kufanya ukatili wowote kwa lengo la kukinga siri zake zilizo njiani kufichuka. Suala la kumuangamiza Colotilda nalo lilileta taswira mpya katika akili yake yake, akamueleza Mr Aloyce Ndosi
“Kumbuka Colotilda ni kama dada yangu wa tumbo moja, nimekua nae toka utotoni na tumesaidiana vitu na mambo mengi mpaka tumefanikiwa kufika hapa tulipo. Sasa nitawezaje kumdhuru endapo akiwa kikwazo katika suala hili?”
Sura ya Mr Aloyce Ndosi ikabadilika, makunyanzi yakaishambulia sura yake iliyotawaliwa na ndevu nyingi mashavuni. Akamuangalia Magoela kwa macho makali kisha akamwambia kwa sauti ya juu kidogo
“Huyo Colotilda umemjua baada ya kukutana Afrika Kusini, huna undugu nae hata kidogo umesikia? Ndugu zako umewaacha Dar es salaam”
Mr Aloyce Ndosi alikua kama mzazi kwa Magoela hivyo basi Magoela hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kufanya kazi hiyo kama alivyosisitizwa. Roho ngumu ikamwingia Magoela akaona pesa za kutosha na Mr Aloyce Ndosi na familia yake ndio kila kitu kwake. Akamtazama Mr Aloyce Ndosi kisha akamwambia
“Mzee hakuna siri itakayovuja”
Kauli hiyo ikaibua tabasamu mororo katika mashavu yaliyofunikwa na ndevu, Mr Aloyce Ndosi akamkumbatia kijana wake kisha akamwambia
“Kuhusu pesa usiwe na shaka, kazi zetu hutengeneza pesa nyingi. Nakuahidi ndani ya muda mfupi utakua kijana tajiri katika nchi hii na hakuna atakaye kutilia mashaka kwa sababu atakaye thubutu atalichungulia kaburi”
Akameza mate fundo moja kisha akavuta pumzi ndefu ndani akairuhusu itoke nje kwa nguvu, akaendelea na maneno yake.
“Fanya uwezalo kazi ianze mara moja”
Waliongea mengi sana na kukubaliana lazima kazi ya kumfatilia Colotilda na Mr Hamisi Ernest ianze siku inayofuata.
YUPO WAPI GOD MOTHER?
NAFIKIRI TUSUBIRI KITABU SASA. SITAPOST TENA RIWAYA HII KATIKA UKURASA HUU.
KAMA UNAHITAJI KITABU TUMA JINA NA NAMBA YAKO KWENYE NAMBA 0758 195 890 ILI NAKALA YAKO IANDALIWE.
LEO NAFUNGUA GROUP LA WHATSAPP TUTAKALOKUWA TUNAPEANA MREJESHO KUHUSU RIWAYA HII, LINI KITABU KITATOKA NA NSHU ZINGINE ZINAZOHUSU KAZI HII.
ASANTE.
Asante
Sawa ndugu lkn wengine huwa ni wapenzi wa soft copy hasa kwa issue ya ubebaji na utunzaji waandishi wenzio huwa wanautaratibu wakuuza hata softcopy. Shida ya nakala ngumu ni pale mtu anapoazima haitarudi kama ulivyompatia. Wengine tunàhifadhi katika electronic library hivyo unapaswa na sisi kutufikiria. Ndiyo maana hata amazon huwa tunanunua sana vitabuTusubiri kitabu ndg
Ndg nitafute kwa namba 0758 195 890 tuongee, tutaelewana tuSawa ndugu lkn wengine huwa ni wapenzi wa soft copy hasa kwa issue ya ubebaji na utunzaji waandishi wenzio huwa wanautaratibu wakuuza hata softcopy. Shida ya nakala ngumu ni pale mtu anapoazima haitarudi kama ulivyompatia. Wengine tunàhifadhi katika electronic library hivyo unapaswa na sisi kutufikiria. Ndiyo maana hata amazon huwa tunanunua sana vitabu
Asante sana kwa ushauri, nafikiri hii itaisha. Lakini yakupasa kukumbuka utunzi wa story ndio kazi niliyochagua, so niki'offer story yote nitakosa hata pesa ya bundle ya ku'post story zingine, ndio maana natoa kitabu nikihitaji support yenu.Mkuu wenzako asilimia kubwa wanao leta story zao wanazimaliza kabisa, ila umekuwa mtu kuzikatisha story zako mapema, watakuja wengine kuzisoma ila nakushauri inabidi uimalize hata stori yako moja mkuu.
Wenzako huwa wana sacrifice hata story moja kwanza, watu wanaona potential yako kwenye utunzi, hivi vitu huwa ni automatically motivatedAsante sana kwa ushauri, nafikiri hii itaisha. Lakini yakupasa kukumbuka utunzi wa story ndio kazi niliyochagua, so niki'offer story yote nitakosa hata pesa ya bundle ya ku'post story zingine, ndio maana natoa kitabu nikihitaji support yenu.