Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
OMG is this true? somebody tell me it is not...
 
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Regia mtema amefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea Ruvu darajani.Poleni makamanda.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina.source Brekn news radio one.

Jamani mbona machozi yamenitoka. Nimetetemeka hapa nilipo hata miguu imeshindwa kuhimili kukanyaga chini. Ni Regia huyu ninayemjua humu JF? Ni huyu aliyetueleza amewafanyia nini watu wa Kilombero?
Sijaamini bado lakini kama ni hivyo basi sisi sote twaenda huko.
 
Nimefuta machozi tayari, JF tunaomba muongozo. uniform za chadema tshirt na tusikie zuio la alshabab kunyimwa kuhudhuria msiba. Mungu tupe uvumilivu katika kipindi hiki familia ya chadema inayopitia. Kamanda wewe ni shujaa, sisi ngojea tuendeleze mapambano na imani hili ulilipenda tufanye.
 
Jamani ni kweli mi nmethibitisha hilo kutoka kwa mtoto wa kaka yake alafu kwa ushahidi zaidi source: ITV na RADIO ONE BREAKING NEWS.
 
Habari zilizothibitishwa na JF ni kuwa Regia Mtema (mb) amepata ajali na Kufariki dunia eneo la Ruvu Darajani.

Ndugu wa Karibu wanasema alikuwa kaenda kukagua Kiwanja alichopewa na Wazazi wake na baadae kwenye mkutano wa CHADEMA huko Kibaha.

Habari hizi zimethibitishwa.
Mama yangu weeee! siwezi amini hiki kitu hata siku moja! jamani hizi habari ni kweli au ninaota?
My God Regia dada angu!
 
Ama kweli Dunia hadaa Ulimwengu shujaa!

Ndiyo imetimia kwa mwenzetu kwa kutuacha ingali tunamhitaji lakini tutasema MUNGU alimhitaji zaidi!
 
Hakika maisha ya binadamu ni kama upepo upitao,siwezi amini kilichotokea,lakini kwa kuwa mungu ndie ajuaye siri ya kila mtu hapa duniani na tunaelezwa kuwa kila goti litapigwa basi KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA

Tulikupenda sana lakini mungu amekupenda zaidi jina la bwana liabudiwe

R.I.P dada yetu
 
Habari hii nimejaribu kuilazimisha kuwa uongo lakini nimeshindwa na nimeamua kukubaliana na hali halisi kwamba hatuna tena KAMANDA anayeitwa REGIA DOTTO MTEMA sisi tulimpenda ila Mungu wetu amempenda zaidi.

Hii imenifanya nikumbuke maneno ya kwenye vitabu vitakatifu kuwa " Mwanadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi", pia " Mwanadamu hataishi katika fahari yake milele naye atakufa tu na kuiacha fahari yake"

Raha ya milele umpe Ee Bwana, na Mwanga wa milele umwangazie. Ampumzike kwa amani. Amen
 
Aiseeeeeeeee hapa kuna mkono wa sisiemu,haiwezekani hapa kuna mkono wa mafioso wa sisiemu,haiwezekani ni juzi juzi tu alikusanya kero mbali mbali wakakinukishe bungeni sasa sisiemu wanafanya nini hapa???? Yani wote wamepona kasoro yeye tu,wassup? Mkono wa mtu hapa
 
Jamani mbona machozi yamenitoka. Nimetetemeka hapa nilipo hata miguu imeshindwa kuhimili kukanyaga chini. Ni Regia huyu ninayemjua humu JF? Ni huyu aliyetueleza amewafanyia nini watu wa Kilombero?
Sijaamini bado lakini kama ni hivyo basi sisi sote twaenda huko.
ni kweli,kazi ya mungu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom