Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Cdm kimekuja juu ghafla kwa nguvu za Slaa, kila mtu nishahidi na mpaka sasa unaona kinavyo jizolea sifa kila kukicha. Sasa Dr. Slaa aachie ngazi kwa sababu tu waislam hawakipendi cdm kwa hiyo aje katibu mwislam ndio waislam wakipende au waweke mkristu tofauti na Slaa au unamaana gani? Slaa hawezi kuachia ngazi na lazima aendelee kuwarambisha mpaka kieleweke. Ngoja ccm wachangue mkristu 2015 tuone kama hao waislam wako wanaipenda ccm au walimpenda mwislam wäo.
 
CCM wana magamba mengi mno ilo ni moja tu, lakini pia nyoka akivua gamba anaendelea kutema sumu kama kawa
 
huyo aliyeileta agenda hii ni mpumbavu tena hana akili, chadema hakuna udini wala ufisadi, ndio maana kura za rais hazikutosha kama ametumwa na ccm amefeli chadema ni chama cha siasa sio taasisi ya dini, kama anataka udini aende kwenye taasisi husika ataukuta tena mwingi.
 
Hili suala la udini lina mshiko sana katika CCM cycles na kuna watu wanalibebea bango sawa sawa. Akiingia kiongozi dhaifu, hawa watu humkaba kiongozi na kuhakikisha kuna watu fulani wananufaika kwa sababu ya dini zao. Ni kama pale walipokuwa wanataka kumuengua Mzee Six waliposema kuwa wanataka Mwanamke! It is like that in CCM. Wakikuchukia wanatoa maelezo ya aina yoyote na religious balancing ni mojawapo ya maelezo yao.

Mkakati wao sasa ni kulihamishia hili suala kila mahala, na ninavyoona wanaanza kufanikiwa kiasi fulani kwani vyama vinaanza kufanya mambo kutafuta uwiano wa kidini hata kama uwiano huo haupo on the ground!

Hivi tunafanya mambo kwa ajili ya kupata uwiano wa kidini au ili kupata maendeleo ya nchi kwa ujumla wake? Ndani ya CCM, hasa ngazi ya kitaifa, hasa utawala huu, uteuzi hajaribu sana kuhakikisha kuwa religious balance imefanyika kwenye ngazi za juu. Hili linakera kwa sababu kwenye ngazi za chini na kati hii ballance haipo!

Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa kuna watu ambao kupanda kwao maofisini kunategemea sana hii karata ya dini. Na hawa watu wanaicheza vizuri sana. Ikiwa hii huu uwiano wa kidini hautokei katika nafasi ambazo ni competitive ila unatokea katika nafasi ambazo zinategemea uteuzi maanake ni kuwa kuna watu dini zao ni qualification kubwa. Kuna watu wana uwezekano mkubwa wa kupanda vyeo au kupandda ngazi kwa sababu watu wa dini yao ni wachache katika ngazi aliyopo. Kwa kuwa kupanda juu kunategemea vile vile dini yako, hawa watu wakifika nafasi za kati hupanda juu haraka sana, kwani kule juu uwiano wa dini ni muhimu.

Hii ni moja ya matatizo tuliyonayo leo. CCM wanajaribu kuliongezea nguvu hili kwa sababu kuna watu wananufaika na hii. Lakini mwishowe ni mbaya kwani wale wanaopanda, zaidi sana kwa ajili ya kupata uwiano wa kidini, wana uwezekano mkubwa wa kuonekana wapo wapo na hivyo tukipima uwezo wao, watu wataanza ku-associate utendaji mbovu na dini.

Ni afadhali dini itoe kiongozi mmoja kwa miaka mia moja lakini awe ni kiongozi wa kuheshimiwa, kuliko kutoa viongozi, ishirini wote wabovu. Lakini msingi wa yote haya ni nini? Ni udhaifu na uwezo mdogo wa jamii tuliomo. Jamii inayoamini kuwa kiongozi akitoka katika kundi lao basi wao ni bora!! Haya mambo nilikuwa nikiyasikia sana wakati nikiwa sekondari huko ............ wengine wakijiona makabila yao kuwa bora kwa sababu yametoa kiongozi fulani na fulani...... Dini hivyo hivyo. Kipindi hicho mtu unadhani huu ni utoto tu ... kumbe hadi juu kabisa mawazo ni yale yale. Wale waliojiona bora sababu watu wa makabila yao au dini zao ni viongozi wanaendelea tu kuwa hivyo hivyo. Ndo maana huu msemo kuwa jamii hupata viongozi inaostahili unabaki kuwa kweli. Viongozi wetu wengi ni wabovu sababu sisi ni wabovu. Tunaamini katika mambo madogo madogo na hatutii fikira jadidi katika tuyafanyao. Viongozi wetu wengi hutumia hizi hizi hisia, fikra na imani potofu katika kujipatia madaraka.

Yaani anayosema muanzisha mada ni kuwa, Slaa anafaa, sifa zote za kuiongoza Chadema anazo, lakini ...... aaaa .... ni Mkatoliki!!! Historia inaonesha kuwa katika jamii zetu dhaifu hizi za kiafrika, mambo hayo yakiendelea sana kuna hatari mbaya zaidi. Hatari niionayo ni ya wakatoliki kuona kuwa wanakuwa "targeted" au "victimizied" kwa sababu ya imani yao! Matokeo yake? Wanaweza waka 'gang' na kupiga kura za chuki. Sidhani kama CCM inaweza kushinda kwa kura za waislam peke yao!!

Ninachosema ni kuwa mada kama hizi, badala ya kutusaidia, zinaturudisha nyuma!! Hazifai!!

Maana
 
Too sad for you my dear! kama ukaribu wangu na Zito ndio unaofanya CDM kichukiwa na unakosa hoja ya kukiokoa kwa sababu ya uhusiano wangu na Zito sawa! umenifanya nicheke, umeenda mbali na hoja, I am not hero, I am not intellectual hayo umenipa wewe na ulinipa wewe!

JIBU HOJA, KATAA kuwa Slaa asiondoke na sema nini wafanye! kwa nini mko kwenye gari mnajua kabisa haliendi popote bali ni kupiga resi tu na makonda kusema linaenda na bado liko stendi?

Huyo Zito wala hafai kuwa katibu mkuu wa chadema, wala sijui na sina ukaribu naye..we are connected with Zitto kwa mawazo yake na itikadi zake na si vinginevyo

Haya waislamu hawakitaki CDM unasema nini?

Conclusion zako kwenye post mbili zimenifanya nikuweke kwenye -ignore list, umeandika kama una uhakika kabisa! my God! namna hiyo unaweza kumgomnaisha mama yako na baba yako, ukimuona mama anaongea na mzee fulani utatoa conclusiona na kumweleza baba! childish, watu wanashindana kwa hoja na si kusingiziana vitu ambavyo personally unajua si kweli na kama unaamini umekosea!

poor MTM!

Wewe binafsi unaamini kwamba waislamu hawaitaki CDM? Ni wazi propaganda ya udini iliyobuniwa na CCM kwa kushirikiana na wapuuzi wanaojiita Usalama wa Taifa, imewaingia vilivyo baadhi ya waislamu wasio na upeo (wewe inaelekea ni mmoja wao). Lakini Watanzania walio wengi, bila kujali dini zao wala kabila, wanaunga mkono mwelekeo wa CDM, na fikra sahihi za viongozi wao, na hasa Dr Slaa. Yeyote aliyefuatilia kampeni za uchaguzi wa Rais mwaka jana, na ambaye alimsikiliza kwa makini Dr Slaa atakubali kwamba ndiye mtu aliyefaa zaidi kushika madaraka ya juu ya nchi kuliko Kikwete wa CCM. Kuna haja ya kuongeza jitihada za kuwaelimisha watanzania ili wajue haki zao na wajibu wao ili wasiendelee kudanganywa na porojo za CCM za 'Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi" huku utajiri wa nchi ukiendelea kuporwa na wahuni wachache na wakati huo huo wenye nchi yao wakiendelea kuwa masikini kwa kasi zaidi.
 
Mkuu wangu bado hujanisoma na hutanielewa mimi nasema nini na hao viongozi wa dini wanasema nini..
Labda niwe wazi kwanza na mimi mwenyewe.

Mimi naamini kabisa kwamba matatizo ya Tanzania yametokana na mfumo mbaya wa kiutawala na sii swala la JK au Mkapa..Serikali, Mahakama na Bunge vitu vyote hivi vinapwaya sana ktk kuongoza nchi bali vipo ktk kujijengea mazingira ya rushwa na Ubinafsi pasipo kujali Katiba wala maadili ya uongozi bora.

Kama kuna sababu ya kukemea Ufisadi nchini inatakiwa sisi sote tupinge au tupige vita tabia yetu sote Watanzania ya Ukabila na Udini. Sasa maadam tayari tumekwisha jitambulisha ktk mafungu ya Udini na Ukabila, lolote utakalosema dhidi ya kabila au dini nyingine tayari ndio Udini unapoingia.

Two wrong can't make it right - Yes, nakubaliana nawe kwa sana tu, lakini ni wangapi kati yao wanaoamini we were wrong then wakati wa Mkapa?.. Hakuna kiongozi wa Kanisa anayekubali wala Kukemea Utawala wa Mkapa kwamba he was wrong ila mimi na wewe..Na kwa mfumo ule ule alouacha Mkapa wa Kifisadi wanamtazama JK na interest zake ambazo kiukweli Waislaam wanaona nafuu kwao pamoja na kwamba hafanyi makubwa..Cha kukemea ni mfumo mzima na sii mtu ila kama kuna Udini au unataka kujenga Udini..

Hii ndio reality ya tanzania leo na sii somo wala elimu inayotakiwa kutambua kwamba Udini nchini umefikia kiwango ambacho watu hawatazami tena mfumo wa kiutawala bali interest zao ktk makundi waliyopo. Marekani wanakemea sana kuhusu Libya while they Know Yemen, Bahrain na Misri kuna tatizo hilo sawa na Libya isipokuwa hawachukui nguvu zaidi ktk nchi hizo kutokana na interest zao..Marekani walijua miaka mingi iliyopita kuwa Mubarak ni tajiri kuliko Bill Gates na wanajua matajiri wengine wa nchi za Kiarabu lakini kwa kulinda interest zao hawazungumzii kabisa..Hivyo it doen't make it right eitherway iwe ya kwanza, ya pili, tatu au nne..

Sasa ni vigumu kusema sababu za Marekani na UN kujikita Libya wakiachia Yemen na Bahrain watu wakiuawa tena basi wamefikia hadi kuwapa silaha mwana mageuzi wa Libya ili kupambana na Ghadafi.. No flyzone wanaruka wao na kuangusha mabomu?...Sasa Waulize wao watakwambia two wrong can't make it right kwa Gadhafi kuwaua raia wake..sasa napopiga vita mtazamo kama huu usifikirie kwamba namuunga mkono Ghadafi isipokuwa nazungumzia Unafiki wa Marekani kama navyozungumzia Unafiki wa Mahseikh na Maaskofu..

Mwisho wa siku itakula kwetu, kama inavyokula kwa Walibya wenyewe.

Bob,

Hii hoja yako ndo mpaka leo wengi inatupa shida. Umeongelea Libya na coincidentally niko naandika paper kuhusu Security Council Resolution No. 1973 ya kuivamia Libya. Your narrative is interesting and warrants a deeper exploration. But should we let the Libyans die, simply because we cant intervene in Bahrain or Syria? should we leave Ivorians to perish because we cant intervene in Somalia? Who should intervene to make intervention legal and legitimate?? who should authorize intervention to make it justifiable in eyes of many? and perhaps important..will Libyans be well off..without Gadhafi? or should the intervening power avoid 'regime change' and leave periah regimes like Gadhafi in power?? tough questions indeed. Mkuu this is another topic worth its own thread. Tuiache.

Bob, contradictions zote ulizoziongelea naziafiki kabisa. Lakini my question is: What is the Solution in this drama? In fact nadhani JK angeichukua hii nafasi kama changamoto na kurekebisha zile kasoro zilizopo. Yes Mkapa alikuwa na makosa na udhaifu wake...so is Mwinyi and Nyerere, lakini should we take the weakness of these people to continue informing our actions and policies in modern day Tanzania? Hapana nadhani sasa umefika tuanze kufikiria majibu. Tatizo lipo. Wote tunakubali. Sasa jawabu ni lipi??

Nakumbuka Mkapa aliwapa Chuo waislamu Morogoro..(how is the university doing?-sijui). To me vitu kama hivi ndo vya msingi na ndo ingebidi wote wenye mapenzi mema na taifa letu tujengee hoja. ...... Kupanua fursa kwa wananchi. Mfano kuliko kulaumu eti serikali inatoa billion 60 kila mwaka kwa taasisi za wakristo..go..deeper and ask yourself....wanapewa hizo hela kwa nini na kwa njia gani? Ask yourself..can we also qualify for the same? Mfano wanapewa pesa za kutoa huduma kama elimu na afya..now can you also do the same and get the same money? Kuna University of Morogoro ya waislamu.....buni ideas za kuanzisha centers of excellence za research muombe pesa serikalini na kwingineko. Mkuu..hii dunia its all about your brain... Ukiwa innovative kuna mengi ya kufanya na pesa itakuja. Sasa kama Saudi Arabia or IOC wanataka kukupa pesa za kuanzisha center ya lugha au Quran.....tell them..we need money for science and training of medical doctors! Ukitaka kuajiri hire the best minds and pay them irrespective wana dini gani. Bob ni initiatives kama hizi zimewasaidia sana taasisi za Kikristo kusonga mbele. They are Creative! Trust me you, kama taasisi za kiislamu zikikaa chini zikasumbua vichwa..watapata pesa nyingi sana mkuu. ni innovative ideas kama hizi zitawafanya watu waache kulalamika. Mimi naamini katika fursa sawa mkuu! Lakini naamini hizi fursa zinatafutwa haziji kama mana toka mbinguni.

Bob, mimi mpaka leo naamini, ukiamua kuplay victim card kwamba unaonewa..utaonewa kweli! Ukishajiwekea kichwani kwamba wewe ni mnyonge utakuwa mnyonge kweli! Na ndilo tatizo kubwa ninaloliona kwa wananchi wenzetu walio wengi. Hivi ni waislamu wangapi wanaokula bata hapa hapa bongo kuliko hata hao maaskofu na mapadre? Ukweli ni kwamba kuna wakristo na waislamu wanakula jasho letu kila siku huku sisi tukirushiwa mifupa tukiachwa kutoana macho wenyewe! Tragic as it may sound. Ulishawahi kurusha mfupa kwenye group ya mbwa?? Yes, thats what these guys are doing with this 'udini' thing!

I am sorry to say, lakini vitu kama udini, they are condemned to make us become poor and poorer and irrelevant kwa sababu hatutakuja tufikie muafaka. Should we really condemn Slaa simply because alishawahi kuwa Padri? Leo mimi Masanja, do I know what the fate has for me in ten to twenty years (God allowing nina uzima?). Ukweli ni kwamba we should learn to look beyond our differences. Ukitaka kumhukumu Ogah kwa sababu ni mrefu, mfupi, Muislam, Mkristo nk. You can if you wish so. But one thing is clear. You wont change anything in that. He is who is. Judge him on his ability to do what you want him to do. Utafanikiwa.

Ain all wa kuonyesha njia ingebidi awe Kikwete na wengineo akina Waberoya na Masanja et al. Yet sisi ndo tunazidi kumwaga hii sumu kwa maslahi yetu. Sad indeed!. Tusipoamka itakula kwetu as you well said above-and I would add: Ile mara ngapi?
 
Mzee Mkandala, Udini hakuna Tanzania. Udini upo kwa watawala na umeasisiwa rasmi baada ya DR. Slaa kugombea URAIS. asingegombea basi haya yote yasingekuwapo.

Hizi move zote unazoziona eti za kujivua magamba or whatever they call it ndiyo results za matokeo ya uchaguzi kwa mwaka jana.

Nani anajua siri ya matokeo halisi? acheni kudanganyika, watu wana njaa, maisha magumu nani anataka udini hapa? Upandeni kwa bidii zote ila nasema siku ukitokea kweli sidhani mtu atakula pilau nyumbani kwake.

ELNINO uko kwenye mstari wangu, jamii ya kitanzania inayoamini udini au kuutukuza udini ni ndogo sana,

dini iko serious kwenye political platform na inasemwa sana huko kana kwamba waislamu woote hawaipendi CDM

Hofu yangu ni kuwa ukisemwa sana utaaminika! CDM wanafanya nini kuondoa hali hiyo?

Kumbukeni nimesema kwenye siasa kuna wakati vitu illogical ndivyo vinaexist! na tunaacha vizuri, Slaa yuko clean lakini backgorund yake inawafanya watu waunde hoja, this is not fair though it is their!

Kukaa kimya au kutosema haya kwa sababu ukisema unaonekana mdini au humpendi Slaa is totally misuse ya ukweli.

Kumbuka political platform ndiyo inasemwa kila siku na kusikika kila siku, moto unaendelea kusambaa.
 
Bob,

Hii hoja yako ndo mpaka leo wengi inatupa shida. Umeongelea Libya na coincidentally niko naandika paper kuhusu Security Council Resolution No. 1973 ya kuivamia Libya. Your narrative is interesting and warrants a deeper exploration. But should we let the Libyans die, simply because we cant intervene in Bahrain or Syria? should we leave Ivorians to perish because we cant intervene in Somalia? Who should intervene to make intervention legal and legitimate?? who should authorize intervention to make it justifiable in eyes of many? and perhaps important..will Libyans be well off..without Gadhafi? or should the intervening power avoid 'regime change' and leave periah regimes like Gadhafi in power?? tough questions indeed. Mkuu this is another topic worth its own thread. Tuiache.

Bob, contradictions zote ulizoziongelea naziafiki kabisa. Lakini my question is: What is the Solution in this drama? In fact nadhani JK angeichukua hii nafasi kama changamoto na kurekebisha zile kasoro zilizopo. Yes Mkapa alikuwa na makosa na udhaifu wake...so is Mwinyi and Nyerere, lakini should we take the weakness of these people to continue informing our actions and policies in modern day Tanzania? Hapana nadhani sasa umefika tuanze kufikiria majibu. Tatizo lipo. Wote tunakubali. Sasa jawabu ni lipi??

Nakumbuka Mkapa aliwapa Chuo waislamu Morogoro..(how is the university doing?-sijui). To me vitu kama hivi ndo vya msingi na ndo ingebidi wote wenye mapenzi mema na taifa letu tujengee hoja. ...... Kupanua fursa kwa wananchi. Mfano kuliko kulaumu eti serikali inatoa billion 60 kila mwaka kwa taasisi za wakristo..go..deeper and ask yourself....wanapewa hizo hela kwa nini na kwa njia gani? Ask yourself..can we also qualify for the same? Mfano wanapewa pesa za kutoa huduma kama elimu na afya..now can you also do the same and get the same money? Kuna University of Morogoro ya waislamu.....buni ideas za kuanzisha centers of excellence za research muombe pesa serikalini na kwingineko. Mkuu..hii dunia its all about your brain... Ukiwa innovative kuna mengi ya kufanya na pesa itakuja. Sasa kama Saudi Arabia or IOC wanataka kukupa pesa za kuanzisha center ya lugha au Quran.....tell them..we need money for science and training of medical doctors! Ukitaka kuajiri hire the best minds and pay them irrespective wana dini gani. Bob ni initiatives kama hizi zimewasaidia sana taasisi za Kikristo kusonga mbele. They are Creative! Trust me you, kama taasisi za kiislamu zikikaa chini zikasumbua vichwa..watapata pesa nyingi sana mkuu. ni innovative ideas kama hizi zitawafanya watu waache kulalamika. Mimi naamini katika fursa sawa mkuu! Lakini naamini hizi fursa zinatafutwa haziji kama mana toka mbinguni.

Bob, mimi mpaka leo naamini, ukiamua kuplay victim card kwamba unaonewa..utaonewa kweli! Ukishajiwekea kichwani kwamba wewe ni mnyonge utakuwa mnyonge kweli! Na ndilo tatizo kubwa ninaloliona kwa wananchi wenzetu walio wengi. Hivi ni waislamu wangapi wanaokula bata hapa hapa bongo kuliko hata hao maaskofu na mapadre? Ukweli ni kwamba kuna wakristo na waislamu wanakula jasho letu kila siku huku sisi tukirushiwa mifupa tukiachwa kutoana macho wenyewe! Tragic as it may sound. Ulishawahi kurusha mfupa kwenye group ya mbwa?? Yes, thats what these guys are doing with this 'udini' thing!

I am sorry to say, lakini vitu kama udini, they are condemned to make us become poor and poorer and irrelevant kwa sababu hatutakuja tufikie muafaka. Should we really condemn Slaa simply because alishawahi kuwa Padri? Leo mimi Masanja, do I know what the fate has for me in ten to twenty years (God allowing nina uzima?). Ukweli ni kwamba we should learn to look beyond our differences. Ukitaka kumhukumu Ogah kwa sababu ni mrefu, mfupi, Muislam, Mkristo nk. You can if you wish so. But one thing is clear. You wont change anything in that. He is who is. Judge him on his ability to do what you want him to do. Utafanikiwa.

Ain all wa kuonyesha njia ingebidi awe Kikwete na wengineo akina Waberoya na Masanja et al. Yet sisi ndo tunazidi kumwaga hii sumu kwa maslahi yetu. Sad indeed!. Tusipoamka itakula kwetu as you well said above-and I would add: Ile mara ngapi?


well said, japo sijaona solution
 
labda yangetolewe mapendekezo katika uchaguzi ujao wa CDM nani awe nani maana Mbowe anamaliza muda wake

kwa hili Dr. Slaa angefaa awe mwenyekiti - sijui kama wazee/waasisi wa CDM watalikubalia (maana walimzuia Mh.Zitto)
 
Mwalimu,
Nidhamu ya woga huanza kwa muathirika kama maradhi..Leo hii watu wanakwenda Loliondo kwa sababu ndiko kwenye tumaini lao la ponya na hatukatazwi kusisitiza watu wakatibiwe Hospital lakini itakuwa fujo kubwa kama ukiwakemea wale wote wanaokwenda Loliondo na kuwaita wajinga na matusi kibao.. haiendi hivyo, maadam wao wamekwisha amini kwamba ndiko tiba yao inakopatikana.

Mimi sina tatizo na Maaskofu wanapotoa hoja zao lakini kumbuka tu uchochezi wowote hutokana na kiongozi wa kundi moja kutotambua kitu fulani na mategemeo yake ni waumini wake wamfuate..
Maaskofu na awanja wa siasa sio mahala pao na hakika kama wao wanaitakia kheri nchi hii waulize kama wapo tayari kurudisha mashule na vituo vya Afya kwa Umma...Nguvu ya sauti zao imekuja baada ya kuwezeshwa na wana hakika kabisa pasipo wao nchi haitawaliki, haikuwa hivyo wakati wa Mwalimu...

Mkuu,

Sizungumzii nidhamu ya woga bali hofu inayopandikizwa kwa wananchi kubagua wagombea kwa misingi ya kutokubalika na watu wa dini tofauti! Ndio maana katika moja ya post zangu nimeuliza ikiwa Dr Slaa amewahi kunena au kutenda jambo lolote kuwakwaza au kuwaudhi waislamu lakini sijapata jibu! Kwa mujibu wa mtoa mada Slaa hakubaliki na waislamu simply because yeye ni mkristo aliyewahi kusomea upadri thats it!

Hivi wakristo nao wakiamka sasa na kuanza kuwakataa viongozi waislamu (believe me hawajafanya hivyo sasa) tutakuwa wapi??
 
Hivi mtu anawezaje kusema kwamba 'waislamu' hawaikubali CHADEMA? Ni data zipi hasa ambazo zinaonyesha kwamba waislamu hawaitaki CHADEMA? Nijuavyo mimi, kuna waislamu wengi tu ambao ni wanachama/wafuasi wa CHADEMA na hata wengine ni viongozi wa kitaifa. Katika hilo simuelewi anayesema kwa ujumla tu kwamba 'Waislamu hawaitaki CHADEMA'. Labda kama ana data kama nilivyouliza hapo mwanzo wa post yangu au vinginevyo itakuwa ni mwendelezo tu wa propaganda!
 
ndugu siyo kwwamba slaa anaiua chadema hapana mimi hakataa,unajua msema kweli siku zote anapendwa na wachache vivevile chama chochote cha siasakkinatakiwa kuwa na watu wenye common vission,goals and mission na slaa yuko mstari wa mbele kuhakikisha chadema followers wanaelewa na wakuwa na uchungu na nchi yao.
 
ELNINO uko kwenye mstari wangu, jamii ya kitanzania inayoamini udini au kuutukuza udini ni ndogo sana,

dini iko serious kwenye political platform na inasemwa sana huko kana kwamba waislamu woote hawaipendi CDM

Hofu yangu ni kuwa ukisemwa sana utaaminika! CDM wanafanya nini kuondoa hali hiyo?

Kumbukeni nimesema kwenye siasa kuna wakati vitu illogical ndivyo vinaexist! na tunaacha vizuri, Slaa yuko clean lakini backgorund yake inawafanya watu waunde hoja, this is not fair though it is their!

Kukaa kimya au kutosema haya kwa sababu ukisema unaonekana mdini au humpendi Slaa is totally misuse ya ukweli.

Kumbuka political platform ndiyo inasemwa kila siku na kusikika kila siku, moto unaendelea kusambaa.

Mkuu mtu yeyote anayesoma between lines..nadhani amejua kabisa from the beginning you dont have ill motive na ndugu Slla (atleast thats what I see-objectively). Lakini sasa mkuu, tayari umeshakubali kwamba hii 'udini thing' ni 'card ya elites' kwenye political platform! Wewe solution yako ni kumuondoa Slaa. Ndo maana mimi katika mabandiko yangu mengi hapo juu nimeona hii solution ni too simplistic nikasema tuaddress tatizo linakoanzia. Tuinue hali za wananchi wetu. Udini is simply hoja mufilisi za watu wanaotuchezea akili.
 
umesema ''Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, "" ukiona wengi ujue una matatizo usikurupuke fanya utafiti wa kina huwezi kuwaweka Makamba na Dr.Slaa kwenye mizania moja umekosea hata CCM wangependa sana kuwa na mtu wa aina ya Dr.slaa lakini tatizo Dr.Slaa anapwaya sana CCM kwani haendani nacho labda aina ya kina Makamba wengine (Mukama) tatizo liko wapi?hata uje msafi vipi CCM lazima Uchafuke tu.
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
Hoja yako ime-base implicitly on udini japo unazunguka na kuzungumza kwa kujifanya unatumia falsafa ambayo hata wewe mwenyewe huna uwezo wa kuifafanua! Slaa leaving his position is not an issue you should have proposed, rather unge-propose ccm wa-withdraw slogan ya udini kwani it has proved to be divisive and polarizing in the country. Mbona hu-propoze JK ajiondoe ili ku-square things up? Tujaribu kuwa open minded kuliko egemeza arguments zetu kwenye udini kitu tunachotambua kwamba kilikuwa introduced kwa manufaa ya kikundi fulani. Kumbe wewe pia unataka kuchagua kiongozi based on his imani ya mimbari!
 
Mkuu,

Sizungumzii nidhamu ya woga bali hofu inayopandikizwa kwa wananchi kubagua wagombea kwa misingi ya kutokubalika na watu wa dini tofauti! Ndio maana katika moja ya post zangu nimeuliza ikiwa Dr Slaa amewahi kunena au kutenda jambo lolote kuwakwaza au kuwaudhi waislamu lakini sijapata jibu! Kwa mujibu wa mtoa mada Slaa hakubaliki na waislamu simply because yeye ni mkristo aliyewahi kusomea upadri thats it!

Hivi wakristo nao wakiamka sasa na kuanza kuwakataa viongozi waislamu (believe me hawajafanya hivyo sasa) tutakuwa wapi??
Mkuu unachozungumzia wewe nakielewa isipokuwa unashindwa kuingia vichwani mwa watu wengine na kujaribu kufikiri kama wao hata kama huamini. Nasema kia siku kwamba sarafu ina pande mbili na muhimu sana kutambua hilo unapojaribu kutatua jambo.

Dr.Slaa sio tatizo la Waislaam isipokuwa amekuwa kiongezeo cha mfumo mbaya wa kiutawala ambao Waislaam wamekuwa wakiulalamikia kuwapendelea Wakristu na kwa bahati mbaya hakuna kiongozi yeyote wa serikali amewahi kukubali/kukana au kuafiki/kutoafiki na hoja hiyo ya Waislaam. Wote wamekaa kimyaaa hali wanaharakati kama kila Mohd na wengine wakiendelea kubomoa...

Sasa maadam wao wanaamini kwamba Mfumo mzima wa Utawala wa nchi yetu unatawaliwa na Kanisa Katoliki, inahitajika nguvu ya ziada kuondoa imani hii kwa Waislaam. Na pia kuna woga mkubwa kwa wakristu wakisikia hoja yeyote inayolihusu kanisa lao kuhusika au kupendelewa pamoja na kwamba sisi sote hatujui kinachoendelea ndani ya mfumo huu wa kiutawala..Sote tupo kizani lakini hatuishi kutetea Upande unaotuhusu.

Kwa hiyo wao kama watu walioumwa na nyoka sii rahisi kuamini kwamba kuna nyoka asiyedhuru hata kama Dr.Slaa mwenyewe hajui CCM ina mkataba gani na kanisa au kanisa lina nafasi gani ktk serikali hii..Kibaya zaidi hakuna mtu toka serikalini amewahi ku deny madai ya Waislaam ila wote wanaonyesha kuogopa au kulihofia Kanisa, kusema ukweli ili wananchi wakawa na uhakika dhidi ya tuhuma zinazotolewa..

Majuzi tu JK aliwaambia Maaskofu au niseme kuwauliza kwa nini wanampiga vita yeye hali kawapa billioni 600 na kuwawezesha ktk kila hali?...Hii haikuwa message ya bure bali kuzidisha hofu ya wananchi hasa Waislaam kuhusiana na nguvu ya kanisa ndani ya mfumo wa Kiutawala... Na hakika hotuba hiyo imekuwa kichocheo kikubwa cha Udini na Waislaam kuanza kujiuliza mengi kwani kulingana na JK ruzuku hii imetokana na MoU...

Mkuu kutolitambua tatizo au kutokubali kuwepo kwa tatizo ndio somo kubwa la Watanzania wote iwe ktk maswala ya Muungano au Udini..na ndicho nachokiona hapa JF.. Watu wanakataa kuwepo kwa Udini hivyo sii rahisi kutibu kitu usichoamini kuwepo.. Na Kwa Upande wa Muungano bara hatuoni tatizo hivyo sii rahisi kuutendea mema Muungano wetu ila siku tukikubali kuna mapungufu na kuanza kuyashughulikia..

Makaburu wa South hawakuwahi kuiamini kwamba watu weusi walikuwa wakionewa nchini mwao. Na ukitazama harakaharaka South ina wasomi kuliko Tanzania iweje watu hao walizungumzia Ubaguzi wakati walipewa nafasi kuliko hata TZ huru?..Na makaburu walipata washirika wengi tu ambao hawakuamini kwamba weusi na weupe walitakiwa kuwa na Uhuru na haki sawa maadam wao sii wamoja. Hivyo mtazamo wa swala zima la Apartheid ulikuwa kwa makundi yao badala ya Kitaifa.

Dr.Slaa ni kiongozi ambaye mimi namkubali wala sii tatizo la Waislaam isipokuwa ni hofu iliyojengwa na viongozi wa CCM kupitia Masheikh kiasi kwamba tunachokiona ni matunda ya fitna iliyopandikizwa. na vigumu huwezi kuwashawishi Waislaam dhidi ya tuhuma hizi unless yeye mwenyewe Dr.Slaa ajitambulishe sera zake na hasa ktk maswala ambayo Waislaam wanafikiria yeye na Chadema hawana mpango...

Wazungu wanasema ni Bora kufanya kitu ukakosea na kukosolewa kuliko kukaa kimya kabisa..Waislaam wanatafuta chama au kiongozi atakaye waondoa woga au niseme hiyo Nidhamu ya Woga iliyokwisha jengwa kwao na kuamini kwamba hakuna Mkristu mwenye kujali maslahi ya Waislaam pamoja na kwamba ni makosa kufikiria maslahi ya makundi badala ya Taifa zima..

Kwao waislaam maslahi ya Kitaifa ni maslahi yanayosimamia na kuwapendelea wakristu..na mifano ndio kama hiyo kurudishiwa mali zao wakati za Waislaam bado zina mgogoro na wapo viongozi wa CDM walosema wazi kwamba mali hizo hazitarudishwa kwa Waislaam..Mara sijui Mahakama ya Kadhi haiwezekani na OIC haina nafasi Tanzania kuashiria mtazamo wa chama..

Hawa wote waliosema haya ni wanachama wa Chadema na wapo chini ya Uongozi wa Dr.Slaa ambaye ni katibu wa chama na mgombea Urais.. Kwa maana kwamba kama angeshinda Urais Waislaam wasitegemee lolote kutoka kwake..Dr.Slaa na CDM wanatakiwa kuwa makini sana na statement kama hizi zinapotolewa na wabunge au madiwani wake..

Hizi ni strong statement na zinajenga fear among Muslim where this country is leading! Kinachofuata ni utekelezaji wa hiyo - Nidhamu ya WOGA.
 
Too sad for you my dear! kama ukaribu wangu na Zito ndio unaofanya CDM kichukiwa na unakosa hoja ya kukiokoa kwa sababu ya uhusiano wangu na Zito sawa! umenifanya nicheke, umeenda mbali na hoja, I am not hero, I am not intellectual hayo umenipa wewe na ulinipa wewe!

JIBU HOJA, KATAA kuwa Slaa asiondoke na sema nini wafanye! kwa nini mko kwenye gari mnajua kabisa haliendi popote bali ni kupiga resi tu na makonda kusema linaenda na bado liko stendi?

Huyo Zito wala hafai kuwa katibu mkuu wa chadema, wala sijui na sina ukaribu naye..we are connected with Zitto kwa mawazo yake na itikadi zake na si vinginevyo

Haya waislamu hawakitaki CDM unasema nini?

Conclusion zako kwenye post mbili zimenifanya nikuweke kwenye -ignore list, umeandika kama una uhakika kabisa! my God! namna hiyo unaweza kumgomnaisha mama yako na baba yako, ukimuona mama anaongea na mzee fulani utatoa conclusiona na kumweleza baba! childish, watu wanashindana kwa hoja na si kusingiziana vitu ambavyo personally unajua si kweli na kama unaamini umekosea!

poor MTM!


Waberoya..
Je wajua kichocheo cha ccm kujivua gamba muasisi wake ni nani,
Je wajua kuwa anguko (mafisadi EL, RA nk) la hao ambao inasemekana wameanguka japo ukweli ni kwamba bado wamesimama unajua ni nini?
Yote haya yalianzia kwenye first eleven ya mafisadi, ikafuata epa, richmond na vingine vingi ambavyo waliofahamu na hawakuwa na uchungu au ujasiri wa kuvisema walinyamaza bali Dr na wenzake kwakuwa wana uchungu wakasema bila kificho wala woga.

Unajua muasisi wa udini ndani ya nchi hii ni nani?
Unajua muasisi wa vurugu ndani ya nchi hii ni nani?
Unajua nani anayevuruga kura, maandamano ya amani, mikutano ya kisiasa na pia kuvigonganisha vyama kiuongozi?

Kama unajua hilo huna haja ya kuwa na pendekezo la Dr kupumzishwa bali sasa ni kukaza buti na kujipanga kupangua hoja dhaifu ambazo hazina mashiko, nataka nikuhakikishie ndugu yangu hata Dr Slaa akitolewa hapo kwakuwa lengo la ccm ni kusambaratisha upinzani hoja hiyo au nyingine yeyote itatangazwa na kuhubiriwa kwa nguvu tu, kwahiyo nivema kujipanga kupangua hoja na sio kuwakimbia

Waambie hatuwakimbii kwa hoja hiyo wala hatuna mashaka, watu wanauwezo sasa kuamua na kufikiri japo kuan aliyesema ni wauza maduka - sawa tu maana ndio wanaotaka mageuzi watayapata tu
 
Slaa is overrated, but CHADEMA has the last say. Hata wakitaka kumsimamisha Regia Mtema poa tu.

As long as demokrasia inafuatwa.
 
Hivi mtu anawezaje kusema kwamba 'waislamu' hawaikubali CHADEMA? Ni data zipi hasa ambazo zinaonyesha kwamba waislamu hawaitaki CHADEMA? Nijuavyo mimi, kuna waislamu wengi tu ambao ni wanachama/wafuasi wa CHADEMA na hata wengine ni viongozi wa kitaifa. Katika hilo simuelewi anayesema kwa ujumla tu kwamba 'Waislamu hawaitaki CHADEMA'. Labda kama ana data kama nilivyouliza hapo mwanzo wa post yangu au vinginevyo itakuwa ni mwendelezo tu wa propaganda!

Nakubaliana na wewe, watu wamejaa mawazo hasi kwamba waislamu hawapendi Chadema kwa sababu Dr wa Ukweli Slaa aliwahi kuwa Padri, je mawazo haya wanaambatanisha na vigezo vipi?, hivi vya waislamu wachache wenye chuki binafis? hivi kwani hakuna wakristo ambao hawapendi Chadema na wapo CUF, CCM au hata NCCR, na Kwa nini iwe waislamu ndio waamuzi wa mambo, na kwa nini topic isiwe kwamba wakristo hawapendi CUF, mimi nafikiri tuache kufikiri kwamba waislamu wachache wenye Chuki na Chadema ndio wanabeba dhamana ya kuwawakilisha waislamu wengi ambao mimi nawafahamu ambao kwao udini hauna nafasi bali wanaangalia ni chama gani kitawakomboa katika hali ngumu ya maisha, waislamu wanaoelewa wengi wamejiunga katika vyama mbalimbali kikiwamo Chadema, na kwa uhakika hawa waislamu wachache wanaoeneza sumu ya udini hata kupiga kura huwa hawapigi, na pia nilishawahi kusema sisi tunaona hali halisi ya maisha ya mtanzania Tunamuhitaji Dr Phd Slaa na hatuna haja na kura chache za hao wanaojiita waislamu amabo wao maisha ni bora, wanapata matibabu safi, Shule bora, na mambo mengine amabyo sisi tunaona ni tatizo wao wanaona ni shwari, mtu kama huyo hata umwambie nini yeye hayupo tayari kubadilika sasa wa nini kupoteza muda kumwelimisha, achana nae. lakini kumbuka kwa kuwa wewe unamaisha bora sio jamii yako yote iko hivyo, kunawengine wanasota, kiukweli wengi wetu tungekuwa wabinafsi hata tusingechangia chochote hapa maana wengi wetu tunaweza hata kwenda Aghakani kutibiwa, sasa fikiria ni wangapi wana hiyo access ya hizo Hospital!? acheni ubinafsi na unafiki, Hali ni mbaya nchi hii, watoto wakaa chini eti wanasoma, mwalimu mmoja shule ya watoto 400, kweli halafu akiomba kazi, mnaangalia anajua kuongea Kiingereza kwanza, kweli!?, watu wanakunywa maji pamoja na mifugo Tanzania hihi, Kweli!?, ili hali kunawengine wanaagiza maji ya kunywa toka USA, unajua wewe!? Acheni Udini na Unafiki.

Mimi nasema CHADEMA NI CHAMA CHA WATZ, wanaume kwa wanawake,Waislamu kwa Wakristo, Wapagani kwa Wahindu, na hata siku moja hakijaenda kumbembeleza mtu kukiunga mkono, kinamwaga sera watu wanajaaa, na wenye wivu ndio hao sasa mara Dr Slaa alikuwa Padri Yes alikuwa na sio Padri kwa sasa Ni Katibu Mkuu wa Chama Kikuu cha Upinzani Full stop.

NDUDU ZANGU MIMI NIMEBAHATIKA KUTEMBELEA NCHI YETU YOTE ni Nchi nzuri sana na ni tajiri sana, haipaswi kuwa na njaa, haipaswi kukosa umeme, haipaswi kuwa na miundo mbinu mibaya, watoto wetu walipaswa kupatiwa elimu bora na sio bora elimu, wanachi walitakiwa kupata matibabu bora, nimetembea Mikoa yote, utashangaa unavyoiona Tanganyika ilivyo nzuri lakini imefanywa kuwa maskini na watu wachache wenye tamaa, na sasa wanawageuza watu wenyeufinyu wa kufikiri eti UDINI, jamani fungueni Bongo zenu ndugu zangu.
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.


Udini haondoki kwa kuondolewa Dk Slaa, Kama kweli hakuna balance mtu mmoja hawezi kuibalance. Suala ni kuamini kila kitu kinachozungumzwa mtaani, bila kukifanyia utafiti. Tatizo kubwa la Tanzania ni chama kimoja cha upinzani ambocho kibase upande mmoja wa muungano na tena kwa bahati mbaya kikajikuta kina jibana katika dini fulani. Ubinafsi umeshindwa kuona umuhimu wa upinzani kushirikiana na Mtu kama prof Lipumba kugombea wakati hana uwezo wa kuitikisa ccm. Kama Hemedi Rashidi angekua mgombea mwenza wa Dk Slaa, leo tungekua tuna zungumza mengine. Si kitu kigumu kuona CUF na CDM wana lulu wasiojua jinsi ya kuitumia. Sasa imabaki taswira ya udini tu badala ya kujitathmini na kuangalia kule tuendako.

Eti unasema Dk Slaa amekishusha cdm, Wabunge wa cdm wameongezeka, sikuelewi kabisa. Kwa Idadi ya wabunge bara CUF imeshuka. Kura za Lipumba zimeshuka. Huoni kwamba CUF CDM combine ni timu nzuri sana. lakini devide and rule imekubali na imekolea. CUF bara inakufa, na nakupa angalizo kwamba Udini cdm unakufa na CUF udini unakua.

CUF haiitaji kujivua Gamba? Je vyama vingine navyo. Je Dk Slaa ni fisadi.
Hii thread ni nzuri lakini ina mapungufu mengi. Leo CCM wanajua aliyewasumbua sana katika uchaguzi uliopita ni Dk Slaa.:hug:
 
Back
Top Bottom