peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,833
- 21,466
Moshi. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka watumishi, watendaji na wadau wa Mahakama kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuweka mifumo mizuri itakayowezesha utatuzi wa migogoro kwa njii ya usuluhishi ili kuondoa mrundikano wa mashauri na kesi mahakamani.
Babu ametoa rai hiyo leo jumatatu Januari 23, 2023 katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, wakati akizindua wiki ya Sheria kwa mkoa wa Kilimanjaro ambapo amesema mkoa huo unaongoza kwa kuwa na migogoro mingi hususani ya ardhi.
Amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi kutawezesha upatikanaji wa haki kwa wakati na kupunguza gharama na mrundikano wa kesi mahakamani
“Kauli mbiu yetu ni umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu, wajibu wa mahakama na wadau, kaulimbiu hii ni muhimu sana na kama tutaitumia vizuri, itasaidia kupunguza mrundikano wa kesi na mashauri mahakamani.
“Niombe wadau wa mahakama wanaoshulikia migogoro kuweka mifumo mzuri ili kuhamasisha utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhshi, kwani hakuna Mkoa una migogoro mingi kama Kilimanharo, na hasa migogoro ya ardhi.
“Lakini pia nitoe rai kwa watumishi na watendajiwa mahakama, kujiepusha na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wamaadili na kuachanana ufanyaji kazi wa mazoea, wahudumieni wale wanaohitaji haki kwa weledi,” Babu.
Amewataka wananchi kujitokeza katika wiki ya sheria kufika kupata msaada na ushauri wa kisheria ili kuweza kutatua migogoro inayowakabili kwa njia ya usuluhishi.
Kwa upande wake, Jaji mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Dk Juliana Massabo amesema katika wiki ya sheria watatoa huduma mbalimbali kwa wananchi na watumishi na wadau wa mahakama wamejipanga vizuri kutoa elimu ya sheria, utendaji kazi wa Mahakama na msaada wa kisheria.
“Mahakama imeona ni vyema utatuzi wa migogoro mbalimbali ikatatuliwa kwa njia ya suluhisho, ambayo hutoa fursa ya migogoro kwa haraka na kwa gharama nafuu ikilinganishwa na gharama zinazotumika katika kuendesha kesi mahakamani.
“Na huduma tutakazozitoa katika wiki hii ni kuonyesha wananchi umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kujenga uchumi endelevu na kila mwananchi atakayefika atapata huduma lakini pia tutatoa elimu mashuleni, vyuoni, masokoni na katika mikusanyiko ya watu,” amesema Jaji Massabo.
Chanzo: Mwananchi