Ridhiwan anapewa escort; Kwanini?

Yote tisa jamani wanaJF suala la umeme inakuwaje au humu watu ni majirani wa kikwete mnapata umeme! Hili limenifanya niichukie nchi yangu sasa aaarggg...
 
polepole jamani tunachaganya madawa. Mashambulizi dhidi ya kijana huyu yameanza kukosa mantiki. mtazamo wako hasi kwa escort ya Ridhwan ni sawa na kupotea njia. sioni kosa. I stand to be corrected
 

Wachache wenye mawazo kama ya kwako Dada.

Pengine sitawalaum wachangiaji ambao umri wao ni mdogo kiasi kwamba hawakuwaona watoto wa Nyerere toka wakiwa teens hadi utu uzima. Hata awamu ya mzee Mwinyi hapakuwa na First Sons cum Celebrities.
Sijui ni nini kilipelekea RK apewe escort ya nguvu kiasi hicho ambayo ni sawa na anayopewa Mwinyi au Mkapa kwa sasa kama sio Ulevi tu!

Kiwango cha threat kwa US President na Familia yake haviwezi kulinganishwa na threat ya usalama kwa Rais wa Tanzania na Familia yake.

Kuna wanaosema tunaona WIVU. Hivi mfanyakazi wako wa nyumbani au mtoto kufuja mali unazozitafuta kwa taabu unamwonea wivu???
RK kama ana jeuri ya pesa anaweza kuajiri ulinzi wake binafsi, tukilalamika basi mtu atuambie tunaona WIVU.
Mbona hatujasikia hofu ya usalama wa RK ili kustahili ulinzi kama ambavyo angepata raia mwingine pindi maisha yake yakiwa under threat??

Kina Manji, Mengi wana walinzi wao binafsi na hujawahi kusikia watanzania tunalalamika.

Kwa walio karibu na RK wamshauri aachane na pomps hizo hata kama baba/mama/ikulu wanalazimisha awe na escort. Miaka mitano si mingi sana kumfanya ajitenge na jamii ya kitanzania. Gamal Al Din Mohammed Hosni Sayed Mubarak leo hii anakimbilia uhamishoni, mwana wa mfalme anakuwa mtumwa nchi ya ugenini.

Modesty life hum-connect mtu na wanajamii ndio maana Princess Diana anakumbukwa hadi leo kwa vile hakuna kuwa kwenye Royal family ni kitu cha kuambatana nacho.
 
Ridhwan kavunja kipengere kipi cha katiba au sheria? Tusiendeshe nchi bila kufuata sheria kamwe hatutaweza kuwa viongozi bora wa baadaye.
 
First son jamani ulinzi lazima, though sipendi but protocol kuzingatiwa muhimu, mwacheni ale mapurupuru ya u-prezidaa, au mpwa unataka ukutane nae kwenye dalalada?
 
Wivu wa kijinga huuu........ Ridhwan sio mtoto wa mkulima ni mtoto wa Rais wa nchi. Kwa hili umechemka.
 

iyo sayari ya ngapi mkuu? Unajua limit ya motorcade kwenye govt.protocol au umeamua kuandika mkuu? Aya bwn,andika andika tu!
 
Ni matusi kufanya kampeni kwamba mtoto wa Rais asipewe ulinzi ama escort. Gharama ya kuwa na kiongozi mkuu wa taifa lolote ni kubwa, pamoja na gharama hiyo ni hiyo ya kumpa escort mtoto wa kwanza (fisrt son) au mama wa kwanza ( first lady) ambao ni sehemu ya baba wa kwanza ( Rais). Usifikiri kuitwa mtoto wa kwanza wa taifa ni lelemama, ni jina linaitwa duniani kote likiambatana na gharama zake.
 
Ridhwan kavunja kipengere kipi cha katiba au sheria? Tusiendeshe nchi bila kufuata sheria kamwe hatutaweza kuwa viongozi bora wa baadaye.

kila kitu kikiwekwa kwenye katiba basi iyo katiba page zake zitakuwa na size ya 6 kwa 6 kama kitanda na tani kama 3000 ivi. Pia si kila ki2 ni sheria sheria!
 
Ni wivu mbadala. Kuna siku utamnyima mkeo ulinzi
 
Tuseme yote lakini hili la escort halina tatizo labda kama angekuwa ndugu wa mbali wa Rais anayepewa escort nisingepuuza kushangaa
 
kwa kuwa hatuoni Ridhwan akipewa escort wakati wote inawezeka siku hiyo ilikuwa inahitaji escort ili aweze kwenda na muda. Ni viongozi wangapi wanatumia magari ya umma kwa kubebea nyasi, na kupeleka watoto shule na kwingineko? Ajabu ni nini kwa hili?
 

mawazo ya kitoto kuhoji escort ya mtoto wa Rais.
 
kama una bifu na Ridhwan tuambie mada ingine ya bifu lako nasi tutasaidia kujadili hapa lakini la escort ni utumbo wa kuwapa mbwa kula haufai kwa binadamu kula. Mada inanuka chuki badala ya hoja ya nguvu. unataka kutuambia huji kuwa Ridhwan ni mtoto wa Mkulu? kama huna jingine hili umetuletea si sawa.
 
mjadala wa kihuni na umeletwa na mhuni wa siasa za maji taka yanayonuka sambamba na kuumiza kifua.
 


KWA HIYO APISHWE KWENYE FOLENI??? WATANZANIA WANAJAZANA KWENYE MABASI - WANASIMAMISHWA MASAA - ETI RIZWAN KIKWETE APITE ..........HALAFU FOLENI NA MFUMO MBAYA WA PUBLIC TRANSPORT BABAKE WALA HASHUGHULIKII ........BAHATI YAKE MIE SIO TRAFFIC POLICE - NISINGEMPITISHA KWENYE FOLENI .............ANGEKAA MASAMAA - AJUE WATANZANIA WANATESEKA KIASI GANI ...

NAMSUBIRI 2015 - LABDA AHAMIE ARABUNI.................... HASTAHILI YOTE ANAYOFANYIWA KWANI BABAKE NA MARAFIKI ZAKE WAMEKULA HELA ZOTE ZA WATANZANIA .....................KODI ZOTE WAMECHAKACHUKUA - KUJIDAI KUISHI MAISHA YA KIFAHARI ......UJINGA MTUPU... MBONA WATOTO WA JULIUS KAMBARAGE WALIKUWA HAWAPANDISHI MABEGA??? KWANZA WAO NDIO WANASTAHILI KUPATA ESCORT KWANI BABA YAO KALETA UHURU TANZANIA BILA UMWAGIKAJI WA DAMU ...................... nawasilisha!!
 
Nasikia ana hisa Dowans? Mwenye data atumwagie jamvini
 

Escort ina maana kubwa kwa mtoto wa Rais
 
Ndio maana tukawaomba mumchague rais mwenye mchumba ili tusipate hasara ya magari ya ikulu kutumiwa na watoto wa rais.

Kwa hiyo mchumba akiolewa, mpaka apate mimba azae, baba anatoka madarakani mtoto bado mdogo. Uchaguzi mwingine anachaguliwa mwenye mchumba!! Lol
 
Kimsingi sishangai lakini pia ninadhani wakati sasa umefika wa sisi kujua ni maana ya kuwa mkuu wa nchi, ni maana ya first lady, nini maana ya upekee wa familia ya rais. Ridhiwan/miradji/khalfan.........wanayo haki sawa ktk upekee wa familia ya jakaya mrisho kikwete. Huu ndio msingi wa jamii kumshangaa sana mtoto wa mkuu wa nchi anaposhindwa ku behave ki upekee ktk jamii.

Tatizo ni msingi alouanzisha mzee kambarage, hakukuza hali hiyo lakini hata pale walipokuwa kilakara au mirambo ni dhahiri shule hizo zilikuwa na waalimu wengi mashushu na pia polisi na wana usalama waliwajibika kiaina.

Jingine la muhimu ni sana ambalo linalomhusu jakaya mkuu wetu" watoto wa jakaya ni vijana wachanga, waliokulia na kusomea hapa nchini, wana marafiki wengi street kama baba yao na pia mama yao mzazi/mlezi ni mwalimu wa primary hivyo naturally yuko attached na jamii direct, sasa ktk mazingira haya ya makuzi, utumishi na siasa ni lazima hawa vijana wenzetu wanalazimishwa kujitenga na jamii na only way ni vyombo vya dola kuwa front ktk kila walifanyalo ili kudhibiti usalama na pia kuhakikisha usalama wa pr yao" na tuzingatie sana hali ya kisiasa ya nchi yetu kwa sasa.

All in all ni wajibu nchi yetu kumlinda jakaya & family
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…