Nenda dada,tangulia na sisi twaja mpendwa,
umeimaliza kazi, vita umevipiga vema,
tutakukumbuka kwa wema wako kujituma na kujitolea kwa watanzania.
ulipigana bila kuchoka mchana na usiku,jamvini hukukosa kutuletea habari.
Mbeya hukukosa,Mwanza ulifika, Arusha nilikuona, Igunga ulitisha.
Bungeni hukulala mpaka kilipoeleweka,kilombero kama kawa, hata jangwani ulishiriki.
Ulikuwa front line,kuitafuta Tanzania tunayoiota,kwenye jua ulisota huku umepiga kaki.
kaki ilikuwa ishara kwako, kwamba hakuna kulemba.
mpendwa dada, najua utaonana na makamanda wengi ila kwa leo naomba kipekee kabisa
unisalimie hawa wafuatao; Chacha Wangwe, Shirembi (IGEMBE),Sylvester Rwegasira, Martini Luther king,Samora Machel,
John Garang,Robert Owuko,Edward Sokoine, Lucky DUbe,Mohamar Gadaf,Patrice Lumumba,Solomon Mahlangu, Jaramog Oginga na Ken Saruiwa. Waambie tunawakumbuka sana na kwamba tunaendeleza mapambano MPAKA KIELEWEKE.
La mwisho kabisa dada mpenzi, nakuomba uniwekee kiti karibu na wewe ili nikija nikae karibu na wewe.
"NOT YET UHURU, ALLUTA CONTINUA"!
Wasalaam,
Mtolewa.