Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Poleni ndugu, marafiki na jamaa wote.Mungu awape faraja ktk kipindi hiki kigumu.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.Amen.
 
Ee BWANA Mungu wangu wewe uketiye juu ya maserafi na makerubi mkumbuke mtumishi wako jinsi alivyopapambana kupigania haki,ee Mungu wangu fanya habari hizi kuwa ndoto kwangu nikiamka nikute SIYO ZA KWELI
 
kwa kweli nimepokea habari kwa mshtuko na mfadhaiko mkubwa sana.ila kama binaadamu ambaye nnaamini kila mtu ataonja mauti sina budi kuuudhibiti moyo wangu na kuyasadiki yaliojiri.pia nnawapa pole wale wote walioguswa na msiba wa kipenzichetu regia. REST IN PEACE OUR BELOVED SISTER
 
RIP Regia. Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi . Hakika umeacha majonzi kwa wanafamilia yako na watanzania.
 
Sad!, Shocking!.

Naikumbuka post yake hii aliyoituma Dec, 31,2011
Halima Mchuka,ni miongoni mwa Watangazaji walionivutia sana.RIP
Kumbe ndio maana Pasco, nilikuwa nakuona Kanisani Msimbazi,Siku hizo nikiwa nasoma shule ya msingi Na sekondari.Nilikuwa nafurahi kukuona.Ulikuwa unakaa karibu Na Priva Mtema?

Ama kweli, " Wanaopendwa na Wengi, Hufa Wangali Vijana"!

RIP REGIA!
 
Ni bahati mabaya kuwa watu tusiowapenda na tusiowahitaji wakati wote huwa hawafi haraka na ni bahati mbaya sana kuwa wale tunaowapenda na kuwahitaji sana mara nyingi huwa wanatutoka mapema lakini ni bahati mbaya zaidi kuwa wale tusiowapenda, wanaotukandamizi na kutunyonya na hata kutukwamisha hawataki hata kujifunza kuwa maisha ya binadamu hutoweka haraka kama upepo uvumao kwa muda mfupi na kutoweka.
Regia Mtema alikuwa ni alama ya wanawake waliojitambua na pia walemavu ambao ulemavu ilikuwa sio kigezo cha kubweteka. Ni dada ambaye nilikuwa nikimuangalia kama mmoja wa watu wa kutumainiwa ktk harakati za kulirudisha taifa letu ktk mstari ulionyooka. RIP dada yangu niliyekuamini sana.
 
Mwenye details za jinsi ajali ilivyotokea, pls!
details za ajali za nini, Mungu ametoa Mungu ametwaa, unataka kuleta analysis za sababu za vifo kwenye msiba wa Kitanzania? Hapa tunasikitika na kumshukuru Mungu kwa kumuua Regia, kazi yake haina makosa, end of story!
 
Nimemuona mnyika kwenye Luninga hapa akilizungumzia... ni habari za uhakika kabisa ........wanafanya mpango wa kuuleta mwili Jijini
 
Regia what a true hero and a truly JF member to the core!

Invisible, Max & JF team, kwa kweli nimefarijika sana na hiyo style yenu ya kumuenzi Regia

Wote tulifadika na michango yako si huko chamani & bungeni bali pia hapa jukwaani.

Upumzike kwa amani.
 
chekini wall ya mwenyekiti wa bavicha fb

HIzo ni Njama za sisi Emu kwani alikuwa anawaumiza sana kwa ubunifu wake hivyo kila siku walikuwa wanamwombea mabaya yampate,hata hivyo hawatuwezi hiyo ni sawa na kuweka petroli katika moto ARUTA KONTINUA WAJESHI.
 
jamani wandg wapi mahali mipango ya mazishi inafanyika kwa watu wa dar???????????????????????????????tunataka kuhudhuria
msiba utakuwa Tabata kwa baba yake Mzazi,Taarifa kamili Nenda makao makuu ya CDM kinondoni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom