Wakuu zangu,
Nilitaka sana kuandika makala yangu inayohusu NIDHAMU YA WOGA lakini kwa muda mrefu sana nilikuwa nimetingwa na mitikasi ya Bongo ambako ni pori la mwenye meno ndio hula nyama..Hata hivyo hii hoja ya ndugu yetu ni nzito sana na haitakiwi kuchukuliwa mzaha hata kidogo pamoja na kwamba haina mantiki...Kama alivyokubali yeye mwenyewe hapo juu.
Nadhani mwandishi kufikia kusema hivi katazama WATU na MAZINGIRA tulitopo na pengine kufikiria kwamba tatizo la Chadema ni Dr.Slaa badala ya kutazama chanzo cha mzizi huu wa fitna umetokana na nini na una malengo gani?..
Mimi nimetoka Bongo juzi tu na hakika swala la Dr.Slaa limewafunga akili kabisa waislaam wengi kwa tuhuma ambazo zimepandwa makusudi kumwengua Dr.Slaa kati ya Watanzania wazalendo wenye kutaka kulitumikia taifa bali kulitumikia kanisa. Mbegu za chuki na fitna zimeisha pandwa na sii rahisi kabisa kuziondoa fikra hizi kwa Wadanganyika ambao kwa miaka yote tumekuwa nyuma kufikiria nje ya kabati kwani makuzi yetu wengi yametokana na tamaduni za kikabila na kidini.. Kifupi, hii ndio identity ya kila Mtanzania na kinachotuunganisha sisi ni imani tu ya kufikirika kwamba sisi sote ni ndugu..
Mimi nilikuwa mmoja kati ya watu kwa kwanza kufikiria kwamba Dr.Slaa ni mtu pekee anayeweza kumshinda Kikwete mbali na Dr Salim A Salim kwa sababu nchi yetu bado kabisa inaongozwa na dhana ya MTU na sii CHAMA anayeweza kuongoza nchi hii vizuri, hivyo mapenzi ya mtu huyo yanatokana na kuaminiwa kwa mtu huyo ktk jamii mbali mbali kama ni Mwenzetu..na hakika Dr.Slaa amethibitisha imani yangu kwa kuweka ushindani mkubwa sana ambao CCM hata siku moja hawakutegemea...Kifupi, I was right on the that!
Sasa tunapozungumzia MWENZETU hapo ndipo utata mkubwa unapojitokeza kwa viongozi wengi kwani ni utamaduni, mila na desturi ya Mtanzania kutegemea mafanikio na neema pindi mtu au ndugu yake anapofanikiwa au kushika madaraka..ukweli huu haukwepeki na sote ktk makundi yetu tumejipanga kujijenga toka familia tegemezi hadi Taifa tegemezi..In Reality sisi ni WATEGEMEZI ambao kiimani tunaamini tukiwezeshwa tutaweza!... Mmmhhh - TUKIWEZESHWA!
Kilio cha Waislaam na Dr.Slaa kipo wazi kabisa.. na itakuwa ujinga sana kufikiria kwamba Waislaam watampokea Dr.Slaa kwa mikono miwili pasipo kuhofia dini yake hasa anapotambulika kama ni Padre ambaye tayari inamweka ktk kundi fulani... hivyo kifikra kuzua tumaini kwa wenzake na kupoteza imani ya Waislaam kwani wao watamwona sii mwenzao.. Ukweli huu haukwepeki hata kidogo na Waislaam wataendelea kumhofia Dr.Slaa kwani ndio msingi wa maisha mapya ya Mtanzania toka tumeingia ktk Ubepari na kubomoa misingi ya Ujamaa na Kujitegemea..
Ujamaa na Kujitegemea kama Ideology ilikuwa na mazuri yake hasa ktk upande wa siasa na Uongozi ingawa ulipwaya sana kiuchumi. Binafsi nilitegema sana kwamba ktk transition ya kutoka ktk siasa za Ujamaa na Kuitegemea tungefikiria mazuri yake kisiasa na kuyatumia ktk mfumo mpya wa Kibepari badala yake tulichukua yote ya Kibepari na kubwaga mazuri ya Ujamaa ambayo yalijengwa kwa lengo la kuondoa tofauti hizi za kimakundi iwe ya koo, makabila, dini na hata rangi za wananchi wake...
Sasa kwa mwenye kufikiria juu juu hataona umuhimu wa kuondoa tofauti hizi kwani uzawa wa mtu yeyote hauwezi kupotea ndani ya mfumo wowote wa kisiasa na Afrika kwa ujumla bado tupo miaka 200 nyuma ya mataifa yaliyoendelea hivyo kifikra bado kabisa tumegawanyika ktk makabila na dini na kikomo cha kufikiria kwetu kitaihia ktk mazingira haya kwani ndio tunayoyaona.
Leo hii siwezi kukubaliana na sheria au siasa zozote zinazonikataza mimi kujitambulisha kama Mkerewe na Muislaam kwa sababu ndio ID yangu pekee iliyobakia ktk uzalendo wa Mtanzania. Ubepari umeondoa kabisa lengo la kuundwa taifa hili na kupoteza kabisa ya Mtanzania, kiasi kwamba Wazanzibar kwa mara ya kwanza wanajisikia wao ni tofauti na Wabara, Waunguja tofauti na Wapemba, hivyo hivyo na tofauti za utengano zipo ktk makabila yao na kadhalika kama ilivyo bara na mikoa yake..
Utengano huu unaendelea hadi ktk dini zetu, Muislaam kujiona ni ndugu na Muislaam mwenzake japokuwa wote ni waislaam wa kuzaliwa kiimani. Mkristu, Budha, Baniani vile vile atajiona tofauti na mtu mwenye imani tofauti na yake...Na utengano huu unazidi kujitikita hadi ktk rangi zetu na matokeo yake ni fursa ya Ubepari kuweza kushika hatamu kama msingi wa Maisha na maendeleo ya binadamu ktk makundi. yake na kwa bahati mbaya sisi bado hatujajenga kundi moja la Utaifa linalotakiwa ndani ya Ubepari ili ushamiri.
Ubepari siku zote kazi yake kubwa ni kutenganisha jamii ktk makundi ili iweze kutawalika na kwa bahati nzuri wenzetu Ulaya walikwisha vunja Makabila yao, walikwisha jitambulisha ndani ya imani moja ya dini na wapo ktk hatua za mwisho kuvunja matatizo ya rangi, na wanajitambulisha Kitaifa zaidi ya makundi ya kikabila au dini, hivyo Ubepari na dhana ya - Kila mmoja wetu atakula kwa jasho lake, inamweka kila raia kuwajibika kwa malengo ya kuboresha maisha yake ndani ya Taifa moja lisilo na kabla, dini au rangi..Kwa mtaji wetu sisi tunaelekea kujenga Nigeria ya kesho, nchi yenye kujigawa makundi makundi ndani na hatari kwa usalama wa Taifa zima..
Tanzania tuna tatizo kubwa sana la kutii sheria, tuna kiburi na tunajifanya tunajua sana pasipo kuelewa athari ya kuiga vitu vya wazungu ili mradi tu nasi tufanane nao..Tumeuvamia Ubepari kisiasa pasipo kuelewa kwamba Tanzania ilikuwa ktk harakati za kuondoa Ukabila, Udini na tofauti za rangi kiasi kwamba tumeunda taifa moja la Watanzania..Katiba ilijieleza wazi kwamba nchi yetu haina dini isipokuwa watu wake ndio wana dini kwa maana njema kabisa ya kwamba nchi itaheshimu imani za watu wake na kuwapa fusra ya kufanya ibada zao maadam imani hizo haziwalazimishi wananchi wote kutii au kufuata ibada hizo..
Lakini badalk yake imeingia imani ya kwamba serikali lazima iwe na sheria moja kwa watu wote na inashadadiwa na wasomi wakubwa wa sheria na Utawala ambao wameshindwa kuelewa kwamba unaporuhusu wananchi kufanya ibada za dini zao huwezi kuweka sheria moja kwa watu hao ndani ya ibada hizo hizo unazowaruhusu kuzifanya, kiasi kwamba leo Mkristu anafikiria umuhimu wa Mahakama ya Kadhi kwa Waislaam hali yeye sii Muislaam..Na hapo kuifanya serikali iwe na dini maadam haikubali ibada ya dini moja ina maana inakubali imani nyingine pinzani na Uislaam...
Kwa hiyo ndugu zangu nimeandika mengi sana na bado kichwa kimejaa mavituz toka Bongo, labda nimalizie tu kwa kusema kwamba Dr.Slaa ataweza tu kukubalika ktk jamii ya Waislaam ikiwa yeye atawahakikishia kwamba yupo nao na Chadema itawakilisha mawazo yao ktk fursa zao za kuabudu na serikali yake haitawakwaza kufanya ibada zao kama wanavyoagizwa na dini yao, isipokuwa tu pale ibada hizo zitavunja haki za waumini wake..
Dr.Slaa must come clean juu ya msimamo wake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi, OIC, Mkataba wa MoU na maswala ya ruzuku, misamaha ya kodi na kadhalika..Haya yote yanatakiwa utafiiti ufanyike na kuelewa kwa undani ukweli unaohusiana na vitu hivi pamoja na kwamba mimi binafsi ningependa kujua ni fursa gani Waislaam wamepewa kuwezeshwa toka kuundwa kwa Bakwata. Je, Bakwata hupewa kiasi gani cha fedha toka serikalini ikiwa kweli Nyerere ndiye aliyekiunda chombo hiki.
Siku zote nawasikia wanaharakati wa Kiisilaam wakilalamika juu ya Wakristu na kanisa Katoliki lakini sijamsikia Mufti au kiongozi wa Bakwata akilaani vitendo vya JK na serikali ya CCM kuwapa Kanisa billioni 60 hali Bakwata imepokea kiasi kadhaa au hawakupewa kabisa na kwani nini kumekuwepo na tofauti hizi. Nimechoka kusikia kilio cha wanaharakati wa kiislaam wakati Mufti na viongozi wetu Masheikh wanazungumzia vitu hivi misikitini, navichochoroni badala ya kutoka hadharani kujisafisha wao wenyewe jinsi gani wanatumia mali za Waislaam na Bakwata kama chombo cha Waislaam wamepewa ruzuku na misaada gani na serikali zote zilizopita..
CCM na viongozi wake wanatafuta mchawi na kwa bahati mbaya Dr.Slaa ni kizee ambaye sii wa kabila wala dini ya kundi kubwa la Waislaam ambao wanafahamu fika kwamba maendeleo ya kundi lao yataletwa na Muislaam mwenzano ingawa sii kweli lakini wanasema ni bora Zimwi likujualo kuliko...Cha kuchehesha ni kwamba hata Wakristu na watu wa imani tofauti wote kwa pamoja wanafikiri hivyo hivyo!
Hapo ndipo tulipofikia..