RC Chalamila: Nahitaji Busara Kuuongoza Mkoa wa Mwanza

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
MWANZA-4.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amewaomba wakuu wa idara na watendaji wa Serikali mkoani humo kumuazima busara akidai za kwake pekee hazitotosha.

Chalamila ametoa ombi hilo leo Jumatatu Mei 24, 2021 wakati akizungumza na watendaji, wafanyabiashara, wakuu wa idara, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo mara baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

Huku walioudhuria katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi wakiangua vicheko, Chalamila amesema, “yaani mimi hivi unataka niwe kama mzee Meck Sadick (mkuu wa mkoa mstaafu), akiwa mzee Sadick pale na mimi unataka niwe na busara hivyo hivyo? Mjue kabisa nitakuwa najilazimisha kitu ambacho sipo nacho kabisa! Na hii kitu ni automatic tu.”
 
Kule fb kuna mahali amekaririwa akiwataka wananchi wote watenge chumba kimoja katika nyumba zao kiwe mortuary!
 
Kule fb kuna mahali amekaririwa akiwataka wananchi wote watenge chumba kimoja katika zao kiwe mortuary!
Ametindikiwa!!! au alitaka aseme chumba cha ibada!!! Hee!!! apimwe akili kuna jambo halipo sawa
 
"Kama gharama ya mochwari ni ghali tenga chumba kimoja kwako kiwe mochwari ya familia".RC Chalamila

Chanzo: itvtz

Kuna Watu GENTAMYCINE nikiambiwa kuwa Wanaugua Akili naweza Kukukatalia ila kwa huyu nitakukubalia upesi sana tu na hata kutoa Msaada wa kumuwahisha katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili ( Kipa Katoka ) Mirembe Mkoani Dodoma.

Kinachonishangaza niliwahi kuambiwa kuwa alishawahi kuwa Mwalimu ( Mkufunzi ) wa Chuo hapa Tanzania hivyo huenda hata hao aliowafundisha hivi sasa nao Akili zao ni za Kipa Katoka ( Wamedata Kichwani ) kama Yeye.

Watu kama hawa CCM inawatoa wapi?
 
Hiyo ndiyo busara ya Mwanza aliyoisema

1621885268039.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom