Ridhiwani Kikwete awapasua wana Yanga na Haji Manara

Nadhani Watu wengi mmebahatika Kuisikiliza Clip inayosambaa kwa Kasi sasa Mitandaoni ya Ridhiwani Kikwete ( MB Chalinze ) hivyo nami nitaweka tu hapa Nukuu zake Tano tu zenye maana na umuhimu.

"Wana Yanga SC Wenzangu yatupasa sasa Kubadilika japo wenyewe tunajiona tunapatia kumbe tunakosea. Kuizungumzia Simba SC kila mara tusidhani kuwa tunaishusha bali tujue kuwa ndiyo Kwanza tunazidi tu Kuipaisha"

"Tukatae tukubali Wenzetu wa Simba SC Kibiashara wametuzidi na hili Wala halihitaji Mjadala hivyo ni Jukumu letu wana Yanga SC nasi Kujitangaza zaidi kwa Mambo na Maendeleo yetu kuliko kila mara Kuizungumzia Simba SC wakati Sisi bado tuna Safari ndefu ya Kufikia pale walipotutangulia"

"Yaani wana Yanga SC Wenzangu tunaacha kutumia Nguvu Kubwa kutangaza Jezi zetu ambazo bado hazijauzika kihivyo Sisi tuko busy Mitandaoni na Vijiweni Kukosoa Jezi za Simba SC ambayo hata Kimafanikio ya Kimpira kwa sasa wameshatuzidi. Huu ni Upuuzi mkubwa na yatupasa kubadilika"

"Nimesikitika sana kuona Leo hii Yanga SC tumemchukua aliyekuwa Msemaji wao Mkuu ambaye ni Mchumia Tumbo na Kumuamini na kuwa nae. Huyu ndiyo Mtu ambaye Kutwa alikuwa akitutukana vibaya wana Yanga SC mpaka Kutudhalilisha leo kwa Upumbavu Wetu na kwa Utashi fulani tumemkaribisha Kwetu"

"Kama ameweza Kuwatukana na Kuwachafua wale aliokuwa akiwapenda na Kuwatumikia kwa Moyo wake wote leo wana Yanga SC tuna uhakika gani kuwa huyu Msemaji mpya Mchumia Tumbo Siku akishindwana nasi na Kuondoka hatoenda Kutusema nasi vibaya huko atakakokwenda? Inasikitisha mno"

Ukiwa mwana Yanga SC mwenye Akili fupi unaweza kudhani hizi ni Hasira zake tu binafsi Ridhiwani Kikwete ( MB Chalinze ), ila kwa wenye Akili Kubwa akina Mightier hapa tumegundua na tuna uhakika kuwa haya aliyoyasema ndiyo haya haya Machungu yaliyomo ndani ya Ubongo na Moyo wa Baba yake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Sasa ni rasmi kuwa Ndoa ya Ridhiwani Kikwete (MB Chalinze) ambaye ndiye kwa Maagizo ya Baba yake wamewaleta hapo Yanga SC akina GSM inaelekea Kuvunjika na hii si dalili njema kuelekea katika Uwekezaji.

Haya wana Yanga SC mliopo hapa JamiiForums (ambao hamchangii Pesa yoyote Yanga SC zaidi ya Kudemka tu) njooni mumbishie mwenye Yanga SC yake Ridhiwani Kikwete (tena mpaka huwa anatoa Pesa zake kuisadia) kama mna Ubavu huo Kudadadeki zenu.

Na baadae ikinipendeza Mightier nitakuja na Exclusive Thread ya kuhusu Matawi Makubwa ya Yanga SC hapa Dar es Salaam dhidi ya Injinia Hersi Said kwani kwa Mapovu yao dhidi yake na Kumchukua Haji Manara Yanga SC ikifungwa na River United FC katika CAF CL na Simba SC katika Ngao ya Hisani anaondoka Yeye na Manara wake.
Mkuu hayo ni mawazo yake lakini wanayanga wengine wanaweza wakawa na mawazo yao pia tofauti yao ni umaarufu tu. Mawazo yangu Mimi yanga IPO sawa kufanya iliyofanya mpira ni burudani tu hasa kwa sisi mashabiki mpira upo kuburudisha si kama siasa au nyanja zingine za maisha kwa hiyo kama kuwasema simba wapozingua ni burudani kwa nini tusipate burudani hiyo. Tukumbuke raha ya mashabiki wa simba/yanga si mpira na timu yao kufanya vizuri bali hata failure ya mwenzake nayo ni burudani tu ndio maana hata Siku ya tamasha la wananchi kile kitendo cha yanga kufungwa match yao ilikuwa burudani mno kwa wanasimba japokuwa hayawahusu wao mambo ya yanga na tamasha lao. Wakuu asili ya michezo hii ilianza na burudani na biashara ikaja baadae hivyo tusijaribu kuua asili ya mchezo huu.
 
Tatizo Ridhiwani anaonekana kabisa Hana akili kwa kumtazama kwahiyo Ushauri wake unakuwa hauna maana
 
Nadhani Watu wengi mmebahatika Kuisikiliza Clip inayosambaa kwa Kasi sasa Mitandaoni ya Ridhiwani Kikwete ( MB Chalinze ) hivyo nami nitaweka tu hapa Nukuu zake Tano tu zenye maana na umuhimu.

"Wana Yanga SC Wenzangu yatupasa sasa Kubadilika japo wenyewe tunajiona tunapatia kumbe tunakosea. Kuizungumzia Simba SC kila mara tusidhani kuwa tunaishusha bali tujue kuwa ndiyo Kwanza tunazidi tu Kuipaisha"

"Tukatae tukubali Wenzetu wa Simba SC Kibiashara wametuzidi na hili Wala halihitaji Mjadala hivyo ni Jukumu letu wana Yanga SC nasi Kujitangaza zaidi kwa Mambo na Maendeleo yetu kuliko kila mara Kuizungumzia Simba SC wakati Sisi bado tuna Safari ndefu ya Kufikia pale walipotutangulia"

"Yaani wana Yanga SC Wenzangu tunaacha kutumia Nguvu Kubwa kutangaza Jezi zetu ambazo bado hazijauzika kihivyo Sisi tuko busy Mitandaoni na Vijiweni Kukosoa Jezi za Simba SC ambayo hata Kimafanikio ya Kimpira kwa sasa wameshatuzidi. Huu ni Upuuzi mkubwa na yatupasa kubadilika"

"Nimesikitika sana kuona Leo hii Yanga SC tumemchukua aliyekuwa Msemaji wao Mkuu ambaye ni Mchumia Tumbo na Kumuamini na kuwa nae. Huyu ndiyo Mtu ambaye Kutwa alikuwa akitutukana vibaya wana Yanga SC mpaka Kutudhalilisha leo kwa Upumbavu Wetu na kwa Utashi fulani tumemkaribisha Kwetu"

"Kama ameweza Kuwatukana na Kuwachafua wale aliokuwa akiwapenda na Kuwatumikia kwa Moyo wake wote leo wana Yanga SC tuna uhakika gani kuwa huyu Msemaji mpya Mchumia Tumbo Siku akishindwana nasi na Kuondoka hatoenda Kutusema nasi vibaya huko atakakokwenda? Inasikitisha mno"

Ukiwa mwana Yanga SC mwenye Akili fupi unaweza kudhani hizi ni Hasira zake tu binafsi Ridhiwani Kikwete ( MB Chalinze ), ila kwa wenye Akili Kubwa akina Mightier hapa tumegundua na tuna uhakika kuwa haya aliyoyasema ndiyo haya haya Machungu yaliyomo ndani ya Ubongo na Moyo wa Baba yake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Sasa ni rasmi kuwa Ndoa ya Ridhiwani Kikwete (MB Chalinze) ambaye ndiye kwa Maagizo ya Baba yake wamewaleta hapo Yanga SC akina GSM inaelekea Kuvunjika na hii si dalili njema kuelekea katika Uwekezaji.

Haya wana Yanga SC mliopo hapa JamiiForums (ambao hamchangii Pesa yoyote Yanga SC zaidi ya Kudemka tu) njooni mumbishie mwenye Yanga SC yake Ridhiwani Kikwete (tena mpaka huwa anatoa Pesa zake kuisadia) kama mna Ubavu huo Kudadadeki zenu.

Na baadae ikinipendeza Mightier nitakuja na Exclusive Thread ya kuhusu Matawi Makubwa ya Yanga SC hapa Dar es Salaam dhidi ya Injinia Hersi Said kwani kwa Mapovu yao dhidi yake na Kumchukua Haji Manara Yanga SC ikifungwa na River United FC katika CAF CL na Simba SC katika Ngao ya Hisani anaondoka Yeye na Manara wake.
Biashara United wao wameshinda ugenini goli 1-O. Ushindani wa Simba na Yanga ndio kikwazo cha kuendelea soka la bongo, japo kwa sasa angalau timu ndogo zinapambana kupata matokeo.

Itafika kipindi, Simba na Yanga watakuwa wanashika nafasi kuanzia ya nne.
 
Back
Top Bottom