Halima Mdee: Serikali Imepuuza na Kukiuka Maagizo ya Bunge ya Kuwafukuza kazi Wezi wa Fedha za Umma Waliotajwa na CAG

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,073
49,761
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC bi Halima Mdee ameishutumu Serikali Kwa Kukiuka na kupuuza Maagizo ya Bunge yaliyotolewa kwenye maasimio kuhusu washukiwa wa Ufisadi Waliotajwa na CAG.

============

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee amesema hakuna azimio la kamati hiyo lililotekelezwa kwa ukamilifu katika mamlaka za serikali za mitaa.

Mdee ameyasema hayo leo Jumanne Juni 27, 2023 akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Bunge yatokanayo na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ukaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kwa masikitiko makubwa naomba kulijulisha Bunge lako kuwa, hakuna azimio hata moja lililotekelezwa kwa ukamilifu. Hali hii imetokana na uzembe wa makusudi uliofanywa na baadhi ya maafisa masuuli katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kudharau maazimio yaliyotolewa na Bunge.

"Hata hivyo, uchambuzi uliofanywa na Kamati katika Taarifa zote mbili umebaini kuwa, mengi yaliyoelezwa na Ofisi ya Rais –Tamisemi, ni ufafanuzi tu wa hoja wa namna ya kutekeleza maazimio hayo badala ya utekelezaji wenyewe. Vilevile, kwa kiasi kikubwa, maelezo yaliyotolewa hayaendani na maazimio yaliyotolewa na Bunge,"amesema Mzee.

Mwananchi

=============

Bunge likiazimia Serikali iwafute kazi washukiwa wote badala yake haijafanya hivyo ila imewashusha vyeo na kuwahamisha Vituo vya kazi huku wakiendelea kulipwa Mshahara ule ule wa Wakuu wa Idara..

My Take:
Bunge Kibogoyo haliwezi kujisimamia Serikali matokeo yake ndio hizi dharau,Mafisadi wanaendelea kupeta..

Mwigulu aliwahi pendekeza wezi wasiishie tuu kushushwa vyeo Bali wafukuzwe au warudishwe kwenye scale ya salary ya zamani kabla ya kuwa naadaraka.
 
Kama Serikali inadharau wawakilishi wa Wananchi ni wazi Kuna haja ya haraka ya Katiba Mpya,Ufisadi sio swala la kuchekelea maana ni Kodi zetu hizo.
 
Yeye anaona kibanzi kilichoko kwenye macho ya wengine mbona wao covid uwepo wao unavunja katiba na serikali imekaa kimya
 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC bi Halima Mdee ameishutumu Serikali Kwa Kukiuka na kupuuza Maagizo ya Bunge yaliyotolewa kwenye maasimio kuhusu washukiwa wa Ufisadi Waliotajwa na CAG.

============

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee amesema hakuna azimio la kamati hiyo lililotekelezwa kwa ukamilifu katika mamlaka za serikali za mitaa.

Mdee ameyasema hayo leo Jumanne Juni 27, 2023 akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Bunge yatokanayo na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ukaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kwa masikitiko makubwa naomba kulijulisha Bunge lako kuwa, hakuna azimio hata moja lililotekelezwa kwa ukamilifu. Hali hii imetokana na uzembe wa makusudi uliofanywa na baadhi ya maafisa masuuli katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kudharau maazimio yaliyotolewa na Bunge.

"Hata hivyo, uchambuzi uliofanywa na Kamati katika Taarifa zote mbili umebaini kuwa, mengi yaliyoelezwa na Ofisi ya Rais –Tamisemi, ni ufafanuzi tu wa hoja wa namna ya kutekeleza maazimio hayo badala ya utekelezaji wenyewe. Vilevile, kwa kiasi kikubwa, maelezo yaliyotolewa hayaendani na maazimio yaliyotolewa na Bunge,"amesema Mzee.

Mwananchi

=============

Bunge likiazimia Serikali iwafute kazi washukiwa wote badala yake haijafanya hivyo ila imewashusha vyeo na kuwahamisha Vituo vya kazi huku wakiendelea kulipwa Mshahara ule ule wa Wakuu wa Idara..

My Take:
Bunge Kibogoyo haliwezi kujisimamia Serikali matokeo yake ndio hizi dharau,Mafisadi wanaendelea kupeta..

Mwigulu aliwahi pendekeza wezi wasiishie tuu kushushwa vyeo Bali wafukuzwe au warudishwe kwenye scale ya salary ya zamani kabla ya kuwa naadaraka.
yeye mwenyewe yuko bungeni kwa sababu ya uwepo wa rushwa na ufisadi nchini. Kama si hivyo asingekuwemo bungeni. Aanze kuondoka yeye!
 
Back
Top Bottom