Richmond + TANESCO: The complete deal

*Kambi za mapambano Richmond zajipanga
*SHELLUKINDO AAPA HAKUNA ATAKAYEJISAFISHA

Ramadhan Semtawa
Mwananchi
Oct/19/2009


WAKATI serikali ikisubiriwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Kampuni ya Richmond Development (LLC) kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kuna taarifa kuwa baadhi ya vigogo waliohusika wameanza mikakati mizito ya kujisafisha katika bunge lijalo.

Mkutano wa 17 wa Bunge unatarajiwa kutawaliwa na mzimu wa Richmond, ambayo ilipewa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006 kwa njia ambazo zilionekana kukiuka taratibu na kusababisha Bunge liunde kamati teule iliyotoa taarifa ambayo ilisababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu.

Katika mkutano wa 16 wa bunge mjini Dodoma serikali ilijaribu kuwasafisha maafisa wake waandamizi, mpango ambao ungewasafisha pia mawaziri waliojiuzulu, lakini bunge likagoma na kurejesha taarifa hiyo kwa kutaka maafisa hao wawajibishwe.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vya kuaminika vimedokeza kwamba vigogo wenyewe waliohusika kwenye kashfa hiyo na wanaotajwa kama wamiliki, wana mpango mzito wa kuhakikisha wanajisafisha.

Lakini mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo, ambaye ni mbunge wa Bumbuli, aliiambia Mwananchi akisema: "Maazimio ya bunge hayarudi nyuma na hukuna fisadi atakayejisafisha.

"Kama kuna mtu alipaswa kujitetea na kutaka kujisafisha ilikuwa ni kipindi kile kile ambacho bunge lilikuwa likijadili na wakati wa uchunguzi. (Kwa sasa) hakuna mtu wa kurudisha nyuma maazimio ya bunge."

Shellukindo alifafanua kwamba, kamati inasubiri taarifa hiyo ya serikali ambayo inatarajiwa wiki hii na kusisitiza: "Tumejipanga kuhakikisha suala hili la Richmond linakwisha."

Aliweka bayana kwamba kamati haitakubaliana na hadithi zozote katika mambo ya msingi ambayo ni utekelezaji wa maazimio ya bunge katika taarifa ya serikali.

"Hawawezi kujisafisha tena bungeni, maazimio ya bunge yanakwenda mbele. Walitakiwa kujitetea wakati ule, sisi tunasubiri kwanza ripoti; nasema tunataka tumalize (suala la)Richmond."

Shellukindo alifafanua kuwa mtu yeyote mwenye ajenda ya namna hiyo ajue kabisa atakwama kwani Richmond inakwenda ukingoni.

Habari za kuaminika zinaeleza kuwa vigogo walioandaa mpango wa kujisafisha ni wale ambao waliwahi kuwa na nyadhifa serikalini.

Ingawa tayari watu wote waliotajwa kwenye Richmond walishazungumza, wengi hawaridhiki na maazimio ya Bunge.

Tayari Rostam Aziz, ambaye alitakiwa kuhojiwa na kamati teule kama anahusika kwenye kashfa hiyo baada ya namba za simu za ofisi yake kutumiwa na Richmond, ameshatamka hadharani kutohusika kwake na sakata la Richmond, lakini amekuwa haridhiki na maamuzi ya bunge kuhusu sakata hilo.

Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, ambao walijiuzulu uwaziri kutokana na taarifa ya kashfa hiyo, walishatoa maelezo yao bungeni na nje ya bunge huku Dk Msahaba akisema kama kuna ushahidi apelekwe mahakamani.

Lakini, vyanzo hivyo viliongeza kwamba, baadhi ya watuhumiwa hao (majina yao tunayo), wanajipanga kutumia mkutano ujao wa Bunge kujisafisha kutokana na malengo yao ya kisiasa.

Suala kama hilo liliwahi kujitokeza mwaka jana wakati wabunge walipoanza kuhoji masuala mbalimbali kwenye taarifa ya kamati teule, lakini aliyeongoza kamati kwenye uchunguzi huo, Dk Harrison Mwakyembe aling'aka na kuhoji sababu za Bunge kuanza kurejea kwenye hoja ambayo ilishajadiliwa na kutolewa maamuzi.

Ilifikia wakati Dk Mwakyembe alilazimika kutishia kuanika mengi zaidi ambayo alisema waliyafunika kwa maslahi ya taifa kama wabunge wangeendelea kujadili suala ambalo lilishatolewa maamuzi na chombo hicho cha kutunga sheria.

Hata hivyo, habari zinadai kuwa tayari vigogo hao wamekutana katika vikao mbalimbali vya siri wakipanga mkakati huo.

Tangu kusainiwa kwa mkataba wa Richmond Juni 23, 2006 na Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu, bunge limewagawanyika kutokana na baadhi kuunga mkono maazimio na wengine kupinga. Mgawanyiko huo umesababisha kundi moja kujiita kuwa ni vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi na jingine likipinga vita hiyo kwa madai kuwa inaichafua serikali ya CCM na chama chenyewe.
 
mie nina mikataba yote..namba yangu ni 0754 77 77 77,waambie hata usalama,
am tired with this bullshit kabisaaaaa,bora kuwa Mungiki tu
Kila nikipiga namba hii sauti inatoka kama ya Mheshimiwa flani ana nywele nyeupe, ni wewe kweli mkuu?
 
Nyaraka kama hizi tunazihitaji sana wana JF. Asante sana Invisible kwa kutuwekea vitu hivi live bila chenga
 
Back
Top Bottom