Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

it was not a good idea kumsimamisha kugombea urais slaa?? ni watu wachache sana Tanzania hii unaweza kuwauliza swali kama hilo
wakakujibu YES. Binafisi ninasema kusimashwa kwa slaa it was the BEST IDEA EVER toka kuanzishwa kwa chama hiki na sababu ni hizi hapa
1.kutoka kura 700,000 za urais mpaka kura 2.5 million that is a success.
2.kutoka wabunge watano mpaka wabunge 47 that is a success.
3.kwa upande wa madiwani sina hakika na idadi labda wachambuzi wengine wanaweza kunisaidia ktk hili lakini i beleive wanaweza kuwa wameongezeka mara kumi ya kuliko waliokuwa nao hapo awali.
4. halmashauri kutoka moja mpaka halmashauri kumi nchi nzima that is a BIG success.
5.wanachama kutoka mamia mpaka milioni plus.
6. ruzuku kutoka milioni 40 mpaka milioni 200 kwa mwezi that is called success. ili uweze kujiimarisha.

bado tu unafikiria kuwa kumsimamisha slaa was a mistake ingawaje ktk maelezo yako umeibuwa issue ya dini lakini umeshindwa kutoa
hoja za kusupport point yako kama kawaida yenu empty skeleton we used to call them.
Baada ya uchakachuaji ndio CDM wakapata kura chache otherwise nchi ingekuwa chini yao.
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

Ndiyo maana huko shule kuna division one mpaka ZERO. Ukweli ni kuwa hatujui ulipata DIVISION GANI! Mawazo yako hayaonyeshi kama uliwahi kufauru shule maana ni kiwango cha kawaida tu cha binadamu siyo ya MUELEWA! hongera.
 
Mkuu Waberoya,

Siasa si mchezo wa kuigiza kwamba kwa kuwa CCM wameyafanya waliyoyafanya katika kile walichokiita kujisafisha basi na CDM nao wawaige ili nao wajisafishe. CDM ni kweli nako kuna matatizo lakini kwa maoni yangu matatizo yaliyomo ndani ya CDM kamwe hatuwezi kuyalinganisha na yale yaliyomo CCM na hata Baba wa Taifa alianza kuyaona siku nyingi sana wakati wa uhai wake. CDM nao ikifika wakati wa kujisafisha basi watafanya hivyo kwa muda wao.
 
Baadaye tuandike CUF nayo imwondoe Prof Lipumba na Maalim ili ipate uungwaji mkono na Wakristo? Tusikae kufikiri kama wanavyofikiri wenye uwezo mdogo wa kuelewa na kuchanganua mambo. Tuwasaidie bila kuchoka waelewe. Ni bahati mbaya tu kwamba hili la UDINI wa Dr Slaa kalikuza makusudi JK baada ya "kushindwa" uchaguzi mwaka jana.
 
WABEROYA,nafikiri bdo upo pree form one ukifika kidato cha 4 and progressvely utaelewa umuhim wa chadema.toa hoja zinazofafanua hoja ya udini na ukabila.acha kupotosha watanzania unatakiwa kuwaelimisha kuhusu uraia na haki zao.ccm haitakusaidia kwa lolote
 
Mwalimu,
Udini utaondoka tu ikiwa serikali na vyama vya kisiasa vitakemea vitendo vya viongozi wa dini kuchochea vitu hivi.
Wakizungumza Maaskofu wakemewe hata kama wanachozungumza kina malengo mazuri kitaifa kwa sababu walengwa wa hoja zao ni kundi moja la waumini wa dini zao, vile vile Masheikh kwani Tanzania ina dini zaidi ya Uislaam na Ukristu mbona hatusikii viongozi wengine wakizungumza..
Tujiulize wanaponya hivyo hivyo huwa wanategemea kina nani kuwasikiliza kama ni Watanzania wote iweje wao wakemee Ufisadi hali ulikuwepo toka Azimio la Zanzibar na wasikemee mfumo dume wa kiutawala kuwa ndilo chimbuko la maasi yote.

Mimi nadhani ipo haja kubwa ya kurudisha miiko na maadili ya viongozi, pili kuendeleza mazuri ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo yalilenga kujenga jamii moja ya WATANZANIA, hizi habari za viongozi wa dini kuachiwa kutamba na kuwaelekeza waumini wao chaguo la mtawala ni kuvunja haki waliyopewa kwani sii ibada ya dini bali wanaingia ktk siasa za nchi.

Wazo zuri...

Lakini pia tuna jukumu kubwa kuwaelimisha na kuwafungua macho watanzania kuhusu kuchagua viongozi bora bila kuangalia kabila, dini, rangi yake n.k.... Tuache WOGA wa kuchagua mtu simply because watu fulani watamkataa sababu ya dini yake.

Leo hii tunazungumzia waislamu kumkataa Slaa kutokana na ukatoliki wake lakini tunasahau ipo siku wakristo nao wataamka na kutamka wazi kumkataa kiongozi muislamu sababu ya dini yake!!

Pamoja na propaganda ambazo zinapigwa huku na huko dhidi ya maaskofu lakini i can asure you bado wakristo hawajafikia huko!! Ila kwa uchokozi huu unavyoendelea its just a matter of time.....
 
Mwalimu,
Udini utaondoka tu ikiwa serikali na vyama vya kisiasa vitakemea vitendo vya viongozi wa dini kuchochea vitu hivi.
Wakizungumza Maaskofu wakemewe hata kama wanachozungumza kina malengo mazuri kitaifa kwa sababu walengwa wa hoja zao ni kundi moja la waumini wa dini zao, vile vile Masheikh kwani Tanzania ina dini zaidi ya Uislaam na Ukristu mbona hatusikii viongozi wengine wakizungumza isipokuwa hawa hawa..

Tujiulize wanaponya hivyo hivyo huwa wanategemea kina nani kuwasikiliza kama ni Watanzania wote iweje wao wakemee Ufisadi leo hali ulikuwepo toka Azimio la Zanzibar na wasikemee mfumo dume wa kiutawala kuwa ndilo chimbuko la maasi yote. Maneno yoote haya yamekuja baada ya makanisa kurudishiwa nguvu kubwa ya kuhudumia Taifa ktk elimu na Afya.. kurudhishwa kwa shule na makanisa inaweza kuwa ndio chanzo cha Uadui na Nyerere alitaifisha vitu hivi kuwa vya Kitaifa hakuwa mjinga kutaka kuondoa Udini nchini.

Mimi nadhani ipo haja kubwa ya kurudisha miiko na maadili ya viongozi, pili kuendeleza mazuri ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo yalilenga kujenga jamii moja ya WATANZANIA, hizi habari za viongozi wa dini kuachiwa kutamba na kuwaelekeza waumini wao chaguo la mtawala ni kuvunja haki waliyopewa kwani sii ibada ya dini bali wanaingia ktk siasa za nchi.

Mzee Mkandala, Udini hakuna Tanzania. Udini upo kwa watawala na umeasisiwa rasmi baada ya DR. Slaa kugombea URAIS. asingegombea basi haya yote yasingekuwapo.

Hizi move zote unazoziona eti za kujivua magamba or whatever they call it ndiyo results za matokeo ya uchaguzi kwa mwaka jana.

Nani anajua siri ya matokeo halisi? acheni kudanganyika, watu wana njaa, maisha magumu nani anataka udini hapa? Upandeni kwa bidii zote ila nasema siku ukitokea kweli sidhani mtu atakula pilau nyumbani kwake.
 
WATANZANIA.tuwe makini sana na watu wanaotueleza kuhusu siasa za tanzania.kwa wale waliobahatika kupata elimu think logically,hawa ambao wanamtuumu chadema kuwa ina udini na ukabila,let us think about ccm the top layer ina waislam wangapi je twaweza kusemaje.msilopoke kwasababu aliyeazisha ni mkubwa kwenu huo ni woga na ni kosa kubwa sana kwa muumba.chadema ni mkombozi na unapoendelea kuiponda kwa dakika moja inapata wanachama 50.
 
Mwalimu,
Nidhamu ya woga huanza kwa muathirika kama maradhi..Leo hii watu wanakwenda Loliondo kwa sababu ndiko kwenye tumaini lao la ponya na hatukatazwi kusisitiza watu wakatibiwe Hospital lakini itakuwa fujo kubwa kama ukiwakemea wale wote wanaokwenda Loliondo na kuwaita wajinga na matusi kibao.. haiendi hivyo, maadam wao wamekwisha amini kwamba ndiko tiba yao inakopatikana.

Mimi sina tatizo na Maaskofu wanapotoa hoja zao lakini kumbuka tu uchochezi wowote hutokana na kiongozi wa kundi moja kutotambua kitu fulani na mategemeo yake ni waumini wake wamfuate..
Maaskofu na awanja wa siasa sio mahala pao na hakika kama wao wanaitakia kheri nchi hii waulize kama wapo tayari kurudisha mashule na vituo vya Afya kwa Umma...Nguvu ya sauti zao imekuja baada ya kuwezeshwa na wana hakika kabisa pasipo wao nchi haitawaliki, haikuwa hivyo wakati wa Mwalimu...
 
Wakuu zangu,

Nilitaka sana kuandika makala yangu inayohusu NIDHAMU YA WOGA lakini kwa muda mrefu sana nilikuwa nimetingwa na mitikasi ya Bongo ambako ni pori la mwenye meno ndio hula nyama..Hata hivyo hii hoja ya ndugu yetu ni nzito sana na haitakiwi kuchukuliwa mzaha hata kidogo pamoja na kwamba haina mantiki...Kama alivyokubali yeye mwenyewe hapo juu.

Nadhani mwandishi kufikia kusema hivi katazama WATU na MAZINGIRA tulitopo na pengine kufikiria kwamba tatizo la Chadema ni Dr.Slaa badala ya kutazama chanzo cha mzizi huu wa fitna umetokana na nini na una malengo gani?..

Mimi nimetoka Bongo juzi tu na hakika swala la Dr.Slaa limewafunga akili kabisa waislaam wengi kwa tuhuma ambazo zimepandwa makusudi kumwengua Dr.Slaa kati ya Watanzania wazalendo wenye kutaka kulitumikia taifa bali kulitumikia kanisa. Mbegu za chuki na fitna zimeisha pandwa na sii rahisi kabisa kuziondoa fikra hizi kwa Wadanganyika ambao kwa miaka yote tumekuwa nyuma kufikiria nje ya kabati kwani makuzi yetu wengi yametokana na tamaduni za kikabila na kidini.. Kifupi, hii ndio identity ya kila Mtanzania na kinachotuunganisha sisi ni imani tu ya kufikirika kwamba sisi sote ni ndugu..

Mimi nilikuwa mmoja kati ya watu kwa kwanza kufikiria kwamba Dr.Slaa ni mtu pekee anayeweza kumshinda Kikwete mbali na Dr Salim A Salim kwa sababu nchi yetu bado kabisa inaongozwa na dhana ya MTU na sii CHAMA anayeweza kuongoza nchi hii vizuri, hivyo mapenzi ya mtu huyo yanatokana na kuaminiwa kwa mtu huyo ktk jamii mbali mbali kama ni Mwenzetu..na hakika Dr.Slaa amethibitisha imani yangu kwa kuweka ushindani mkubwa sana ambao CCM hata siku moja hawakutegemea...Kifupi, I was right on the that!

Sasa tunapozungumzia MWENZETU hapo ndipo utata mkubwa unapojitokeza kwa viongozi wengi kwani ni utamaduni, mila na desturi ya Mtanzania kutegemea mafanikio na neema pindi mtu au ndugu yake anapofanikiwa au kushika madaraka..ukweli huu haukwepeki na sote ktk makundi yetu tumejipanga kujijenga toka familia tegemezi hadi Taifa tegemezi..In Reality sisi ni WATEGEMEZI ambao kiimani tunaamini tukiwezeshwa tutaweza!... Mmmhhh - TUKIWEZESHWA!

Kilio cha Waislaam na Dr.Slaa kipo wazi kabisa.. na itakuwa ujinga sana kufikiria kwamba Waislaam watampokea Dr.Slaa kwa mikono miwili pasipo kuhofia dini yake hasa anapotambulika kama ni Padre ambaye tayari inamweka ktk kundi fulani... hivyo kifikra kuzua tumaini kwa wenzake na kupoteza imani ya Waislaam kwani wao watamwona sii mwenzao.. Ukweli huu haukwepeki hata kidogo na Waislaam wataendelea kumhofia Dr.Slaa kwani ndio msingi wa maisha mapya ya Mtanzania toka tumeingia ktk Ubepari na kubomoa misingi ya Ujamaa na Kujitegemea..

Ujamaa na Kujitegemea kama Ideology ilikuwa na mazuri yake hasa ktk upande wa siasa na Uongozi ingawa ulipwaya sana kiuchumi. Binafsi nilitegema sana kwamba ktk transition ya kutoka ktk siasa za Ujamaa na Kuitegemea tungefikiria mazuri yake kisiasa na kuyatumia ktk mfumo mpya wa Kibepari badala yake tulichukua yote ya Kibepari na kubwaga mazuri ya Ujamaa ambayo yalijengwa kwa lengo la kuondoa tofauti hizi za kimakundi iwe ya koo, makabila, dini na hata rangi za wananchi wake...

Sasa kwa mwenye kufikiria juu juu hataona umuhimu wa kuondoa tofauti hizi kwani uzawa wa mtu yeyote hauwezi kupotea ndani ya mfumo wowote wa kisiasa na Afrika kwa ujumla bado tupo miaka 200 nyuma ya mataifa yaliyoendelea hivyo kifikra bado kabisa tumegawanyika ktk makabila na dini na kikomo cha kufikiria kwetu kitaihia ktk mazingira haya kwani ndio tunayoyaona.

Leo hii siwezi kukubaliana na sheria au siasa zozote zinazonikataza mimi kujitambulisha kama Mkerewe na Muislaam kwa sababu ndio ID yangu pekee iliyobakia ktk uzalendo wa Mtanzania. Ubepari umeondoa kabisa lengo la kuundwa taifa hili na kupoteza kabisa ya Mtanzania, kiasi kwamba Wazanzibar kwa mara ya kwanza wanajisikia wao ni tofauti na Wabara, Waunguja tofauti na Wapemba, hivyo hivyo na tofauti za utengano zipo ktk makabila yao na kadhalika kama ilivyo bara na mikoa yake..

Utengano huu unaendelea hadi ktk dini zetu, Muislaam kujiona ni ndugu na Muislaam mwenzake japokuwa wote ni waislaam wa kuzaliwa kiimani. Mkristu, Budha, Baniani vile vile atajiona tofauti na mtu mwenye imani tofauti na yake...Na utengano huu unazidi kujitikita hadi ktk rangi zetu na matokeo yake ni fursa ya Ubepari kuweza kushika hatamu kama msingi wa Maisha na maendeleo ya binadamu ktk makundi. yake na kwa bahati mbaya sisi bado hatujajenga kundi moja la Utaifa linalotakiwa ndani ya Ubepari ili ushamiri.

Ubepari siku zote kazi yake kubwa ni kutenganisha jamii ktk makundi ili iweze kutawalika na kwa bahati nzuri wenzetu Ulaya walikwisha vunja Makabila yao, walikwisha jitambulisha ndani ya imani moja ya dini na wapo ktk hatua za mwisho kuvunja matatizo ya rangi, na wanajitambulisha Kitaifa zaidi ya makundi ya kikabila au dini, hivyo Ubepari na dhana ya - Kila mmoja wetu atakula kwa jasho lake, inamweka kila raia kuwajibika kwa malengo ya kuboresha maisha yake ndani ya Taifa moja lisilo na kabla, dini au rangi..Kwa mtaji wetu sisi tunaelekea kujenga Nigeria ya kesho, nchi yenye kujigawa makundi makundi ndani na hatari kwa usalama wa Taifa zima..

Tanzania tuna tatizo kubwa sana la kutii sheria, tuna kiburi na tunajifanya tunajua sana pasipo kuelewa athari ya kuiga vitu vya wazungu ili mradi tu nasi tufanane nao..Tumeuvamia Ubepari kisiasa pasipo kuelewa kwamba Tanzania ilikuwa ktk harakati za kuondoa Ukabila, Udini na tofauti za rangi kiasi kwamba tumeunda taifa moja la Watanzania..Katiba ilijieleza wazi kwamba nchi yetu haina dini isipokuwa watu wake ndio wana dini kwa maana njema kabisa ya kwamba nchi itaheshimu imani za watu wake na kuwapa fusra ya kufanya ibada zao maadam imani hizo haziwalazimishi wananchi wote kutii au kufuata ibada hizo..

Lakini badalk yake imeingia imani ya kwamba serikali lazima iwe na sheria moja kwa watu wote na inashadadiwa na wasomi wakubwa wa sheria na Utawala ambao wameshindwa kuelewa kwamba unaporuhusu wananchi kufanya ibada za dini zao huwezi kuweka sheria moja kwa watu hao ndani ya ibada hizo hizo unazowaruhusu kuzifanya, kiasi kwamba leo Mkristu anafikiria umuhimu wa Mahakama ya Kadhi kwa Waislaam hali yeye sii Muislaam..Na hapo kuifanya serikali iwe na dini maadam haikubali ibada ya dini moja ina maana inakubali imani nyingine pinzani na Uislaam...

Kwa hiyo ndugu zangu nimeandika mengi sana na bado kichwa kimejaa mavituz toka Bongo, labda nimalizie tu kwa kusema kwamba Dr.Slaa ataweza tu kukubalika ktk jamii ya Waislaam ikiwa yeye atawahakikishia kwamba yupo nao na Chadema itawakilisha mawazo yao ktk fursa zao za kuabudu na serikali yake haitawakwaza kufanya ibada zao kama wanavyoagizwa na dini yao, isipokuwa tu pale ibada hizo zitavunja haki za waumini wake..

Dr.Slaa must come clean juu ya msimamo wake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi, OIC, Mkataba wa MoU na maswala ya ruzuku, misamaha ya kodi na kadhalika..Haya yote yanatakiwa utafiiti ufanyike na kuelewa kwa undani ukweli unaohusiana na vitu hivi pamoja na kwamba mimi binafsi ningependa kujua ni fursa gani Waislaam wamepewa kuwezeshwa toka kuundwa kwa Bakwata. Je, Bakwata hupewa kiasi gani cha fedha toka serikalini ikiwa kweli Nyerere ndiye aliyekiunda chombo hiki.

Siku zote nawasikia wanaharakati wa Kiisilaam wakilalamika juu ya Wakristu na kanisa Katoliki lakini sijamsikia Mufti au kiongozi wa Bakwata akilaani vitendo vya JK na serikali ya CCM kuwapa Kanisa billioni 60 hali Bakwata imepokea kiasi kadhaa au hawakupewa kabisa na kwani nini kumekuwepo na tofauti hizi. Nimechoka kusikia kilio cha wanaharakati wa kiislaam wakati Mufti na viongozi wetu Masheikh wanazungumzia vitu hivi misikitini, navichochoroni badala ya kutoka hadharani kujisafisha wao wenyewe jinsi gani wanatumia mali za Waislaam na Bakwata kama chombo cha Waislaam wamepewa ruzuku na misaada gani na serikali zote zilizopita..

CCM na viongozi wake wanatafuta mchawi na kwa bahati mbaya Dr.Slaa ni kizee ambaye sii wa kabila wala dini ya kundi kubwa la Waislaam ambao wanafahamu fika kwamba maendeleo ya kundi lao yataletwa na Muislaam mwenzano ingawa sii kweli lakini wanasema ni bora Zimwi likujualo kuliko...Cha kuchehesha ni kwamba hata Wakristu na watu wa imani tofauti wote kwa pamoja wanafikiri hivyo hivyo!

Hapo ndipo tulipofikia..

Mkandara I salute you!

Asante sana for this notable contribution
 
Mzee Mkandala, Udini hakuna Tanzania. Udini upo kwa watawala na umeasisiwa rasmi baada ya DR. Slaa kugombea URAIS. asingegombea basi haya yote yasingekuwapo.

Hizi move zote unazoziona eti za kujivua magamba or whatever they call it ndiyo results za matokeo ya uchaguzi kwa mwaka jana.

Nani anajua siri ya matokeo halisi? acheni kudanganyika, watu wana njaa, maisha magumu nani anataka udini hapa? Upandeni kwa bidii zote ila nasema siku ukitokea kweli sidhani mtu atakula pilau nyumbani kwake.
Mkuu heshima kwako,
Umesema hakuna Udini.. sawa tuseme nakukubaliana nawe, ila naomba wewe na wote mnaokataa Udini kuwepo nchini nambieni maoni yenu kuhusu Mahakama ya Kadhi, OIC, Mkataba wa MoU, JK na chaguzi za viongozi wake, Mufti na Pengo kuzungumzia Siasa zaidi jambo ambalo hawakulifanya ktk tawala zilizopita.. haya yote wewe unayatazama vipi na nini maoni yako..
 
Siamini mtu anaweza kufikiria kwa jinsi yako (Webs)..Ok nikijaribu kutumia logic yako ni kwamba CUF nao wakitaka kujivua gamba la Uislamu wawafukuze wanachama wake woote wa Zanzibar (kwa maana karibu wote ni waislamu) ..? Yaani Chadema wamtose Dr.Slaa kwasababu ya imani yake (Ukristo)? kwanini isiwe Mbowe (ambae ni mwenyekiti na mgombea urais 2005)? mmmh napata maswali zaidi badala ya majibu...!
 
WABEROYA,nafikiri bdo upo pree form one ukifika kidato cha 4 and progressvely utaelewa umuhim wa chadema.toa hoja zinazofafanua hoja ya udini na ukabila.acha kupotosha watanzania unatakiwa kuwaelimisha kuhusu uraia na haki zao.ccm haitakusaidia kwa lolote

Waberoya ni mwerevu, ameleta mada kwa makusudi ili aone sisi tuna msimamo gani kuhusu CHADEMA na udini, watawala na udini na dhana nzima ya udini katika nchi yetu, na hapa anasoma maoni yote kwa makini kisha atapata anachokitaka.

Mimi bado msimamo wangu ni ule ule, hakuna udini wala ukabila ila kuna watu wachache tu wanajikomba kwa watawala kuuhubiri huu udini mbaya zaidi rais naye anaubariki - ref: kikao cha kwanza bungeni

Amini amini nawaambia endeleeni kuuhubiri na kuubariki lakini siku misikiti na makanisa yakianza kuchomwa moto sijui nani na familia yake atabakia salama.

