Binafsi sina tatizo juu ya kupewa escort Riz1. Tatizo ni jinsi gani wanatumia mali ya umma kwa fujo. Fikiria, hata kama ana threats Je, gari moja ya Polisi isingetosha? Hapa si ulaya Bwana! Atumie mali ya watanzania kwa kiasi, hapo tutamwona kidogo mstaarabu.
Mtoa mada ameona jumla ya gari 5 zikimpeleka riz1 uwanja wa ndege! hebu fikiria jamani... Kweli tunamwonea wivu?
Riz1, ungetuliza mapepe kwani sisi si wapiga kura wako. Shuka huko ulipo matawini!
Nakubaliana na wewe!Kwasababu kabla ya uchaguzi wengi walisema kampeni ilikuwa ni ya kifamilia zaidi kuliko ya kichama.Hata hivyo wameshinda,ina maana hata kama ingekuwa ni Ridhwani mwenyewe kwenye uchaguzi wa rais angeshinda pia,so naona ni baba anarudisha shukrani.Kwa wengine mnaoshangaa,ndo bongo yenu hiyo, mtafanyaje?Wakati wa kampeni, baba alimtuma mwana ...sasa baba anamlipa mwana kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuksanya wadhamini...
Ubia wa Urais! Ingawaje mkulu alisema urais wake hauna ubia.
Baba Rais, watoto wanapewa ulinzi kwa usalama wao...hayo hufanywa katika nchi za wenzetu sijui sisi huwa tuna mfumo upi.
Ridhwan kavunja kipengere kipi cha katiba au sheria? Tusiendeshe nchi bila kufuata sheria kamwe hatutaweza kuwa viongozi bora wa baadaye.
kwa kuwa hatuoni Ridhwan akipewa escort wakati wote inawezeka siku hiyo ilikuwa inahitaji escort ili aweze kwenda na muda. Ni viongozi wangapi wanatumia magari ya umma kwa kubebea nyasi, na kupeleka watoto shule na kwingineko? Ajabu ni nini kwa hili?
Members of the 1st family deserve state-sponsored personal security during the tenure of their parent/president. Ask Jenna & Barbara Bush or Chelsea Clinton, and they will explain this argument to you.
this is so funny, but a poignant point. Lakini angeweza kupanda dcm la gongo la Mboto, kina Makongoro walikuwa wanatembea mguu kwenda na kurudi shule Upanga-Msasani. Ndio maana mpaka kesho baba yao anaheshimika na Watanzania kama vile mtume wa Mwenyezi Mungu.sasa jamani mlitaka apande dcm la gongo la mboto?
Members of the 1st family deserve state-sponsored personal security during the tenure of their parent/president. Ask Jenna & Barbara Bush or Chelsea Clinton, and they will explain this argument to you.
Nijuavyo mimi watoto wa marais wengi tu duniani(wanaounda first family) hupewa ulinzi na ama polisi,jeshi,secret service ama chombo chochote kinachosimamia usalama wa viongozi kwa nchi husika(ikiwa ni pamoja na kuwa na motorcade yenye escort ya walinzi) so Ridhwan kama mmojawapo wa watoto wanaounda first family ulinzi ni stahili yake...
Mkuu Ulaya nina uhakika hawana huo ujinga, nilishuhudia mwenyewe kwa macho yangu raisi wa sasa wa ujerumani akitoka Bellevue (ikulu yake) na gari moja tu na piki piki. Tena hamna mbwe mbwe kama za Kikwete hadi ambulance ya knight support inamsindikiza na kusababisha foleni Dar. This is wastage of resources.