Richmond: Sitta anahusika pia?

nyie wa Tanzania Daima mnatumiwa na mafisadi? mbona kila siku mnatueleza mabaya ya Sitta tuu? Mbona siku hizi Lowasa, Chenge na Rostam kwenu hatajwi?
 
Inashangaza sana Samuel Sitta anaposifiwa na kuonyeshwa kuwa ni mtu mahiri, mwenye staha ya kuwa Rais.

Akiwa Waziri wa Ujenzi alifanya nini?

Alipokuwa CDA alifanya nini cha maendeleo kugeuza Dodoma kuwa mji mkuu na mkoa wenye maendeleo?

Alipokuwa Mkuu wa Mkoa alileta maendeleo ya namna gani?

Alipokuwa TIC, aliliongoza vipi Taifa letu kuingia katika mfumo wa soko huria na utandawazi na uwekezaji?

Kama Spika wa Bunge, ameleta mapinduzi gani?

Je anafaa kuwa Rais wetu?
 
Kufaa ama kutofaa hakutokani na alifanya nini, kwani Mwinyi, Mkapa na JK walifanyanini kabla hawajachaguliwa?.

Kwa maoni yangu, pamoja na mapungufu yake yote, bado anafaa zaidi kuliko aliyepo, tatizo by 2015 he'll be bypassed by time.
 
Mh! Samweli hata haeleweki
 
Kufaa ama kutofaa hakutokani na alifanya nini, kwani Mwinyi, Mkapa na JK walifanyanini kabla hawajachaguliwa?.

Kwa maoni yangu, pamoja na mapungufu yake yote, bado anafaa zaidi kuliko aliyepo, tatizo by 2015 he'll be bypassed by time.

Pasco.... Mwinyi, Mkapa na JK hawajafanya chochote. Tulifanya makosa kutowauliza walifanya nini katika nyadhifa zao za awali kabla hawajawa marais.
Kwa maoni yangu, kiongozi alifanya nini huko nyuma kunapelekea kabisa kueleza kama kiongozi anafaa au hafai. Kama JK alikuwa ni waziri mbovu, tutegemea nini ktk urais wake?
 
Kama Spika 6 ni msafi katika kuwasiliana na Kampuni hewa na kukaribishwa lunch na mmiliki wake, basi sioni sababu ya kumlaumu Rostam kwa kuwa anwani yake ilitumiwa na kampuni hiyo! Ni sawa na kumlaumu Hoseah kwa ripoti yake na kuisifu ile ya Mwakyembe pamoja na kwamba aliliambia taifa kwamba kuna mambo aliyaacha (haijulikani ameyahifadhi kwa ajili ya familia yake au kwa ajili ya kutumia kama fimbo ya kisiasa wakati utakapofika)! Tusiwe makengeza pindi tuhuma zinapoanza kuchukua mkondo mpya! Tupigane na ufisadi kama ulivyo na sio kupigana na watu (we against them)!
 
Mimi sioni jipya hapa kwani kama unasoma report ya kamati ya Mwakyembe utaona ilitamka kuwa Richmond waliwahi kupewa tenda ya bomba la mafuta huko Mwanza na walishindwa hiyo tenda, na hii ni miongozi mwa sababu ambazo akina Mwakyembe waliwatuhumu akina Lowassa kuwa walipaswa kujua kuwa hiyo kampuni haina Uwezo. Kama kuna mwenye report ya Mwakyembe atubandikie sehemu inayosema habari za bomab la mafuta. Kwa hiyo hii sio habari mpya ile imekuja na kichwa cha habari kipya.

sasa basi kama walipewa tenda ya kujenga bomba la mafuta lazima kulikuwa na mtu alihusika kutoka upande wa TZ, issue muhumi ni kuwa je huyo muhusika alihusika kwa njia chafu? tuangalie je alicheza rafu? Kama alikuwa sita na kituo cha uwekezaji na walifanya vizuri kwa mujibu wa sheria na sio kama walivyofanya akina Lowassa then Sitta apewe heko na Akina Lowassa Ziii!
 
Old news I may say, hawa Tz Daima wana-refer topic hii ya mwezi Oktoba: Richmond: Sitta anahusika pia?

Bandiko hilo liliwekwa na Zalendohalisi.

Halafu hawajatoa hata credit walau kwa kutaja doc hiyo waliinyonya JF.

Kazi kwelikweli, lakini nawashukuru wana JF kwa kuweka source za kila inapotoka info yoyote ili kutoa credit kwa wenye kuwa chanzo cha habari.
 
Na wewe naye unaboa

almost miaka miwili mfulululizo nakuambia dawa ya haya magazeti na waandishi wao uchwara ni kuwa expose wewe uliamua kuchukua softly softly approach

kiko wapi sasa?
 
Pasco.... Mwinyi, Mkapa na JK hawajafanya chochote. Tulifanya makosa kutowauliza walifanya nini katika nyadhifa zao za awali kabla hawajawa marais.
Kwa maoni yangu, kiongozi alifanya nini huko nyuma kunapelekea kabisa kueleza kama kiongozi anafaa au hafai. Kama JK alikuwa ni waziri mbovu, tutegemea nini ktk urais wake?
Tunachagua kwa curent merit, sio past legacy, nikikuuzia sera za kwenye ilani yangu, ukanikubali, hii ijajustfy kunichangua, issue ni kama nikishindwa kutekeleza kile nilichoahidi. JK bado hajashindwa ila amechelewa kidogo tuu, hiyo miaka mitano ijayo tutampa tena ili amalizie na kuacha legacy.
Legacy ya Nyerere ni Freedom na Unity
ya Mwinyi ni Mzee wa Ruhksa
Ya Mkapa ni Mr Clean
Tusubiri ya ya JK aka Mr. Trips.
 
Mugongo Mugongo huko nyuma alisema hivi kuhusus huyu bwana:

1. Samuel Sitta – now, this is the epitome of hypocrisy. How can a man, with straight face, pose as a champion of virtues and ethics while his entire life is defined by unremarkable political achievements and countless allegations of abuse of office at TIC, in Bunge office and everywhere?

He has screwed up, and inserted himself as the main news item, in every major issue that has come before the Parliament. However, in this ongoing theatre, you have to give him credit for wrestling the Parliament from CCM's control and for using the Speakership to build his own little empire of patronage and clientelism.

At the moment, he is one of, if not THE, most powerful men in Tanzania . He coordinates his political mischief with Mr. Reginald Mengi, a tax-evading divorced showman with taste for younger women, to ensure that those scandalized in the Parliament get similar treatment in the media.

all of a sudden amekuwa hero wa the so called "WAPIGANAJI" ndio maana nikauliza kwenye ile thread nyingine hivi hawa wapiganaji wanataka kutufanya sisi wajinga au vipi?

I weje one minute wanasema CCM WOTE MAFISADI then on the next say wanasema kuwa Sitta ni mpiganaji mwenzao?
 
Inashangaza sana Samuel Sitta anaposifiwa na kuonyeshwa kuwa ni mtu mahiri, mwenye staha ya kuwa Rais.

Akiwa Waziri wa Ujenzi alifanya nini?

Alipokuwa CDA alifanya nini cha maendeleo kugeuza Dodoma kuwa mji mkuu na mkoa wenye maendeleo?

Alipokuwa Mkuu wa Mkoa alileta maendeleo ya namna gani?

Alipokuwa TIC, aliliongoza vipi Taifa letu kuingia katika mfumo wa soko huria na utandawazi na uwekezaji?

Kama Spika wa Bunge, ameleta mapinduzi gani?

Je anafaa kuwa Rais wetu?

naona unataka kufukua makaburi hapa

kwanza ushafika kwenye ile ofisi yake ?

Ukishafika ulikaribishwa kwenye sitting room ipi? umeona lile JITANDA analolalia pale ofisini? Jiulize yumba viwili vya kulala ofisini vya nini?

if anything huyu mzee ana taste kama AL MARHUM gavana BALALI ambaye ofisi yake mpaka leo Ndulu anaogopa kukaribisha wabunge maana inatisha kwa samani na manjonjo

ohh kabla sijasahau unajua lile Carpet ale bungeni Dom lilinunuliwa Spain? sasa jiulize kiasi gani na kamisheni ya Sitta ilikuwa kiasi gani

Na mbaya zaidi ina bendera ya taifa ambayo kila kukicha inakanyagwa bila wasi wasi

shows how out of tuch wabunge wetu walivyo
 
Kufaa ama kutofaa hakutokani na alifanya nini, kwani Mwinyi, Mkapa na JK walifanyanini kabla hawajachaguliwa?.

Kwa maoni yangu, pamoja na mapungufu yake yote, bado anafaa zaidi kuliko aliyepo, tatizo by 2015 he'll be bypassed by time.

Lakini si unaona matokeo ya kuto kuangalia past records za watu wanao tafuta uongozi? Hayo majina uliyo yataja sasa yaliishia kufanya nini walipo ukwaa uraisi?
 
Hivi motive ya hii thread ni nini? Kwani Sitta ametaka Uraisi? je ni muda muafaka wa kumwongelea Spika wakati matatizo lukuki bado hajawa resolved, au ndio njia ya ku-distract watu kutoka kwenye issue za kweli tunazo pambana nazo kwa sasa? mbona tunataka kurushana madarasa wakati hesabu za darasa la pili bado hatuziwezi au wengi wetu hatuziwezi?
 
Jamani huu sasa ni upuzi wa hali ya juu. Samweli Sita wakati akiwa mkurugenzi pale TIC alikuwa na jukumu la kuongea na kuwasikiliza watu wote waliokuwa wakija nchini kwa lengo la kuwekeza. Sita aliwasikiliza wawekezaji na kuwatambulisha kwa makampuni husika na wala si kuingia mikataba na hao wawekezaji. Sasa kwa hapa kosa la Sita ni lipi?
 
Anawakaribisha bila kujiridhisha na uhalali wa Kampuni yenyewe? Anyway, uwekezaji wenyewe nako ni "wizi in disguise", if you like! Mkapa mwenyewe anajuta kuwaalika wezi (jina zuri la wawekezaji) kuja kupora rasilimali zetu! Wakati Mkapa anajutia vitendo hivyo JK yuko busy kuwaalika wezi kuja kuendeleza uporaji! Hivi watu kabla ya kuingia Ikulu huwa wanaacha akili zao nje ya Ikulu na kuzirudia wakati wanatoka huko? Simwelewi kabisa JK kwa kuwaalika wezi kuja kupora mali zetu!
 
Back
Top Bottom