RC Chalamila: Nahitaji Busara Kuuongoza Mkoa wa Mwanza

Ila huyo Chalamila dish lake limeyumva si kawaida .....angalia kile kichwa chake lazima alikunywa yale maji na kubanwa siku ya kuzaliwa sio kwa ropo ropo ile
 
Bahati mbaya unaweza kutu unaowamba wakuongezee busara nao hawana hizo busara
 
Mie aiseee namwomba kwa kutumia staili yake ya umwamba, alotumia Mbeya, aje asafishe mji wa Mwanza yaani ni karahaaa hakupitiki........ yule aliye kuwa wa Dar,naona yeye kama yalimshinda......kazi kwelikweli.
Na 'Wasukuma' watamkoma hakyanani.
 
MWANZA-4.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amewaomba wakuu wa idara na watendaji wa Serikali mkoani humo kumuazima busara akidai za kwake pekee hazitotosha.

Chalamila ametoa ombi hilo leo Jumatatu Mei 24, 2021 wakati akizungumza na watendaji, wafanyabiashara, wakuu wa idara, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo mara baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

Huku walioudhuria katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi wakiangua vicheko, Chalamila amesema, “yaani mimi hivi unataka niwe kama mzee Meck Sadick (mkuu wa mkoa mstaafu), akiwa mzee Sadick pale na mimi unataka niwe na busara hivyo hivyo? Mjue kabisa nitakuwa najilazimisha kitu ambacho sipo nacho kabisa! Na hii kitu ni automatic tu.”
Mods kwanini mmebadilisha heading yangu? Headinga yangu ilikuwa inasomeka hivi "KUMBE WALIKUWA WANAJUA WANAONGOZA BILA HEKIMA/BUSARA"
 
Ongoza kwa kufuata miiko za Uongozi acha uoga, acha kutafuta kiki, acha kutetemeka naamini utaongoza vizuri tu
 
MWANZA-4.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amewaomba wakuu wa idara na watendaji wa Serikali mkoani humo kumuazima busara akidai za kwake pekee hazitotosha.

Chalamila ametoa ombi hilo leo Jumatatu Mei 24, 2021 wakati akizungumza na watendaji, wafanyabiashara, wakuu wa idara, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo mara baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

Huku walioudhuria katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi wakiangua vicheko, Chalamila amesema, “yaani mimi hivi unataka niwe kama mzee Meck Sadick (mkuu wa mkoa mstaafu), akiwa mzee Sadick pale na mimi unataka niwe na busara hivyo hivyo? Mjue kabisa nitakuwa najilazimisha kitu ambacho sipo nacho kabisa! Na hii kitu ni automatic tu.”
Huyu hapa
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom