Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Zimethibitishwa,

ni habari ya kweli, ni pigo kwa wapigania haki na maendeleo ya taifa hili.
Mungu akurehemu kadri ya matendo yako.
 
Habari zilizothibitishwa na JF ni kuwa Regia Mtema (mb) amepata ajali na Kufariki dunia eneo la Ruvu Darajani.

Ndugu wa Karibu wanasema alikuwa kaenda kukagua Kiwanja alichopewa na Wazazi wake na baadae kwenye mkutano wa CHADEMA huko Kibaha.

Habari hizi zimethibitishwa.

Sisi tulimpenda Regia Mungu anampenda zaidi.
 
nani atakaye wakilisha ile michango ya wanaJF bungeni maana regia is no more..
 
Kero ulizopewa Jamvini hapa majuzi tafadhali sana Regia zifikishe Mbinguni
 
Habari zilizothibitishwa na JF ni kuwa Regia Mtema (mb) amepata ajali na Kufariki dunia eneo la Ruvu Darajani.

Ndugu wa Karibu wanasema alikuwa kaenda kukagua Kiwanja alichopewa na Wazazi wake na baadae kwenye mkutano wa CHADEMA huko Kibaha.

Habari hizi zimethibitishwa.

Hakika Regia Mtema simfahamu kwa SURA tofauti na kukutana humu JF. Lakini, CHADEMA kweli mmepoteza JEMBE, poleni sana WATANZANIA. Machozi yamenilenga kwa kifo cha Regia Mtema! RIP Regia Mtema.

ANGALIZO: CHADEMA toeni mafunzo ya Usalama kwa viongozi wote wa chama, la sivyo watakwisha!
 
Rest in peace kamanda regia mtema..nasikitika umekufa ikiwa bado sijakwambia navyokukubali...nakukubali sana regia from ze bottom of my heart..r.i.p
 
Khee airtel nao wamesikia huo msiba mungu ilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina
 
Wakati mwingine unaweza kujiuliza maswali mengi sana bila majibu-kwamba kwa nini Mungu umeruhusu hili litokee, kwa nini litokee leo, kwa nini litokee kwa huyu nk nk!!
Kweli Wema hawana maisha.... Mavumbini tulitoka na mavumbini tutarudi. Daima utakumbukwa na wengi na tutakukosa sana. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yako dada Regia mahali pema peponi, Amina.
 
Kama ni kuchanganyikiwa leo ndo nimechenganyikiwa baada ya kupata radio one breaking news, eeeh Mungu mbona imekuwa hivi jamani?

Regia mpenzi tulikupenda sana lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi, ni habari ambayo mtu unaweza shindwa kusadiki lakini ndio ukweli wenyewe, poleni sana familia ya Regia, poleni sana wana JF na watanzania wote kwa ujumla.

Ttutakumiss sana Regia, Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe
 
Zile kero ulizokusanya naomba ukampelekee Mungu,pengine yeye anaweza kutusikiliza..
 
Hakika tutakukumbuka Regia Mtema.....kapumzike kwa Amani
 
habari ya kusikitisha sana hii..! kweli nimeamini chema hakidumu..! Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe..!
 
Kwa nini umekwenda mapema hivi dada yangu,mbunge wetu mtarajiwa wa kilombero?ooh no!rest in peace Regia,u ll miss u sister!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom