RC Mghwira: Misiba mingi Kilimanjaro inatoka maeneo mengine nchini. Si kweli kuwa watu wanafariki dunia kutokana na Covid 19

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,282
Mghwira.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema misiba mingi iliyopo mkoani humo inatoka maeneo mengine na si kweli kuwa watu wanafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Amesema Mkoa huo upo salama na kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli akifafanua kuwa misiba hiyo hutokea mikoa mingine na watu wanakwenda kufanya mazishi mkoani Kilimanjaro.

Mghwira ameeleza hayo leo Jumatano Februari 17, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari, “kuna taarifa zipo kwenye mitandao ya kijamii zikieleza Mkoa wa Kilimanjaro hasa mji wa Moshi kuwa na maambukizi makubwa ya corona, taarifa hii inadai uwepo mkubwa wa vifo vinavyotokana na maambukizi haya na kudai Hospitali zetu za Mawenzi na KCMC zimezidiwa kutoa huduma za msingi.”

"Taarifa hizi zinalenga kuwajengea hofu wananchi na hasa wanamichezo wanaotegemea kuja kushiriki Kilimanjaro Marathon itakayofanyika Februari 28 mwaka huu. Nitumie fursa hii kuwaambia Mkoa wa Kilimanjaro uko salama na niwatake wananchi kupuuza taarifa hizi ambazo sio za kweli.”

“Ifahamike kuwa Mkoa wetu huu una idadi kubwa ya watu waliopo ndani na nje ya Mkoa na ifahamike kuwa utaratibu uliopo ni kwamba watu wanapenda kuleta misiba nyumbani ya kila aina. Ni kawaida hapa nyumbani misiba ipo mingi wakati wote kwa sababu inaletwa lakini unashangaa wanaokuja na misiba wanasema sisi ndio tuna corona.”

Chanzo: Mwananchi

Pia soma

- Meya Raibu: Hakuna Corona Moshi, Haya ni Mashambulizi dhidi ya Uchumi wetu

- Moshi: International School of UWCEA yasitisha masomo Baada ya Wanafunzi 2 kupatwa na Corona
 
Huyu mama kwa hili sijamuelewa.

Je watu wameanza kupeleka misiba miezi ya hivi karibuni?
Kama sio kwanini miezi hii ndio wapeleke sana ? Swali ni kwamba kwanini trend imeongezeka?

Na je anapima kila maiti au kila maiti ina death certificate hadi aseme kwamba vifo sio ugonjwa fulani?

Unajua mara nyingine kukaa kimya ni bora kuliko kuongea vitu ambavyo havina logic.
 
Nyinyi wanasiasa ndiyo mnaotuua na hii corona kwa kuwa waongo na wapingaji wa kila taarifa ili tu msalie madarakani. Mwogopeni Mungu, mbona huku Uru wenyeji wengi tu wamekufa kwa covid.
 
Nakubaliana naye anayebisha awe anafungua radio one mida ya saa saba mchana huwa wanakuwa na kipindi cha matangazo ya vifo huwa ni wachaga watupu ukisikiliza waweza dhani ni wachaga pekee hufa Tanzania na vifio hutoka maeneo tafauti tofauti ya nchi.

Anayebisha atege sikio radio one stereo saa saba mchana na saa kumi baada ya taarifa zao za habari za saa saba na saa 10 hata leo saa saba iko jirani tu asikilize
 
Sikiliza radio one matangazo ya vifo muda si mrefu uone matangazo ya vifo vya wachaga toka mikoa mbalimbali ambao mazishi yatafanyika kilimanjaro

 
Kwa hiyo ni mkoa wako tu ndio wanafia mikoa mingine wanaletwa nyumbani! Kwanini idadi hiyo isiwe mikoa mingine?! Msitufanye watto na nyie viongozi msikubali kukiri uongo kumfurahisha mtu huku unaenda ibadan kusali.
 
Back
Top Bottom