Rasmi nimeamua kuachana na betting. Kubet ni kutafuta umasikini na ufukara

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
407
1,000
We endelea kulia, izo zote nimepiga ndani ya wiki hii. Cheza live than angalia mpira vizuri kabla ya kustake
View attachment 1771945 View attachment 1771946 View attachment 1771947 View attachment 1771948 View attachment 1771950
Achilia mbali mikeka yote niliokula kuna mwezi upepo uliniijia vizuri nikapiga 9million but mpaka sasa nimepiga hesabu nimejikuta na hasara kubwa mno. Soo hiyo kula laki au 50,000 kwangu sio ishu. Unaweza kula 50,000 ukarudi kupoteza 200000 mfululizo soo hakuna unachokifanya
 

Maybe2021

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
615
500
Umefanya la maana kuliko kupoteza bora ufanye investment
Mwaka 2019 wakati bitcoin ina drop watu wanaipigia kelele ilifika hadi usd 3000 na kipindi hicho nilikuwa naweza kutoa usd 1500 ninunue hata nusu bitcoin lakini washikaji wakaanza kusema tohold kwanza inaweza drop hadi 500 ndio hadi leo unaona imefika 60000 roho inauma
Mbaya zaidi watu wanasema by 2028 huko inaweza fika 500,000usd roho inaniuma kwa kweli
Karibu tufanye holding mkuu lak yako Leo baada ya miaka 3 mamilion ya pesa
 

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
407
1,000
Hapo umemuonesha upande wako wa bahati ili kumufanya awe inspired.
Muoneshe pia upande wa maumivu ili awe cautious.

Nijuavyo mimi, watu wa gambling ni kama motivational speakers. Wanakuonesha upande mmoja mzuri. Mengine utakutana nayo huko mbele ya safari.
Ndio maisha ya social media mtu anaonesha upande mmoja wa shilingi
 

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
407
1,000
Hapo umemuonesha upande wako wa bahati ili kumufanya awe inspired.
Muoneshe pia upande wa maumivu ili awe cautious.

Nijuavyo mimi, watu wa gambling ni kama motivational speakers. Wanakuonesha upande mmoja mzuri. Mengine utakutana nayo huko mbele ya safari.
Kuna mikeka ya lost kibao kaificha. Kulikuwa hakuna haja ya ku screenshot picha moja moja, yeye angeenda pale kwenye settled history yote loss and win inajionesha kisha ana screenshot picha moja anaiweka hapa.
 

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,042
2,000
Kwanza niseme tu mimi nikati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga amakuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takriban mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau ,yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama,, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu jamii forum nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea dar es salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia ,na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita jkt halafu 60000 naweka mfukoni,.kisha wale vibarua badala ya kuwa lipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari ,tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu ,muda wote sina furaha ,nilikuwa napenda kusoma,kuongeza ujuzi,kutafuta kazi,kuwekeza,kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, ninamuda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama nitatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui,na adui wangu ane hujumu uchumi wangu ni betting.
Unaacha michezo ya hela mkuu acha utani
 

Ramah eid

JF-Expert Member
Dec 15, 2020
507
1,000
Kwakwel mkuu umenichekesha sana umenifanya kukumbuka hiyo kauli nilitamkaga 2018 lkn nikarud ulingoni ila tambua betting ni km upepo flan hasa hizi mechi za mwisho wa ligi mzee mikeka inachanika mpk unasema sibet tena yan mwisho wa ligi usishanga timu ipo top 6 inapewa odd 3 na ambayo ipo mkian kabisa inapewa odds 2 yan timu za mkiani ni nuksi mwisho wa ligi ila pole sana pia hela ya betting usije kutoa zile pesa muhimu km nauli,chakula itakucost sana
 

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
407
1,000
Kwakwel mkuu umenichekesha sana umenifanya kukumbuka hiyo kauli nilitamkaga 2018 lkn nikarud ulingoni ila tambua betting ni km upepo flan hasa hizi mechi za mwisho wa ligi mzee mikeka inachanika mpk unasema sibet tena yan mwisho wa ligi usishanga timu ipo top 6 inapewa odd 3 na ambayo ipo mkian kabisa inapewa odds 2 yan timu za mkiani ni nuksi mwisho wa ligi ila pole sana pia hela ya betting usije kutoa zile pesa muhimu km nauli,chakula itakucost sana
Sio poa ndugu napenda pesa sana,pia na tamaa lakini pesa ya kanji ni ngumu asee. Kama utajiri unatoka kwenye kubet ngoja ikae sitoweka pesa yangu tena hata sh 10,
 

Leloo June

JF-Expert Member
May 5, 2016
863
1,000
Ahaaaaa hatari tumuombee asirudi tena mchezo aumfai.
Huo uamuzi wa hasira tu! Kapumzika tu huyo! Akirudi akala mikeka miwili atarudi rasmi!

Tatizo wasichokijua watu betting ina upepo! Ukiona siku umebeti mara 3 mfululizo unamla bookmarker tu jua siku hio una upepo! Jiwashe mpaka ambapo utaona game zinaanza kukukataa.Zikichana 2 mfululizo tulia jua upepo umebadilika!

Sasa utakuta pale mtu ndio anaingia mawenge anataka arudishe hasara matokeo yake anafumuliwa marinda! Mi nishaliwa na game moja hela yote nilikuwa nazuia corner kila nikizuia inachana kwa kuongezeka corner moja mara ya tatu mchezo uko mwishoni nikasema narudisha hasara weee 😂😂😂😂😂😂 account ilifuka moshi!
 

Dr Dre

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,579
2,000
mimi baada ya kufanya analysis kwa strategy yenye lowest risk yaani odds ndogo nikaona ili niwe na continues winning inabidi katika mikeka 5 nishinde angalau 3 nikaacha huu ujinga.betting ni game tu asee usifanyie kupata pesa weka jero tulia. mambo ya kuweka laki gemu moja upate laki 2 . ndani ya mikeka mitano tu tayari una loss tayari una stress tayari una umaskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,021
2,000
Kwanza niseme tu mimi ni kati ya watu, waliokuwa wakiamini betting kwa asilimia 100, nilikuwa na imani betting ndio kitu itanitoa kimaisha, kuhusu betting ulikuwa huniambii kitu, kuna ile kauli watu huwa wanasema beti kama starehe, Lakini mimi nimekuwa nikiifanya kama kazi ya kujiingizia kipato.

Nilikuwa mstari wa mbele kutoa Matusi, kejeli husda na masimango kwa wale wote, waliokuwa wakionesha kupinga ama kuleta hoja kinzani kuhusiana na gambling/betting.

Katika kipindi kifupi takribani mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo ndio nilianza kuifanya betting kama kazi.

Lakini kwa huo muda mfupi, imeniletea hasara kubwa kubwa kubwa ambayo sitokuja kuisahau, yaani zile pesa ambazo nimepoteza ningesema badala ya kutuma kwenye betting company, niziweke kwenye kibubu now ningeweza kufungua biashara kubwa sana.

Baada ya vipigo kuzidi, huwa kuna msemo wanasema sikiliza wataalamu inaonekana strategies unazotumia sio salama, Hao wanaojiita watalamu watakwambia usiweke timu nyingi weka timu chache ,"tafuta odds mbili halafu tia laki," Aloo huo msemo ndio umenifukia kabisa hadi sasa naandika hapa sina hata mia mbovu.

Jana kuna mkeka niliucopy kutoka kwa jamaa mtata sana humu Jamiiforums nikaweka pesa ya nauli ambayo leo nilikuwa naelekea Dar es Salaam, kwa mazingira ya kutatanisha sana pesa yote nimeliwa, mpaka muda huu nimejilaza hapa nasingizia naumwa.

Kwenye betting sio kwamba watu hawashindi wanashinda ila kunautofauti mkubwa sana kati kuliwa na kushinda so ukiifanya kwa muda mrefu ukaja piga mahesabu baada ya mwaka utajikuta na hasara kubwa Hadi utaogopa kama sio kulia.

Betting imefanya nashindwa hata kununua nguo mpya hadi zile nilizomaliza nazo masomo zimeanza kupauka sio kwamba hela sipati hapana zote zinaishia kwenye mikeka, yaani getto unaweza kuta nimenunua sukari robo, mchele kilo mbili halafu kwenye simu nimebet 50000 na yote inaliwa.

Mwaka jana nilikuwa nasimamia mashamba ya jamaa fulani sasa nilikuwa nikipokea hata pesa za kupalilia, na mimi boss wa vibarua najitengea ekari yangu moja ya palizi maana nimepita JKT halafu 60000 naweka mfukoni kisha wale vibarua badala ya kuwalipa 60000 nawalipa 40000 kwa ekari, tutalima weee nikimaliza pesa yote naenda kuliwa kwenye betting.

Usiku wa leo nimekaa nikafanya projection nikiendelea hivi baada ya miaka 5 ijayo nitakuwa mmoja kati ya watu masikini zaidi Tanzania, At 20s vijana wengi hutumia kujenga future zao mimi natumia kubomoa, Betting imeniletea uvivu, muda wote sina furaha, nilikuwa napenda kusoma, kuongeza ujuzi, kutafuta kazi, kuwekeza, kuchangamana na watu, kufanya kazi, mdau wa michezo, mapenzi but now nimekuwa kama mtu aliepigwa bomu.

Bado sijachelewa, nina muda wa kutosha kusahihisha makosa niliyoyafanya, sihitaji tena kuwa mtumwa, nimekubali kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya, sioni kama ni tatizo kuanza moja, ninaamini tatizo ni kuendelea kukumbatia adui na adui wangu anaehujumu uchumi wangu ni betting.
Hiyo ni Jana tu. Tunacheza kujifurahisha. Hapo ungetia laki moja yako ungepata ngapi?
Screenshot_20210503-181122_M-Bet.jpg
Screenshot_20210503-181109_M-Bet.jpg
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
9,069
2,000
Mimi huwa naamini kila kitu maishani ni kamari. Hivyo betting nitaacha siku wao wakiacha
Nina rekodi ya kuliwa 4.9mil baada ya Chelsea kudraw.
Nina Rekodi ya kupiga 10mil stake 250K
Duh mkuu unamuwekea muhindi hadi 250,000/=? Jamani watu mna hela hadi naona wivu?🤔 hongera kwa kupata 10mil
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom