Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Ni kweli ni jambo la kusikitisha sana,lakini inapotokea makosa lazima tuangalie tumekosea wapi ili marekebisho yafanywe na lisije tokea jambo kama hili tena.Mimi nina maswali kadhaa:

  1. Huyu dada alikuwa ni mlemavu wa mguu na bunge limempatia gari kwa ajili yake la mkopo,bunge halikuweza kuconsider hali yake na kumpatia gari special kuendana na hali yake.
  2. Pili wabunge huwa wanapewa allowance ya madereva, ili waweze kupata madereva ambao ni professional kwa kazi yao ilikuwaje mbunge wetu akaendesha hilo gari mwenyewe?
  3. Sheria ya nchi inasemaje katika uendeshaji wa magari halihaji mtu unaulemavu?
Tukiweza kuyajibu hayo maswali tutaweza kujua tujirekebishe wapi na tumekosea wapi.

RIP Regia Mtema
 
Kuna thread inayohusiana na hayo maswali yako,ingekuwa vema upeleke huko au uisome hiyo thread .
 
Regia

RIP shujaa wetu.
Tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe.

Amen.
 
Ratiba ya msiba: Kesho tarehe 16 Jan saa 9 jioni Mwili wa Ndugu yetu Regia Estelatus Mtema utakuwa kanisa Katoliki Tabata Chang'ombe kwa ibada na heshima za mwisho kwa familia,ndugu na marafiki. Tarehe 17 saa 4 asubuhi mwili utakuwa viwanja vya Karimjee kwa heshima za mwisho kwa Wanachama wa Chadema, vyama vingine vya siasa,wabunge, viongozi wa serikali na wananchi wote. Tarehe 18 mwili utazikwa Morogoro

kunani tena.
Kwetu hairuhusiwi kabisa kuiweka maiti siku zote hizo. Mtu akifariki tu jambo la kwanza ni kumsitiri na kumzika. Hakuna zaidi.

Ok poleni sana .

Ni kweli ni jambo la kusikitisha sana,lakini inapotokea makosa lazima tuangalie tumekosea wapi ili marekebisho yafanywe na lisije tokea jambo kama hili tena.Mimi nina maswali kadhaa:
  1. Huyu dada alikuwa ni mlemavu wa mguu na bunge limempatia gari kwa ajili yake la mkopo,bunge halikuweza kuconsider hali yake na kumpatia gari special kuendana na hali yake.
  2. Pili wabunge huwa wanapewa allowance ya madereva, ili waweze kupata madereva ambao ni professional kwa kazi yao ilikuwaje mbunge wetu akaendesha hilo gari mwenyewe?
  3. Sheria ya nchi inasemaje katika uendeshaji wa magari halihaji mtu unaulemavu?
Tukiweza kuyajibu hayo maswali tutaweza kujua tujirekebishe wapi na tumekosea wapi.

RIP Regia Mtema

Angalizo hapo.

Ni vizuri mnapoendesha au kupanda gari ni vizuri mfunge safety belt. Kwani inasaidia sana kwa usalama wako wakati wa mushkirah
 
kunani tena.
Kwetu hairuhusiwi kabisa kuiweka maiti siku zote hizo. Mtu akifariki tu jambo la kwanza ni kumsitiri na kumzika. Hakuna zaidi.

Ok poleni sana .

Ni vema kujifunza kuheshimu imani za watu wengine ilimradi hazitudhuru...Hapo ndipo kiini cha amani kilipo
 
Ndio maana ninabaki kushangaa lakin tupo pamoja. Kwani tembea uone. nami najifunza mengi hapo kwa ndugu zetu wa upande wa pili.
Tupo pamoja kwa yote ingawa vile vile tupo darsani tunajifunza kwa kuona na kusikia.

RIP Bi Regia.

Nataka kujua kama AIRBAG z-lifunguka au ziligoma ili tuwashtaki TOYOTA
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Regia mahali pema peponi.
 
kwa kweri ni jambo la kusikitisha sana kwa kuondokewa na mpendwa wetu, namfahamu regia kwa uchangamfu wake, ila tuendelee kumuombea kwa mungu, TUTAKUKUMBUKA DAIMA SHUPAVU WETU KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Nataka kujua kama AIRBAG z-lifunguka au ziligoma ili tuwashtaki TOYOTA

mara nyingi huwa naona gari ikipinduka airbag huwa hazifunguki ni mara chache sana kufunguka...ila kama ikigongana au kugonga kitu mfano mti au gari lililoegeshwa barabarani hapo hufunguka...mara nyingi nimeona hivyo
 
maisha haya jamani bac 2, bado siamini kabsa....

Pole mae
Kifo ndio mwanzo wa safari yetu kuelekea kwa Muumba, ni kuzaliwa upya kwa sisi tunaoamini maisha baada ya kifo!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom