Richmond + TANESCO: The complete deal

Many thanks to Dr. Mwakyembe and Team!!!

At last paka kafungwa kengele ... patamu hapo
 
Nimependa hii kwenye ile sehemu ya kuangalia

"Usihangaike kujua nani kaleta, hangaika kuangalia hali halisi na kuchambua maoni ya watanzania"

You have made my day!
Inshallah,

Mwenyezi Mungu alijaalia wakafanya kuangalia hali halisi na wakachambua maoni ya watanzania badala ya kuangalia SOURCE ya hii kitu. Nimefurahi kupata pongezi toka kwa kamati husika.

Hii walau imeleta changamoto, bado BoT. Guys, we need to shout once again... Tusiridhie kuondoka kwa Ballali ilhali mambo hayajakaa sawa.

Shukrani kwa wote waliowezesha issue hii kuweza kufikia hatua hii.

Tanzania yenye neema INAWEZEKANA.

Invisible
 
Many thanks to Dr. Mwakyembe and Team!!!

At last paka kafungwa kengele ... patamu hapo

Wote tunamshukuru Invisible.

Kwa mimi ambaye sehemu ya utafiti wangu wa shahada ya uzamili inahusu sakata ka Richmond, bado naamini kuwa taarifa ya Dk. Mwakyembe na kamati yake haijasomwa na Watz, hususan wanaJF walio wengi.

Mara nyingi niko Dodoma, library ya Bunge, nikipitia taarifa ya kamati teule. Kwenye Hansard na Volume two ya taarifa hiyo kuna documents zote muhimu zinazoonyesha mapungufu makubwa ya viongozi wetu kimaadili na kiuongozi: ushahidi wa Waziri mmoja akienda nyumbani kwa Mohamed Gire (Upanga) usiku wa manane akiwa kavaa kapelo; vijimemo kutoka kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwenda kwa Waziri; maamuzi yasiyoeleweka ya kuichukua kampuni ya mwisho kukidhi vigezo, kupewa mkataba.

Ujinga wa viongozi wetu kumhangaikia mzungu, hata akiwa tarishi au mzibua vyoo; nyaraka zinazothibitisha kuwa Richmond si kampuni ya umeme bali ya kutengeneza business cards; uvunjwaji waziwazi wa sheria na maagizo ya wazi ya Cabinet, ukuwadi wa baadhi ya viongozi wetu usiojali maslahi ya Taifa n.k.! Tunahitaji mabadikiko makubwa.

Obama alisema: ni sasa si kesho na ni sisi wala si wale!
 
Huu mkataba ulikuwepo hapa muda mrefu uliopita. Kuna maswali ya watu kwenye mjadala wa Dowans unaoendelea wamekuwa wakihoji juu ya mambo yaliyomo kwenye mkataba wa Richmond. Kwa vile si vyema kuandikia mate, basi naona tutumie wino.

Niwaangalize kipengele cha 15:5 (kuhusu sheria ya nchi gani itatumika) na kipengele cha 15:14 kuhusu suala la third parties.

Please enjoy. Kuna mahali hapa nimesema uongo na ninatanguliza kukiri mapema. (just covering my behind...)!!
 
Attachments

  • Rich-Monde.pdf
    1.6 MB · Views: 215
Kama ikipatikana na ripoti ya Mwakyembe itakuwe vema zaidi kwa sababu kamati ilieleza jinsi ambavyo serikali inaweza kujipatia mitambo mipya kama hii kwa bei nafuu kutoka moja kwa moja kiwandani
 
Tusibabaishane huu utawala wa CCM na vikaragosi vyake umemaliza muda wa kuwepo madarakani, walichonacho hivi sasa ni kununua muda na kujaribu kujipanga upya,kwa kweli wasipewe muda huo wa kujipanga upya waondolewe tu,hakuna kutazama kipengele wa kikengele,muda na wakati wao umekwisha,wafunge funge na kukaa pembeni.

Watawala wanaokaribia nusu karne na hawajaweza kuiendeleza Nchi yao watawala hao hawafai ni lazima waondoke tu.Waondolewe kwa kura wakiiba waondolewe kwa nguvu

Muda wote huo Tanzania iliyojaa mito kila kona wameshindwa kumpatia mwananchi maji safi na ya uhakika, Tanzania iliyojaa uranium wameshindwa kuwapatia umeme wa uhakika tunabaki kusulubiana kwa mitambo ya watu wengine ambao wameshatuibia na kuyoyomea mbele sisi tumebaki nani aliruhusu nani alibania nani alipokea ! Yatatufikisha wapi ? Zaidi ya CCM kubadilisha na kutia rizavu mwengine.

Utawala wa CCM unatuharibia muda wetu wa kupiga hatua mbele ,hapa tulipokwama nao hatuendi mbele zaidi ya kuporomoka kwani hawana hata jipya moja watakalo kuja nalo zaidi ya ubabaishaji ,mawazo yao yamejifunga katika wizi ni vipi watafanikiwa kuanza kuiba tena ,ni vipi wavuke hewa hii inayowachafulia mirija yao.

Hivyo muda wa kujadiliana nao utafikiwa wakishaondoka kwenye madaraka ,huku wanakong'ang;ania ni kununua muda ili tusiwakurupushe katika mambo mengine ,mambo ambayo ni muhimu katika kujikwamua na shida zao.

Mambo ya kudai Katiba mpya ,mambo ya kudai tume mpya ya uchaguzi,mambo ya mahakama huru ,haya ndio mambo ambayo utawala wa CCM unajaribu kuyakwepa ni mambo ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zetu zote na baadae ndio tutaweza kupambana na CCM katika ufisadi wao,lakini kuyarukia wanayoyafanya nyuma ya pazia ni kujihangaisha.

Vyama vya Upinzani havina budi kwanza kuyadai mambo makuu hayo na yakishakupatikana ndio tuwageukie wahujumu uchumi njia yao ya kutubabaisha itakuwa ndogo sana na pengine isiwepo kabsaa ,hapo ndipo patakapokuwa patamu.
 
Kashafa ya Richamond ilipoanza ilisemekana Kampuni hiyo ni hewa na watendaji wake hawafahamiki. Kumbe hata vikao vya makubaliano na wawakilishi wa uma vilifanyika.

Huyu 'Manager' Mohamed Gire simtu hai anoweza kutueleza wenzake ni kina nani na wana uhusiano wake na Downs mpaka RA ukoje? Tukipata hilo, je? hoja ya kushindwa kufua umeme kadiri ya mkataba haitoshi kuwamilikisha TANESCO mitambo hiyo kama ilivyodokezwa kwnye mkataba huo? Nimeona kitu kama masaa 72 somewhere.

Waua nchi kweli wananchi.
 
Huyu Singi R. Madata ndiyo nani????????? Kuna mtu ana CV yake, tunaomba atuwekee hapa tafadhali.
 
haya sasa mambo yote yako OPEN, mkataba wa rich-monduli unatuonyesha jinsi viongozi wetu walivyokuwa si makini
 
wanajamii ndiyo natoka Lunch .Nimekula na mmoja wa vigogo wa Tanesco wa mkoa huu .Yeye anadai kwamba wanacho kifanya sasa kusema wazi ni just kuwapa info lakini Serikali imeamua kununua mitambo hiyo.Anasema sisi Serikali akiwa na maana tanesco ni sehemu ya serikali wamesha amua na hakuna atakaye zuia .Si Bunge wala Mbunge the game is over watu wangojee kuona transfer ya mitambo pamoja na kwamba makelele ni mengi .Mie nimebaki mdomo wazi .Yangu macho sasa
 
Tusibabaishane huu utawala wa CCM na vikaragosi vyake umemaliza muda wa kuwepo madarakani, walichonacho hivi sasa ni kununua muda na kujaribu kujipanga upya,kwa kweli wasipewe muda huo wa kujipanga upya waondolewe tu,hakuna kutazama kipengele wa kikengele,muda na wakati wao umekwisha,wafunge funge na kukaa pembeni.

Watawala wanaokaribia nusu karne na hawajaweza kuiendeleza Nchi yao watawala hao hawafai ni lazima waondoke tu.Waondolewe kwa kura wakiiba waondolewe kwa nguvu

Muda wote huo Tanzania iliyojaa mito kila kona wameshindwa kumpatia mwananchi maji safi na ya uhakika, Tanzania iliyojaa uranium wameshindwa kuwapatia umeme wa uhakika tunabaki kusulubiana kwa mitambo ya watu wengine ambao wameshatuibia na kuyoyomea mbele sisi tumebaki nani aliruhusu nani alibania nani alipokea ! Yatatufikisha wapi ? Zaidi ya CCM kubadilisha na kutia rizavu mwengine.

Utawala wa CCM unatuharibia muda wetu wa kupiga hatua mbele ,hapa tulipokwama nao hatuendi mbele zaidi ya kuporomoka kwani hawana hata jipya moja watakalo kuja nalo zaidi ya ubabaishaji ,mawazo yao yamejifunga katika wizi ni vipi watafanikiwa kuanza kuiba tena ,ni vipi wavuke hewa hii inayowachafulia mirija yao.

Hivyo muda wa kujadiliana nao utafikiwa wakishaondoka kwenye madaraka ,huku wanakong'ang;ania ni kununua muda ili tusiwakurupushe katika mambo mengine ,mambo ambayo ni muhimu katika kujikwamua na shida zao.

Mambo ya kudai Katiba mpya ,mambo ya kudai tume mpya ya uchaguzi,mambo ya mahakama huru ,haya ndio mambo ambayo utawala wa CCM unajaribu kuyakwepa ni mambo ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zetu zote na baadae ndio tutaweza kupambana na CCM katika ufisadi wao,lakini kuyarukia wanayoyafanya nyuma ya pazia ni kujihangaisha.

