Ridhiwani Kikwete aishukuru DAWASA kutatua changamoto ya maji Chalinze. Rais Samia atoa fedha kusambaza kwa wananchi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete ameishukuru serikali na Uongozi wa Wizara na DAWASA kwa kutatua tatizo la Maji katika halmashauri ya Chalinze.

Akiongea mbele ya Kamati ya Bunge ya Mitaji kwa Umma, Mbunge huyo wa Chalinze amewashukuru pia kamati kwa niaba ya Bunge kwa jinsi walivyosimamia kuhakikisha tatizo Unaondoka kwa kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji.

Akimshukuru Mtendaji Mkuu wa DAWASA , Injinia Kingu, Mbunge wa Chalinze alimshukuru kwa kutenga pesa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara jimboni hapo mwaka jana.

Katika ziara hiyo Rais Samia alielekeza kutengwa kwa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya mradi wa Kusambaza maji katika mji wa chalinze na viunga vyake. DAWASA wametenga Shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya usambazaji Halmashauri ya Chalinze ikiwa ni mara mbili ya maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia.


#KaziInaendelea #Maji #JimboniChalinze
 
Back
Top Bottom