Leo hii Dr. Slaa akienda Tekeme na vitongoji vyake (Ambapo kuna waislamu wengi may be) watu watajitokeza kwa hiari yao kumsikiliza tena kwa shangwe na nderemo sasa hapo anakuwa kaenda kuhubiri dini? na kama ni dini kwa nini watu wanamfuata? wake kwa waume, waislamu na wakristo? jiulize mara mbili.

Naomba mtu anifafanulie zaidi huu udini upo wapi hasa? mimi nazunguka kote mitaani - mabibo, tandare, mbagala, manzese, kigamboni, sijawahi kusikia watu 10 wamekusanyika barabarani wanaongelea udini wa CHADEMA na Ukiristo wa J.K ila nasikia kwa watawala tu.

Sisi tuna shida zetu za msingi msitupotoshe na udini wenu. Mimi hata aje Rais IMAM au MCHNGAJI lakini kama ana busara na nauhakika atanivusha nakotaka nifike LAZIMA NIMCHAGUE awe Rais wangu sababu sichagui dini au rangi au kabila ya mtu.
 
kwa mtu kama wabe hana budi kwenda kwa babu,ogopa sana kitu kiitwacho vita ya udini hapa duniani utaona ni bora hata taabu ya libya.kwamsomi vita ya udini ni balaa.watanzania tuwe na critical thinking kama hujui maana yake mtafute msomi wa mtaani kwako akwambie kwani tanzania by now kila mtaa una msomi ila si kama wabe.
 
Mwalimu,
Udini utaondoka tu ikiwa serikali na vyama vya kisiasa vitakemea vitendo vya viongozi wa dini kuchochea vitu hivi.
Wakizungumza Maaskofu wakemewe hata kama wanachozungumza kina malengo mazuri kitaifa kwa sababu walengwa wa hoja zao ni kundi moja la waumini wa dini zao, vile vile Masheikh kwani Tanzania ina dini zaidi ya Uislaam na Ukristu mbona hatusikii viongozi wengine wakizungumza..
Tujiulize wanaponya hivyo hivyo huwa wanategemea kina nani kuwasikiliza kama ni Watanzania wote iweje wao wakemee Ufisadi hali ulikuwepo toka Azimio la Zanzibar na wasikemee mfumo dume wa kiutawala kuwa ndilo chimbuko la maasi yote.

Mimi nadhani ipo haja kubwa ya kurudisha miiko na maadili ya viongozi, pili kuendeleza mazuri ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo yalilenga kujenga jamii moja ya WATANZANIA, hizi habari za viongozi wa dini kuachiwa kutamba na kuwaelekeza waumini wao chaguo la mtawala ni kuvunja haki waliyopewa kwani sii ibada ya dini bali wanaingia ktk siasa za nchi.

Bob heshima mbele,

Wakati mwingine nashindwa kuielewa narrative yako kuhusu swala zima la udini. Hivi wewe unaona ni sawa kama maaskofu na hao mapdre wangekaa kimya simply because ufisadi ulikuwepo tangia zamani? To me I would be the most happiest Tanzanian ningeona hata Mufti mkuu anaita vyombo vya habari ku-condemn huu ufisadi uliokithiri wa akina EPA, RICHMOND NK!! Mkuu I hope this is not what you meant. Two wrong do not make it right. Reality check is, JK aliomba kura awe raisi wa watanzania na atuondolee kero za umasikini na magonjwa. Sasa hiyo narrative kwamba ufisadi ulikuwepo kwa hiyo JK ndo anaonewa naona haina mashiko. This is Kikwete`s responsibility. Otherwise hana haja ya kuwa Raisi! Kumu-excuse JK ni kutaka kuhalalisha maovu tuu na uzembe wa kushindwa kuwachukulia hatua akina Lowassa na Rostam.. Maovu ni maovu tuu, haijalishi nani kayafanya. Kama alivyosema muungwana mmoja, hili swala la udini limeibuka kama kiini macho cha kuficha uzembe na weakness za uongozi uliopo madarakani.

Bob, hivi unaamini kwamba CCM wakimsimamisha mgombea mkristo come 2015, malalamiko tunayoyaona na kuyasikia leo kuhusu CDM yatakuwepo? Unafikiri ukaribu tunaouona kati ya Mashekhe na serikali ya CCM utakuwepo? History is the best teacher. What happened to CUF as Chama cha Wanyonge??? I can bet my watch!

Kwamba waislamu na wasio waislamu tuna shida sawa..alishaimba Bob Marley........When rain falls, it doesnt fall on one man`s roof!

Kwangu mimi hata serikali yote ingejaa waislamu..as long wana deliver, wanaleta umeme na huduma muhimu na kujenga fursa za kuwafanya watanzania wajikomboe kiuchumi. I have no problem at all! Appoint all Muslim Ministers, if that is what it will take for our country to move foward! I will support that with all my heart!
 
a piece of treasure thoughts
 
Yaani mtu aliyewafanya wakubalike zaidi na kupata kura zaidi na kuwa chama cha kitaifa zaidi ndio aondolewe? Well.. itakuwa ni kufanya mambo kinyume nyume. Wenzenu wameondoa watu waliokiletea chama matatizo siyo waliokijenga. Sasa pendekezo kuwa Dr. Slaa aondoke kwa sababu ni tatizo - ni gumu kuliwekea msingi kwa sababu itabidi uangalie namba na kulinganisha namba uweze kusema kuwa Dr. Slaa ni tatizo.

Kama Chadema inataka ife kwa haraka na ikose hata nafasi ya pili 2015 basi ifanye hili unalopendekeza. Ukiniuliza mimi Dr. Slaa anahitaji kuwa mwenyekiti kabisa wa Chadema tena mtendaji. Na I have to admit it kwa sababu nilimuunga mkono na ninaamini kabisa kuwa Tanzania inahitaji mtu kama yeye kulipeleka taifa kunakotakiwa.
Hata upupu huu wa Mwanakijiji pia unapata watu wa kutoa shukrani!.Poleni nyote mfuatao
Capitol Hill (Yesterday), Chimunguru (Yesterday), Dingswayo (Yesterday), Field Marshall ES (Yesterday), Interested Observer (Yesterday), Iza (Yesterday), msaragambo (Yesterday), Mwalimu (Yesterday), Mwasi (Yesterday), Mwita Maranya (Yesterday), Ng'wanangwa (Yesterday), Nguruvi3 (Yesterday), niweze (Yesterday), Shalom (Yesterday), The Finest (Yesterday), Vumbi (Yesterday

Muanzisha mada ametoa ushauri wa bure pamoja na kwamba ni mtu muoga na Ndumilakuwili.Anayepuuza ushauri wake kama yule aliyesema "NILIFIKIRI WATANZANIA,KUMBE WAISLAMU....".hajui siasa wala kusoma alama za nyakati.
Ushauri huu mbovu wa Mwanakijiji haunishangazi kwani ni yeye huyu aliyewahi kusema UHUSIANO WA CCM NA WAISLAMU UMEANZA LINI?.sijui Mwanakijiji amezaliwa na kusoma wapi?
Baada ya yote hayo na mimi natoa mchango wa bure.CHADEMA kwa 2015 si chama na kikiendelea kuwa chama hakina mgombea wa uraisi.
 
Mkandara,
Mbona Mwinyi, Mkapa, JK hawakuulizwa msimamo wao juu ya OIC, MoU ya ruzuku, fursa za kuabudu, Mahakama ya kadhi, wakati wanagombea mwaka 1985, 1995, 2005. Hili linamfaa zaidi Dr Slaa kwa kuwa aliwahi kuwa Padri?
 
Bob heshima mbele,

Wakati mwingine nashindwa kuielewa narrative yako kuhusu swala zima la udini. Hivi wewe unaona ni sawa kama maaskofu na hao mapdre wangekaa kimya simply because ufisadi ulikuwepo tangia zamani? To me I would be the most happiest Tanzanian ningeona hata Mufti mkuu anaita vyombo vya habari ku-condemn huu ufisadi uliokithiri wa akina EPA, RICHMOND NK!! Mkuu I hope this is not what you meant. Two wrong do not make it right. Reality check is, JK aliomba kura awe raisi wa watanzania na atuondolee kero za umasikini na magonjwa. Sasa hiyo narrative kwamba ufisadi ulikuwepo kwa hiyo JK ndo anaonewa naona haina mashiko. This is Kikwete`s responsibility. Otherwise hana haja ya kuwa Raisi! Kumu-excuse JK ni kutaka kuhalalisha maovu tuu na uzembe wa kushindwa kuwachukulia hatua akina Lowassa na Rostam.. Maovu ni maovu tuu, haijalishi nani kayafanya. Kama alivyosema muungwana mmoja, hili swala la udini limeibuka kama kiini macho cha kuficha uzembe na weakness za uongozi uliopo madarakani.

Bob, hivi unaamini kwamba CCM wakimsimamisha mgombea mkristo come 2015, malalamiko tunayoyaona na kuyasikia leo kuhusu CDM yatakuwepo? Unafikiri ukaribu tunaouona kati ya Mashekhe na serikali ya CCM utakuwepo? History is the best teacher. What happened to CUF as Chama cha Wanyonge??? I can bet my watch!

Kwamba waislamu na wasio waislamu tuna shida sawa..alishaimba Bob Marley........When rain falls, it doesnt fall on one man`s roof!

Kwangu mimi hata serikali yote ingejaa waislamu..as long wana deliver, wanaleta umeme na huduma muhimu na kujenga fursa za kuwafanya watanzania wajikomboe kiuchumi. I have no problem at all! Appoint all Muslim Ministers, if that is what it will take for our country to move foward! I will support that with all my heart!
Mkuu wangu bado hujanisoma na hutanielewa mimi nasema nini na hao viongozi wa dini wanasema nini..
Labda niwe wazi kwanza na mimi mwenyewe.

Mimi naamini kabisa kwamba matatizo ya Tanzania yametokana na mfumo mbaya wa kiutawala na sii swala la JK au Mkapa..Serikali, Mahakama na Bunge vitu vyote hivi vinapwaya sana ktk kuongoza nchi bali vipo ktk kujijengea mazingira ya rushwa na Ubinafsi pasipo kujali Katiba wala maadili ya uongozi bora.

Kama kuna sababu ya kukemea Ufisadi nchini inatakiwa sisi sote tupinge au tupige vita tabia yetu sote Watanzania ya Ukabila na Udini. Sasa maadam tayari tumekwisha jitambulisha ktk mafungu ya Udini na Ukabila, lolote utakalosema dhidi ya kabila au dini nyingine tayari ndio Udini unapoingia.

Two wrong can't make it right - Yes, nakubaliana nawe kwa sana tu, lakini ni wangapi kati yao wanaoamini we were wrong then wakati wa Mkapa?.. Hakuna kiongozi wa Kanisa anayekubali wala Kukemea Utawala wa Mkapa kwamba he was wrong ila mimi na wewe..Na kwa mfumo ule ule alouacha Mkapa wa Kifisadi wanamtazama JK na interest zake ambazo kiukweli Waislaam wanaona nafuu kwao pamoja na kwamba hafanyi makubwa..Cha kukemea ni mfumo mzima na sii mtu ila kama kuna Udini au unataka kujenga Udini..

Hii ndio reality ya tanzania leo na sii somo wala elimu inayotakiwa kutambua kwamba Udini nchini umefikia kiwango ambacho watu hawatazami tena mfumo wa kiutawala bali interest zao ktk makundi waliyopo. Marekani wanakemea sana kuhusu Libya while they Know Yemen, Bahrain na Misri kuna tatizo hilo sawa na Libya isipokuwa hawachukui nguvu zaidi ktk nchi hizo kutokana na interest zao..Marekani walijua miaka mingi iliyopita kuwa Mubarak ni tajiri kuliko Bill Gates na wanajua matajiri wengine wa nchi za Kiarabu lakini kwa kulinda interest zao hawazungumzii kabisa..Hivyo it doen't make it right eitherway iwe ya kwanza, ya pili, tatu au nne..

Sasa ni vigumu kusema sababu za Marekani na UN kujikita Libya wakiachia Yemen na Bahrain watu wakiuawa tena basi wamefikia hadi kuwapa silaha mwana mageuzi wa Libya ili kupambana na Ghadafi.. No flyzone wanaruka wao na kuangusha mabomu?...Sasa Waulize wao watakwambia two wrong can't make it right kwa Gadhafi kuwaua raia wake..sasa napopiga vita mtazamo kama huu usifikirie kwamba namuunga mkono Ghadafi isipokuwa nazungumzia Unafiki wa Marekani kama navyozungumzia Unafiki wa Mahseikh na Maaskofu..

Mwisho wa siku itakula kwetu, kama inavyokula kwa Walibya wenyewe.
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

Webby bana......naona umekuja kivingine aisee,................notwithstanding hoja yako nzuri.....kwamba tatizo lipo...na inabidi lishughulikiwe......Je Dr W. Slaa ni Tatizo kweli?......au ni matatizo ya UELEWA?........ well, kisiasa technically itakuwa ni suicidal move kwa CDM kufanya mabadiliko kama unavyopendekeza............kwa maoni yangu watakuwa wanalikuza tatizo si ndani ya CDM pekee bali hata kwenye vyama vingine......i'm asking you to "just imagine"..........then what........I'm afraid to say propaganda za Majambazi CCM zimefani kiwa somehow..............
 
Back
Top Bottom