Sikutaka kurudi kwenye hii thread, however, your post made me to embrace as if nakuona
Nimefarijika kaka kwa kunielewa ASANTE and your post ninahifadhi moyoni na akilini kama ni memorable post ever!!
Asante sana natuma shukrani zangu na kwenye PM yako. At least umenipa nguvu ya kunywa chai
Waberoya, nakuheshimu sana. Natamani sana wachangiaji wote wa JF wangekua kama wewe,yaani hata wale ambao napingana nao ki-hoja basi wangekua wastaarabu,wenye kuacha hoja zipambane badala ya either kupaza sauti, kupiga mayowe, kutoa kashfa, kutumia mind games na provocations zisizo za msingi n.k.
Napenda kupingana nawe kwenye hili though;
M-Tz 1 ameeleza vyema, ikanifanya nirudi tena kwenye original post yako nione kama ndivyo ulivyomaanisha. Nachelea kusema,kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa sana katika uwasilishaji wako wa mada ambalo unapaswa ulifanyie kazi.
Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa
Makosa? Sina uhakika. Tunajua sasa kama ANC kumfanya Zuma kuwa rais wa SA na CCM kutuletea JK badala ya Dr Salim maana yake nini. Hapo ndipo tunapoweza kusema CDM ilifanya makosa kumteua Dr Slaa au la.
Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..
Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo
Hapa nina shaka: Hivi huo muonekano wa "kukiua chadema" unatilia maanani ongezeko la wanachama, ongezeko la kura za urais, ongezeko la wabunge na madiwani na ongezeko la ufuasi wa chadema lililopo sasa? Umetazama pia kukubali kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya (potelea mbali kama kwa nia thabiti au la, mchakato umeanza!) .Muonekano huo unatazama kivumbi kinachoendelea kwenye kambi ya jirani (CCM) hivi sasa? Je unatazama kujibainisha mbele ya wananchi kwa aina ya "upinzani" ambao vyama vingine vya siasa vinao? Unatazama ukali wa vita, hasa vita chafu zinazoeengezeka kila uchao kuelekezwa kwa Chadema? Na kama muonekano huo umetazama haya kwa uchache, je unaona uhusiano wowote wa hayo na uteuzi wa Dr. Slaa kubeba bendera ya chadema kwenye uchaguzi uliopita?
Kama unauona basi, pengine tunatofautiana namna tunavyoyatazama mambo hayo machache niliyoyataja hapo:
- Ni wazi kuwa ongezeko la kura,wabunge,madiwani na wanachama ni jambo CHANYA
- Rais kukubali uanzishwaji wa mchakato wa katiba kinyume na matakwa ya CCM yenyewe na baraza lake la mawaziri, mie naona ni jambo CHANYA (nadhani hili nalo li wazi)
- Pangua pangua inayoendelea CCM hivi sasa, mimi ninaiona kama jambo CHANYA kwa chadema kwa maana kuwa inawapa ujasiri kuwa karata waliyoitupa (kumteua Dr Slaa) inalipa. How? Katika ndondi, ukiweza ku-expose weakness ya mpinzani wako ni hatua muhimu kuelekea ushindi. Itamchukua muda kuiongezea ulinzi na wakati inakufanya mashambulizi yako yawe focused zaidi. You capitalize in it, and look for a killer blow to finish him off.
- Wanaovipiga vita vichafu kwa silaha ya udini, yes wanaweza kuungana kama unavyosema, lakini mie bado naona hiyo ni alama CHANYA pia. How? Penya ukweli uongo hujitenga, na KWELI hu-survive siku zote. Siku kweli itakapo dhihirika, waongo tutawakuta wamejikusnaya pamoja na ni rahisi kuwa-identify. Hili ni gumu na litaeleweka tu na wale ambao wanaamini kuwa hakuna short-cut kuelekea kwenye ukombozi wa kweli wa nchi hii.
Hebu tujiulize kama waberoya wa kweli wa kwenye Acts of apostles,Je, "risk management" ya CDM itaishia kwenye kumtoa Dr Slaa pekee? Au itabidi na Mbowe atoke ili kuondoa lile la u-kaskazini? Halafu waahidi mahakama ya kadhi kama mrema na CCM ya 2005? Halafu watafute sasa mgombea mwenye dini nyingine mbali na ukristo. Halafu awe mwenye rekodi ya utakatifu, halafu awe mzalendo kama Dr Slaa, siyo? Sisemi kuwa haya hayawezekani,la hasha! Ila yeyote atakayeniahidi kuniletea haya kesho, He is simply too good to be true! Sina imani ya kiwango hicho! Hebu nikasome tena kuhusu RISK MGT shalafu pengine nitarejea. Asante