Ridhiwan Kikwete: Hatutokuwa na huruma na wanaowaonea wanyonge

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze ameanza ziara ya Mkoa wa Mara kwa kutembelea na kuongea na Watumishi wa Manispaa ya Musoma na kisha kufanya ziara kukagua utekelezaji wa mpango wa kuondoa Umaskini yaani TASAF katika jiji hili.

Naibu Waziri ambaye ana ziara ya siku tatu katika Mkoa huo alikuwaelekeza Watumishi wa Umma kujikita katika kuhakikisha wanazingatia na kutafsiri maono ya Rais Samia Suluhu Hassan pale aliwahimiza kuwe na Utumishi wenye kuleta tija, mbora, ulio kimkakati unaolenga kuwatumikia Wateja ambao ni wananchi. Akizungumza na watumishi, Ndg. Naibu Waziri aliwaasa kuwa wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo.

Pia katika tukio jengine,Naibu waziri Ndg. Kikwete amewaondoa kwenye Uratibu wa mpango wa TASAF waratibu wa Mkoa na Wale wa Wilaya kwa kile alichokiita kushindwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wangonge ambao wanahitaji sana huduma hii katika muda. Akionyesha kukaairishwa na kushindwa kwao , Ndg. Kikwete alimuelza RAS wa Mkoa wa Mara ndugu Makungu kutoelewa kwa nini hadi leo wahitaji hao hawajalipwa wakati Fedha kwa ajili ya wanufaika zilishatumwa wakalipwe wanufaika. Naibu Waziri anaendelea na ziara Mkoani hapo kwa kuelekea Wilayani Tarime.

FB_IMG_1694500566944.jpg
FB_IMG_1694500568903.jpg
FB_IMG_1694500570816.jpg
FB_IMG_1694500574102.jpg
FB_IMG_1694500576690.jpg
FB_IMG_1694500579158.jpg
FB_IMG_1694500582605.jpg
FB_IMG_1694500588501.jpg
 
Wanajitahidi kuuzima moto wa Chadema kwa kutumia mchanga kuwapofusha wananchi.
Kutumia umaskini wa kipato chao..
Ila wamechelewa kidogo....
Gari aina ya TEC kutoka Roma!
liliwakia bandarini na sasa limepaki kule vigangoni vijijini na linaoshwa kila jumapili.
Kwa sasa bado linaendelea kula Silence kwa wiki zingine tatu zijazo
Mchawi wa CCM ni Deep World (DP-WORLD).
 
Mambo ya kijinga sn, unakuta hapo wanapewa elfu 40,000 kwa mwaka, na wakati yeye perdiem yake tu kwa siku ni 250,000
 
Back
Top Bottom