RIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri
SEHEMU: 20
ILIPOISHIA
King akawatazama wanafunzi wake waliokua makini wakimsikiliza pasipo hata kupepesa umakini wao kisha akawaambia
“Ninyi nyote mpo vizuri, mmekidhi vigezo vya kuwa Afisa Usalama, naamini mtavumilia mafunzo na kila kitu ili muweze kuhitimu kada hii”
Akauliza swali
“Mpo tayari kulitetea na kulilinda taifa teule la Tanzania dhidi ya mienendo mibaya?”
ENDELEA
Wanafunzi wote wakajibu
“Ndio, TISS”
King akaendelea kwa kusema
“Mnajua vyanzo watumiavyo Maafisa Usalama kupata taarifa wazitakazo?”
Wanafunzi wote wakatazamana kitu kilichoashiria hakuna aliyekuwa na jibu sahihi la swali hilo. King alielewa nini kinachoendelea, akawaambia.
“Kuna vyanzo vingi vya habari ambavyo hutumiwa na mashushu kujipatia habari muhimu, baadhi ya vyanzo au njia hizo nia “Open sources” kwa kifupi huitwa OSINT yaani vyanzo vya wazi kama vile mikataba, intaneti, magazeti, vitabu na vipeperushi. Kifungu namba 20 cha sheria zinazoongoza idara ya Usalama wa Taifa, Tanzania humlinda au hulinda chanzo cha habari. Njia nyingine ni mawasiliano ambayo kitaalamu huiita “Communication Intelligence”, kwa kifupi hufahamika kama COMMINT, njia hii mashushushu hunasa mawasiliano ya watu kama vile simu, barua pepe, fax na kadhalika. Njia nyingine inayoendana na njia hiyo ni “Eavesdropping” inayohusu kusikiliza maongezi fulani ya watu pasipo wao kujua. Njia nyingine ni “Wire tapping”, hujumuisha pia kunasa mawimbi ya sauti, kitu kinachojulikana kama “Signal Intelligence” kwa kifupi hujulikana kama SIGINT. Njia nyingine ni kunasa mawasiliano Kieletroniki, kwa kifupi hufahamika kama ELINT. Njia nyingine ni kunasa picha au taswira ya mtu au kitu, njia hii mara nyingi hufanywa na ndege au Drones, njia hii hufahamika kama IMINT yaani “Imagery Intelligence”. Njia nyingine hufahamika kama “Financial Intelligence” kwa kifupi FININT. Njia nyingine ni “Incorrect Supposition”, njia hii inahusu kumwambia mtu taarifa za uongo ili akurupuke kuongea ukweli mfano mtu anaambiwa nasikia wewe huna chochote, pesa ya kula tu una omba omba ovyo. Taarifa kama hiyo humfanya mtu kuanza kuongea ukweli kuwa ana nini na nini hivyo basi hawezi kuomba omba ovyo. Lakini njia inayopendelewa zaidi kuliko zote ni matumizi ya binadamu inayofahamika kama “Human Intelligence” kwa kifupi HUMINT, kwa sababu hata kama mtatumia teknolojia lakini bado binadamu atahusika kuongoza teknolojia hiyo. Ndio maana leo mpo hapa, kwa kiasi kikubwa tunahitaji binadamu wa kutekeleza shughuli za Usalama wa Taifa.”
King akaweka nukta. Muda wote alikuwa amesimama kama nguzo ya umeme, hakuonesha dalili yoyote ya kuchoka au kutamani kukaa. Akapiga hatua moja mbele walipo wanafunzi wake kisha akawauliza
“Mnayafahamu mataifa ambayo yapo mstari wa mbele katika idara hii ya Usalama wa Taifa? Namaanisha mataifa yenye nguvu katika idara hii!”
Mago akanyoosha mkono, King akamtazama kama mtu asiyemuangalia, alikua anafahamu uwezo wa Mago darasani lakini aliamini mambo ya idara hiyo lazima yatakuwa mageni sana katika akili ya kijana huyo. Akamwambia
“Nakusikiliza Magoela”
Mago akasimama kisha akajibu
“Baadhi ya mataifa hayo ni Marekani, Uingereza na Ufaransa”
King alitabasamu kidogo, jino lake la dhahabu likaonesha utofauti uliopo na meno mengine. Akamwambia Mago
“Hauko mbali na uhalisia”
Umati wa vijana wengine akiwemo Colotilda ulikuwa kimya ukisubiri maelezo ya kina kuhusu mataifa hayo. King akaanza kuwafundisha taratibu
“Nchi karibu zote zina idara maalumu inayosimamia Usalama wa Taifa, unapoona nchi ina amani na utulivu jua kuwa watu hawalali ndio maana amani na utulivu huo ukapatikana. Mojawapo ya watu hao ni idara yetu.”
Akameza mate fundo moja, akapiga chafya kisha akaendelea
“Zifuatazo ni idara kumi imara za Usalama wa Taifa duniani, watoto wa mjini mnaita “Top ten”. Namba kumi ni idara ya Australia inayoitwa “Australia Secret Intelligence Service” au ASIS. Idara hiyo iliundwa tarehe 13/05/1952 na makao makuu yapo katika mji wa Canberra. Kiongozi wa idara hiyo anaitwa Paul Symon. Namba tisa ni idara ya Ufaransa inayoitwa “General Directorate for External Security” au DGSE. Idara hiyo iliundwa tarehe 02/04/1982 na makao makuu yapo 141 Boulevavard Mortier jijini Paris. Kiongozi wa idara hiyo anaitwa Bernard Emie. Namba nane ni idara ya Ujerumani inayoitwa “Bundesnachrichtendienst” au BND. Idara hiyo iliundwa tarehe 01/04/1956 na makao makuu yapo katika jiji la Berlin. Kiongozi wa idara hiyo ni Meja Jenerali Werner Sczesny. Namba saba ni idara ya India inayoitwa “Research and Analysis Wing” au RAW iliundwa na R.N Kao na Indira Gandhi, tarehe 21/09/1968. Makao makuu ya idara hiyo yapo CGO Complex, jijini New Delhi. Kiongozi wa idara hiyo anaitwa Samant Goel. Namba sita ni idara ya China inayofahamika kwa jina la “Ministry of State Security” au MSS iliyoanzishwa Julai, 1983. Makao makuu ya idara hii ni jijini Beijing na inaongozwa na Chen wenqing. Namba tano ni idara ya Urusi inayoitwa “Main Intelligence Agency” au GRU, iliundwa tarehe 07/05/1992. Makao makuu yapo Grizodubovoy, jijini Moscow. Kiongozi wa idara hiyo anaitwa Igor Kostyukov. Namba nne ni idara ya Uingereza inayofahamika kama “Main Intelligence, Section 6” au MI6, iliundwa Julay 1909 na makao makuu yake yapo SIS building, jijini London. Kiongozi wa idara ya Uingereza anaitwa Alex Younger. Namba tatu ni idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani inayoitwa “Central Intelligence Agency” au CIA, iliyoundwa na Harry S. Truman tarehe 18/09/1947 miaka miwili baada ya vita ya pili ya Dunia. Makao makuu yapo Virginia, idara hii inaongozwa na Gina Haspel na Vaughn Bishop. Namba mbili ni idara ya Israel inayoitwa
“HaMossad leModi in ule – Tafkidim Meyuhadim” au MOSSAD inayo maanisha “Institute for Intelligence and Special Operations”, iliyoundwa na waziri mkuu David Ben – Gurion tarehe 13/12/1949. Makuu makuu yapo Tel Aviv, idara hiyo inaongozwa na Yossi Cohen. Idara inayoaminika inashika namba moja kiutendaji ni idara ya Pakistan inayoitwa “Inter Service Intelligence” au ISI iliyoundwa na Robert Cawthome tarehe 01/01/1948 baada ya vita ya Pakistan na India ya mwaka 1947 mpaka 1948. Makao makuu yapo jijini Islamabad".
King akajinyoosha kwa mara ya pili kisha akawaambia wanafunzi wake
“Kuna mambo mengi yasiyoeleweka yanayotishia amani na utulivu ndani ya nchi yetu ya Tanzania, na ninyi ndio watu pekee mnaotegemewa kuja kupambana na waovu wote. Kufa au kupona mpaka nchi iwe safi”.
Akavuta pumzi ndani kisha akaendelea
“Mliandaliwa kuja kuwa Maafisa usalama tangu mtipokua watoto wadogo, mpo mnao fahamiana lakini wengi wenu hamfahamiani hata kidogo lakini jambo la msingi mnalotakiwa kujua, ninyi nyote ni Watanzania”
Baada ya kuongea maneno hayo King aliondoka eneo lile bila kuoga, wanafunzi wakamsubiria lakini hawakuona hata dalili ya King kurudi eneo lile. Saa moja likapita, wanafunzi wakaamua kurudi vyumbani kwao kwa ajili ya kupumzika. Hazikupita hata dakika kumi wanafunzi wote wakatolewa vyumbani kwao kwa kichura chura mpaka eneo waliokuwepo awali, jambo hilo lilifanywa na wanajeshi wasiopungua tisa. Walipofika eneo la mazoezi, mwanajeshi mmoja mwenye kovu kubwa kwenye shavu lake la kushoto akafoka kwa hasira
“Msilete tabia za kijinga ndani ya jumba hili, hutakiwi kufanya lolote pasipo kuambiwa na anayewaongoza”
Wanafunzi wale walishangazwa sana na suala lile la kushurutishwa kama watoto wadogo, vile vile hawakujua wale wanajeshi walitokea wapi kwa sababu hawakuwahi kuwaona awali. Walipigishwa pushapu “push up” na kichura chura kwa kipindi cha saa moja na nusu, wanafunzi wote walikuwa hoi bini taabani. Wanajeshi wale walivyoona hali ya wanafunzi wale wakaondoka eneo lile pasipo kuwapa taarifa yoyote. Colotilda, Magoela na wanafunzi wengine waliwasubiri wanajeshi wale lakini hakuna aliyerudi, wakajifikiria labda utakuwa ni mtego mwingine. Wanafunzi wote wakakubaliana kutokuondoka eneo lile mpaka watakapopewa ruhusa na kiongozi. Sasa waliona ni mateso na sio mafunzo, wapo waliowaza kutoroka mafunzo, hakika ulikuwa ni utoto kwa sababu hawakujua ugumu wa kutoka ndani ya jumba hilo lenye ulinzi wa kila namna. Colotilda alimsisitiza Mago lazima wafuate maneno waliyoambiwa na Mr Hamisi Ernest kuwa uvumilivu unatakiwa katika kila hatua ya mafunzo yao.
### ### ###
Masaa, siku, miezi na miaka ilisogea ndani ya jumba la mafunzo. Hakika vijana waliiva ipasavyo, waliweza kutumia silaha za moto za aina nyingi, walikuwa vizuri kwa mapigano ya bila kutumia silaha (anarmed combat), walikuwa vizuri katika usomaji wa ramani za vijiji, miji na maeneo ya kivita. Ville vile walizimudu vyema njia maalumu za kutafuta taarifa za kiusalama za ndani na nje ya nchi. Walifunzwa uzalendo, kufa kwa ajili ya Taifa. Walipewa msemo wa kizalendo, msemo ulioonesha umuhimu wa Taifa, msemo uliosema.
“Tanzania kwanza, raia kwanza, roho yangu baadae”
Walikuwa tayari kupambana na Maafisa usalama toka mataifa mengine kwa lengo la kudumisha amani ya Tanzania. Colotilda alikuwa vizuri sana katika mapigano ya bila silaha, siku zote alifanikiwa kumpiga mpingani wake aliyepangwa nae kwenye mazoezi, alikuwa mwepesi sana kitu kilichowashangaza na kuwafurahisha walimu na hata wanafunzi wenzake. Magoela alikuwa mzuri sana katika kulenga shabaha, haikuwa rahisi kukosa kitu alicholenga. Alikuwa mdunguaji (sniper) mzuri . Kila silaha aliweza kuitumia ipasavyo, hakuna kilichombabaisha. Walimu wao akiwemo King walifurahishwa na muungano wa Colotilda na Mago kwa sababu walikuwa watu wawili tofauti ambao wakiwa pamoja wanakamilisha matumizi ya silaha na mapigano ya ana kwa ana.
Mafunzo yalipokamilika vijana wote walirudishwa Tanzania kwa siri kubwa, ilikuwa siri ya idara ya Usalama wa Taifa. Ulikuwa umefika wakati wao wa kutimiza kila kitu walichofundishwa. Colotilda na Magoela walikutanishwa na Mr Hamisi Ernest na Mr Aloyce Ndosi mkoani Kigoma. Hapo ndipo ushushushu ulipoanza rasmi. Siku tatu baada ya kuwasili kwa vijana hao, idara ya Usalama wa Taifa ilipata pigo kubwa na kupelekea hali kutokuw shwari hata kidogo. Ulikutwa mwili wa mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa wa mkoa wa Kigoma Mr Paul Paulo alimaarufu kwa jina moja la Kaginga ukining`inia kwenye kamba ya katani chumbani kwake, hakuacha ujumbe wowote wa kuashiria nini chanzo cha kifo chake. Katika mfuko wa kulia wa suruali ya marehemu huyo kilikutwa kitambaa kama kile ambacho hutumiwa na majambazi na kuambatanisha maandishi ya damu mbichi yanayosomeka “Very sorry marehemu”, lakini kitambaa hicho hakikua na maandishi ya aina yoyote.
