Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Unaweza kuthibitisha waislamu hawakitaki CDM? Unajua waislamu ni kina nani? hivi unadhani hizi kilele zinazopigwa na waislamu wachache walioshibishwa na CCM ndio msimamo wa waislamu wote TZ? hivi waislamu wanapigiwa kura na viongozi wao au kila mmoja anapiga peke yake? acha kutoa mawazo ya waislamu kwa kusiliza vyombo vya habari, wewe unadhani tumesahau CCM ilivyo iua CUF?. Una maana waislamu tunapangiwa tujiunge chama gani na viongozi wetu?. Umeniudhi sana na hii post yako hapo chini, kama hujui uislamu tafadhali usitake kutujumuisha kwenye maamuzi ya watu binafsi.

Angalieni hoja za wana CDM-JF mpaka wanatia huruma, kichefuchefu tupu

SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
 
Huwezi kuzuia propaganda. Na sidhani kama chadema wanaweza kupoteza muda kujadlili propaganda badala ya kuconcetrate kwenye national issues
 
Ndugu Wabe, Chadema hawajalala wanayafanyia kazi hayo unayosema, kumbuka juzi juzi wamemsajili Prof. Abdalla Safari, huoni hiyo kama hatua in the right direction?
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.
Mkuu wewe umeona mbali sana!! Huyu mtu Slaa inabidi aondoke,, hakuna jinsi, na baadaye Mbowe ili Chama kiwe safi kabisa.
 
Kwakweli cjakuelewa wabe !! Chadema inakua kwa kasi j'mosi wamevuna zaidi ya wanaudom 8000 na hayo ni matunda ya dr slaa..na kama unasubiri cdm ife utangoja utachoka mark my word.

sifikiri kama hizo kwenye bold ndiyo fikra za wabe...

sijaribu kumtetea wala kumsemea bali namna nimemuelewa ni kuwa wakati CDM inaendelea kujitangaza na kuvuna wanachama from other groups za potential voters kuna watu miongoni mwa watanzania...a sizeable portion ya waislamu(voters as well)...very vocal amongst the muslims wanaendesha kampeni za wazi dhidi ya CDM kwa madai hayo aliyoya-observe Wabe...hii ni changamoto kwa CDM walau kwa mtazamo wangu...

swala ni je...CDM wana-adress vipi hiyo situation????

as per Wabe...anaona immediate solution ni kumuweka Dr pembeni....

ikiwa hii observation yangu ni sahihi...basi na tujadili nini CDM wafanye!!!!

ni mtazamo tu na bila shaka kila mtu ana mtazamo wake na ilivyo hii ni nchi huru...basi ruksa...lakini si uungwana ku-attack personality badili ya hoja

pengine nikumbushe tu a similar situation iliibuka back in 1995..waislamu walimpinga waziwazi A. L. Mrema...sina hakika na asilimia ya chakachua ya CCM wakati huo bali naamini ilimkosesha sana kura...

tunaweza walau kwa sasa kuona kuwa Wabe anapotea kifikra lakini wakati hufika katika mchezo wa siasa ambapo kila kura ina sauti...tujifunze kwa uchaguzi wa uingereza mwaka uliyopita..nani alitegemea kuwa Lib Dems leo hii wangekuwa na sauti kuliko Labour????:help:
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

rafiki yangu mbona unapenda sana kuwaita watu wajinga?
 
Hapo kwenye read hapo chini.

Hii hoja yako waislamu hawaipendi CDM umefanya sensa na kuona ni asilimia ngapi haiwaipendi CDM? Je ni waislamu wote wanaipenda CCM? Je ni wakirsto wote wanaipenda CDM? au ni wkristo wote wanaipenda CCM?. Acha kutumia waislamu kwa maslahi yako binafsi au ya kutumwa. Kwani ni lazima waislamu wote wajiunge CDM au CCM au CUF?. kwa mujibu wa rekodi za serikali TZ in 35% waislamu, 30% wakristo na 35% wasio kuwa na dini, hivyo kuna 65% wasio amini katika uislamu hili kundi ni kubwa sana na linaweza kufanya mageuzi makubwa ndani ya nchi. Nikusaidie watu wanaiogopa CDM kutokana na nguvu yake mbele wananchi na mtu aliipa nguvu CDM ni Dr. Slaa tangu akiwa bungeni mchango wake ni mkubwa kuliko unavyo dhania. Dr. slaa anatumiwa na wapinzani wa CDM kama chambo kwa wanachi lakini wamegundua wananchi wamekataa hiyo mbinu, sasa wamehamia njia nyingine ya kusema wanataka kumtoa raisi madarakani mbona wazanzibar wamechoma na kuchana ule uswada wa katiba hiyo sio kumdhalilisha raisi na serikali yake?

Too sad for you my dear! kama ukaribu wangu na Zito ndio unaofanya CDM kichukiwa na unakosa hoja ya kukiokoa kwa sababu ya uhusiano wangu na Zito sawa! umenifanya nicheke, umeenda mbali na hoja, I am not hero, I am not intellectual hayo umenipa wewe na ulinipa wewe!

JIBU HOJA, KATAA kuwa Slaa asiondoke na sema nini wafanye! kwa nini mko kwenye gari mnajua kabisa haliendi popote bali ni kupiga resi tu na makonda kusema linaenda na bado liko stendi?

Huyo Zito wala hafai kuwa katibu mkuu wa chadema, wala sijui na sina ukaribu naye..we are connected with Zitto kwa mawazo yake na itikadi zake na si vinginevyo

Haya waislamu hawakitaki CDM unasema nini?

Conclusion zako kwenye post mbili zimenifanya nikuweke kwenye -ignore list, umeandika kama una uhakika kabisa! my God! namna hiyo unaweza kumgomnaisha mama yako na baba yako, ukimuona mama anaongea na mzee fulani utatoa conclusiona na kumweleza baba! childish, watu wanashindana kwa hoja na si kusingiziana vitu ambavyo personally unajua si kweli na kama unaamini umekosea!

poor MTM!
 
NCCR kilipokuwa tishio kiliundiwa tuhuma. CUF nayo ilipokuwa tishio kwa CCM kilijengewa propoganda chafu na sasa hivi zimeamia Chadema, kwa sababu sio tishio tu kwa CCM na mafisadi vile vile.

Kwa sababu hizo mbinu chafu zimekuwa zikiundwa kwa chama chochote ambacho ni tishio kwa CCM,wakibadilisha kiongozi una uhakika gani hizo mbinu chafu hazita endelea hata kama sio za kidini?

Na kwa sababu hizo propoganda ni za kidini ni kiongozi wa aina gani anaweza kuziondoa?
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
Umezungumza na Waislamu gani na wangapi ambao wamekwambia hawaitaki Chadema mbali na wale waliolipwa au wale wanaofuata mkumbo na kuamini kuwa CDM ni chama cha kidini bila kutafakari? Hivi akitokea mwenda wazimu na kueneza kuwa Chadema ni chama cha wakomunisti utakubali tu na kukitaka Chadema kijisafishe tuhuma za ukomunisti? Nionavyo mimi so far so good, Chadema waendeleze tu mambo yao mwendo mdundo.

Hao wanaokiona ni chama cha udini watafilia mbali kama wale waliokuwa wanakiona kuwa chama cha ukabila, ukanda. Huwezi kujibu shutuma za kila mtu eti Dr Slaa ajiengue sijui ampishe nani atakayeonekana kwa Waislamu kuwa Chadema hakina udini. Ni upuuzi mtupu.
 
waberoya,.Is islamic fundamentalist.
A friend to Zitto who destroyed Zitto's family. by separating zitto &wife.
Now ur ccm go and advice them how to go about their internal fights.
With MWIGULU another makamba in action wabe n u know that from udsm! With January a disaster!
Have u taken ur time 2 think a little bi t! what will happen without a union btn Tanganyika n Zanzibar?
Dr. Slaa has done a lot 2 CDM. Who are u 2 judge him? just a forumnist? or a fundamentalist? 4 2day is enough 4 u on my way 2 dom!
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.
Ama kweli nyani haoni kundule.Unakosoa logic ya uwepo wa Dkt Slaa ilhali umeshindwa kuangalia japo logic ya hoja yako.Anyway,it doesn't even need a one-minute assessment kutambua kuwa tatizo la wengi wanaompinga Dkt Slaa (including you) ni UDINI.Hivi vichwa maji nyie ni lini mtaangalia mtu beyond dhehebu lake?Ni wapuuzi wa aina yenu mnaodhani critcism kwa Kikwete ni kwa sababu ****** huyo ni Muislam.Mnakemea wanaokosoa ufisadi kwa vile Rostam Aziz ni Muislam.Mtafika hatua ya kutetea vibaka,wakwapuaji,wezi,majambazi,mafuska,wabakaji,na all kinds of criminals kwa vile tu ni Waislam.

Tatizo lenu ninyi ndugu zetu (yes,you're still our Tanzanian brothers despite our religious differences) ni kuwekeza nguvu nyingi kwenye mambo ambayo kimsingi hayasaidii utatuzi wa matatizo yenu ya msingi kama vile ELIMU.Mnatumia nguvu nyingi kulalamika badala ya kujibidiisha kujikwamua ktk matope ya kifikra na kiakili mlimozama.

Pilipili usiyokula yakuwashia nini?Kama Dkt Slaa ni choice mbovu hilo ni tatizo la Chadema na halikuhusu.Why Dkt Slaa na sio Lipumba au Seif Sharif,ambao miaka nenda miaka rudi wameeendelea kuwa wasindikizaji tu na sasa wamefunga ndoa ya mkeka na CCM?Huwezi kuwalaumu hao kwa vile ni Waislam.

If ain't broken just don't fix it.Assess magamba ya CCM before jumping into a nonexistent problem.

Takbiiiir!!
 
kama huna cha kufanya wewe lala tu usituletee assumption za kindergaten eti kosa kubwaa kumchagua slaa, mkuu uko possesed na evil spirit wa ccm au?
 
Yaani mtu aliyewafanya wakubalike zaidi na kupata kura zaidi na kuwa chama cha kitaifa zaidi ndio aondolewe? Well.. itakuwa ni kufanya mambo kinyume nyume. Wenzenu wameondoa watu waliokiletea chama matatizo siyo waliokijenga. Sasa pendekezo kuwa Dr. Slaa aondoke kwa sababu ni tatizo - ni gumu kuliwekea msingi kwa sababu itabidi uangalie namba na kulinganisha namba uweze kusema kuwa Dr. Slaa ni tatizo.

Kama Chadema inataka ife kwa haraka na ikose hata nafasi ya pili 2015 basi ifanye hili unalopendekeza. Ukiniuliza mimi Dr. Slaa anahitaji kuwa mwenyekiti kabisa wa Chadema tena mtendaji. Na I have to admit it kwa sababu nilimuunga mkono na ninaamini kabisa kuwa Tanzania inahitaji mtu kama yeye kulipeleka taifa kunakotakiwa.
 
Huu udini umepikwa na fanatics wachache wakishirikiana na mafisadi, Kwa mtazamo wangu Chadema cant do anything whatsoever.Kumbadilisha kiongozi kwa sababu za kidini kama hizi haziwezi kukuondolea tatizo bali ni kuongeza matatizo siku za usoni
 
tatizo la CHADEMA wengi hawana uwezo wa kufikiri kwa kina wengi ni WAUZA DUKA ukijua kujumlisha na kutoa basi inatosha.
kujivua gamba ni kuboresha baada ya kuji assess wenyewe. CCM haijivui gamba eti kisa ni SLAA.wakati kwenye uchaguzi CHADEMA Mmeshindwa vibaya. wanacho taka ccm ni ushindi wa kishindo 90% ambazo zimepunguzwa kutokana na UDINI wa CHADEMA na CUF. mwaka 2015 ndiyo kifo rasmi cha CHADEMA maana ccm ikimsimamisha mkristo (KATOLIKI) MAASKOFU WATAKIUNGA MKONO na kukiacha CHADEMA SOLEMBA na waislamu wengi wanakipenda ccm kwasababu ndiyo waliokiasisi
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
MKUU SIKUTAKA KUCHANGIA TOKA MWANZO ULIPOANDIKA UCHAFU HUU, LAKINI HAPO KWENYE RED NAONA KAMA UMEFINYA FIKRA ZAKO CDM SIO CHAMA CHA WAISLAMU, MBILI NCHI HII HAIONGOZWI NA MASHEHE AU MAASKOFU, KWA HIYO KAMA KUNA DINI INAPINGA UKWELI KWA MASLAHI BINAFSI CDM HAIPO KWA MPANGO HUO NA WALA HATO BEMBELEZWA MTU, NA WAISLAMU NANI KAWAPA MAMLAKA YA KUCHAGUA JINSI GANI SIASA ZA NCHI HII ZIENDESHWE, mimi nina rafiki wengi waislamu na hawana tatizo na dr wa ukweli, mkuu uwezi kuendesha chama au nchi kwa kufurahi kikundi cha watu wenye tamaa mbaya, hao hao kenyo ccm wakiweka MWANDOSYA AU MAGUFULI watarudi kwenye chama chao cha C.. na kuihacha CCM
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawataki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

Natumaini hiki ulichosema hapo juu kimetoka kwenye mwitikio wa kihisia (emotional response) na siyo kutoka katika mwitikio wa kiakili (a rational response) kwani inasema mengi:

a. Umejuaje Waislamu "hawawataki"?
b. Waislamu gani hawawataki?
c. Kwanini ni Waislamu tu hawawataki?
d. Je ndani ya Chadema kuna muislamu yeyote?
e. Kama kuna muislamu japo hata mmoja - inaweza vipi kusemwa kuwa "waislamu hawawataki"?
f. Unafikiri Dr. Slaa akiondoka ndio Waislamu wataitaka hata kama haiwakilishi maslahi yao?

Nadhani ni hoja nyingine ambayo ni extremely prejudicial, biased and inherently offensive. Yaani, kukubalikwa kwa Chadema kunapimwa na kukubakika na Waislamu? Sasa wakimuondoa Dr. Slaa halafu waislamu wakakubali na Wakristu wakianza kukimbia wamuondoe huyo mtu mwingine ili wakubalike na "wakristu". Yaani, hatuna kanuni tena isipokuwa kufanya mambo kwa kujaribu kuridhishana tu?

Kuita majibu ya watu wengine wasiokubaliana nwewe kuwa ni "ujinga" ni kujaribu kulazimisha hoja pale ambao umeshindwa kusimamia hoja yako.
 
tatizo la CHADEMA wengi hawana uwezo wa kufikiri kwa kina wengi ni WAUZA DUKA ukijua kujumlisha na kutoa basi inatosha.
kujivua gamba ni kuboresha baada ya kuji assess wenyewe. CCM haijivui gamba eti kisa ni SLAA.wakati kwenye uchaguzi CHADEMA Mmeshindwa vibaya. wanacho taka ccm ni ushindi wa kishindo 90% ambazo zimepunguzwa kutokana na UDINI wa CHADEMA na CUF. mwaka 2015 ndiyo kifo rasmi cha CHADEMA maana ccm ikimsimamisha mkristo (KATOLIKI) MAASKOFU WATAKIUNGA MKONO na kukiacha CHADEMA SOLEMBA na waislamu wengi wanakipenda ccm kwasababu ndiyo waliokiasisi

umenichekesha sana, umekurupuka usingizini nini ukakuta mada ukaona na wewe uandike?
sasa wewe na hao wa chadema wanaojua kutoa na kujumlisha nani angalau?
Yani hata ccm wenzako wakisoma hii post yako watakushanga, me naona endelea kulala ili ugain weight.
 
Back
Top Bottom