Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Eeeeh Mungu,kwanini umeruhusu hili litusononeshe kiasi hiki,nimesikitika sana na natoa pole kwa familia,Chadema na WanaJF wenzangu,she was really my role model and she taught me nothing is impossible,Mungu akulaze mahali pema peponi,tutakukumbuka daima.
 
mmmmh!!!! tumempoteza kamanda mpigania haki...Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi..
Amina
 
Ooohhhh nooooo...................Ooohhh noooo.........dah....ni ngumu sana kuamini.......
 
"Mbowe for Presidency 2015 usikubali Rais aliyewahi kuwa Padre na katibu wa TEC""
Hii signature yako unamaanisha nini?Dr Slaa anawanyima usingizi eeh?Hamuwezi kuwagombanisha Mbowe na Dr Slaa hata mfanyaje!halafu kwa taarifa yenu wanajua mipango yenu yote .....

Nimependa sana namna alivyomjibu......kuna juhudi za dhati za kuwagombanisha ...slaw,mbowe,na Zitto naomba waendelee kushikamana wakati huu na wakati wote kumuenzi mheshimiwa Regia....

Mmeonanbaadhi ya magazeti Leo Kama majira...watu wapo msibani wao habari walioipa umuhimu ni mbio za urais Chadema mmwaka 2015....na kuweka hoja ya kufikirika ya slaw,mbowe na Zitto.....kukinzana,,....
 
pole kwa wafiwa wote, inauma sana.
R.I.P dada yetu Regia.
 
Oooooooohhhhhhhhhhhhhhh maaaaaaaaaa gooooooooddddddddddddddddddddd
rip dada reg
jamani msiba ukowapi maziko wapi ,.....
 
Regia hakuumwa,ni asubuhi tu aliamka na huenda alikuwa na mipango yake ya kukamilisha kwa siku ya leo, lakini kufumba na kufumbua hatunaye tena! Tukio hili linatufundisha kuwa Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana, tena yamejaa taabu na shida, laiti tungelijua kuwa kila dakika tunayoipitisha tukiwa hai ni muujiza wa Mungu tungeliomba msamaha wa dhambi zetu kila dakika na kuwa na amani na watu wote.........!!Mungu utuwezeshe kuzihesabu siku zetu, ili siku la kutufika likitufika tufe tukiwa mikononi mwako!!

Nawaombea ndugu wote, watanzania wote na chadema wote wawe na subira na Mungu awapatie wepesi katika kuomboleza msiba huu mzito wa dada yetu Regia.

Mbele yetu ni wewe, nyuma yako ni sisi, Mungu ametwaa kiumbe chake, kazi yake haina makosa
najaribu kukutafutia jina la ASKOFU,MCHUNGAJI,MWINJILIST NAONA YOTE UKO JUU
MUNGU AMUWEKE PEMA PEPONI LAITI USEMI WAKO HAPO JUU TUTAUFWATA AKUNA MWANA JF
ATAKAELIA SIKU AKIONDOKA DUNIAN MAANA NI FURAHA ANAKWENDA KWA BABA AMBAPO TULIO DUNIANI
TUNAKUJA UKO JAMANI DADA AMETOKA MAPEMA SANA SANA ANYWAY
 
Nakumbuka mengi kuhusu Dada Regia..alikuwa anapenda kutumia neno "MKUU" anapotaka kukupa jambo,hakuwa na hasira hata kama umchafue kwenye hoja yako,alikuwa na nafasi ya kukaa na wanaJF na nadhani ni mbunge na mwanasiasa pekee ambaye alikubali kutumia muda wake mwingi hapa JF..wanasiasa wengi ni wanachama hapa lakini hawachukui muda kukaa na sisi...

Alikuwa ni mtoa habari mzuri,hata wakati fulani watu walianza kumpa chapuo kuwa katibu mwenezi wa CDM...alikuwa na thread zenye mashiko..alikuwa sio mtu wa kupost sana,lakini akishuka anakuja na thread nzito ambazo unakuta wachangiaji wake na wasomaji wanakuwa wengi...alikuwa ni dada wa watu,nakumbuka kipindi fulani aliwai kupost kwenye FB profile kuwa anatafuta mchumba,watu wakamcheka sana...akawa anasema anataka familia sasa..lol!! Regia!!!

Alikuwa tayari kukosolewa tena bila hata hasira alikuwa anasema nimepokea maoni yenu wakuu...Dada Regia zaidi ya mwanamke!! alikuwa ni mlemavu lakini alikuwa mstari wa mbele kwenye mapambano...alikuwa ni mlemavu lakini alifanya kazi zaidi ya mtu mlemavu..we will miss Regia wangu!!

Mungu tupe uvumilivu!!
 
Wakuu tumeongea mengi sana katika post zetu na tunazidi kupeana pole,ila mimi naona kuna haja ya kupeana habari sasa zinazohuzu utaratibu halisi wa mazishi,ni lini na wapi,je ni DAR au Kilombero?ili sasa tuanze kujipanga kuhitimisha safari ya dada yetu mpendwa,maana kama itakuwa withini week days tuanze kujipanga.Mwenye taarifa rasimi juu ya hilo atujuze.Na je hapo Baracuda unaelekea wapi?
 
hakuna njia mbadala ila kama kungekuwa na watu mojawapo ambao ningeambiwa niwakatie rufaa ya kifo
kuacha baba yangu mzazi,2mwl jk nyerere,bob nesta marley,muammar gaddafi,nkrumah,zakayo chacha wangwe n..........pia mh regia mtema lazima ningekata rufaaa urudi duniani
 
Dah inabidi nikubali tu.........RIP Regia....poleni sana wandugu wote
 
JF tunaomba mwongozo maana wengi tumeguswa na msiba huu na tunatamani angalau kutoa chochote kwa ajili ya kuifuta machozi familia ya Dada Regia.

Nashauri kama itawezekana wekeni namba ya Mpesa/Tigo pesa hapo kwenye front page kwa wadau kuchangia au kama utaratibu mwingine ulioandaliwa tunaomba tupeane taarifa.

Kuna mjumbe hapo juu nae ameulizia kuhusu utaratibu wa shughuli nzima,kwa hiyo tunaomba taarifa ili tuweze kushiriki kwa namna moja ama nyingine katika msiba huu.

Jina la BWANA lihimidiwe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom