Vikao vya Bunge kurejea tena Agosti 29, 2023, Miswada miwili kujadiliwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mkutano wa 12 wa Bunge unaoanza kesho unatarajia kujadili miswada miwili na maazimio matatu.

Ratiba ya Bunge iliyotolewa leo Agosti 28, 2023 inaeleza kuwa mkutano huo utafanyika kwa muda wa wiki mbili kuanzia kesho Agosti 29 hadi Septemna 8, 2023.

Kesho wabunge wataanza na kupokea taarifa ya Spika, maswali ya wabunge na muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba mbili wa Mwaka 2023.

Siku ya Jumatano wabunge wataanza na Maswali kisha Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya kuridhia Katiba ya Tume ya Usafiri wa Anga ya Afrika ya Mwaka 2009 na Alhamisi kutakuwa na Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakati Ijumaa itakuwa ni kipindi cha maswali tu.

"Jumatatu utakuwa na Maswali kisha Taarifa ya Kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusu Changamoto na Malalamiko yaliyojitokeza katika kutekeleza Mkataba wa mauziano ya Matrekta ya Kampuni ya Ursus kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Wakulima kwa Utaratibu wa Mikopo na taarifa ya Kamati ya Sheria Ndogo," inasema taarifa hiyo.

Miswada mwingine utakaowasilishwa ni Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 kabla ya Ijumaa kuwa na maswali na hoja ya kuahirisha Bunge.
 
Back
Top Bottom