Mzozo ukaibuka na idara ya Usalama wa Taifa ikagawanyika. Wapo Maafisa Usalama walioamini Mr Paulo Siafu aliuliwa na majambazi wanaotafutwa kila siku alafu akawekewa kitambaa hicho bila maandishi yoyote kwa lengo la kuwahadaa wapelelezi na Maafisa Usalama wenzake, lakini kundi lingine lilimuhusisha mkuu huyo na majambazi hao. Kundi hilo liliamini kiongozi huyo alikuwa akishirikiana na majambazi hao na walikuwa mbioni kufanya mauaji mengine lakini kabla ya kutimiza mauaji hayo wakageukana, ndio maana akauliwa na kitambaa kilichoandaliwa kwa mauaji kikabaki kwenye mfuko wake. Mwisho wa siku hakuna upande ulioonekana kuwa sahihi na hapo ndipo ugumu wa kutafuta ukweli ulipoanzia. Mr Hamisi Ernest na Mr Aloyce Ndosi hawakuonekana kuunga mkono upande wowote lakini vichwa vyao vilikua vikiwaka moto na kufikiria mambo mengi zaidi. Baada ya uchunguzi wa madaktari ilibainika kuwa Mr Paulo Siafu alipigwa sana masaa machache kabla ya kifo chake, hivyo basi waliomuua waliamua kumning`iniza kwenye kamba ili isadikike kuwa kiongozi huyo alijinyonga mwenyewe.
Madaktari walisema pia, mwili wa Mr Paul Siafu haukukutwa na alama zozote za vidole (finger print) kitu kilichomaanisha kuwa wauaji walivaa soksi mikononi ili kuzuia alama za mikono yao kubakia kwenye mwili wa Mr Paulo Siafu . Hakika walizamilia kumuua kinyama. Mwili wa Mr Paulo Siafu ulizikwa siku ya tatu baada ya kifo chake huku upelelezi wa polisi ukiendelea kimya kimya. Idara ya Usalama wa Taifa ilimteua Mr Hamisi Ernest kufatilia kwa kina ili kuwabaini wahalifu wote, aliipokea kazi hiyo kwa mikono na kuihakikishia idara kuwa lazima awapate wahusika.
Mr Hamis Ernest aliamua kumuita Colotilda nyumbani kwake ili amshirikishe jambo hilo, Colotlda alipofika kila kitu kilienda sawa kwa sababu mke wa Mr Hamisi Ernest hakuwepo. Maongezi yakaanza
“Ulikuwa unamfahamu Mr Paulo Siafu kabda ya kifo chake?”
Lilikua swali la kwanza la Mr Hamisi Ernest kwa Colotilda. Pasipo kuchelewa wala kukupesa maneno, Colotilda alijibu kwa kujiamni
“Hapana mkuu, sikuwahi kumfahamu. Sura yake nimeiona siku ya kuuaga mwili wake”
Mr Hamisi akamshika mkono Colotilda kisha akamwambia
“Kifo cha Mr Paul Siafu kinaleta maswali na mashaka sana, Mr Paul Siafu hakutakiwa kufa kipindi hiki tena namna ile”
Akameza mate kisha akaendelea
“Mr Paul Siafu alikua akiandaliwa kuwa mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa ngazi ya kanda ya Magharibi, lakini alipewa sharti moja tu ambalo kama angefanikiwa kulitimiza kwa wakati kusingekuwa na kipingamizi chochote”
Swali likaibuka kwenye akili ya Colotilda, akauliza
“Sharti gani hilo na unahisi kwanini Mr Paul Siafu aliuliwa?”
Mr Hamisi Ernest akatabasamu kama mtu aliyefurahishwa na swali hilo kisha akajibu taratibu kwa sauti ya chini
“Ofisi ya Rais ilimpa kazi Mr Paul Siafu kuchunguza na kubaini wahalifu wanaofanya mauaji na kuacha kitambaa chenye maandishi yanayosomeka ‘very sorry marehemu’. Alipewa muda wa miaka mitatu, miaka hiyo imeisha na inasemekana Mr Paul Siafu ameshakamilisha kazi hiyo na ameshaandaa ripoti maalumu ya kuwasilisha ofisi ya Rais”
ITAENDELEA
MLIONIAMBIA MNAHITAJI KITABU HIKI NITUMIENI NAMBA ZENU INBOX AU KWENYE NAMBA 0758 195 890. AU COMMENT NAMBA YAKO HAPA HAPA TUTENGENEZE GROUP LETU LA WHATSAPP LA KUPEANA MREJESHO WA KITABU CHETU.
KAMA KUNA MTU MPYA ANAYEHITAJI KITABU CHA AFISA USALAMA, ASISITE, ATUME JINA NA NAMBA YAKE.
ASANTE.