Kumbe mwamba kwenye mishe serious unaamini uwepo wa Mungu na kumtakia kiumbe wa Mungu pumziko jema hongera kwa hiloRIP Valentina.
Nilikuwa na matani naye sana!
Haha wenzako tunasocialize nje ya JF kitambo na ni zaidi ya miaka 13 sasa tangia tufahamiane. Binafsi nakiri kwamba Valley alikuwa vyanzo vya mimi kujiunga na JF tukiacha kuingia na kujisomea tangia ikiitwa Jambo Forum.Watu wanajuanaje humu kiasi wakiaga dunia taarifa zao huletwa? Ila wengine humu wakiaga dunia ndio basi, hakuna atakayejua
Hakuna nilipomtaja Mungu acha fujo msibani.Kumbe mwamba kwenye mishe serious unaamini uwepo wa Mungu na kumtakia kiumbe wa Mungu pumziko jema hongera kwa hilo
NB: Sote ni wa Mungu na kwake tutarejea
Nipe maana ya RIPHakuna nilipomtaja Mungu
Ooh!! My dear good friend!!Mimi. Sina maneno mengi ya kuandika ilaa nima huzuni kubwa juu ya taarifa ya msiba juu ya mpendwa wetu Valentina 😭😭
Wengi wetu tunamjua kwa kuunganisha watu na kujenga upendo katikati ya chuki na hasira, lakini leo Mungu amempenda zaidi.
Nitatoa updates kadri nitakavyojaliwa.
Rest in Peace. Pumzika kwa Amani.Nipe maana ya RIP
Kumbe amefariki kutokana na changamoto za uzazi 💔Taarifa ya Msiba 🕊️
Kwa huzuni kubwa tunapenda kutangaza kifo cha mwenzetu @Valentina Jf 💔, ambaye amefariki dunia baada ya kuingizwa kwenye operesheni katika Hospitali ya Babuu Mkoani - Arusha
Madaktari wamefanikiwa kumwokoa mtoto wa kiume, ambaye anaendelea vizuri.
Taarifa kamili kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tunaomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja familia pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 💔
Which peace?Rest in Peace. Pumzika kwa Amani.
Hakuna Mungu hapo.
Ukifa unaondokana na matatizo yote ya maisha unapumzika kwa amani.
Ila wewe kwa sababu hujui kusoma kwa ufahamu, unasoma kitu ambacho hakipo.
Unalazimisha kuona Mungu sehemu ambayo hajaandikwa.
Mpaka sasa unanichafua sana kwa sababu Valentina ni mtu niliyeishi naye poa sana hapa JF halafu unaleta mabishano ya kijinga kwenye uzi huu wa msiba.
Mungu apumzishe Vallentin namfahamu kwa sehemu ( moyo wake mzuri sana, na kwa mwenza wake alie kuwa rafiki yangu )Taarifa ya Msiba 🕊️
Kwa huzuni kubwa tunapenda kutangaza kifo cha mwenzetu @Valentina Jf 💔, ambaye amefariki dunia baada ya kuingizwa kwenye operesheni katika Hospitali ya Babuu Mkoani - Arusha
Madaktari wamefanikiwa kumwokoa mtoto wa kiume, ambaye anaendelea vizuri.
Taarifa kamili kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tunaomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja familia pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 💔
Alikuwa anatamani sana tukutane, ila ratiba zangu hazikuwahi kuwa easy. Kila akiwa Dar Mimi nakuwa mkoani mpaka nilipohama mazima Dar. Alinialika Arusha, ila sikuwahi pata route ya kule.Nina deni kubwa kwa Valentina na sijui nitalilipaje.. Labda kwa kichanga alichokiacha😭 Mungu nisaidie🙏🏿
Marehemu Valentina ndiye Mwana JF wa kwanza kufanya naye mawasiliano ya simu wayback 2013... Baadae nikawa mmoja wa wana JF aliowashirikisha kwenye fursa mbalimbali za kutafutq pesa na ajira.. Alipenda sana kuwa mbunifu wa fursa za pamoja japo nadhani wengi kama si wachache hawakumuelewa..
Tuliendelea kuwasiliana na akatamani tuonane ana kwa ana.. Lakini kila nilipokuwa na safari za Arusha mambo yangu yakawa mengi hivyo nikakosa kabisa muda wa kuonana naye😪
Mwaka 2021 nikiwa nafanya kazi Kigamboni Kibadq akanijulishq kwamba kwasasa yuko Dar.. Nikamuelekeza nilipo lakini akaniambia kwa situation yake hawezi kutumia usafiri wa jumuiya.. Nikaahidi kumchukulia usafiri wa binafsi ama mimi nimtembelee alipo lakini sikufanikiwa kufanya yote mawili mpaka naondoka Kigamboni🥱
Nadhani harakati na changamoto za maisha zinatunyima nafasi adhimu za upendo na kujali... Tuliendelea kuwasiliana mara moja moja lakini mwishowe mawasiliano yakakatika kabisa mpaka nililokuja kusoma hii taarifa ya kutwaliwa kwake!
Kwa moyo wa dhati naamini nina deni kwake.. Lakini naamini kuna siku nitalilipa. Pumzika kwa amani rafiki mwema😪