Richmond: Sitta anahusika pia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond: Sitta anahusika pia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Oct 25, 2009.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  WAKATI tukielekea katika Mkutano wa 17 wa Bunge unaoanza keshokutwa Jumenne Oktoba 26, 2009, tujikumbushe yaliyojiri Mkutano wa Kumi na Saba miezi michache iloyopita haswa Agosti mosi, 2009 siku ambayo Kamati za bunge ziliwasilisha taarifa zao ikiwamo ile kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Kwa kuwa sasa gumzo ni Dk. Edward Hosea wa TAKUKURU, nimeweka msisitizo katika Azimio namba 20 la Bunge, ambalo kamati hiyo ilimsafisha Hosea, ili tuone kama watabadili msimamo wao ama watatoa maelezo?

  Katika maelezo ya kamati yaliyosomwa na Shelukindo, walikubaliana na maelezo ya serikali kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa kisheria uliofanywa na TAKUKURU kwa kusema, "Mheshimiwa Spika Kamati inaridhika na taarifa hiyo."

  Tuisome kwa makini taarifa hiyo tuone UADILIFU wa WABUNGE WETU.

  Kwa heshima ya mdau mmoja hapa JF nimeambatanisha na barua ya Sitta kwenda kwa Gire (wakati akiwa TIC).

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Tina ahsante sana kwa kuiweka ripoti hiyo hapa. Nilitaka niiweke hapa lakini ni file kubwa sana lina page 78. Nimeisoma page chache za mwanzo lina mambo mazito sana inabidi kutafuta muda na kulisoma file lote. Kwa mara nyingine ahsante sana.
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Balaa!
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Thanks Tina, ngoja nipitie 'highlighted section', najua ndo penye content muhimu!
   
 5. Zalendohalisi

  Zalendohalisi Senior Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good job Tina;
  Ninakubaliana nawe fika, hasa kuhusu swala la sisi watanzania wengi kutokusoma taarifa kwa makini. Nilifanikiwa kuipata nakala ya taarifa halisi aliyosiniwa na Mheshimiwa Shelukindo na kuisoma kwa makini hasa nikitafuta yale ambayo yanahusu yafuatayo:
  1. Kuwepo kwa rushwa kwenye mchakato mzima wa ulioipa zabuni kampuni ya Richmond Development Company
  2. Kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa kampuni ya Richmond Development Company
  3. Kuharibiwa nakubadilishwa kwa ripoti halisi ya uchunguzi kuhusu rushwa katika mchakato ulioipa kampuni ya Richmond Development Company zabuni ya kufua umeme.
  4. Kutokuwepo kwa kampuni ya RDEVCO, LLC na ile Richmond Development Company.

  1. Nashangaa kusoma kwenye ripoti ya kamati haya yafuatayo
  Labda mimi ndiye sielewi linalosemwa na kamati na hata wabunge kulipigia makofi. Kama hapakuwepo dalili za rushwa wala mazingira ya rushwa wakati wa kufanya machakato, kazi aliyosimamia ndugu Madata na ni kwa kuhisi kuwepo kwa rushwa ndiyo maana TAKUKURU ilibidi waitwe kufanya uchunguzi. Sasa ikiwa wao wenyewe wanawasilisha taarifa inayosema kuwa hakukuwepo mazaingira na wala dalili za rushwa ni kwa vipi TAKUKURU na hasa Dr. Hoseah walililia damu yake?

  2. Kamati inakubaliana na uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusu allegations za kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa Richmond Development Company na pia kuharibiwa na kughushiwa ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya rushwa uliofanywa na TAKUKURU.
  3. La kusikitisha ni hili la kung'ang'ania kuwa kuna tofauti kati ya Richmond Development Company na REDVCO LLC; na kwa hili TAKUKURU wanasulubiwa eti walizembea kuona hiyo tofauti.

  Naambatanisha copy ya nyaraka walizotumiwa BRELA na Ubalozi wetu Marekani ili kuliweka bayana hilo, na BRELA aidha wameminya au waliwawapa kamati na kamati imeshindwa kuliweka wazi kuwa, Richmond Development Company is an assumed name for REDVCO LLC.

  Labda wataalamu washughuli za kusajili makampuni watusaidie kutueleza hili la assumed name, je lina maana kuwupe kwa makumpuni mawili au jina tu la kibiashara? TAKUKURU walisema hili nawakaambiwa hawajui kazi.

  Kama vile Tina livyoshauri naomba mziangalie hizi nyaraka kwa uangalifu na kuona jinsi tunavyodanganywa na hizi kamati za kisiasa. Nyaraka hizi hata Bibie Condi Rice amezikubali kuwa ni authentic ila kamati ya waheshimiwa wa bongo wanasema ni za kughushi!

  La mwisho ni la kujiuliza kuwa hivi ni nani aliyewaleta Richmond hapa nchi kwa mara ya kwanza, Rostam Aziz au Samwel Sitta. Hebu angalia kwa ungalifu (Zoom kweye kibao cha jina la Samwel Sitta likiwa limetinga mezani) na pichani akiwa amekaribishwa na Mohamed Gire kaka yake Adam Gire (mshatikwa wa Richmond hapa nyumbani). Picha zingeni nazihifadhi kwa sasa!

  Ndugu Sitta wakati huo alikuwa ni CEO wa TIC na hapo anaonekana akikutana na wawekezaji wa Richmond kwenye ukumbi wa Greater Houston Convention and Visitors Bureau (GHCVB) ambao Mohamed Gire ni mmoja wa wamiliki wa ukumbi na bureau hiyo; http://www.rdevco.com/mohamedgire.html.

  Pia naambatanisha copy ya FAX ambayo ndugu Sitta analimtumia Mohamed Gire wa Richmond Development Company na kumwambia andike hiyo barua ya recommendation aliyoiomba toka TIC kwenda AEC, yaaani aiandike jinsi anavyotaka yeye mwenyewe halafu yeye Sitta kama Executive Director wa TIC atamwaga sahihi tu! Inatisha, jama inatisha.

  Ila ndugu Sitta analalama kuwa ndugu Gire pia ana mahusiano na Mr. Sela kitu ambacho inaonekana hakimpendezi bwana mkubwa! ........

  Au ndiyo maana Mheshimiwa Spika alilivalia njuga sakata la Richmond?
  Just a wild guess.

  ZalendoHalisi

  BTW AEC ni : African Economic Community na Tanzania ni washiriki wazito tu
   

  Attached Files:

 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mungu wangu, mimi simo naona mambo yanazidi kunoga kuelekea BUNGE LIJALO
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  sasa sijui kuna nini kipya kitaibuka huko, najua moto utawaka, na sasa hivi nasema CCM hakuna kuitana pembeni na kukanyana, safari hii ni unyama unyama tu. Wabunge okoeni nchi yenu jamani
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nadhani wengi hawajaona kilichomo humu ndani!!! Kazi kweli kweli
   
 9. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Jamani hata mzee Six???? Kumbe Rich Monduli ni dude la ajabu sana eheee??!!!! Haya tutaona mengi mwaka huu
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kila chenye mwanzo kina mwisho
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Lakini hakuna jipya kutoka kwa wabunge. KWANI WAMESHALAINISHWA apunguze kasi ya kuisulubu Serikali.
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Richmond kila siku kuna kitu gani kipya au kelele tu. Watu walioiba wawekwe jela, utaratibu wa tender ubadilishwe na bunge lianze kujadili vitu vya maana hatuwezi kutumia miaka zaidi ya miwili kuongelea kitu kimoja. Mikataba mibaya iko kila siku na si Richmond pekee!. I am sick of this shit
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu sita kila siku mi nasemaga hapa hana lolote la maana sasa kiko wapi.naye ni fisadi tu
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na huyo sita awekwe jela maana naye alikuwemo kwenye mchalato kumbe haaaaa
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Tina, nakupongeza sana kuhusiana na uchangiaji wako hapa ukumbini. Maana ni mmoja wa akina dada wachache sana hapa jukwaani wanaoshiriki sana katika jukwaa hili la siasa na hasa haya mambo ambayo yameikumba nchi yetu katika miaka hivi ya karibuni ya ufisadi.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Oct 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani sii katika maelezo ya kwanza ktk ununuzi wa mitambo ya Dowans tuliambiwa Dowans hawajapewa hata senti moja? hii tena imetoka wapi?..
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ...what happened bungeni?...
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Haya kule dodoma kulikoni rich?
   
 19. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #19
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Hivi hakuna anayefuatilia Bunge kwa karibu mida hii?
   
 20. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Yanini twaandikia mate na wino upo, tuombe uzima na afya njema tutaona hayo yatakayojiri, kila la heri
   
Loading...