Vyama vya Upinzani havina budi kwanza kuyadai mambo makuu hayo na yakishakupatikana ndio tuwageukie wahujumu uchumi njia yao ya kutubabaisha itakuwa ndogo sana na pengine isiwepo kabsaa ,hapo ndipo patakapokuwa patamu.
Mwiba, hakuna kitu huwa kinaniuma kama kuona (with my naked eyes) kuwa nilizaliwa Tanzania ikiwa nchi masikini na nitakufa nikiihacha nchi masikini. Hiki kitu huwa kinaniuma sana!!
 
wanajamii ndiyo natoka Lunch .Nimekula na mmoja wa vigogo wa Tanesco wa mkoa huu .Yeye anadai kwamba wanacho kifanya sasa kusema wazi ni just kuwapa info lakini Serikali imeamua kununua mitambo hiyo.Anasema sisi Serikali akiwa na maana tanesco ni sehemu ya serikali wamesha amua na hakuna atakaye zuia .Si Bunge wala Mbunge the game is over watu wangojee kuona transfer ya mitambo pamoja na kwamba makelele ni mengi .Mie nimebaki mdomo wazi .Yangu macho sasa
...ni mchezo mchafu, wamejua kisheria mitambo hiyo ilipaswa kutaifishwa maana walioileta "waligushi" nyaraka. Sasa wamezunguka mlango wa nyuma na kuwahonga akina Rashid ili mitambo inunuliwe kabla issue ya kutaifisha haijawekwa wazi na mahakama. NAOMBA WASUBIRI MPAKA KESI YA GIRE IISHE, Pleeeese!!
 
Uamuzi huu unatokana na kauli ya Zitto.. CCM wameitumia nafasi hii kuonyesha kwamba sio wao waliopitisha kitu hiki isipokuwa ni mtu wenu mnayemwamini.. Nilijua mapema kwamba baada ya Zitto kutoa kauli ile CCM wasingechelewa kabisa kuitumia... na habari hizi nilizipata kupitia Ka nzi..zwii zwii zwii!.... tumekwisha....uchaguzi karibu sasa hivi wengi watanunuliwa bila wao kujitambua..
Maskini Zitto sasa hivi CV yake kwa wananchi tayari imeisha ingia DOA!...
 
Yaani ZITO anawambia wengine stupid wakati yeye ndio BURE kabisa, hana maana yoyote, yaani baada ya kuona tumemwamini anafikiri kila kitu tutamfuata.

Unajua sisi wote hatuwezi kuwa viongozi, sasa inapotokea walio kwenye madaraka wakaona wasio na madaraka ni wapumbavu inakuwa haina maana kabisa. Natamani kuvunja screen ya laptop yangu hapa. Yaani Zito kichwa kimemvimba anajiona yeye kila kitu anakijua yeye.

Athari ya maamuzi yao ya kuibeba Downs ni mzigo mkubwa sana kwa wanamageuzi. Sijui nyuso tutazificha wapi? CHADEMA KWISHA KHABARI YAKE. Watawambia nini tena wananchi wakati sera ya UFISADI ndio imewapandisha chati sasa wameamua kujiunga nao. Hivi hawa jamaa wamepewa kiasi gani?
 
Inabidi sasa tuonyeshe kwa vitendo kuwa hatupendi na hatuwezi kuvumilia vitendo vya kifisadi. Lazima tuwatangazie mafisadi wote wakae wakijua kuwa ni maadui na hatuwaruhusu wachukue advantage ya unyonge wetu kutuhadaa kila mara bila hata chembe ya aibu.

Kwanza tujiulize kwa nini wanakuwa na jeuri hii - ni kwa sababu tuna huruma nao, tunawavumilia, tunakaa nao , tunakula nao na wengine wao tunalala nao. Mafisadi ambao ni watu wa kutengwa sasa tunakaa na tunacheka nao iwe kwenye misiba, harusi na tafrija mbali mbali.

Kanisani tunasali nao, Misikitini tunaswali nao na tukitoka hapo hatuoni tena tofauti kati yetu nao. Kazini tunashinda nao na tumewaruhusu hadi leo hii bungeni wanatuwakilisha. Tunashuhudia wakitoa hoja zenye malengo yaliyojificha na kuzima ama kubeza hoja pinzani.

Leo wanajitokeza wazi wazi - baada ya kuona hatuwachomi moto kama vibaka, hatuwazomei kama wapuuzi, hatuwatengi kama wagonjwa wa ukoma na sasa hawaoni tena haja ya kujifichaficha. Ngamia tumemruhusu akaingiza kichwa, miguu na sasa anaingia mzima mzima.

Sasa hapatoshi na lazima tuamue kusuka ama kunyoa - juzi tulinunua ndege chakavu, leo tunanunua mitambo ya umeme chakavu na kesho tutanunua shirika chakavu - kisa ? Ufisadi umehalalishwa na sasa ni ruksa kufanya nao biashara hata kama ni biashara kichaa.
 
Mada kama hizo ndio za kujadiliwa kipindi kama hiki cha mgao wa umeme! Hapa nilipo joto linanitesa katika jiji la Lukuvi, huku wehu walioua mitambo ya umeme wakikenua tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom