Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
hayo yote ni mipango yamungu,kazi yake bwana haina makosa,yeye ametangulua sisi tuko nyuma yake
Jina la bwana liabudiwe
R.I.P Mpiganaji mwenzetu
 
mh.mtema alikua mlemavu na gari ilikua ya kawaida sio maalumu kwa walemavu.kifo cha huyu dada kimenishtua na kunisikitisha sana,she was so lovely.mwenyezi mungu awe pamoja nasi katika msiba huu,poleni ndugu , na marafiki.
..........kwa jinsi nijuavyo .....gari yenye automatic unaweza kuendesha kwa mguu mmoja pasipo tatizo lolote maana pale chini hakuna pedal tatu.

Inauma sana sana kumpoteza dada, rafiki, mwana jf kamanda na mtu alietumia nguvu zake na mali zake zote kulitumikia taifa.....majuzi ni kama alikuja kutuaga wana jf kwa thread yake ya kero za watanzania.

......nategemea wana jf tuliopo dar tutafika mahali msiba ulipo tabata chang'ombe. Haya shime twendeni tukaomboleze ''gender sensitive hatunae tena''

pole sana mama regia,pole ndugu wote,poleni wanachadema, poleni wabunge, poleni wana kilombero,
mwisho poleni watanzania wote.

''bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe''
 
daah niikua na chati nae juzi kati alipotoa ile thread ya kukusanya maoni yetu she was too humble daaaah....yani cdm wamepoteza mtu muhimu kupita maelezo...nachomkumbuka regia ni ile hali ya kuwa mpiganaji kiukweli....na alipenda sana kuwahabarisha funs/friends wake juu ya chochote kinachoendelea cdm na siasa kwa ujumla, she was a true leader...ingawa walimchakachua kwenye matokeo ya ubunge kule kilombero but she remained strong and she was really coming up....R.I.P our lovely sis and a true soldier...we loved you but God loves you more...we`ll meet in paradise.
 
Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie.apumzike kwa amani.
 
Umeondoka wakati Watanzania bado wanakuhitaji sana, JF itakosa mchango wako kwani ulikuwa mstari wa mbele kutujuza kinachotokea kwenye matukio muhimu hatua kwa hatua. Ukimuona Nyerere mfikishie ujumbe wa hali ya kisiasa nchini na unyang'au unaoendelea katika rasilimali alizotuachia. Mungu akuweke mahali pema peponi Regia!
 
Nikiwa bado naendelea kuomboleza msiba huu na kutafakari kuhusu kuondoka kwa ghafla kwa dada Regia, mengi yamenijia kichwani mwangu, nimejiuliza why Regia alikuja na maneno ya namna ile ya kufungia mwaka? tunao wabunge wangapi JF akiwemo Mnyika na wengineo, tunao viongozi wa vyama wangapi JF, tunao member wangapi ambao wanajulikana nje yaJF lakini hakuna hata mmoja alikuja na kauli zenye mguso kiasi kile.....jibu ni kwamba ni wengi lakin kwanini Regia peke yake? Kiroho napaswa kukubali kwamba huenda roho wa Mungu alishamuonesha kwamba safari yake duniani imekaribia kikomo, hivo atengeneze mambo yake yaliyosalia.......,Kwa kauli zile alizozisema na namna watu wanavomshuhudia mema nina imani ya kumuona dada huyu baada ya masha haya ya dhiki (kama nitatengeneza maisha yangu kabla ya umauti wangu) kwani nashawishika kuamini kwamba hakuondoka na deni bali Mungu alimsafisha na yeye alijisafisha kabla ya safari yake......

Ndugu zangu, tulie na tuomboleze lakin tukumbuke pia kuzililia nafsi zetu kwani kazi imebaki kwetu sasa, je tutaondoka kama Regia ambaye aliisafisha njia yake kabla ya safari yake ya kurudi mavumbini, na je watu watatushuhudia mema kama ambavyo Regia ameshuhudiwa mema na jamii yake yote tokea alipokuwa machame sec hadi leo hii.

Regia, umeniachia somo, umenifundisha namna ya kuishi na watu, umenifundisha nini hasa natakiwa kufanya nikiwa hai!! Nenda dada yangu, kila mmoja kwa zamu yake, hii ni zamu yako ila najua na mimi zamu yangu itafika kwani biblia inasema kila nafsi lazima itaonja mauti!!
 
polen sana sana watanzania kwa msiba uliotukuta mungu ailaze roho ya marehem REGIA mahal pema
 
[h=6]Ratiba ya msiba: Kesho tarehe 16 Jan saa 9 jioni Mwili wa Ndugu yetu Regia Estelatus Mtema utakuwa kanisa Katoliki Tabata Chang'ombe kwa ibada na heshima za mwisho kwa familia,ndugu na marafiki. Tarehe 17 saa 4 asubuhi mwili utakuwa viwanja vya Karimjee kwa heshima za mwisho kwa Wanachama wa Chadema, vyama vingine vya siasa,wabunge, viongozi wa serikali na wananchi wote. Tarehe 18 mwili utazikwa Morogoro[/h]
 
Wakuu,
Je kuna mtu ana updates zozote kuhusu hali ya mamake pamoja na wengine waliopata ajali?

Tunawaombea wapate nafuu haraka.
 
It is true, kaondoka lakini katuachia mengi ya kumkumbuka nayo. Mwananchi la leo tarehe 15 January limeandika baadhi ya mambo ambayo alipanga kuyafanya kama mbunge na amefanikiwa kwa 70% kwa mujibu wake lilivyoaandika Mwananchi. Alikuwa kiongozi mwelewa,mwenye mipango makini na anayofuatilia kimaandishi. Alikiri kushindwa 30% ya malengo hayo kwa sababu za kiuchumi za nchi yetu na bajeti ya serikali na mipango yake. Mungu amjalie kuiona na kuishi ndani ya mbingu milele.Amin
 
Mungu ailaze roho ya mama yetu mahali pema peponi AMEEN,ni pigo kubwa sana kwa Taifa letu.
 
..........kwa jinsi nijuavyo .....gari yenye automatic unaweza kuendesha kwa mguu mmoja pasipo tatizo lolote maana pale chini hakuna pedal tatu.
Traffic Police wa kibongo wameshatoa conclusion kwamba Regia kuwa na mguu mmoja ndio kumefanya ashindwe kuchukua maamuzi mazuri kabla ya ajali! (Habari Leo)
 
tulikupenda dada yetu, lakin mungu amekupenda zaidi yetu.
upumzike kwa amani dada.
amina.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom