Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Wakuu kutokana na mafanikio na hasara mlizopata kupitia hiyo Betting je would you recommend wengine ambao hawaijui kujaribu bahati zao ama tusiingie kabisa huko? Hizo wins zinatamanisha ila pia hivo vipigo mmh
Sista kama unataka uzeeke mapema ,jaribu kubet. Kama njia ya kutafuta kipato utachakaa haswa.

Pengine uifanye kama starehe unabet hizi 200, 300, 1000 au 2000 uwe unatafuta ya vocha.
 
Sista kama unataka uzeeke mapema ,jaribu kubet. Kama njia ya kutafuta kipato utachakaa haswa.

Pengine uifanye kama starehe unabet hizi 200, 300, 1000 au 2000 uwe unatafuta ya vocha.
Aisee sasa mbona watu hawaachi tu! Mkuu ukicompare ushindi na vipigo je mhindi kakupa hasara ama wewe umempa hasara yeye?
 
Aisee sasa mbona watu hawaachi tu! Mkuu ukicompare ushindi na vipigo je mhindi kakupa hasara ama wewe umempa hasara yeye?
Hawaachi kwa sababu asilimia kubwa wameumizwa sana, wamepoteza pesa nyingi wanataka revenge warudishe pesa zao na huo ndio unakuwa mwanzo wa kupoteza pesa nyingi.

Kiufupi betting ni hasara hasara hasara. Profitable gambler sidhani kama wanafika hata asilimia moja ya wote wanaobeti,
Ingekuwa inalipa asilimia 80 ya vijana na boda boda tungekuwa tunatembelea mavieite humu mjini
 
Kuhusu hasara kuna mwezi nilibahatika nikampiga million 9 ila nikirudi kuangalia kwenye betting history bado ninahasara kubwa mno.
 
Pamoja na kupitia maisha yenye changamoto mbali mbali, sikuwahi hata mara moja kucheza betting, bahati nasibu, network marketing au Forex. Hizo habari za kuvuna pesa kirahisi rahisi nilishazikataa. Akili yangu imegoma kabisa katika hayo.

Najua nikijaribu kujiingiza huko nitakuwa teja wa hizo mambo. Wacha niendelee kuwa maskini lakini nisiwe mtumwa wa kitabia tena nikiangamia huku nikijiona.
 
Yaani mnaoingia kwenye betting,forex na gambling games zozote.... wakati shuleni mlifeli hesabu za probability, differentiation na integration wala statistics...mnajitafutia kifo.
sasa ndugu (integration na differentiation) Inahusika vip kwenye Gambling/betting. Hiyo proba ambayo ni zao la statistics itakusaidia kujua chance ya event fulani kutokea whether ni 0.5,0.1 etc lakini haikupi majibu halisi. Ukirusha shilingi hesabu itakwambia majibu ni mawili either kichwa au mwenge p(×)=0.5 Ila nikazi yako wewe kubashiri kama ni kichwa au tail itatokea.

Nimesoma hadi stochastics process, ina dili na game of chance tu,.Nimefundishwa mpaka Gods of luck anavyo fanyakazi kwenye gambling/betting lakini nimeishia kupoteza
Screenshot_20210505-053107_Google.jpg
 
Wakuu kutokana na mafanikio na hasara mlizopata kupitia hiyo Betting je would you recommend wengine ambao hawaijui kujaribu bahati zao ama tusiingie kabisa huko? Hizo wins zinatamanisha ila pia hivo vipigo mmh
Jiongeze ww ...hela unayo Hongwa ndo uibetie ....hata ukiliwa Huna la kupoteza
Japo hata hiyo ya kuhongwa lazima uliwe kwanza
 
Pamoja na kupitia maisha yenye changamoto mbali mbali, sikuwahi hata mara moja kucheza betting, bahati nasibu, network marketing au Forex. Hizo habari za kuvuna pesa kirahisi rahisi nilishazikataa. Akili yangu imegoma kabisa katika hayo.

Najua nikijaribu kujiingiza huko nitakuwa teja wa hizo mambo. Wacha niendelee kuwa maskini lakini nisiwe mtumwa wa kitabia tena nikiangamia huku nikijiona.
Mkuu hiyo ASP ni Afro Shiraz Party au As Soon as Possible??
 
Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.
Huyo jamaa si ndo yule bro wako aliyekufukuza home🤣🤣
 
Yaani mnaoingia kwenye betting,forex na gambling games zozote.... wakati shuleni mlifeli hesabu za probability, differentiation na integration wala statistics...mnajitafutia kifo.

Duuuhhhh, Mnapoongelea Forex jitahidini muwe mna elimu kidogo, sasa waliopata A za hayo uliyoyaweka ndio wana uwezo wa kubeti?
 
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
Vp mkuu Naona mkeka wako wa Jana ulitick
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom