Bunge la 12, Mkutano wa 14, Kikao cha 1, Januari 30, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkutano wa 14 wa Bunge la 12 umepangwa kufanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia leo Januari 30, 2024 hadi tarehe Februari 16, 2024. Taarifa ya Bunge imeeleza kuwa Mkutano huu umeongezewa wiki moja kutokana uzito wa majukumu yaliyopangwa ikiwemo uzito wa Miswada itakayoshughulikiwa.

Miswada ambayo imepangwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.

Miswada mingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023.

Vilevile katika Mkutano huu wa Bunge Kamati za Kudumu za Bunge zitawasilisha taarifa za shughuli zilizotekelezwa na Kamati kwa mwaka 2023.

Aidha, wastani wa Maswali 250 ya kawaida na Maswali 24 ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge.


View: https://www.youtube.com/live/1sfGD-2aEIM?si=x6df0J9zzq_ITXmI
bf06f0d1-650b-47f0-9f8e-199a505b09a6.jpg



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikiwasilisha taarifa yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 imependekeza kusiwe na ulazima wa Sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi au Wasimamizi wasaidizi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwasababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa Uchaguzi

Wadau mbalimbali hawakubaliani na suala la Wakurugenzi wa Halmashauri na Watumishi wa Umma kusimamia Uchaguzi kwa kuwa hawawajibiki kwa Tume ya Uchaguzi bali wanawajibika kwa Rais na Chama Tawala hivyo wanakosa sifa ya kuwa Mamlaka ya Uchaguzi Huru na Haki. Vifungu hivyo vifutwe na Tume iajiri Watumishi wake wenyewe.

da2c2d55-7084-4d75-b070-9be4ebc62cc7.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom