Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Na Mimi pia naungana na jamaa
Screenshot_20210514-115816.jpg
 
Maisha yote ni kamari.
Unasoma ukitegemea kutoka kimaisha ila mambo yanakuwa tofauti
For sure tena ki Africa Africa particularly Tanzania bongo kila kitu almost ni kubet

Kutafuta wenza tunabet
Kusoma watu wana bet
Siasa kuchagua viongozi tunabet

Almost every where tuna bet
 
nishakula kama laki tano hivi,nishaliwa zaidi ya hela hiyo.

nimerudisha hela yangu kidogo.

bv am happy.

i loved the whole adventure.
 
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
Haina noma Mkuu,
Sasa hauna tips za mechi za leo nikatupia mzigo hata sikukuu hii nisitoke kapa?
We endelea kubaki tu Mpenzi mtazamaji, Tips unanipa mimi.
 
Kuna uzi humu ndugu kama wewe ni gambler mzoefu utakuwa unaufahamu
 
Chris wood vp umefanikiwa kuacha kubeti au ndo umeamua kurudi kuzikimbiza hasara zako? Hii kitu ni kama drugs..niliingia tu nione experience yake ikoje ila i still regret the decision i made that day aisee
 
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
Da pole sana, kwakua umechelewa sana kuujua ukweli
 
watu wanakula wewe unaliwa, waachie wanaokula ndugu. kuna ndugu yangu anaweka elfu moja tu na anaweka timu 30 (thelathini), ameshinda mara mbili mbele yangu, kwanza akashinda 1.6milion, mara ya pili akawala 1.4millin
on kwa elfu moja. mm nashukuru wakati wote kanipa elfu kumi kumi :p
 
Bet with only what you can afford to loose.Shida ya vijana wengi wameichukulia betting Kama ajira/ kiteka uchumi.
Pia too much expectations ndo huwa zinaumiza watu kwenye betting.
 
U
watu wanakula wewe unaliwa, waachie wanaokula ndugu. kuna ndugu yangu anaweka elfu moja tu na anaweka timu 30 (thelathini), ameshinda mara mbili mbele yangu, kwanza akashinda 1.6milion, mara ya pili akawala 1.4millin
on kwa elfu moja. mm nashukuru wakati wote kanipa elfu kumi kumi :p
Upo mkoa gani mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom